Rev Mtikila's case no 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rev Mtikila's case no 2

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Hiphop, Jul 17, 2010.

 1. Hiphop

  Hiphop Member

  #1
  Jul 17, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nina maswali mengi juu ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya rufaa juu ya rufaa ya serikali kwenye kesi ya mgombea binafsi;
  1.Hukumu ina defects maana hakuna mahala kulipoonyesha appeal allowed au appeal dismissed?
  2. Kama imeandikwa kwenye katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kuchaguliwa au kuchagua kiongozi ampendaye iweje hoja ya mgombea binafsi iitwe ya kisiasa?
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 17, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa, Mahakama ya Rufani haikusema kwamba appeal imekuwa "upheld" au "dismissed" isipokuwa imejifunga "pingu" yenyewe eti kwamba "suala hilo ni la kisiasa zaidi kuliko kisheria!"
   
 3. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 772
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Si lazima watumie maneno "rufani imekataliwa." Hukumu ilisema Mahakama hazina mamlaka ya kusikiliza kesi hii. Maana yake amuzi lolote la mahakama ya chini kuhusu kesi hii ni batili. Mwisho wa hadithi.
  Kubadilisha Katiba si kazi ya mahakama, ni ya bunge, wanasiasa. Mahakama kazi yake kutafsiri katiba.

  Hukumu haukusema hili ni swala la kisiasa kwa hiyo basi mwisho wa kesi. Hicho ndio kilichoripotiwa ovyo, lakini walieleza kinaga ubaga kuwa Katiba ndio imesema mgombea huru hakuna. Wakasema wao hawawezi kuibadilisha, japo wanapenda mgombea huru. Mtikila alishitaki kipengele cha Katiba si halali. Wakasema, wenye mabavu ya kutangua vipengele vya katiba ni wabunge. Hamuitaki waambieni.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 17, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kwamba Mahakama haina uwezo wa kubadili kifungu cha Katiba, lakini ina Mamlaka kukiona kifungu fulani kinaenda kinyume na haki ya binadamu ya kuwa huru kushiriki katika shughuli za kiserikali bila kulazimika kujiunga na chama chochote cha siasa. Kwa mfano katika Ibara ya 21 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inasema kama ifuatavyo: "Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria." Lakini Ibara ya 39 (2) ya Katiba hiyo inataka wanaotaka kugombea urais LAZIMA wajiunge kwanza na Chama cha Siasa. Huoni kwamba vifungu hivi vinagongana?
  Kwa nini Mahakama ifumbe macho na kuamua kutokuona kwamba haki zinaminywa na kuagiza kwamba chombo kinachohusika (Bunge) kirekebishe Ibara zinazominya uhuru wa raia?
   
 5. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 772
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Ahsante sana.

  Sasa tunavutana nini tena?

  Ndio hicho walichosema, hawana mamlaka ya kubadili kifungu cha Katiba. Kwishne.

   
 6. Hiphop

  Hiphop Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli kuwa mahakama haina uwezo wa kubadili ila ina uwezo wa kutoa directions ya nini kifanyike,hicho ndiyo kilichofanywa na mahakama kuu pale ipoipa bunge jukumu la kutunga sheria itakayowezesha uwepo wa independent candidate.Hiyo ndio tunaita Checks and Balance,mahakama kuu na busara zake zote imeshindwa kutoa solution ikaishia kuiita hoja ni ya kisiasa as per page 48 of the judgement.
   
 7. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 772
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Ahsante tena.

  Na hicho ndicho Mahakama ilichokisema, haina uwezo wa kubadili katiba.
   
 8. Hiphop

  Hiphop Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sisi kama wananchi tulitegemea mahakama itoe mwongozo wa nini kifanyike maana suala la independent candidate ni haki ya msingi ya kila mtanzania na sio suala la kisiasa kama mahakama ilivyodai.Unaporudisha mjadala kama huu bungeni ili warekebishe haijasaidia maana bunge linaongozwa na siasa za chama tawala,sasa matokeo yake ni kuwa siasa zitazuia utekelezaji wa haki ya msingi kwa watanzania.
   
Loading...