Rev. Msigwa dhidi ya Prof. Shivji

Rev. Msigwa dhidi ya Prof. Shivji

Katufu

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2012
Posts
523
Reaction score
309
Peter Msigwa

Kwa HESHIMA zote, napinga mtazamo wa prof. Issa Shivaji, kuwa eti, uzalendo ni kuitii serikali iliyokomadarani. Na utaifa eti ni ukereketwa wa nchi yako hata Kama huipendi serikali. Kwa mtazamo huu, Nyerere hakuwa mzalendo kwa kuwa aliipinga serikali ya mkoloni? Vipi Mandela aliyepinga serikali ya kibaguzi kule bondeni naye hakuwa mzalendo? Vipi waganda walioipinga serikali ya Idd Amini? Vipi serikali Kama ya Mabutu wa DRC?

Kuna wakati kuichukia serikali serikali iliyopo madarakani ni uzalendo, serikali huja na kuondoka, ila taifa hubaki, serikali yoyote ambayo, inatumia vibaya raslimali za nchi yake, ikichukiwa ni uzalendo. Serikali ya kifisadi, inayoendekeza ujangili, wizi na uporaji wa Mali za umaa inafaa kuchukiwa kwa nguvu zote na huo ndio uzalendo.

Serikali inayokiuka haki za binadamu, inayokandamiza demokrasia, kuitii serikali Kama hiyo sio uzalendo. Ndugu Issa Shivji... Sijakuelewa hasa msomi Kama wewe. ..how would you say that? saw you on news yesterday (ITV).
 
Kwanza shavji si kashiriki kuandika uhalo wa chenge…!! hostoria itamuhukumu huyo mpuuz
 
Mbona mnataka kumvunjia heshima Prof. Shivji kumfananisha na Msigwa.

hizo ndizo za CHADEMA mara zote huwa wanajaribu kuwalinganisha makanjanja wao na watu maarufu siyo Tanzania hata Duniani.
 
Kwanza shavji si kashiriki kuandika uhalo wa chenge…!! hostoria itamuhukumu huyo mpuuz

Kamati ya CHENGE inatokana na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, acha ukanjanja wako.
 
Mbona mnataka kumvunjia heshima Prof. Shivji kumfananisha na Msigwa.
Heshima sio uprofesa wa cheti bali mambo mazuri unayoyafanya/sema yenye manufaa kwa jamii. Unaweza kuwa prof lakina bado ukawa mpumbavu na unaweza usijue hata kusoma na kuandika lakini ukawa na mabo yenye maana na yanayojenga jamii. Kwahiyo kama prof ni mjinga lazima tumseme kwa ujinga wake.
 
Hata Teja ana haki ya kutoa maoni yake, vivyo hivyo Msigwa naye, lakini Prof. atabaki kuwa prof. tu
 
Mbona mnataka kumvunjia heshima Prof. Shivji kumfananisha na Msigwa.

Havunjiwi mtu heshima ila ukiongea pumba lazima ujibiwe kwa hoja na kamwe pumba haijibiwi kwa pumba.Inatakiwa kujibiwa kwa hoja na Msigwa kajibu kwa hoja kwa kutumia mifano halisi.

Naamini nimekujibu swali lako
 
Mbona mnataka kumvunjia heshima Prof. Shivji kumfananisha na Msigwa.

Tatizo tunataka kuwasifu watu hata wakikosea.
Tunaogopa kuwarekebisha watu wamapokosea ndio maana inafikia watu wameiba, bado wanaambiwa warudishe walichoiba badala ya kuwafikisha mahakamani kisa ni kuogopa wataaibika kwa sababu tunawaogopa.Nawakumbusha tu ya EPA.
tunaipeleka wapi hii nchi?Hatukatai kuwa huyu Mzee anaheshima yake hapa Tanzania.Lakini akikosea aambiwe ili asilewe na sifa kufanya mambo kwa tafakari zaidi.
 
Peter Msigwa

Kwa HESHIMA zote, napinga mtazamo wa prof. Issa Shivaji, kuwa eti, uzalendo ni kuitii serikali iliyokomadarani. Na utaifa eti ni ukereketwa wa nchi yako hata Kama huipendi serikali. Kwa mtazamo huu, Nyerere hakuwa mzalendo kwa kuwa aliipinga serikali ya mkoloni? Vipi Mandela aliyepinga serikali ya kibaguzi kule bondeni naye hakuwa mzalendo? Vipi waganda walioipinga serikali ya Idd Amini? Vipi serikali Kama ya Mabutu wa DRC?

Kuna wakati kuichukia serikali serikali iliyopo madarakani ni uzalendo, serikali huja na kuondoka, ila taifa hubaki, serikali yoyote ambayo, inatumia vibaya raslimali za nchi yake, ikichukiwa ni uzalendo. Serikali ya kifisadi, inayoendekeza ujangili, wizi na uporaji wa Mali za umaa inafaa kuchukiwa kwa nguvu zote na huo ndio uzalendo.

Serikali inayokiuka haki za binadamu, inayokandamiza demokrasia, kuitii serikali Kama hiyo sio uzalendo. Ndugu Issa Shivji... Sijakuelewa hasa msomi Kama wewe. ..how would you say that? saw you on news yesterday (ITV).

Mbangaizaji Msigwa uwezo wa kuelewa na kutafsiri mantiki ya alichokisema Prof Shifji. Ni wa kumpuuza tu kama wapuuzi wengine. Na hajui kuwa anachokisema kina maana gani katika Sheria za Uhaini.
 
Kwa kweli Profaser wa siku hizi, wanapenda mno hata nyumba ikiharibika ni wagumu kuwaeleza ukweli. Inanikumbusha story ya mfalme Daudi alivyocheza hadi akabaki uchi, wapambe wake walishindwa kumuambia amekaa uchi. shame you professor
 
Kinachoimaiza hii nchi ni unafiki na kuwaogopa watu kiasi cha kushindwa kuwashauri wanapokosea kwa sababu wanawadhifa fulan au tuna maslahi nao.
Kama Pro. kakosea naye anakosolewa kwa sababu si kwamba alikuwa anaongelea ndani ya fani yake ya sheria. \
Tuache ujinga wa kuogopa majina ya watu.
Kama baba yako ni mlevi anampiga mama yako kila siku bila sababu utanyamaza kwa sababu yeye ni baba?
INAUMIZA KWA SABABU HAYA YANASHABIKIWA NA VIJANA AMBAO WATAENDELEA KUWEPO MIAKA MINGI IJAYO,NI HERI WANGEKUWA WAZEE AMBAO TUNAJUA KIZAZI CHAO KITAKWISHA.
NAOMBA TUAMKE SI KUSHABIKIA NA KUONA NI SAHIHI KWA KILA JAMBO LINALOSEMWA NA MTU KWA SABABU YA JINA AU WADHIFA WAKE.
 
Back
Top Bottom