Rev. Msigwa dhidi ya Prof. Shivji

Rev. Msigwa dhidi ya Prof. Shivji

Sijaelewa kitu ngoja wasomi waje watuchambulie hiyo lugha
 
Prof,issa shivj:uzalendo niki to i na luge shiny serikali iliyopo madarakani

una miaka mingapi upo Tanzania? Tafuta walimu wa kiswahili wakufundishe utaelewa tu sababu kiswahili si kigumu kama unavyotaka kutuaminisha!
 
Duuuh, hata mimi nimetoka kapa! Mwanzoni nilidhani heading imekosewa. Ila ulipoirudia na kumkosoa mchangiaji wa kwanza nikaamini kuwa kumbe hata mimi sijaelewa. Nitakuwa nachungulia kujua wasomi wameelewaje na michango yao ikoje.
 
Wana jamvi hayo hapo juu maneno ya msomi toka udsm,naomba wana jamvi tuyajadili sote kwapamoja hapa,kikubwa katika mjadala tujikite kwenye hoja na mifano

Mkuu hicho ulichoandika kuwa prof shivji kasema, ni kigagagigikoko. Maana yake ni"mimi ni mpumbavu"
 
Samahani wana jamvi wakati na edit ghafla ikatokea ajali hapa mtaani ya pik pik na mtoto amekufa wa miaka 7 ila maana yake"-uzalenfo ni kutii serikali iliyopo madarakani by issa shivji"
 
Peter Msigwa

Kwa HESHIMA zote, napinga mtazamo wa prof. Issa Shivaji, kuwa eti, uzalendo ni kuitii serikali iliyokomadarani. Na utaifa eti ni ukereketwa wa nchi yako hata Kama huipendi serikali. Kwa mtazamo huu, Nyerere hakuwa mzalendo kwa kuwa aliipinga serikali ya mkoloni? Vipi Mandela aliyepinga serikali ya kibaguzi kule bondeni naye hakuwa mzalendo? Vipi waganda walioipinga serikali ya Idd Amini? Vipi serikali Kama ya Mabutu wa DRC?

Kuna wakati kuichukia serikali serikali iliyopo madarakani ni uzalendo, serikali huja na kuondoka, ila taifa hubaki, serikali yoyote ambayo, inatumia vibaya raslimali za nchi yake, ikichukiwa ni uzalendo. Serikali ya kifisadi, inayoendekeza ujangili, wizi na uporaji wa Mali za umaa inafaa kuchukiwa kwa nguvu zote na huo ndio uzalendo.

Serikali inayokiuka haki za binadamu, inayokandamiza demokrasia, kuitii serikali Kama hiyo sio uzalendo. Ndugu Issa Shivji... Sijakuelewa hasa msomi Kama wewe. ..how would you say that? saw you on news yesterday (ITV).

Serikali ya Makaburu AU ya Wakoloni ziliwekwa madarakani na nani?
 
Shivji tuache tu ipigania Tanganyika yetu zidi ya serikali hi ya kifisadi
 
hizo ndizo za CHADEMA mara zote huwa wanajaribu kuwalinganisha makanjanja wao na watu maarufu siyo Tanzania hata Duniani.

Ukijua mantiki ya kitu, lazima ujibu kwa kutoa facts. Si lazima kila anachoongea Prof. Shivji ni sahihi, tafakari pia na siyo kumeza kama bongo tulivozoea. Msigwa aweza kuwa sahihi katika hili. jamani, tembeleeni hata nchi zilizoendelea basi muulize na kuona wao walifikaje hapo walipo, sio kubishi tu. Watanzania tujaribu kujifunza jamani. si kubishi tu sababu ya kuokoa upande unaoshibia, angalia mantiki ya hoja, ni sahihi, kama sio, nawe argue pia.
 
It is practically career suicide for a professor to profess conformance to the same views [ political and academic] as the rullers and those having influence in awarding the professorships
 
Back
Top Bottom