Rest In Peace Prof Leonard Shayo

Rest In Peace Prof Leonard Shayo

Na Said Njuki, Arusha

MWANASIASA na msomi aliyegombea urais wa Tanzania mwaka 2005, Profesa Leonard Shayo, amefariki dunia.
Profesa Shayo ambaye pia alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati katika wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, alifariki dunia jana saa 5.30 mchana katika hospitali ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Profesa Shayo ambaye alikuwa mmoja wa wataalamu wachache wa Hisabati na Sayansi pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini (MAKINI) ambacho kilimsimamisha kugombea urais mwaka huo.
Kwa mujibu wa mdogo wake, Bw. Habibu Mandari, Profesa alilazwa Ijumaa iliyopita baada ya kuzidiwa akiwa mjini hapa kikazi.
"Profesa aliugua ghafla na alipopelekwa hospitalini, waligundua kuwa na shinikizo la damu, kisukari na homa ya mapafu. Walifanikiwa kuishusha sukari lakini Mwenyezi Mungu aliamua kumchukua," alisema Bw. Habibu.
Alisema mwili wake umehifadhiwa kwenye mochari ya hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Profesa Shayo katika kampeni za urais mwaka 2005 alikuwa kivutio kikubwa kwa wapiga kura, kwani tofauti na wagombea wengine, yeye aliendesha kampeni akitumia gari dogo na kipaza sauti bila wapambe.
Katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, alishinda kwa kuzoa kura zaidi ya milioni tisa kati ya 10,590,016 zilizopigwa, huku marehemu Shayo akiambulia kura 17,O33.
Wengine ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata 1,317,220, Bw. Freeman Mbowe wa CHADEMA aliyepata kura 671,780, Bw. Augustino Mrema wa TLP kura 84,131, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP (39,990), Bw. Edmund Mvungi wa NCCR-Mageuzi(56,423).
Wagombea wengine walikuwa ni mwanamke pekee Bibi Anna Senkoro wa PPT Maendeleo (18,741), Bw. Paul Kyara wa SAU (16,380) na Dkt. Emmanuel Makaidi wa NLD (21,525).
Marehemu Shayo alizaliwa katika kijiji cha Mamba Kotela na kukulia Rombo mkoani Kilimanjaro. Ameacha mjane na watoto wanne, watatu wakiwa ni wa kike.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikowahi kufanyakazi marehemu, Profesa Rwekaza Mukandala, alishitushwa na kifo hicho na kumwombea marehemu alazwe mahali pema peponi na kuahidi kutoa taarifa baadaye kupitia kwa wasaidizi wake kwani hakuwa amepata taarifa kuhusu kifo hicho.
 
'Mwenyezi ailaze roho ya marehemu Shayo mahali pema peponi...'
 
RIP PROFF LEONARD SHAYO,umefanya kazi kubwa ktk jamii yetu,hata kama kuna wasiokubali ulichowahi kufanya kwa taifa hili aidha kitaaluma au kisiasa sisi TUNAKUTAMBUA
MUNGU AIWEKE ROHO YAKE PEMA PEPONI.
 
RIP prf. Shayo, tangulia mpiganaji, hiyo ni njia yetu sote, kila nafsi itaonja mauti. Mungu wetu awafariji wapendwa wako wote walio guswa na msiba huu.
 
Ahaaa..nimempoteza mwalimu wangu wa hesabu za kikomputa( Discrete Mathematics)!!
Mungu amlaze pema peponi!!

Amen.
 
Faith na wadogo zako poleni sna kwa kufiwa na baba... pia wantanzania wote poleni maana hiyo ilikuwa resource ya nchi yetu!!!
 
RIP Proffessor L. Shayo.
Poleni familia ya Prof. Shayo. Mungu awape moyo wa ujasiri muweze kukabili msiba huu wa kuondokewa na mlezi wenu. Watanzania wote tuko nyuma yenu katika maombolezo hayo. Kumbukeni: Mapenzi ya Mungu yametimia. Sote tulimpenda Shayo, lakini Mungu alimpenda zaidi. Roho za Marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani. Amina.
 
RIP Prof Shayo

tutamiss sana makala zako kwenye Mwananchi na utetezi wako kwa wanyonge wa nchi hii wanaoonewa.

Mungu aipumzishe roho yako kwa amani milele.
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe, Amen
 
RIP Prof, wafiwa polei sana na msiba.

Mungu awape nguvu ya kutekeleza yote mazuri aliyowafundisha marehemu wakati wa uhai wake.
 
Apumzike kwa amani.

Wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki poleni.

Ni pigo kwa Taifa.
 
profesa leornard shayo amefariki dunia jana saa nne asubuhi katika hospitali ya aicc ya mjini Arusha kwa ogonjwa wa homa ya mapafu,mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi amina
 
NA SAID NJUKI, ARUSHA

MWANASIASA na msomi aliyegombea urais wa Tanzania mwaka 2005, Profesa Leonard Shayo, amefariki dunia.

Profesa Shayo ambaye pia alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati katika wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, alifariki dunia jana saa 5.30 mchana katika hospitali ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Profesa Shayo ambaye alikuwa mmoja wa wataalamu wachache wa Hisabati na Sayansi pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini (MAKINI) ambacho kilimsimamisha kugombea urais mwaka huo.

Kwa mujibu wa mdogo wake, Bwana Habibu Mandari, Profesa alilazwa Ijumaa iliyopita baada ya kuzidiwa akiwa mjini hapa kikazi.

"Profesa aliugua ghafla na alipopelekwa hospitalini, waligundua kuwa na shinikizo la damu, kisukari na homa ya mapafu. Walifanikiwa kuishusha sukari lakini Mwenyezi Mungu aliamua kumchukua," alisema Bwana Habibu.

Alisema mwili wake umehifadhiwa kwenye mochari ya hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Profesa Shayo katika kampeni za urais mwaka 2005 alikuwa kivutio kikubwa kwa wapiga kura, kwani tofauti na wagombea wengine, yeye aliendesha kampeni akitumia gari dogo na kipaza sauti bila wapambe.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, alishinda kwa kuzoa kura zaidi ya milioni tisa kati ya 10,590,016 zilizopigwa, huku marehemu Shayo akiambulia kura 17,O33.

Wengine ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata 1,317,220, Bwana Freeman Mbowe wa CHADEMA aliyepata kura 671,780, Bwana Augustino Mrema wa TLP kura 84,131, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP (39,990), Bwana Edmund Mvungi wa NCCR-Mageuzi(56,423).

Wagombea wengine walikuwa ni mwanamke pekee Bibi Anna Senkoro wa PPT Maendeleo (18,741), Bwana Paul Kyara wa SAU (16,380) na Dkt. Emmanuel Makaidi wa NLD (21,525).

Back
Top Bottom