Report ya Jairo full text

Hiyo tume iliwahusisha Ngeleja/Jairo/Luhanjo na Adam Malima - Hawa wanaosukuma hili gari kwa njia moja au nyingine walihusika kwenye utafunaji wa hela za walalahoi lazima sheria ifuate mkondo kwakuwashitaki!
 
Tume iliyoundwa kuchunguza ubadirifu wa fedha walizokula kina Jairo hawa kwanini hawakuhusishwa nao pia lazima sheria iwachukulie hatua tena kali sana ikiwezekana hata kufungwa!
PICHA+NA+2.jpg

Wanafiki tu hawa, mmoja wao ndiye aliyeiba nyaraka na kuwapa hao ze wabunge
 
Tume iliyoundwa kuchunguza ubadirifu wa fedha walizokula kina Jairo hawa kwanini hawakuhusishwa nao pia lazima sheria iwachukulie hatua tena kali sana ikiwezekana hata kufungwa!
PICHA+NA+2.jpg

Hivi huyo mama upande wa kushoto kabisa mume wake alimuona? Usikute hajwai hata sukuma baiskeli ya mume wake anaenda kusukuma gari la mwanaume mwingine.....
 
Du!! Nyie ni Nooooma! Halafu kuna yule mama sijui alibeba maua yule! Yaani kama ningekuwa mumewe lazima pangechimbika maana furaha yake ilipitiliza!
 
Kweli Permanent Secretaries ni miungu watu. Mtu mzima unatoka nyumbani unaaga familia unakwenda kazini halafu kamera inakuchukua uko kwenye shughuli ya aibu hivi? Kweli rushwa na ufisadi vinaleta upofu. Kama Mch. Israel Natse (Karatu) alivyosema kwenye kuchangia ripoti ya kamati teule (yeye alikuwa mjumbe), Mungu amependa kuleta ukombozi kwa waja wake kupitia uozo huu wa maadili. Hii ilikuwa dharau kubwa kwa Bunge. Itakumbukwa kuwa muda mfupi baada ya zoezi hili Jairo alitoka akachukua Taxi kuondoka ofisini baada ya JK kuagiza vinginevyo. Wanatakiwa wamalizie kazi ya kumsukuma kuelekea nyumbani na baadaye Segerea. Bahati mbaya ni hao hao wanafurika kwenye nyumba za Ibada kumwomba Mungu. Ni Mungu yupi wanayemlilia? Ni huyu huyu ambaye watoto wanaokaa chini darasani, wajawazito wanaojifungulia barabarani, wagonjwa wanaokufa bila dawa kwenye zahanati zetu, watu wanaochangia maji ay tope na wanyama hata baada ya miaka 50 ya uhuru?. Nadhani atakuwa Mungu tofauti.
 
Hawa ilikuwa lazima walambe miguu ya bosi wao.Maana bosi akila anachobakisha wao wanamalizia.Si mlisikia tume ilisema kwamba watumishi zaidi ya mia mbili walitoka wizarani kwenda kwenye uwasilishwaji wa bajeti Dodoma<kugawana mijiposho>?Ndio hao na uniform zao za suruari nyeusi!
 
mbele ya ubwabwa wa buleeee hata wewe ungesukuma, mtu kashinda pale feli njaa kali kasikia mnuso angefanyaje wengine ni wale waoshamagari wa pale wizarani , mama yule ni mpika chai pale ofisini hajui chocote, hawa tuwaache jamani maana njaa, lakini wale wa kuongezea 1 kwenye makumi ni wakuua kabisa
 
Haya wakuu ile taarifa ya kamati teule kuchunguza uhalali wa uchangishaji feddha aliofanya Jairo hii hapa. Enjoy!!!!!
 

Attachments

  • KAMATI+TEULE-yaJairo.pdf
    419.1 KB · Views: 89
Kweli Permanent Secretaries ni miungu watu. Mtu mzima unatoka nyumbani unaaga familia unakwenda kazini halafu kamera inakuchukua uko kwenye shughuli ya aibu hivi? Kweli rushwa na ufisadi vinaleta upofu. Kama Mch. Israel Natse (Karatu) alivyosema kwenye kuchangia ripoti ya kamati teule (yeye alikuwa mjumbe), Mungu amependa kuleta ukombozi kwa waja wake kupitia uozo huu wa maadili. Hii ilikuwa dharau kubwa kwa Bunge. Itakumbukwa kuwa muda mfupi baada ya zoezi hili Jairo alitoka akachukua Taxi kuondoka ofisini baada ya JK kuagiza vinginevyo. Wanatakiwa wamalizie kazi ya kumsukuma kuelekea nyumbani na baadaye Segerea. Bahati mbaya ni hao hao wanafurika kwenye nyumba za Ibada kumwomba Mungu. Ni Mungu yupi wanayemlilia? Ni huyu huyu ambaye watoto wanaokaa chini darasani, wajawazito wanaojifungulia barabarani, wagonjwa wanaokufa bila dawa kwenye zahanati zetu, watu wanaochangia maji ay tope na wanyama hata baada ya miaka 50 ya uhuru?. Nadhani atakuwa Mungu tofauti.
Mkuu, umasikini huu ni shida kweli, ukiwaona hao jamaa walivyotunisha masaburi yao utadhani wanatafuta promotion, nadhani na baba yao wizarani pia alikimbia bunge siku ile kwenda kuhudhuria mapokezi ya mdogo wake huyo.. gharama zote hizo zinalipiwa na sisi..duh
 
Haya wakuu ile taarifa ya kamati teule kuchunguza uhalali wa uchangishaji feddha aliofanya Jairo hii hapa. Enjoy!!!!!

Ngoja tusubiri kuona maamuzi ya msanii Kikwete, lakini kwa jinsi yeye mwenyewe alivyo mchafu sidhani kama ataweza kumfukuza kazi Jairo sana sana atamwambia labda astaafu ili alipwe mafao yake yote. Tusubiri.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIABUNGE LA TANZANIA​
__________​
TAARIFA YA KAMATI TEULE YA BUNGEILIYOUNDWA KUCHUNGUZA UHALALI WAUTARATIBU WA WIZARA KUCHANGISHAFEDHA KWA AJILI YA KUPITISHABAJETI BUNGENI​
___________________________​
DODOMA​
Novemba, 2011​
ii​
Y A L I Y O M OUtangulizi​
11.1 Chimbuko 11.2 Kuundwa kwa Kamati Teule 31.3 Hadidu za Rejea, Wajumbe wa Kamati Teule na Muda wa Kazi 6
1.0​
1.4 Njia Zilizotumika katika Kukamilisha Kazi 8​
Utaratibu Uliobainika​
122.1 Uchunguzi kuhusu Utaratibu Uliobainika wa kukusanya fedha kwaajili ya kukamilisha uwasilishwaji wa Hotuba za Bajeti za WizaraBungeni132.2 Uchunguzi kuhusu Uhalali wa Utaratibu wa Uchangishaji Kisheriana Kikanuni202.3 Uchunguzi Iwapo Taasisi zilizochangia zina Kasma kwa ajili yauchangiaji huu27
2.0​
2.4 Uchunguzi kuhusu Matumizi Halisi ya Fedha Zilizokusanywa 32​
Kupitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu zaSerikali kuhusu Uchunguzi alioufanya​
403.1 Uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali413.2 Uchambuzi wa Yaliyojitokeza kwenye Taarifa ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali503.3 Upungufu Uliojitokeza katika Hitimisho la Katibu Mkuu Kiongozi 60​
3.0​
3.4 Maoni ya Kamati Teule Kuhusu Taarifa ya Ukaguzi Maalum 63​
4.0​
Mfumo wa Serikali kujibu Hoja zinazotolewa Bungeni 664.1 Misingi ya Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge kwa Hojazinazotolewa Bungeni66
iii​
Usahihi wa Utaratibu Uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozikwa Suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Ndugu David Kitundu Jairo​
755.1 Taratibu za Kuliarifu Bunge chini ya Katiba, Sheria na Kanuni zaBunge na Misingi ya Utawala Bora755.2 Usahihi wa Utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi 78​
5.0​
5.3 Kubaini kama Utaratibu huo Umeathiri Dhana ya Haki na Madarakaya Bunge81​
Kuangalia Nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa Ngazi yaMakatibu Wakuu katika Kushughulikia Masuala yaNidhamu ya Anaowateua​
966.1 Misingi ya Katiba, Sheria na Kanuni za Utumishi kuhusiana naMamlaka ya Uteuzi kwa Makatibu Wakuu966.2 Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa naRais976.3 Taratibu za Kushughulikia Masuala ya Kinidhamu kwa Watumishiwa Umma wanaoteuliwa na Rais99​
6.0​
6.4 Uchambuzi wa Yaliyojitokeza 101​
Mambo Mengine yenye Uhusiano​
1047.1 Uvujaji wa Nyaraka za Serikali 1047.2 Nafasi za Uteuzi, Ajira na Mpango wa kurithishana MadarakaSerikalini1117.3 Uhusiano wa kikazi kati ya Mawaziri na Makatibu Wakuu 1177.4 Uchangishaji wa Sh.22,000,000.00 wa Taasisi Nne za Wizara yaNishati na Madini kwa ajili ya Semina ya Wabunge1207.5 Uhusiano Miongoni mwa mihimili ya Dola 124
7.0​
7.6 Mamlaka ya Hiari (​
Discretionary Powers) kwa Makatibu Wakuu waWizara na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma129
iv​
8.0​
Hitimisho 138
Maoni na Mapendekezo ya Kamati Teule​
1409.1 Maoni ya Kamati Teule 140
9.0​
9.2 Mapendekezo ya Kamati Teule 145​
10.0​
Shukrani 149
Viambatisho​
1​
TAARIFA YA KAMATI TEULE YA BUNGE ILIYOUNDWA KUCHUNGUZAUHALALI WA UTARATIBU WA WIZARA KUCHANGISHA FEDHAKWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI BUNGENI____________________1.0 UTANGULIZIMheshimiwa Spika,​
Katika Kikao cha 56 cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, tarehe 26 Agosti, 2011 ukirejea Azimio la Bunge lililopitishwa katikaKikao cha 54, tarehe 24 Agosti, 2011, uliunda Kamati Teule ya Bunge kwamujibu wa Kanuni 2(2) na 117(4) za Kanuni za Bunge, Toleo la 2007​
1.Kamati Teule iliundwa kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizarakuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha Bajeti na kubainisha endapo kitendocha Katibu Mkuu Kiongozi kutoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari juu yauchunguzi wa suala la fedha zilizokuwa zikichangishwa na Wizara ya Nishati naMadini kimeingilia au kuathiri madaraka ya Bunge. Kamati Teule imekamilishakazi hiyo na ifuatayo ni Taarifa kamili kwa mujibu wa Kanuni ya 119: -1.1 ChimbukoMheshimiwa Spika,
Taarifa Rasmi (​
Hansard) ya Majadiliano ya Bunge ya Kikao cha 27 cha Mkutanowa Nne, tarehe 18 Julai, 2011 inaonyesha kwamba wakati wa Mjadala waHotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, miongoni mwa WaheshimiwaWabunge waliopata fursa ya kuchangia ni Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo,(Mb.). Katika mchango wake, pamoja na mambo mengine, Mhe. BeatriceShellukindo, (Mb.) aliweka Mezani kwa Spika kivuli cha barua aliyoitoleamaelezo kama ifuatavyo: -
1​
Hansard ya Tarehe 26 Agosti, 2011, Ukurasa wa 139.
2​
Kwamba barua hiyo ilisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na MadiniNdugu David Kitundu Jairo, na ilielekezwa kwa Wakuu wa Taasisi, Vitengo naIdara zilizo chini ya Wizara kuwataka wachangie kufanikisha mawasilisho yaHotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni.​
(Tazama Kiambatisho I)
Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.) alisema kuwa anadhani fedha hizo zinazidiSh.1,000,000,000.00 kwa hiyo akahoji zimekwenda wapi wakati kwa utafitialioufanya Taasisi zimejigharamia zenyewe katika ushiriki wake zoezi la Bajetiya Wizara Bungeni Dodoma.Aidha, alihoji ukusanyaji wa fedha nyingi kiasi hicho na kupelekwa kwenyeakaunti ya Taasisi ya GST iliyoko chini ya Wizara na ambayo makao yake niDodoma. Pia aliuzungumzia ukusanyaji wa fedha kiasi hicho na matumizi yakeakilinganisha na changamoto kadhaa zilizoko katika Sekta ya Umeme nchini.Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.) alitamka kusudio lake la kutaka kutoa hojamahsusi kuhusu masuala ya umeme na changamoto zake likiwemo hili lauchangishaji, baadaye kabla Mheshimiwa Waziri hajahitimisha Hoja yake​
2.Mhe. Christopher Ole-Sendeka, (Mb.) alikuwa miongoni mwa wachangiaji katikaHoja ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Katika mchango wake pamoja namambo mengine alichangia kuhusu ukusanyaji wa Sh.50,000,000.00 kutoka kwakila Idara iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini na akahoji fedha hizozilikuwa ni kwa matumizi yapi? Alielezea mashaka yake kuwa huenda umma waWatanzania wakahusisha fedha hizo na uvumi uliokuwepo wa uwepo wa kilekilichoitwa mgao wa fedha usiokuwa rasmi. Mhe. Ole-Sendeka naye alishtushwana kiwango hicho cha fedha kuwa kikubwa na hasa akihoji matumizi yake.Akasisitiza kuwa Waziri Mkuu amuagize Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kufanya ukaguzi wa dharura. Mhe. Ole-Sendeka, (Mb.) aliahidikumuunga mkono Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.) wakati atakapotoa Hojayake kuhusu masuala haya3.
2​
Hansard ya tarehe 18 Julai, 2011, Ukurasa wa 68 – 70.
3​
Hansard ya tarehe 18 Julai, 2011, Ukurasa wa 77.
3​
1.2 Kuundwa kwa Kamati TeuleMheshimiwa Spika,​
Jumatano Agosti 24, 2011, kabla ya Kipindi cha Maswali, Mhe. Kabwe ZuberiZitto, (Mb.) aliomba Mwongozo wa Spika. Akitoa maelezo ya Mwongozo,alirejea tukio la Jumanne Agosti 23, 2011 ambapo Katibu Mkuu Kiongozi alitoataarifa kwa umma juu ya suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinikuchangisha fedha Taasisi zilizo chini ya Wizara yake kwa ajili ya kuwezeshamaandalizi na uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni. Akifafanuaalisema Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi inaonyesha kwa umma waWatanzania kwamba tuhuma zilizotolewa na Mhe. Beatrice MatumboShellukindo, Mbunge wa Kilindi, dhidi ya Katibu Mkuu wa Nishati na MadiniNdugu David Kitundu Jairo hazipo kwa kuwa hazikuweza kuthibitishwa.Akihusisha uamuzi huo na kauli ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kiongozi waShughuli za Serikali Bungeni, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, (Mb.); naakirejea kauli ya Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu uwezekano wa Wabungekushtakiwa kwa “​
defamation”, Mhe. Kabwe Zitto, (Mb.) alisema kuwa hadhi yaBunge imeingiliwa na hivyo akatoa Hoja kwamba Bunge lisitishe kujadiliShughuli za Serikali hadi Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali itakapoletwa mbele ya Bunge ili ijadiliwe.Mhe. Kabwe Zitto, (Mb.) alitoa Hoja hii kwa mujibu wa Kanuni ya 51 ya Kanuniza Kudumu za Bunge inayohusu Haki za Bunge ikisomwa pamoja na Kanuni ya55(3)(f) inayohusu Hoja ambazo zinaweza kutolewa bila taarifa ikiwemo jambololote linalohusiana na haki za Bunge4.
Mheshimiwa Spika,​
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. WilliamLukuvi, (Mb.) alisimama na alipopewa nafasi ya kuzungumza, pamoja na kukirikuwa jambo hili lilivuta hisia za umma wakiwemo Waheshimiwa Wabunge,​
4​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011, Ukurasa wa 4.
4​
(​
public interest), alizungumzia Kanuni ya 51(1) ya Kanuni za Kudumu za Bungena akataka kujua kama masharti ya Kanuni hii yalizingatiwa katika kufikia Hojahiyo kutolewa na kuungwa mkono. Mhe. William Lukuvi, (Mb.) aliisoma Kanunihiyo kama ifuatavyo: -
“Mbunge anayetaka kuwasilisha jambo ambalo anaamini linahusianana haki za Bunge atafanya hivyo wakati unaofaa kufuatana nampangilio wa Shughuli za Bunge uliowekwa na Kanuni hizi na atakuwaamemwarifu Spika mapema kuhusu kusudio lake hilo na jambo ambaloanataka kuwasilisha.”​
Akitoa majibu kwa Mhe. William Lukuvi, (Mb.), Naibu Spika Mhe. Job YustinoNdugai, (Mb.) alitoa maelezo kwamba wakati Kikao cha siku hiyo kinaanzaalipokea taarifa fupi ya maandishi kutoka kwa Mhe. Kabwe Zitto, (Mb.) yakusudio la kutaka kutoa Hoja hiyo, na akasisitiza kwamba Hoja imetolewakiutaratibu na imeungwa mkono na Wabunge wengi. Hata hivyo, akakirikwamba Hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge ni nzito na hawezi kuitoleauamuzi yeye peke yake, hivyo akawaomba Wajumbe wa Kamati ya Uongoziwakutane muda huo kwa ajili ya kujadili jambo hilo​
5.
Mheshimiwa Spika,​
Baada ya Kipindi cha Maswali kumalizika, Naibu Spika alitoa taarifa ya kikaocha dharura cha Kamati ya Uongozi, ambapo pamoja na mambo menginealisema:​
“Kamati ya uongozi imepima Hoja iliyotolewa na Mheshimiwa KabweZitto na kuiona ni Hoja ambayo inahitaji kupata fursa ya kusikilizwana Bunge. Na kwa maana hiyo sasa namuomba Mheshimiwa KabweZuberi Zitto achukue fursa hii kutuweka sawa anasema nini kuhusujambo hili sasa...”​
6
5​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011, Ukurasa wa 5.
6​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011, Ukurasa wa 14 - 15.
5​
Mhe. Kabwe Zitto, (Mb.) alitoa maelezo kufafanua Hoja yake na baadayeiliungwa mkono na Wabunge wengi. Hoja hii ilichangiwa na Mhe. ChristopherOle-Sendeka, (Mb.) na Mhe. Zainab Matitu Vullu, (Mb.). Wakati akichangiaHoja hii Mhe. Ole-Sendeka, (Mb.) alitumia fursa hiyo pia kutoa Hoja yakuundwa kwa Kamati Teule ambapo pamoja na mambo mengine alisema:​
“... Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Bunge hili liniunge mkono kwakutoa Hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 117 fasili ya (1), (2) mpaka ya(4) ambayo inaweka masharti ya utaratibu wa kuundwa kwa KamatiTeule na hii itasaidia sana kuitendea haki Hoja hii na kulinda hadhi yaBunge lako Tukufu na ndiyo maana nimesimama hapa kutoa Hoja.Naomba kutoa Hoja na naomba mniunge mkono WaheshimiwaWabunge​
7
Hoja hii iliungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wengi na katikakuhitimisha, Naibu Spika akasema: -​
“... katika kujadili Hoja hii ambayo imeibuliwa na Mheshimiwa ZittoKabwe, sasa Mheshimiwa Ole-Sendeka ameiboresha kwa kutoa hoja yakuundwa Tume Teule [Kamati Teule] ambayo Waheshimiwa Wabungemmeiunga mkono kwa wingi sana kwa kutumia Kanuni ya 117 ambayoinasema “…Kamati Teule inaweza kuundwa na Bunge kwa madhumunimaalum kwa hoja mahsusi itakayotolewa na kuafikiwa”. Hoja hiiimetolewa na imeafikiwa na kwa jinsi hiyo mimi ninakubaliana najambo hili. Kwa jinsi hiyo kufuatana na Kanuni hii ya 117 Bunge hililitaunda Tume Teule [Kamati Teule] kwa ajili ya kulichunguza jambohili...”​
8
7​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011.
8​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011, Ukurasa wa 14 – 17.
6​
Mheshimiwa Spika,​
Wakati hatua hii ikifikiwa, Mhe. Nimrod Mkono, (Mb.) aliomba Mwongozo waSpika akitumia Kanuni ya 68 na kurejea Ibara ya 15(6)​
[13(6)] ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayohusu usawa mbele yaSheria. Katika rejea hii Mhe. Nimrod Mkono, (Mb.) alitaka kujua ikiwa Bungehalikiuki Katiba kwa kumhukumu Ndugu David Jairo bila kumpa nafasi yakujitetea. Naibu Spika, alitoa ufafanuzi kwamba mpaka wakati ule badohakukuwa na hukumu yoyote na kwamba kuundwa kwa Kamati Teule nimojawapo ya hatua muafaka za kutenda haki kwa kuwa Kamati Teule itakuwana madaraka kamili na uhuru wa kuita watu mbele yake na kuwahoji akiwemomtuhumiwa anayetajwa, hivyo itakuwa ni jambo linalofaa ikiwa Ndugu DavidKitundu Jairo atatumia fursa hiyo kujibu hoja ama kuuliza maswali na kutoautetezi9.
1.3 Hadidu za Rejea, Wajumbe wa Kamati Teule na Muda wa KaziMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kwa Azimio la Bunge la tarehe 24 Agosti,2011 ilipewa Hadidu za Rejea Tano kama ifuatavyo: -(a) Kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili yakukamilisha uwasilishwaji wa Hotuba za Bajeti za Wizara Bungeni.​
•​
Uhalali wa utaratibu huo Kisheria/Kikanuni.
•​
Iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika Bajeti husika.
•​
Matumizi halisi ya fedha zinazokusanywa.(b) Kupitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalikuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha Taasisi zilizo chini ya
9​
Hansard ya tarehe 24 Agosti, 2011, Ukurasa wa 18.
7​
Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizarahiyo Bungeni.(c) Kuchunguza Mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa Bungeni nataratibu za kuliarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa Hoja hizo.​
•​
Usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozikwa suala la Ndugu David Kitundu Jairo, Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini.
•​
Kubaini kama utaratibu huo umeathiri dhana ya haki namadaraka ya Bunge.(d) Kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi ya Makatibu Wakuukatika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua.
(e)​
Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na masuala haya.Kamati Teule iliundwa na Wajumbe watano kama ifuatavyo: -(i) Mhe. Eng. Ramo Matala Makani, (Mb.)(ii) Mhe. Martha Jachi Umbulla, (Mb.)(iii) Mhe. Gosbert Begumisa Blandes, (Mb.)(iv) Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, (Mb.)(v) Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa, (Mb.)Mara baada ya Kamati kuundwa, Wajumbe walikutana kumchagua Mwenyekitiwa Kamati kwa mujibu wa Kanuni ya 117(4) na hivyo Mhe. Eng. Ramo MatalaMakani, (Mb.) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti. Aidha, kwa kuona umuhimu wakuwepo kwa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe walimchagua Mhe. Martha JachiUmbulla, (Mb.) kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati. Kamati Teule ilianza kazirasmi tarehe 5 Septemba, 2011 huko Dar es Salaam.
8​
Kamati Teule ilikuwa na Wajumbe wa Sekretarieti wafuatao: -(i) Ndugu Nenelwa Mwihambi-Wankanga(ii) Ndugu Lukago Alphonce Madulu(iii) Ndugu Asia Paul Minja(iv) Ndugu Mswige Dickson Bisile​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilipewa muda usiozidi Wiki Nane kukamilisha kazi hii na piailitakiwa kuwasilisha Taarifa yake Bungeni wakati wa Mkutano wa Tano waBunge kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 119 ya Kanuni za Bunge, Toleo la2007.​
1.4 Njia Zilizotumika katika Kukamilisha Kazi​
Kamati Teule imezifanyia kazi Hadidu za Rejea Tano ilizopewa kwa kufanyayafuatayo: -(a) Kusoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Sheriambalimbali na kuzichambua kwa kuziwianisha na Hadidu za Rejea. Sheriazilizohusika ni pamoja na: -(i) Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 na Kanuni zake za mwaka2003;(ii) Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009, Toleo la Tatu;(iii) Sheria ya Fedha za Umma, 2001 na Kanuni zake za mwaka2001;(iv) Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008 na Kanuni zake za mwaka2009;(v) Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, 1988;(vi) Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007;(vii)​
The Government Loans, Grants and Guarantees Act, 1974,(viii) Waraka wa Katibu Mkuu - Hazina Namba 3 wa Machi, 2011;(ix) Waraka wa Utumishi wa Serikali Namba 2 wa Mwaka 2010;
9​
(x) Kanuni za Fedha na Mipango Mikakati ya Taasisi nnezilizochangishwa fedha, n.k(b) Kupitia maoni kwa njia ya maandishi kutoka Mabunge ya Australia (​
Houseof Representatives) na Uingereza (House of Commons).(c) Kupitia maoni kwa njia ya maandishi kutoka Wizara 26 za Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania.(d) Kupitia Taarifa zilizotolewa kwa Vyombo vya Habari kwa maandishikuhusiana na suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Ndugu David Kitundu Jairo na kusikiliza sehemu ya Taarifa hizo kamazilivyotolewa kwenye vituo mbalimbali vya luninga.(e) Kusoma na Kuchambua Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.(f) Kufanya mahojiano na watu mbalimbali kama ifuatavyo: -(i) Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, (Mb.) Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania.(ii) Katibu Mkuu Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.(iii) Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Pius Msekwa.(iv) Mhe. William Ngeleja, (Mb.), Waziri wa Nishati na Madini.(v) Mhe. William V. Lukuvi, (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya WaziriMkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe. Mustafa Haidi Mkulo,(Mb.), Waziri wa Fedha, Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, (Mb.),Waziri wa Ujenzi, Mhe. Dr. Cyril Agust Chami, (Mb.), Waziri waViwanda na Biashara na Mhe. Ezekiel Magolyo Maige, (Mb.),Waziri wa Maliasili na Utalii.
10​
(vi) Waheshimiwa Wabunge 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.(vii) “​
Senior citizens” wakiwemo Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba,Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe. Dr. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu naMhe.Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais naWaziri Mkuu Mstaafu.(viii) Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwemo KatibuMkuu, Ndugu David Kitundu Jairo, Kaimu Katibu Mkuu,Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Mkurugenzi wa Utawala naRasilimali Watu, Mkaguzi Mkuu wa Ndani na Mhasibu Mkuu.(ix) Watendaji na Taasisi saba (7) zilizo chini ya Wizara ya Nishatina Madini, wakiwemo Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi husika,Watendaji Wakuu na Wakuu wa Idara za Sera na Mipango,Rasilimali Watu, Ukaguzi wa Ndani na Fedha.(x) Watendaji wa Wizara mbalimbali katika ngazi tofauti hususanMakatibu Wakuu, Wakurugenzi katika maeneo ya Sera naMipango, Rasilimali Watu, Ukaguzi wa Ndani na Fedha.(xi) Watendaji wa Taasisi tisa (9) zilizo chini ya Wizara za Fedha,Ujenzi, Maji, Viwanda na Biashara na Maliasili na Utalii katikamaeneo ya Sera na Mipango, Rasilimali Watu, Ukaguzi waNdani na Fedha.(xii) Wakongwe wa Siasa za Tanzania na Watu waliobobea katikamaeneo mbalimbali yakiwemo ya Katiba, Sheria, Bunge,Serikali, Mahakama, Utumishi wa Umma, Utawala Bora,Uongozi na Rasilimali Watu n.k. wakiwemo Makatibu wa BungeWastaafu na Makatibu Wakuu Wastaafu.
11​
(xiii) Wanazuoni waliobobea katika taaluma za Katiba, Sheria, Elimuya Sayansi ya Siasa na Utawala na Utumishi wa Umma kutokaChuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Mzumbe.(xiv) Wawakilishi wa Asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo​
PolicyForum, TGNP na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.(xv) Wawakilishi wa Jukwaa la Wahariri.Orodha kamili ya waliohojiwa na waliopata nafasi ya kuishauri Kamati Teule inajumla ya watu 146 na imeambatishwa kama Kiambatisho II kwenye Taarifa hii.
12​
2.0 UTARATIBU ULIOBAINIKA WA KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUKAMILISHAUWASILISHWAJI WA HOTUBA ZA BAJETI ZA WIZARA BUNGENIMheshimiwa Spika,​
Hadidu ya Rejea ya Kwanza iliitaka Kamati Teule kuchunguza utaratibuuliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilisha uwasilishaji wa Hotubaza Bajeti za Wizara Bungeni kwa kuchunguza mambo matatu yafuatayo: -(a) Uhalali wa utaratibu huo Kisheria/Kikanuni.(b) Iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika Bajeti husika.(c) Matumizi halisi ya fedha zinazokusanywa.Ili kukamilisha jukumu hili, Kamati Teule ilifanya yafuatayo:-(a) Kupitia Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Nyaraka mbalimbali.(b) Mahojiano na Katibu Mkuu Kiongozi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Watendaji wa Wizara naTaasisi mbalimbali, Wanazuoni, Wabunge, Viongozi Wastaafu, Jukwaa laWahariri na wawakilishi wa baadhi ya asasi za kiraia.(c) Kukusanya taarifa mbalimbali kwa njia ya Dodoso kutoka Wizara zote.(d) Kupitia Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu jambo hili.​
13​
(e)​
2.1 Uchunguzi kuhusu Utaratibu Uliobainika wa Kukusanya Fedha kwa ajili yaKukamilisha Uwasilishwaji wa Hotuba za Bajeti za Wizara BungeniMheshimiwa Spika,​
Utaratibu uliokuwa ukichunguzwa na Kamati Teule ni ule uliotumiwa na Wizaraya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwenye Taasisi zilizo chini yake kwa ajiliya kuwezesha maandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti yake Bungeni.Aidha, ili kukidhi haja ya Hadidu ya Rejea hii, Kamati ilifanya uchunguzi katikaWizara zote nchini ili kubaini kama utaratibu huo pia upo katika Wizara nyinginena vile vile kuweza kubaini kama ni wa kawaida, na kwa kiasi gani.Uchunguzi wa Kamati Teule ulibaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini ina jumlaya Taasisi na Mashirika saba ambayo ni:​
Tanzania Petroleum DevelopmentCorporation (TPDC), Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO),
Rural Energy Agency​
(REA), State Mining Corporation (STAMICO), GeologicalSurvey of Tanzania (GST), Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) na MineralResources Institute (MRI).Kati ya Taasisi hizo ni REA, TPDC na TANESCO tu ndizo ziliombwa michango kwakuzingatia uwezo wao wa kifedha. Taasisi ya EWURA ambayo kiutawala iko chiniya Wizara ya Maji iliombwa mchango kwa sababu baadhi ya majukumu yakekatika udhibiti wa nishati, yapo chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Taasisi nnezinazobakia hazikuombwa kuchangia kwa maelezo kwamba hazina uwezo wakifedha.
Mheshimiwa Spika,​
Tarehe 21 Juni, 2011 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliwaandikiabarua Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake kuchangiagharama kwa ajili ya kukamilisha maandalizi na uwasilishwaji wa Hotuba yaBajeti ya Wizara ya Mwaka 2011/12 Bungeni Dodoma. Kila barua aliyoandikiwaMtendaji Mkuu wa Taasisi ilielekeza kwamba fedha hizo zitumwe​
GeologicalSurvey of Tanzania (GST) kwenye Akaunti Na. 5051000068 NMB Tawi la Dodoma
14​
na kuwa baada ya kutuma fedha hizo Wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DPkwa uratibu.​
(Tazama Kiambatisho III)
Taasisi zilizoandikiwa barua kuombwa kuchangia, viwango walivyoombwa namwitikio wa maombi ni kama inavyoonekana katika​
Jedwali Na. 1 na Jedwali
Na.​
2 kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1: Taasisi zilizoandikiwa barua kuombwa kuchangiaNa. TaasisiKiasiKilichoombwa(Tshs)​
1. Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO)40,000,000.002. Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA)40,000,000.003. Wakala wa Umeme Vijijini (REA) 50,000,000.004. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC)50,000,000.00​
JUMLA 180,000,000.00Jedwali Na. 2: Mwitikio wa maombi ya Michango kutoka katika TaasisiNa. TaasisiKiasiKilichoombwa(Tshs)​
1. Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO)40,000,000.002. Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA)*---3. Wakala wa Umeme Vijijini (REA) 50,000,000.004. Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC)50,000,000.00​
JUMLA 140,000,000.00​
*----EWURA haikuchangia kiasi cha Sh.40,000,000.00 kama ilivyoombwa, badala yakeiligharamia chakula cha mchana kwa siku tatu (Sh.3,656,000.00) na tafrija ya tarehe18 Julai, 2011 (Sh.6,141,600.00) siku ambayo bajeti ya Wizara ilitarajiwa kupitishwa.Kwa maana hiyo EWURA ilichangia jumla ya Sh.9,797,600.00 (Tazama Kiambatisho IV).​
15​
Mheshimiwa Spika,​
Fedha zilizokusanywa toka Idara za Wizara na jumla ya fedha zote zilizoingizwakatika Akaunti ya GST ni kama inavyoonekana katika Jedwali 3 na Jedwali 4kama ifuatavyo: -​
Jedwali Na. 3: Fedha zilizokusanywa toka Idara za WizaraNa. Idara Kiasi Kilichokusanywa(Tshs)​
1. Uhasibu 150,720,000.002. Sera na Mipango 278,081,500.00​
JUMLA 428,801,500.00Jedwali Na. 4: Jumla ya Fedha zote Zilizoingizwa katika Akaunti ya GST​
Tarehe Stakabadhi Mlipaji Kiasi (Sh.) Madhumuni​
14 Juni, 2011 02427 Wizara ya Nishati na Madini(Idara ya Sera na Mipango)50,143,500 Shughuli za Bunge24 Juni, 2011 02429 Wizara ya Nishati na Madini(Idara ya Uhasibu)150,720,000* Kikao chakazi/Semina25 Juni, 2011 02428 Wizara ya Nishati na Madini (OC) 171,542,000 Shughuli za Bajeti25 Juni, 2011 02428 Wizara ya Nishati na Madini(Idara ya Sera na Mipango)56,396,000 Shughuli za Bajeti04 Julai, 2011 02432 TPDC 50,000,000 Shughuli za Bunge13 Julai, 2011 02431 REA 50,000,000 Shughuli za Bunge18 Julai, 2011 02430 TANESCO 40,000,000 Shughuli za Bunge​
JUMLA 568,801,500​
* … Jumla ya Sh.150,720,000.00 ziliingizwa kwenye Akaunti ya GST kwa ajili ya gharama zavikao vya kazi na semina. Kwa hiyo, kiasi cha Sh.418,081,500.00 ndicho kilikuwa mahsusikwa ajili ya shughuli za uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Bungeni.​
16​
Mheshimiwa Spika,​
Ili kuweza kuuchunguza vema uwepo na ukawaida wa utaratibu huu ndani yaWizara za Serikali, Kamati Teule ilifanya mahojiano na watu mbalimbali nakutuma Dodoso kwa Makatibu Wakuu wa Wizara 25.(a)​
Mahojiano
(i)​
Ndugu Ludovick Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali
Kamati Teule ilizingatia ukweli kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali ndiye Mwangalizi Mkuu wa nidhamu ya matumizi yafedha za umma Serikalini kwa niaba ya Bunge. Hivyo ilikuwa nimuhimu sana kupata kauli yake kuhusu utaratibu huu kamaumebainika katika Kaguzi zake katika vipindi vilivyopita. Majibu yakeyalikuwa ni kwamba utaratibu huu siyo wa kawaida. Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali alisema: -​
“…Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema ni kwambanime-instruct ukaguzi wa wizara zote za mwaka huu, tu-diginto this issue ili tuweze ku-establish extent ya tatizolilivyo kiserikali in totality…lakini the other reason alsoambayo iko kwenye ripoti, ile kwamba most of theseinstitutions they don’t budget for contribution yakuchangia, unless institutions ziwe zinajua from the timego, kwamba they have an obligation ya kuchangia katikaku-process Bajeti ya Wizara ili wa- make that provision”.​
10
10​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
17​
(ii)​
Mhe. Mustafa H. Mkulo, (Mb.), Waziri wa Fedha
Lengo la Kamati Teule kufanya mahojiano na Waziri wa Fedha kuhusujambo hili ilikuwa ni kupata kauli yake kama amewahi kuuonautaratibu huu katika usimamizi wake wa matumizi ya fedha za ummaSerikalini. Waziri wa Fedha alitamka: -​
“…the whole transaction, the whole issue, haikuwa issueambayo ni proper within the accounting system, within themonetary systems za kiserikali, ilikuwa nje ya utaratibuproper wa kiserikali”.​
11
(iii)​
Mhe. John M. Cheyo (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaHesabu za Serikali
Lengo la Kamati Teule kufanya mahojiano na Mwenyekiti wa Kamatiya Bunge ya Hesabu za Serikali ilikuwa ni kupata kauli yake kamaKamati yake imewahi kukutana na matumizi ya aina hii kwenyetaarifa za hesabu za Wizara, naye alisema:-​
“…katika miaka yote mimi nimekuwa chair wa PublicAccounts Committee (PAC), sijaona hata siku mojamiscellaneous income, because hii exercise ya kwendaBungeni ni ya kila mwaka, kila mwaka Wizara lazima iendeBungeni kupata idhini ya kutumia fedha, that means budgetsession; sijaona hata wakati mmoja pamekuwa namiscellaneous income ambayo ni fedha hiyo. Kwa hiyo,question number one becomes; wewe unayekusanya hizofedha unazipeleka wapi? Kama unatumia Mfuko Mwinginebasi ndiyo kusema kuna non-disclosure ya funds ambazozinakuwa collected na Serikali, kitu ambacho pia kihasibusiyo sawasawa.”​
12
11​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 6 Oktoba, 2011
12​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 4 Oktoba, 2011.
18​
(iv)​
Ndugu Philemon Luhanjo, Katibu Mkuu Kiongozi
Kamati Teule iliona ni vema kufanya mahojiano na Katibu MkuuKiongozi ambaye ni Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Barazala Mawaziri. Kwa kuwa katika Mkutano wake na Vyombo vya Habarialitoa kauli kuwa “huu ni utaratibu wa kawaida”, alipoulizwa swalikwamba utaratibu aliousema kuwa ni wa kawaida unatumika katikaWizara ngapi, alisema:-​
“… siwezi kusema Wizara ngapi, hiyo siyo rahisi sana, kwasababu kwanza kwanini uchangishe, issue inaanzia hapo,kwa nini uchangishe… utaratibu huu siyo formalized as such,ni mpango unaofanywa kiutawala kwa maana shughuli ipombele yako huna resources, lakini unazo Taasisi unazowezakuzi-pull together mkaweza kushirikisha… kwa hiyo mtuukiwa na shida unakwenda Hazina kuomba kwambanimetindikiwa na fedha nipeni fedha.”​
13
(v)​
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali
Baadhi ya Makatibu Wakuu waliohojiwa ni kutoka katika Wizara zaUjenzi, Maji, Viwanda na Biashara, Nishati na Madini na Fedha (NaibuKatibu Mkuu). Lengo la Kamati kuwahoji Makatibu hawa ilikuwa nikujiridhisha na uwepo wa utaratibu huu pamoja na ukawaida wake.Isipokuwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, MakatibuWakuu wa Wizara zilizotajwa walisema kuwa utaratibu huu haupokatika Wizara zao.​
13​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
19​
(b)​
Barua/DodosoMheshimiwa Spika,
Kamati Teule ilituma Barua/Dodoso kwa Makatibu Wakuu wa Wizara 25 zaSerikali ili kuweza kubaini kama Wizara hizo zinaendesha uchangishajikatika Taasisi zao kwa ajili ya kuweza kuwasilisha Hotuba za Bajeti zaoBungeni. Makatibu Wakuu wa Wizara zote 25 zilizoandikiwa barua walisemakuwa utaratibu wa kuzichangisha Taasisi zilizo chini yao kwa ajili ya kupatafedha za kuisaidia Wizara kuwasilisha Hotuba za Bajeti Bungeni haupo.Makatibu Wakuu hao walijibu kuwa Bajeti zao zina kasma maalum kwa ajiliya uwasilishaji wa Hotuba za Bajeti za Wizara zao Bungeni. Na kwambaendapo limetokea tatizo la kasma kutokuwa na fedha kwa ajili ya shughuliiliyokusudiwa Wizara hufanya uhamisho wa fedha (​
reallocation) katikavifungu vyake kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Fedha za Umma.
(Tazama Kiambatisho V)Mheshimiwa Spika,​
Kwa kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara 25 zilizohojiwa kwa njia ya mazungumzona Dodoso walikataa kuwa na utaratibu wa kuchangisha fedha kwenye Taasisizilizo chini ya Wizara zao kwa ajili ya kuwezesha uwasilishaji wa Hotuba zaBajeti zao Bungeni, na kwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu zaSerikali alikataa kuwahi kuona matumizi ya namna hii kwenye Taarifa za kilaMwaka za Hesabu zinazokaguliwa za Wizara mbalimbali, na kwa kuwa Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pia alikataa kuwahi kuliona jambo hilina kuahidi kuwa ataanzisha Ukaguzi Maalum kwenye Wizara kwa ajili ya jambohili tu kwani katika Ukaguzi wa kawaida halijabainika kuwepo, hivyo basiKamati Teule imejiridhisha kuwa huu siyo utaratibu wa kawaida.​
20​
2.2 Uchunguzi kuhusu uhalali wa utaratibu wa uchangishaji Kisheria na KikanuniMheshimiwa Spika,​
Ili kuweza kuchunguza uhalali wa utaratibu huu Kisheria na Kikanuni, KamatiTeule ilirejea kwa kina Sheria ya Fedha za Umma, 2001 pamoja na Marekebishoyake ya Mwaka, 2004 na Kanuni za Fedha za Umma, 2004. Miongozo mingineiliyorejewa kwa kina ni Mipango Kazi ya Taasisi zilizochangia na Mpango Kazi waWizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2010/2011. Lakini pia,Kamati ilifanya mahojiano na wadau mbalimbali wakiwemo Waziri wa Fedha,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Mhe. Cleopa D. Msuya (Makamu waKwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu).​
2.2.1 Msingi wa KikatibaMheshimiwa Spika,​
Ibara ya 136 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inatamkawazi kwamba, hakuna fedha itakayotolewa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali, isipokuwa tu fedha hizo ziwe ni kwa ajili ya matumizi ambayoyameidhinishwa na Bunge. Hii pia ni kwa mujibu wa Ibara ya 137 ambayoinahusu utaratibu wa Serikali kuandaa Makadirio ya Bajeti ya Mwaka na namnaMakadirio hayo yanavyopaswa kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupata idhini yaBunge.Uchunguzi wa Kamati Teule ulibaini kuwa ni kweli fedha zilizochangishwaziliidhinishwa na Bunge katika Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha wa2010/2011 lakini siyo kwa matumizi ya kuichangia Wizara ili iweze kuwasilishaHotuba ya Bajeti yake Bungeni bali ni kwa ajili ya utekelezaji wa mipango yaTaasisi zenyewe kama Taarifa hii itakavyoendelea kufafanua.​
21​
2.2.2 Kanuni ya 4(4) ya Kanuni za Fedha za Umma, 2001Mheshimiwa Spika,​
Mahojiano kati ya Kamati Teule na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madiniyaliifanya Kamati kuelewa kwamba Wizara ya Nishati na Madini ilifikia uamuziwa kuomba michango kwenye Taasisi zake kwa sababu Kifungu wanachokitumiakwa shughuli za Bajeti yaani​
Project Coordination and Monitoring kilikuwakimebakiwa na Sh.35,500,000.00 tu wakati makisio ya gharama za kukamilishamchakato wa maandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ilikuwani Sh.207,042,000.00 (Tazama Kiambatisho VI) na kwamba Fedha za OtherCharges (OC) kwa robo ya nne ya mwaka zilikuwa hazijapatikana hadi kufikiatarehe 21 Juni, 2011 hivyo kuleta hofu ya kukamilika kwa zoezi zima lauwasilishaji wa Bajeti ya Wizara Bungeni.
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule haikubaliani na sababu zilizotolewa na Wizara kwa kuwa endapokunatokea mahitaji na kasma inayohusika haina fedha ama hakuna kasmautaratibu unaopaswa kufuatwa umeainishwa katika Kanuni ya 4(4) kamaifuatavyo:-​
“…​
The Appropriation Act shall allocate funds by vote and anyvariation in such allocation shall be approved by the NationalAssembly in a further Appropriation Act(s). The division of the fundsby sub-Head and item shall be controlled by the Minister under theauthority of Section 5(1) (b) of the Public Finance Act and anyvariation in the amount allocated to a sub-head or item by suchdivision shall have a prior approval of the Minister.”
Mheshimiwa Spika,​
Uchunguzi wa Kamati Teule ulibaini kwamba Kanuni hii haikuzingatiwa, kwasababu mtiririko wa maelezo ya Wizara kuhusu uchangishaji ulitakiwa kuishiakatika mabadiliko ya vifungu vya Bajeti ya Wizara yenyewe na mabadiliko hayo​
22​
yalipaswa kupata idhini ya Waziri wa Fedha badala ya kuamua kuzichangishaTaasisi. Ndiyo maana katika mahojiano Waziri wa Fedha alisema:-​
“…kama Wizara ina shortfall, kuna utaratibu maalum wa AfisaMasuuli kumwandikia Mlipaji Mkuu wa Serikali na kuelezea tatizo lahiyo shortfall limetokea namna gani, kwa nini halikuwepo kwenyeBajeti na umuhimu wa hicho ambacho kina shortfall na kwa niniwanaomba Wizara iongezewe fedha… Waziri wa Fedha anatoa kibalikwamba, okay, sawa, hebu pelekeni hizo fedha huko kunakotakiwa…kwa hiyo, hakuna popote panaposema kwamba kama una shortfallmahali fulani unaweza kwenda kuwaambia watu fulani wakuchangieili uweze kufidia shortfall, bado nasisitiza kwamba the whole thingwas not proper… ”.​
14
Mheshimiwa Spika,​
Kwa maelezo haya ya Kanuni ya 4(4) ambayo yameungwa mkono na maelezoya Waziri Mwenye dhamana ya Fedha, Kamati Teule imejiridhisha zaidi kuwautaratibu huu siyo halali na wala siyo wa kawaida.Aidha, sababu zilizoifanya Wizara kuchangisha fedha haziwezi kutiliwa maananikwa sababu hadi kufikia tarehe 25 Juni, 2011 Wizara ya Nishati na Madiniilikwishakupata mahitaji yote ya fedha za uwasilishaji wa Bajeti baada yakupokea Sh.171,542,000.00 za​
Other Charges (OC) kutoka Hazina. Hivyo Wizarahaikuwa na sababu yoyote ya kuendelea kukusanya michango ya fedha tokakwenye Taasisi zake. Ukweli wa maelezo haya ulithibitishwa na Mkurugenzi waSera na Mipango wa Wizara ya Nishati na Madini ambaye ndiye mratibu wa kaziza Bajeti. Katika mahojiano na Kamati Teule alipoulizwa endapo kulikuwa nahaja ya kuendelea kukusanya michango kutoka Taasisi hata baada ya kupokeafedha za OC Sh.171,542,000.00 alijibu kwa mkazo kuwa “ni kweli hakunahaja”15
14​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 6 Oktoba, 2011.
15​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 11 Oktoba, 2011.
23​
2.2.3 Kanuni ya 53(1) na (2) ya Kanuni ya Fedha za Umma, 2001Mheshimiwa Spika,​
Kimantiki, Kanuni hii inaweka utaratibu kwamba fedha zinapokuwazimeidhinishwa na Bunge kwa ajili ya matumizi ndani ya Taasisi ya umma,inapaswa fedha hizo zionekane kwenye​
appropriation accounts za Taasisi hiyokwa namna zilivyoingia na kutumika katika mwaka husika. Kanuni hii inatamkakuwa:
“53(1) The Government account shall be kept on a cash basis in orderthat the amount of cash spent on a particular service becompared with the amount authorized by the NationalAssembly.(2) “…for purposes of sub-regulation (1) all actual receipts andpayments made during the financial year shall be recorded inthe Appropriation accounts.”​
Uchunguzi wa Kamati Teule ulibaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini ndiyoiliyochangisha fedha hizi na kuzitumia lakini mapato na matumizi ya fedha hizihayatapatikana kwenye vitabu vya Hesabu vya Wizara. Mmoja wa wataalam wamasuala ya fedha Serikalini alitoa ufafanuzi ufuatao kuhusu utaratibu huu: -​
“… System ya payment ambayo ni ya Wizara ya Fedha inatumikakatika Wizara zote na inategemea Bajeti ambayo imepitishwa naBunge. Bunge likisema kwamba tumepitisha milioni moja kwa ajili yasafari there is no way ukatumia Milioni moja na nusu. Kwa sababuBajeti ile inakuwa tayari imefungwa kwenye system, kwa maanahiyo, ili uweze kutumia milioni moja na nusu ni lazima Wizara yafedha wapanue ceiling na Wizara ya fedha kupanua ceiling ni mpakakibali cha Bunge …”​
16
16​
Hansard Kamati Teule, tarehe 29 Septemba, 2011.
24​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa utaratibu huu wa Wizara kuchangisha Taasisi na kuelekeza fedha hizokuingia kwenye Akaunti ya GST ni dhahiri kuwa katika Hesabu za Mwaka, Bungehalitaweza kuona wala kuhoji ongezeko la sh. 140,000,000.00 na matumizi yafedha hizo katika Fungu 58 la Wizara ya Nishati na Madini. Kwa maana hiyoutaratibu huu siyo halali kwa sababu unachochea matumizi ya fedha za ummakinyemela bila ya usimamizi wa Bunge.​
2.2.4 Waraka Na. 3 wa Mwaka 2011 wa Katibu Mkuu HAZINA na MlipajiMkuu wa SerikaliMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilipitia na kuchambua​
Waraka Na.3 wa Mwaka 2011 wa KatibuMkuu - HAZINA na Mlipaji Mkuu wa Serikali kwa Makatibu Wakuu wa Wizarana Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma kutoa Mikopo kwa Wizara.(Tazama Kiambatisho VII). Msingi wa Waraka huu ni Sheria ya The GovernmentLoans, Guarantees and Grants Act, 1974 na unaweka masharti kwa Wizarakuhusu kupata mikopo, dhamana, na misaada kutoka kwenye Taasisi chini yaWizara. Katika utafiti wake Kamati Teule imebaini kuwepo kwa mitizamo miwilitofauti kuhusu tafsiri ya Waraka huu kama ifuatavyo:-(a) Michango siyo sehemu ya mikopo, ruzuku au dhamana
Mawazo ya wanaosema kwamba michango si sehemu ya mikopo, ruzukuau dhamana kulingana na Waraka yanajengwa katika Hoja kwambakilichoombwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa Taasisi hakikuwamkopo, ruzuku, wala dhamana bali ni michango.(b)​
Michango ni sehemu ya mikopo, ruzuku na dhamana
Mawazo ya wanaosema kwamba michango ni sehemu ya mikopo, ruzukuau dhamana kulingana na Waraka yanajengwa katika Hoja kwambakilichoombwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa Taasisi kilikuwa ni​
25​
ruzuku kwa sababu ruzuku ni aina ya msaada. Waziri wa Fedha,Mhe. Mustafa Mkulo, (Mb.) alisisitiza hili kwa kusema:-​
“… nadhani tulichozoea ni kwamba msaada lazima uweunatoka World Bank lakini msaada unaweza kutoka kwa Mkulo,naweza kutoa shilingi milioni moja zangu za mwezi natunafanya pale na tunasema Wabunge wote changieni. Ule nimsaada kwa hiyo walichokifanya wao kina-fit in kwenye ile yapili, misaada…”​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inasisitiza kwamba uchangishaji uliofanywa na Wizara ya Nishatina Madini ulipaswa kuwa chini ya Masharti ya Waraka huu kutokana nauchambuzi ufuatao: -(i) Kilichoombwa na Wizara siyo mkopo kwa kuwa hapakuwekwamakubaliano ya urejeshaji.(ii) Kilichoombwa na Wizara siyo dhamana kwa kuwa Wizara ilikuwahaidhaminiwi kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungeni.(iii) Kilichoombwa na Wizara ni msaada kwa kuwa haikuwa na fedha zakutosha kukamilisha jukumu lake la kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yakeBungeni, na hapakuwa na makubaliano ya kurejesha fedha mara baadaya matumizi. Ndiyo maana hata zile fedha zilizokuwa zimebakihazikurejeshwa kwa Taasisi zilizochangia kwa sababu zilitoa msaada kwaWizara.(iv) Waraka ulielekezwa kwa Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu waMashirika na Taasisi za Umma Tanzania Bara. Uchunguzi wa KamatiTeule ulibaini kwamba Waraka huu ulipokelewa kwenye Wizara yaNishati na Madini tarehe 15 Machi, 2011 na kutolewa maelekezo yakusambazwa kwenye Mashirika na Taasisi za Wizara hiyo tarehe​
26​
16 Machi, 2011. Maelekezo hayo yalitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini, Ndugu David Kitundu Jairo mwenyewe. Hivyo, KatibuMkuu aliyeendesha uchangishaji huu alikuwa na taarifa za kutoshakuhusu kuwepo kwa Waraka huo.(v) Wizara, Mashirika na Taasisi wanaandaa na kuidhinishiwa Bajeti zao kilaMwaka na inatakiwa Bajeti hiyo izingatiwe. Uchunguzi wa Kamati Teuleulibaini kwamba Taasisi zilizochangishwa hazina Kasma mahsusi kwa ajiliya kuichangia Wizara ili iwasilishe Hotuba ya Bajeti yake Bungeni. Hivyo,kitendo cha Taasisi kutoa fedha zake kuichangia Wizara hakikuzingatiasharti hili.(vi) Wizara huandaa na kupewa Bajeti zake kwa mujibu wa majukumu namalengo yaliyopangwa na kuidhinishwa. Uchunguzi wa Kamati Teuleulibaini kuwa Wizara inayo Kasma mahsusi kwa ajili ya kuwezakuwasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungeni. Hivyo, hili lilikuwa ni jukumula Wizara yenyewe siyo jukumu la Taasisi.(vii) Waraka unasisitiza kwamba: -​
“…Endapo kutatokea mahitaji yatakayolazimu kutumia fedhakutoka katika Mashirika ama Taasisi za umma chini ya Wizarani lazima kupata kibali cha Waziri wa Fedha baada yakushauriwa na Mlipaji Mkuu wa Serikali (PMG) na Msajili waHazina.”​
Hivyo, Wizara hazipaswi kupewa fedha za ziada kupitia Mashirika na Taasisizilizo chini yake. Lakini Wizara ya Nishati na Madini inaonekana ilipata fedha zaziada kutoka kwenye Taasisi zake kupitia uchangishaji huu. Hii ni kinyume namasharti ya Waraka huu.​
27​
Mheshimiwa Spika,​
Ili kujielimisha zaidi, Kamati ililazimika kufanya mahojiano na Waziri wa Fedhaambaye kwa mujibu wa Waraka huu ndiye mtoa kibali. Akitoa maelezo yakembele ya Kamati Teule, Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkulo, (Mb.) alisemakwamba baada ya kuonekana kuna matatizo mengi ya Wizara mbalimbalikuomba fedha kutoka kwenye Taasisi zilizo chini yao, Baraza la Mawazirililijadili suala hili na kuazimia kwamba itafutwe namna ya kudhibiti matumizi,dosari na matatizo, ndipo ikakubalika kwamba Hazina itoe Waraka wa kudhibitimambo haya. Waziri wa Fedha alifafanua zaidi juu ya Waraka huu kwakusema:-​
“…(Katibu Mkuu) hakuutoa yeye kama mtu binafsi, alitoa ule Warakamimi kama Waziri nikiwa na full knowledge na Rais akiwa na fullknowledge kwamba tuweze ku-control matumizi ya ajabu ajabuambayo hayahusiki. Kwa hiyo, kilipokuja kutokea kile ambachokilitokea Bungeni hata sisi Hazina kwa kweli ilitushangaza kwambakuna kitu kama hicho kimetokea.”​
17
Baada ya kukamilisha uchunguzi wake kuhusu jambo hili Kamati Teule ilibainikwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini hakuomba kibali cha Waziriwa Fedha ili kupata ridhaa ya kuchangisha hivyo alikiuka masharti ya Warakahuu.​
(Tazama Kiambatisho VIII)2.3 Uchunguzi Iwapo Taasisi zilizochangia zina Kasma kwa ajili ya Uchangiaji huuMheshimiwa Spika,
Ili kuweza kukamilisha jukumu hili, Kamati Teule ilipitia Mipango Kazi na Bajetiza Taasisi zilizochangia kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011. Nyaraka hizizilibainisha kuwa Taasisi husika (TANESCO, REA, TPDC na EWURA) hazina kasmamahsusi kwa ajili ya kuichangia Wizara iweze kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yakeBungeni. Uchambuzi zaidi ulikuwa kama ifuatavyo:​
17​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 6 Oktoba, 2011.
28​
2.3.1 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)​
Taasisi hii ilichangia kiasi cha sh. 50,000,000.00 kutoka kasma ya mapato ya Gesiya Serikali (​
Government Gas Revenue). Kasma hii, kama inavyojieleza yenyeweni ya mapato ya gesi ya Serikali na siyo kasma ya kuchangia Wizara kuwasilishaHotuba ya Bajeti.Kamati ilipitia Kanuni za Fedha za TPDC, 2008 zikisomwa pamoja na Mwongozowa Ukomo wa Mamlaka ya kuidhinisha malipo mbalimbali (Powers of Authority).Nyaraka hizi zinaonyesha kuwa katika matumizi yote yanayohusiana na mitaji,miradi na mapato mengineyo, mamlaka ya Mtendaji Mkuu hayana ukomo kwamatumizi ambayo yamepitishwa na Bodi. Hata hivyo, matumizi yote ambayohayajapitishwa katika Bajeti yatafanyika kwa idhini ya Bodi tu.
Mheshimiwa Spika,​
Katika mahojiano na Watendaji wa TPDC, Kamati ilibaini kuwa TPDC ililazimikakuchanga fedha hizo bila idhini ya Bodi kama inavyotakiwa na Kanuni zake zaFedha na​
Powers of Authority ili kutii maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini. Kwamba TPDC walilazimika kuchanga kinyume na utaratibukwa kuhofia kuitwa wakaidi kutokana na uzoefu waliokwishaupata siku zanyuma.18
Hali hii ilijidhihirisha zaidi kupitia maombi ya Menejimenti ya TPDC kwa Bodi(​
Board Paper) yaliyoandaliwa ili kupata idhini baada ya matumizi (Retrospectiveapproval) kama ifuatavyo: -
“Management thought that it did not have any choice in the mattersince in its view, failure to make the contribution might cause untoldconsequences. However, since the Corporation has no money, andthis item not having budgeted for, Management saw it fit to pay themoney requested out of Government Gas Revenue.​
” (TazamaKiambatisho IX)
18​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 14 Septemba, 2011.
29​
2.3.2 Mamlaka ya Nishati ya Umeme Vijijini (REA)Mheshimiwa Spika,​
Kiasi kilichochangwa na taasisi hii cha Sh.50,000,000.00 kilitoka kwenye kasmaya kuandaa Mpango Kazi na Bajeti ya REA (​
Preparation of REA Business Plan andBudget). Kasma hii ilikuwa na Sh.37,500,000.0019, hata hivyo, tarehe 15 Aprili,2011, kasma hiyo ilikuwa na bakaa ya Sh.7,792,425.00 tu, lakini ikaongezewaSh.75,177,575.00 kwa utaratibu wa kuhamisha fedha (reallocation) hivyokufanya kasma ya kuandaa Mpango Kazi na Bajeti ya REA kuwa na jumla yaSh.82,970,000.0020. Hatua ya kuchangia Sh.50,000,000.00 na wakati katikakipindi kifupi kilichotangulia REA ilishachangia Sh.22,000,000.00 hivyo kufanyajumla ya michango kwa Wizara kuwa Sh.72,000,000.00 kutoka katika kasmailiyotengewa Sh.82,970,000.00 inaonyesha wazi kuwa kasma hii isingewezakutekeleza jukumu lililokusudiwa kwani ilibaki na Sh.10,970,000.00 tu ambayoni sawa na asilimia 13 ya kasma yote.Kamati Teule ilipitia Mwongozo wa REA wa matumizi ya fedha ambaoumezingatia Sheria na Kanuni mbalimbali zikiwemo Sheria ya Rural Energy Act,2005, Sheria ya Fedha za Umma na Kanuni zake na Sheria ya Manunuzi ya Ummana Kanuni zake na kubaini kuwa Kifungu cha 16.4 cha Mwongozo wa Fedha naMatumizi (Financial Accounting Manual) kinachohusu unplanned activities orexpenditure kinaweza kutumika vibaya kwa kuidhinisha matumizi yasiyo na tija.Kifungu hicho kinasomeka: -
“No activity may be carried out or expenditure be incurred withoutits prior inclusion in the annual plan and budget, except approval hasbeen obtained from the DG or Board”​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati ilibaini kuwa uamuzi wa REA kuchangia ulifanyika kwa idhini yaMkurugenzi Mkuu kwa kutumia Kifungu hiki cha Mwongozo. Kamati Teule ina​
19​
Bajeti ya REA, Ukurasa wa 14.
20​
Internal Memo for Budget Reallocation – Request for Approval.
30​
maoni kwamba maudhui ya Kifungu cha 16.4.1 yanatoa mwanya kwa matumizimabaya ya fedha za umma kwa shughuli ambazo hazikupangwa na Taasisi.​
Discretionary powers​
za namna hii zisipowekewa mipaka ni mojawapo yamambo yanayoweza kusababisha kudhoofisha Mashirika na Taasisi zetu zaUmma.2.3.3 Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO)Mheshimiwa Spika,
Shirika hili lilitumia Kasma ya​
Donations and Subscriptions kuchangiaSh.40,000,000.00. Tafsiri isiyo rasmi ya kasma hii ni Michango ya Kijamii na adaza Uanachama. Katika Bajeti ya TANESCO ya Mwaka 2011, kasma hiyo ilikuwana Sh.200,000,000.00 ambazo ziko ndani ya mamlaka ya Mkurugenzi Mtendaji.Hapo ndipo fedha za kuichangia Wizara ili iwasilishe hotuba ya bajeti yakeBungeni zilipochukuliwa. Lakini kuichangia Wizara kwa ajili ya kuwasilishaHotuba ya Bajeti yake Bungeni siyo shughuli mahsusi iliyolengwa katika kuisaidiajamii wala siyo ada ya uanachama katika Wizara. Akitoa maelezo yake mbele yaKamati Teule, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa TANESCO alisema:-
“… kwa jinsi ninavyoelewa mimi ni kwamba, kasma hiyo haipo kwa niahiyo. Kunaweza kuwa na kasma kwa ajili ya donations nasubscriptions, lakini sidhani kama kuna kasma ya kutoka ndani yakampuni kwenda Wizarani… Kasma ambayo naijua ambayo inaitwadonation na subscription, labda kwa Kiingereza tungeiita kwa ajili yaphilanthropic activities ambayo inakuwa ni ya donations za kutoamisaada katika vikundi, makampuni na shughuli za kijamii. Natakanitofautishe shughuli za kijamii na shughuli ya kusaidia Bajetiipite….​
21”
21​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 14 Septemba, 2011.
31​
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kwamba kasma ya​
Donations and Subscriptions
haikutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.​
2.3.4 Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA)Mheshimiwa Spika,​
Mamlaka hii iko chini ya Wizara ya Maji kimuundo ingawa baadhi ya majukumuyake yapo chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Katika suala hili la kuichangiaWizara ya Nishati na Madini, EWURA haikuwa tayari kuchanga Sh.40,000,000.00badala yake wakaomba wachangie kwa kulipia gharama za chakula na vinywaji(Sh.3,656,000.00) na tafrija siku ya kuwasilisha Bajeti (Sh.6,141,600.00)gharama ambazo zilifikia jumla ya Sh.9,797,600.00. Fedha hizi zilitolewa katikakasma ya Elimu kwa Umma.Kutokana na mahojiano na Watendaji wa EWURA msingi wa ombi hili lakuchangia chakula na tafrija ni kuwa maombi ya Sh.40,000,000.00 kutokaWizarani hayakuainisha mchanganuo wa matumizi. Hivyo walipima wenyewe nakutumia busara kwamba badala ya kupeleka fedha hizo Wizarani watagharamiachakula na tafrija wao wenyewe. Kwa hali hiyo, busara ya EWURA ilisaidiakuokoa Sh.30,202,400.00.Hata hivyo, Kamati Teule ilipitia​
Financial and Accounting Manual ya EWURA nakubaini uwepo wa Kifungu cha 16.4.1 ambacho kinaweza kutumika vibaya.Kifungu hicho kinasomeka:-
“No activity may be carried out or expenditure be incurred withoutits prior inclusion in the annual plan and budget, except approval hasbeen obtained from the DG or Board”​
Uamuzi wa EWURA wa kulipia gharama zilizotajwa kwa Sh.9,797,600.00 badalaya kuchanga Sh.40,000,000.00 kama walivyoombwa uliwawezesha kufanikiwakudhibiti matumizi na hivyo kuokoa fedha za Taasisi. Vilevile umewezesha​
32​
uwekaji wa kumbukumbu za fedha kuwa kwenye mamlaka yao. Hata hivyo halihii haihalalishi uchangiaji walioufanya kwa sababu kasma ya Elimu kwa Umma,kama jina linavyosomeka, siyo mahsusi kwa ajili ya kuichangia Wizara kwa ajiliya maandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Bungeni.​
2.4 Uchunguzi kuhusu Matumizi Halisi ya Fedha ZilizokusanywaMheshimiwa Spika,​
Katika mahojiano na uchambuzi wa nyaraka za bajeti na matumizi ya Wizarajuu ya fedha zilizochangishwa, Kamati Teule ilibaini kuwa mahitaji halisi yamaandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti yalikuwa Sh.207,042,000.00ambayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyaridhia (​
TazamaKiambatisho VI). Kati ya Sh.207,042,000.00 zilizohitajika, Sh.35,500,000.00zilitoka kwenye Kifungu cha Project Coordination and Monitoring cha Wizara.Kwa mantiki hiyo, Wizara ilibaki na upungufu wa Sh.171,542,000.00.Kwa lengo la kuziba upungufu wa fedha ulioelezwa hapo juu, mnamo tarehe25 Juni, 2011 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alituma kiasi chaSh.171,542,000.00 kwa njia ya TISS BOT kwenye Akaunti Na. 5051000068 yaGST Dodoma. Fedha hizo zilipokelewa na GST Dodoma kwa stakabadhi Na.02428 ya tarehe 25 Juni, 2011. Hivyo, kufikia tarehe 25 Juni, 2011 Wizarailikuwa tayari ina fedha za kutosha kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungenibila ya kuhitaji michango kutoka kwenye Taasisi. Lakini pia, hiyo tarehe 25Juni, 2011 ni siku tano tu (5) baada ya Wizara kutuma barua za kuombamichango kwenye Taasisi na ni siku 20 kabla ya Wizara kuwasilisha Hotuba yaBajeti yake Bungeni.Hivyo Wizara ilikuwa na muda wa kutosha kuzuia michango isiendelee kamaingetaka kufanya hivyo, baada ya kuona fedha zilizokuwepo hadi wakati huozilikuwa zinatosha kwa maandalizi na uwasilishaji wa Bajeti yake.
33​
Mheshimiwa Spika,​
Kama ilivyoainishwa katika maelezo chini ya Jedwali Na. 4 fedha zilizoingizwakatika Akaunti ya GST kwa ajili ya shughuli za uwasilishaji wa Hotuba ya BajetiBungeni ni Sh.418,081,500.00. Kwa msingi huo, Kamati Teule ilijielekezakuchambua namna Sh.418,081,500.00 zilivyotumika kuanzia tarehe 14 Julai,2011 siku moja kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa hadi20 Julai, 2011 siku ambayo fedha iliyobaki ilirejeshwa katika Akaunti ya GST.Uchambuzi wa matumizi hayo ni kama ifuatavyo: -(a)​
Posho ya Kujikimu
Kamati ilibaini kwamba jumla ya watumishi 69 walilipwa posho yakujikimu. Hii ni kwa mujibu wa orodha ya malipo ya posho ya kujikimuiliyowasilishwa na Wizara mbele ya Kamati Teule. Jumla yaSh.32,425,000.00 zililipwa kwa watumishi hao kwa muda wa siku saba(7), kuanzia tarehe 14 Julai, 2011 hadi 20 Julai, 2011.(b)​
Posho ya Kikao
Malipo ya posho ya kikao yalifanyika kwa muda wa siku tano (5) kuanziatarehe 14 Julai, 2011 hadi 18 Julai, 2011 kwa watumishi 243 ambapojumla ya Sh.127,820,000.00 zilitumika. Hata Hivyo, Kamati ilibaini kuwaKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alielekeza kuwa Maofisasitini na mmoja (61) ndio waliotakiwa kwenda Dodoma kwa shughuli yaBajeti​
22.
Mheshimiwa Spika,​
Kwa kuwa watumishi 61 ndio walioidhinishwa kwenda Dodoma kwashughuli ya Bajeti ya Wizara, Kamati ilishtushwa na ongezeko lawatumishi 182 hadi kufikia 243 ambayo ni karibu asilimia 400 yawalioidhinishwa na Katibu Mkuu.​
22​
Kifungu 1.4.11, Ukurasa wa (ix) wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
34​
Kamati Teule ilipitia kwa kina mihtasari ya vikao ambavyo ndivyovilikuwa msingi wa ulipaji wa posho ya kikao. Mihtasari ya vikao hivyo nikuanzia tarehe 14 Julai, 2011 hadi 18 Julai, 2011; jumla ya vikao vitano(5). Kwenye mihtasari ya vikao vyote hivyo yafuatayo yalidhihirika: -(i) Akidi ya kila kikao ni wajumbe mia moja na tatu (103).(ii) Malipo ya posho ya kikao yalifikia wajumbe 243 kutoka 103, ziadaya wajumbe 140.(iii) Hakuna yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita.(iv) Mihtasari yote haikuthibitishwa kuwa ni kumbukumbu sahihi zavikao vilivyopita.Kamati Teule haikuweza kubaini ni mambo gani yaliyosababisha idadi yawalipwaji wa posho ya kikao kuongezeka kutoka 103 hadi kufikia 243.Muundo na maudhui ya mihtasari ya vikao vyote inaleta taswira kwa mtuwa kawaida kuwa iliundwa mahsusi kwa ajili ya kupata posho ya vikao.(c)​
Chakula na VinywajiMheshimiwa Spika,
Kumbukumbu zilizowasilishwa kutoka Wizarani zinaainisha kuwa mnamotarehe 19 Julai, 2011, Wizara ililipa kiasi cha Sh.17,480,000 taslim kwa​
African Dreams Conference Centre Ltd.​
ikiwa ni gharama ya chakula naviburudisho kwa watu 160 kwa siku tano za kazi.23 Malipo ya fedha hizoyalikiuka Kanuni Na. 86(1) ya Kanuni za Fedha za Umma, 2001 pamoja namarekebisho yake ya mwaka 2004. Kanuni hiyo inasema: -
23​
Receipt No. 919 ya tarehe 19 Julai, 2011 ya African Dreams Conference Centre Ltd.
35​
“86-(1) All disbursements of public money shall be properlyvouched on the prescribed form of payment whichvouchers must be typewritten or made out in ink orballpoint pen and must contain or have attachedthereto full particulars of the service for whichpayment is made, such as dates, numbers, distances,rates so as to enable them to be checked withoutreferences to any other document​
Kwa mujibu wa Kanuni iliyonukuliwa hapo juu, dosari zinazotokanana malipo ya aina hiyo ni kama ifuatavyo:-(i) Hapakuwa na orodha ya watu mia moja sitini (160) waliopatahuduma hiyo.(ii) Malipo kufanyika kwa fedha taslim badala ya hundi.(iii) Siku tano za kazi zilizoainishwa katika stakabadhi ya malipohazibainishi tarehe husika kwani Bajeti ya Wizara iliwasilishwatarehe 15 Julai, 2011 hadi 18 Julai, 2011 ambazo ni siku mbili (2)tu za kazi.(iv) Kukosekana kwa Hati ya Madai na mchanganuo wa kuonesha jinsimadai hayo yalivyofikiwa.(d)​
Mafuta ya MagariMheshimiwa Spika,
Kamati Teule ilichambua stakabadhi za manunuzi ya mafutayaliyotumiwa na magari 15 yaliyoshiriki katika shughuli ya uwasilishajiwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Bungeni Dodoma kamainavyoonekana kwenye Jedwali Na. 5.​
36​
Jedwali 5: Orodha ya Magari ya Wizara ya Nishati na Madiniyaliyotumika Dodoma kipindi cha Bajeti​
Na. Na.ya Gari Tarehe Lita Shilingi JumlaNdogo Jumla Kuu​
1. STK 7925STK 7925STK 792513 Julai, 201117 Julai, 201117 Julai, 201110610050230,000.00210,000,00105,000.00 545,000.00 545,000.002. STK 7920STK 7920STK 792013 Julai, 201117 Julai, 201118 Julai, 201110010050210,000,00210,000,00105,000.00 525,000.00 525,000.003. STK 3528 16 Julai, 2011 50 105,000.00 105,000.00 105,000.004. STK 8214STK 8214STK 821413 Julai, 201117 Julai, 201118 Julai, 201110010050210,000,00210,000,00105,000.00 525,000.00 525,000.005. STK 5213 17 Julai, 2011 100 210,000.00 210,000.00 210,000.006. STK 8215(DSM)STK 8215STK 8215STK 821513 Julai, 201114 Julai, 201116 Julai, 201118 Julai, 2011231095010040,000.00230,000,00105,000.00210,000.00 585,000.00 585,000.007. STJ 9429STJ 9429STJ 9429STJ 942913 Julai, 201117 Julai, 201117 Julai, 201117 Julai, 201112030100100252,000.0063,000.00210,000.00210,000.00 735,000.00 735,000.008. STK 1801STK 1801STK 1801STK 180113 Julai, 201117 Julai, 201118 Julai, 2011-1205010030252,000.00105,000.00210,000.0063,000.00 630,000.00 630,000.009. STK 8213(DSM)STK 8213STK 8213STK 821313 Julai, 201115Julai, 201117 Julai, 2011-1205010030252,000.00105,000.00210,000.0063,000.00 630,000.00 630,000.0010. STK 3525 18 Julai, 2011 100 210,000.00 210,000.00 210,000.0011. STK 9868(DSM)STK 986813 Julai, 201116 Julai, 201180.1480.6167,000.00182,000.00 349,000.00 349,000.0012. STK 8186 21 Julai, 2011 71.4 150,000.00 150,000.00 150,000.0013. STK 8184 21 Julai, 2011 71.4 150,000.00 150,000.00 150,000.0014. STK 8191 17 Julai, 2011 71.4 150,000.00 150,000.00 150,000.0015. STK 8189 21 Julai, 2011 71.4 150,000.00 150,000.00 150,000.00​
JUMLA 5,754,000.00 5,754,000.00​
37​
Taarifa zilizoonyeshwa kwenye​
Jedwali Na. 5 zinadhihirisha yafuatayo:-(i) Gari Na. STJ 9429 lilitumia kiasi cha lita 230 za mafuta kwa sikumoja wakati kitabu cha kumbukumbu za safari (Log Book)hakionyeshi kama gari hii ilikuwa na safari ndefu nje ya Dodomakatika siku hizo.(ii) Jumla ya magari 15 kutoka Wizarani peke yake inaashiria idadikubwa ya watumishi walioshiriki kwenye zoezi la uwasilishaji waBajeti ambayo yanasababisha matumizi makubwa ya mafuta namatengenezo ya magari yasiyokuwa ya lazima.(e) Vifaa vya Kuandikia
Shughuli hii ya uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti Bungeni ilihusisha piamatumizi ya vifaa mbalimbali vya kuandikia. Vifaa Hivyo vilinunuliwamjini Dodoma na Wizara kati ya tarehe 15 – 18 Julai, 2011 kwa gharamaya Sh.625,020.00 kama ilivyoonyesha kwenye​
Kiambatisho X.
(f)​
Takrima na Viburudisho
Kamati Teule ilipitia kwa kina nyaraka zinazohusiana na takrimailiyotolewa kwa Viongozi wa Wizara na pia viburudisho kwa wafanyakaziwa Wizara katika kipindi cha uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Bungenikati ya tarehe 14 - 20 Julai, 2011 kwa gharama ya Sh.494,600.00 kwaajili ya viburudisho na Sh.8,000,000.00 kwa ajili ya takrima kwa Wazirina Naibu Waziri kama ilivyoonyesha kwenye​
Kiambatisho XI.Mheshimiwa Spika,
Kwa muhtasari, matumizi ya fedha zote zilizoingizwa kwenye Akaunti ya GST nikama ifuatavyo: -​
38​
Fedha zilizoingizwa Akaunti ya GST -​
Sh.418,081,500.00
Matumizi:posho ya kujikimu 32,425,000.00Posho ya kikao 127,820,000.00Chakula na vinywaji 17,480,000.00Mafuta ya magari 754,000.00Vifaa vya kuandikia 625,020.00Takrima na Viburudisho 8,494,600.00​
Sh.192,598,620.00
Baki ................................................​
Sh.225,482,880.00
Toa kiasi kilichorejeshwa Benki .................​
Sh. 99,438,400.00
Salio halisi (fedha mkononi)… ...................​
Sh.126,044,480.00Mheshimiwa Spika,
Ukokotoaji wa matumizi ya fedha zilizoingizwa kwenye Akaunti ya GST, Dodomaumetokana na nyaraka zote za matumizi zilizowasilishwa na Wizara ya Nishatina Madini mbele ya Kamati Teule. Hata hivyo, nyaraka hizi hazikubainishamatumizi halisi ya kiasi cha Sh.126,044,480.00.Kutobainika kwa matumizi halisi ya kiasi hicho cha fedha kuliifanya KamatiTeule imhoji tena kwa maandishi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara yaNishati na Madini (Barua Kumb. Na.CBE.50/155/03A/94 ya tarehe 27 Oktoba,2011). Maelezo yake ilikuwa ni kwamba matumizi ya Sh.126,044,480.00 yalikuwakama ifuatavyo: -(a) Sh.50,143, 500.00 - Ziligharamia ukamilishwaji na marekebisho yaRandama kwa mara ya pili kwenye vikao vya Kamatiya Bunge ya Nishati na Madini.(b) Sh.20,000,000.00 - Ziligharamia vikao vya Kamati Ndogo ya Wataalamwaliobaki Dodoma kujibu Hoja za Wabunge baada yavikao.​
39​
(c) Sh.56,386,000.00 - Ziligharamia marekebisho ya MTEF ya Wizara baada yamapendekezo ya Wabunge.​
Mheshimiwa Spika,​
Hata hivyo, maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi huyu hayakukubaliwa naKamati Teule kwa sababu zifuatazo: -(i) Hakukuwa na mchanganuo wowote wa matumizi na nyaraka zauthibitisho wa malipo.(ii) Kiasi cha Sh.50,143,500.00 kilichoonyeshwa kama matumizi yakurekebisha na kuwasilisha randama kwa mara ya pili kwenye Kamati yaBunge ya Nishati na Madini iliyokutana Dodoma Juni, 2011 kimeonyeshwamara mbili kwa matumizi yale yale.​
40​
3.0 KUPITIA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALIKUHUSU UCHUNGUZI ALIOUFANYAMheshimiwa Spika,​
Mwongozo kwa Kamati Teule kuhusu Hadidu ya Rejea ya Pili ulikuwa KamatiTeule ipitie Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusuUchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini kuchangisha fedha Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili yakuwezesha maandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyoBungeni.Ili kukamilisha Hadidu ya Rejea ya Pili, Kamati Teule ilifanya yafuatayo:-(a) Kupitia Katiba, Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Nyaraka mbalimbali.(b) Kupitia Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali.(c) Kufanya mahojiano na mashahidi mbalimbali akiwemo Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali na Watendaji wa Ofisi yake waliohusika katikaukaguzi huo na Katibu Mkuu Kiongozi.​
Mheshimiwa Spika,​
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwamujibu wa Ibara ya 143 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.Majukumu ya Ofisi hii yameainishwa katika Ibara ya 143(2) ya Katiba. Kwamujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008, Ofisi hii ina wajibu wa kukaguamahesabu ya fedha za Umma kwa niaba ya Bunge ili kuhakikisha kuwa Serikaliinatumia fedha za umma kama zilivyoidhinishwa na Bunge kwa namna yenyekuleta tija.​
24
24​
Kifungu cha 10 (1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008 na Kifungu cha 31(1) cha Sheria ya Fedha zaUmma, 2001
41​
Chini ya Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008​
25 Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali inafanya kaguzi zifuatazo: -(a) Ukaguzi wa Kawaida (Regularity Audit)(b) Ukaguzi wa Kiuchunguzi (Forensic Audit)(c) Ukaguzi wa Ufanisi (Performance Audit)(d) Kaguzi Nyingine/Kaguzi Maalum (Other Audits/Special Audit)Kifungu cha 29(2) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008 kinaruhusu Taasisiyoyote kumwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanyaUkaguzi Maalum katika maeneo ambayo Taasisi hizo zinaona inafaa. Kifunguhicho kinasomeka kama ifuatavyo: -
“The Controller and Auditor-General may, on request by any person,Institution, Public Authorities, Ministries, Departments, Agencies,Local Government Authorities and such other bodies to undertake anyspecial audit.”​
Kwa kutumia Kifungu hiki Katibu Mkuu Kiongozi aliona inafaa Ukaguzi Maalumufanyike kwa kumtumia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilikubaini uhalali wa utaratibu wa kuchangisha michango na kubaini matumizi yafedha zilizochangishwa.​
3.1 Uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikaliMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilifanya uchambuzi wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum wa Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (​
Tazama Kiambatisho XII) kamainavyofafanuliwa hapa chini:
25​
Kifungu cha 26, 27, 28 na 29.
42​
3.1.1 Namna Suala hili lilivyomfikia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali​
Baada ya mahojiano kati ya Kamati Teule na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali na baadaye mahojiano kati ya Kamati Teule na Katibu MkuuKiongozi; na kwa kutumia nyaraka mbalimbali za mawasiliano yaliyokuwepokati ya Katibu Mkuu Kiongozi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali, Kamati Teule ilibaini kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alimuomba Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye Uchunguzi wa Awali (​
PreliminaryInvestigation) kwa kufanya Ukaguzi Maalum (Special Audit) (TazamaKiambatisho XIII). Katibu Mkuu Kiongozi alifanya hivyo kwa kutumia madarakayake ya kisheria kwamba yeye ndiye Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuualiyetuhumiwa, Ndugu David Kitundu Jairo.
3.1.2 Nakala Halisi ya Taarifa ya Ukaguzi MaalumMheshimiwa Spika,​
Ili kuweza kuipata nakala hii, Kamati Teule ilizingatia Kanuni ya 81(a) yaKanuni za Ukaguzi wa Umma, 2009. Kanuni hii inaweka wazi utaratibu kwambaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anapokuwa amekamilishakufanya Ukaguzi Maalum aliyoombwa kwa maandishi, atakabidhi Taarifa yakeya Ukaguzi kwa aliyeomba. Katika suala hili, Katibu Mkuu Kiongozi ndiyealiyeomba kwa maandishi Ukaguzi huu Maalum ufanyike. Hivyo, Kamati Teuleilimwandikia Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata nakala ya Taarifa hiyo na mnamotarehe 9 Septemba, 2011 ilipata nakala ya Taarifa hiyo.​
3.1.3 Hadidu za Rejea alizokabidhiwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza SerikaliMheshimiwa Spika,​
Uchunguzi wa Kamati Teule ulibaini kwamba barua ya Katibu Mkuu Kiongozikuomba kufanyika kwa Ukaguzi Maalum dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini ilikuwa na Hadidu za Rejea mbili tu ambazo ni:​
43​
(a) Kuchunguza uhalali wa Michango.(b) Kuchunguza namna fedha hizo zilivyotumika.Hata hivyo, Taarifa ya Ukaguzi Maalum inaonyesha kuwa palikuwepo na Hadiduza Rejea Kumi na Tano kama ifuatavyo: -(i) Kufuatilia Wizara ya Nishati na Madini ili kupata idadi na majina yaTaasisi na Idara zilizoagizwa kuchangia fedha pamoja na kiasi husika.(ii) Kuchunguza ili kujua namna uamuzi wa kuchangisha fedha kuziwekakatika akaunti ya GST ulivyofikiwa.(iii) Kutembelea Taasisi na Idara zilizochangishwa fedha na kuangalia kamaziliagizwa kufanya hivyo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini naupatikane ushahidi wa stakabadhi za kukiri mapokezi ya michango hiyo.(iv) Kuulizia kutoka Taasisi na Idara zilizochangishwa fedha kamazililazimishwa kufanya hivyo au ilikuwa ni hiari na kama walitoa taarifakwa mamlaka husika iwapo walilazimishwa.(v) Kuchunguza chanzo cha fedha zilizochangwa na Taasisi/Idara nakuangalia kama zilikuwa katika bajeti zao za mwaka kwa kazi hiyo nakama malipo hayo ya michango yaliidhinishwa na Bodi za Wakurugenzi.(vi) Kwa kila mchango, kufanya uhakiki wa nambari ya akaunti ya Benki naTawi la Benki ambako fedha ziliwekwa.(vii) Kupata taarifa za akaunti za Benki za GST na kufanya uhakiki wa usahihiwa taarifa hizo na kisha kukokotoa jumla ya fedha zote zilizochangwana kuhamishiwa katika akaunti ya GST – Dodoma.(viii) Kuchunguza ili kubaini kama Wizara ilishawahi/kuagiza michango yanamna hii kufanyika katika miaka ya nyuma na kufuatilia katika Taasisi​
44​
na Idara zilizo chini ya Wizara ili kujua kiasi kilichochangwa. (Tanbihi:Maelezo yatakayotolewa yatasaidia uchunguzi wa kina kufanyika baadaya ripoti ya awali kuhusu tuhuma hizo kutolewa).(ix) Kuuliza kwa mwenye akaunti ya Benki iliyopokea fedha (GST) ili kubainikama aliagizwa kupokea fedha zilizochangwa na pia kama alipewamaagizo ya jinsi malipo yatakavyofanyika.(x) Kupata maelezo ya malipo yaliyofanywa kutokana na fedhazilizochangwa, na malipo hayo yaainishwe yakionyesha madhumuni,majina ya waliolipwa na kiasi cha fedha kwa kila mmoja.(xi) Kama sehemu ya kupata ukweli wa yale yaliyotokea, Maofisawaliohusika katika kadhia hii wafanyiwe usaili kwa kadriitakavyoonekana inafaa.(xii) Kuangalia kama malipo yaliyofanyika yamezingatia matakwa ya Sheriaya Fedha za Umma Na. 6 ya 2001 (iliyorekebishwa 2004) na Kanuni zakeza Mwaka 2005.(xiii) Kuangalia kama waliolipwa huko Dodoma walikuwa wameshalipwa naTaasisi zao kwa kazi hiyo hiyo.(xiv) Endapo malipo yaliyofanywa yatathibitika kuwa ni rushwa, taarifaitolewe kwa vyombo husika kwa mujibu wa Kifungu cha 27 cha Sheria yaUkaguzi wa Umma Na. 11 ya Mwaka 2008.​
26
(xv) Kuandaa ripoti maalum itakayowasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongoziikionyesha matokeo ya uchunguzi pamoja na viambatanisho kwa kadriitakavyoonekana inafaa​
27.
26​
Ukurasa wa (v) – (vi).
27​
Ukurasa wa (v) – (vi).
45​
Mheshimiwa Spika,​
Baada ya kupitia Hadidu za Rejea hizi Kumi na Tano, Kamati Teule ilipatamashaka, hivyo kuhoji kuhusu kutofautiana kwa idadi ya Hadidu za Rejeazilizopo kwenye barua ya Katibu Mkuu Kiongozi na zile zilizopo kwenye Taarifaya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Alipohojiwa na KamatiTeule kuhusu tofauti ya Hadidu za Rejea hizo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali alijibu kwamba Kanuni ya 80(1) inayohusu​
Scope of Audit
inampa mamlaka ya kurekebisha Hadidu za Rejea atakazopewa na aliyeombaUkaguzi Maalum (​
Special Audit).Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Kamati Teule na Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali:
Swali: Labda tunaweza kuwa tunakaribia kwenye jibu lakini bado hatujafika. Ukurasawa v na vi ni zile ambazo zimeitwa pale kuwa ni Hadidu za Rejea?Jibu: Mheshimiwa Mwenyekiti ni​
procedures.Swali: Mnabadilisha?Jibu: Yes!Swali: Ni procedures sasa, sio Hadidu za Rejea?Jibu: Ni procedures.Swali: Kama zilivyoandikwa kwenye ripoti, sio Hadidu za Rejea, ni procedures, kwaKiswahili ni nini?Jibu: Ni taratibu.
Kama inavyodhihirika katika sehemu hii ya mahojiano, Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali alikiri kwamba hizo hazikuwa Hadidu za Rejeakama alivyoeleza katika Taarifa ya Ukaguzi Maalum, bali ni taratibu.​
28
28​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2010.
46​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilifanya pia mahojiano na Katibu Mkuu Kiongozi kuhusiana nakutofautiana kwa Hadidu za Rejea zilizopo kwenye barua ya agizo la kazi nazile zilizopo kwenye Taarifa ya Ukaguzi Maalum. Ifuatayo ni sehemu yamahojiano kati ya Kamati Teule na Katibu Mkuu Kiongozi:​
Swali: Sawa, halafu twende kwenye ukurasa wa pili wa​
item number four, unisomeeneno linaloanzia ‘pamoja na…’Jibu: Pamoja na kuchunguza uhalali wa michango hiyo, pia uchunguze namna fedhahizo zilivyotumika.Swali: Kwangu mimi hizi nadhani ndio Hadidu za Rejea ulizompatia.Jibu: Ndio.Swali: Ndizo ulizompatia hizi au kuna nyingine?Jibu: Pamoja na zile za details.Swali: Katibu Mkuu Kiongozi, naomba twende pamoja. Mimi nasoma barua yakoambayo umeandika, sijaona kiambatanisho hapa. Hii barua inajitosheleza,kwahiyo nilitaka twende pamoja tu na hapo nina point ya msingi sana. Sasamimi nilitaka niulize, ndio hizi Hadidu za Rejea au unasema una nyingine tenakwa barua nyingine?Jibu: Mheshimiwa Mwenyekiti, Hadidu za Rejea sijui ilikuwaje hapa…. Hadidu zaRejea ambazo ni detailed ndio hizi. Nilitaka nikusomee hizi kwenye nambaambazo zipo fourteen.Swali: Mimi bado. Labda hujanielewa vizuri. Ulisema uliwasiliana na barua kwendakwa Ofisi ya CAG. Sasa barua niliyonayo ndio hii ambayo tunaisoma wote kwapamoja. Ambayo imeainisha Hadidu za Rejea, achana na ripoti ya CAG. Miminazungumzia barua, kwenye ripoti ya CAG tutakwenda baadaye. Sasa nilitakaniulize, kuna Hadidu za Rejea nyingine ambazo ulimuandikia mbali na barua hii?
47​
Jibu: Sasa ndio nakwambia hivi sijui imekuwaje katika​
attachment, lakini zilikuwa
detailed​
. Hizi zilikuwa ni barua summarized, lakini zilikuwa detailed zileambazo ziko kumi na nne… I don’t understand how it went about it…!29
Mheshimiwa Spika,​
Katika mahojiano na Kamati Teule Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali alisema kuwa alipewa Hadidu za Rejea mbili tu, na zile zilizoandikwakwenye ukurasa wa (v) –(vi) wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum sio Hadidu za Rejeabali ni taratibu zilizotumika kufanya Ukaguzi Maalum.Wakati huo huo Katibu Mkuu Kiongozi aliieleza Kamati Teule kwamba alimpatiaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Hadidu za Rejea kumi na nne.Huo ni mkanganyiko wa Hadidu za Rejea zilizotumika kufanya uchunguzi. Hatahivyo, Kamati Teule iliendelea kufanyia kazi Taarifa ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyowasilishwa.​
3.1.4 Yaliyojitokeza kwenye Taarifa ya Ukaguzi MaalumMheshimiwa Spika,​
Katika Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali juu ya suala hili, yapo masuala muhimu (​
audit facts)yaliyojitokeza ambayo aliyeomba kufanyika kwa Ukaguzi Maalum alipaswakuyatumia kupima uhalali wa uchangishaji na namna fedha zilizochangishwazilivyotumika. Mchanganuo wa masuala haya kutoka kwenye Taarifa ya UkaguziMaalum ni kama ifuatavyo: -(a) Tarehe 9 Agosti, 2011, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalialikamilisha Ukaguzi wake na kukabidhi Taarifa ya Ukaguzi Maalum kwaKatibu Mkuu Kiongozi.30
29​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2010.
30​
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Barua Kumb. Na. DAC.37/314/01ya tarehe 9 Agosti, 2011 kwenda kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
48​
(b) Kugharamia uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni nijukumu la Wizara yenyewe​
31. Hivyo, Taasisi hazikupaswa kuchangishwakwa sababu hazina kasma mahsusi kwa ajili ya kuichangia Wizarainapowasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungeni32. Na kwamba fedhazilizochangishwa zilitumika kwa ajili ya kulipia posho za vikao kwaWajumbe 243 wa Wizara na Chakula cha Wajumbe kwa muda wa sikutano (5).(c) Wizara imekuwa na utaratibu wa kuchangisha Taasisi zake kwa zaidi yamiaka miwili sasa.33
(d) Jumla ya fedha zilizochangwa kwa ajili ya kuwezesha uwasilishaji waHotuba ya Bajeti ya Wizara Bungeni (2011/2012) ni Sh.418,801,500.00.Ndani ya kiasi hicho, Taasisi zilichangia Sh.140,000,000.00 na Wizarayenyewe ilichangia Sh.278,801,000.00.(e) Baadhi ya malipo yalifanyika pasipo kuzingatia matakwa ya kisheriakatika maeneo yafuatayo: -​
•​
Jumla ya Sh.20,000,000.00 zililipwa kama honoraria kwa Watumishiwa Wizara kabla ya Bajeti kupitishwa Bungeni. Utaratibu huu nikinyume na Kifungu Q.18 cha Kanuni za Kudumu za Utumishi waUmma, 2009, Toleo la Tatu.34
•​
Kanuni ya 86(1) ya Kanuni za Fedha za Umma, 2001 zilizorekebishwaMwaka 2004 zilikiukwa pale EWURA ilipotumia Sh.9,797,600.00 kwakulipa fedha taslim badala ya hundi katika manunuzi ya chakula,malipo kutoonyesha orodha ya watu waliohudumiwa, nahayakuonyesha tarehe kamili za siku tano (5) za gharamazilizolipwa35.
31​
Kifungu 4.3 Ukurasa wa15 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
32​
Kifungu 3.5 Ukurasa wa 7 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
33​
Kifungu 3.8 Ukurasa wa 9 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
34​
Kifungu 3.12, Ukurasa wa 11 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
35​
Kifungu 3.12, Ukurasa wa 11 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
49​
(f) Ukaguzi Maalum haukuthibitisha kwamba Idadi ya Taasisizilizochangishwa zilikuwa ishirini (20) na kwamba jumla ya fedhazilizochangishwa zilikuwa Sh.1,000,000,000.00​
36.(g) Ukaguzi Maalum haukuthibitisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa dhidiya Waheshimiwa Wabunge kwa madhumuni ya kuwashawishi wapitisheHotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kirahisi37.(h) Idadi ya Maofisa wa Wizara na Taasisi zake waliohudhuria mchakato wakuwasilisha Hotuba ya Bajeti Bungeni Dodoma walikuwa kati ya 211 na243 badala ya Maofisa 61 waliokuwa wameidhinishwa na Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini38.(i) Hapakuwepo na vikao vya makubaliano miongoni mwa Menejimenti zaTaasisi zilizochangia na Uongozi wa Wizara kuhusu kiasi cha kuchangia.Kadhalika hapakuwepo na makubaliano kati ya Menejimenti za Taasisizilizochangia na Bodi za Wakurugenzi wa Taasisi hizo kuidhinisha fedhakwa ajili ya shughuli iliyoombewa michango39.(j) Taarifa ya Ukaguzi Maalum juu ya suala la Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini kuchangisha fedha kwenye Taasisi zake inawezakubadilika baadaye endapo zitapatikana taarifa na vielelezo vya ziada40.(k) Mambo yaliyoibuliwa na ukaguzi huu maalum yatazingatiwa katikaukaguzi wa kawaida wa kisheria wa Fungu hili kwenye ukaguzi wa hesabuzilizoishia tarehe 30 Juni, 2011 na kujumuishwa kwenye ripoti ya ukaguziwa Wizara.
36​
Kifungu 4(4.1), Ukurasa wa 15 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
37​
Kifungu 4.2, Ukurasa wa 15 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
38​
Kifungu 3.12, Ukurasa wa 13 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
39​
Kifungu 3.2, Ukurasa wa 5 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
40​
Ukurasa wa (xi) wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
50​
(l) Fedha zilizochangishwa zilitumika kwa ajili ya kulipia posho za vikao nachakula kwa wajumbe kwa muda wa siku tano (5).​
3.2 Uchambuzi wa yaliyojitokeza kwenye Taarifa ya Ukaguzi MaalumMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilifanya uchambuzi kwa yaliyojitokeza kwenye Taarifa ya UkaguziMaalum kama ifuatavyo: -(a) Mnamo tarehe 20 Julai, 2011 Katibu Mkuu Kiongozi alimwomba Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi Maalum wa sualala uchangishaji wa Taasisi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Ukaguzihuu ulikamilishwa katika muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia tarehe25 Julai - 9 Agosti, 2011.Kwa kuzingatia uzito wa suala hili na jinsi lilivyohusisha mifumo yakibenki na Taasisi mbalimbali ambazo ziko katika maeneo tofauti, KamatiTeule inaamini kuwa huu ulikuwa ni muda mfupi sana kwa Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuweza kukamilisha jukumu hilikikamilifu. Hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalialipohojiwa juu ya jambo hili alikiri kwamba muda huu ulikuwa finyukwake na kwamba alimjulisha Katibu Mkuu Kiongozi kwa maongezi yamdomo juu ya ufinyu huo wa muda.Madhara yaliyotokana na ufinyu huu wa muda ni kwamba Taarifa ilitolewakabla ya baadhi ya vielelezo muhimu kupatikana. Ndiyo maana Taarifa yaMatokeo ya Ukaguzi Maalum iliweka bayana kwamba “matokeo ya Ukaguzihuo yangeweza kubadilika endapo vielelezo vya ziada vingepatikana”​
41.Hii ni kwa sababu wakaguzi hawakuwa na muda wa kutosha kusubirivielelezo.
41​
Ukurasa wa (xi) wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
51​
(b) Taarifa ya Ukaguzi Maalum inaonesha kuwa Taasisi zilizochangishwahazina kasma mahsusi kwa ajili ya uchangiaji huu. Kamati Teule ilifanyauchunguzi katika Nyaraka za Mpango Kazi wa Mwaka 2010/2011 waWizara ya Nishati na Madini na kubaini kuwa Wizara ina Fungu lake laBajeti linalojulikana kwa jina la​
Fungu 58 – 1003 - D01S04 (tocoordinate and prepare budget speech for the year 2010/11). Kazizilizokusudiwa katika Kasma hii ni pamoja na maandalizi ya Hotuba yaBajeti ya Wizara kwa Mwaka husika42.Uchunguzi ulionyesha pia kwamba Taasisi zilizochangishwa zinazo Kasmakwa ajili ya masuala ya maandalizi ya Bajeti za Taasisi zenyewe siyo kwaajili ya kuichangia Wizara katika kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yakeBungeni. Ni kwa msingi huu ambapo Kamati Teule inaona kuwa Taasisihazikupaswa kuchangishwa kwa sababu hazina Kasma Mahsusi kwa ajili yakuichangia Wizara inapowasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungeni. Maonihaya yapo pia kwenye Taarifa ya Ukaguzi Maalum43. Haya ni miongonimwa maoni ambayo Katibu Mkuu alipaswa kuyatumia kupima kuwepo amakutokuwepo kwa kosa la kinidhamu katika utendaji wa Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini. Ni maoni ambayo Katibu Mkuu Kiongozialipaswa kuyatoa pia kwenye Vyombo vya Habari ili “ukawaida” wautaratibu wa uchangishaji uweze kupimwa vizuri.(c) Kuhusu Wizara kuwa na Utaratibu wa kuzichangisha Taasisi, Taarifa yaUkaguzi Maalum imegusia kwamba Wizara imekuwa na utaratibu wakuchangisha Taasisi zake kwa zaidi ya miaka miwili sasa44. Kwa mfano, ilikuchangia uandaaji na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara yaNishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, Taasisi za REA,TANESCO na TPDC zilichangia jumla ya Sh.125,000,000.0045. YawezekanaKatibu Mkuu Kiongozi aliuita utaratibu huu kuwa ni wa kawaida kwa
42​
Wizara ya Nishati na Madini, Fungu 58. Mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Matumizi yaKawaida kwa Mwaka 2010/2011.
43​
Kifungu 3.5, Ukurasa wa 7 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
44​
Kifungu 3.8, Ukurasa wa 9 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
45​
Ukurasa wa 9 na 10 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
52​
sababu umekuwa ukitumika Wizara ya Nishati na Madini kwa muda wazaidi ya miaka miwili sasa.​
46
Ni maoni ya Kamati Teule kwamba hata kama utaratibu huu upo Wizaranikwa zaidi ya miaka miwili sasa, ni utaratibu ambao haujajengwa katikamisingi ya kisheria, kanuni na taratibu zingine za fedha za umma. Hivyo,ni utaratibu ambao hauwezi kuhalalishwa kwa kigezo cha kuwepoWizarani kwa zaidi ya miaka miwili. Huu ni utaratibu unaopaswakukomeshwa kabisa isipokuwa tu kwa kibali maalum kama ambavyoWaraka Namba 3 wa Machi, 2011 kutoka kwa Mlipaji Mkuu wa Serikaliunavyoelekeza.(d) Uchunguzi wa Kamati Teule umebaini kuwa mnamo tarehe 14 Juni, 2011,Wizara iliandaa Bajeti kwa ajili ya kukamilisha zoezi la uandaaji nauwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti yake Bungeni. Zoezi hili lilikadiriwakugharimu kiasi cha Sh.207,042,000.00​
47. Hata hivyo, katika kipindi chatarehe 14 Juni - 20 Juni, 2011, Wizara ilijitathmini na kuona kwambakasma ambayo Wizara huitumia kwa shughuli za Bajeti (ProjectMonitoring and Coordination) ilibakiwa na Sh.35,500,000.00 hivyo kuwana upungufu wa Sh.171,542,000.00. Ndipo tarehe 21 Juni, 2011 Wizaraikaamua kuziandikia Taasisi zake barua za kuomba michango ili kuzibapengo hilo. Hata hivyo, tarehe 25 Juni, 2011, kiasi cha Sh.171,542,000.00kilitumwa na Wizara kwenye akaunti ya GST, Dodoma kwa ajili yashughuli za Bajeti yake kutoka kwenye Kifungu cha OC. Kwa mantiki hiyo,kuanzia tarehe 25 Juni, 2011 tayari Wizara ilikwishapata fedha za kutoshakukidhi gharama za mchakato wa uandaaji na uwasilishaji wa Hotuba yaBajeti yake.
46​
Kifungu 3.8, Ukurasa wa 9 wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
47​
Mchumi Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dokezo EB.88/612/01/13 kwenda kwa DP.
53​
Mahojiano kati ya Kamati Teule na Mkurugenzi wa Sera na Mipango waWizara ya Nishati na Madini katika eneo hili yalikuwa kama ifuatavyo:-​
Swali: Kwa maana hiyo Mr. Swai, utakubaliana na mimi kwamba baada ya kupokeaile milioni 171…Jibu: Ndiyo.Swali: Kulikuwa hakuna haja kabisa ya kuwa na fedha nyingine kutoka kwenyeTaasisi zenu, hilo nadhani tutakubaliana?Jibu: Kama tungekuwa tumekwishazipata hizo fedha tungeweza kuwa namahitaji, lakini siyo yale ya kusema kwamba lazima tuombe.Swali: Hapa tunazungumza lugha moja!Jibu: Ndiyo!Swali: Kwamba, hapa kuna mtu alikuwa mahututi bin taaban, anahitaji milioni207.Jibu: Ndiyo.Swali: Akawa na wasiwasi kama atazipata.Jibu: Ndiyo.Swali: Lakini akatoa taarifa kwa wenzake, jamani eeh, naomba muwe tayarikunisaidia, ghafla fedha zake zinaingia, huyu mtu ana shida ya fedha tena?Jibu: Ni kweli hakuna haja.Swali: Kwa hiyo, ule umuhimu wa kuhitaji tena fedha za Taasisi ulikwisha kabisa?Jibu: Ndiyo.​
4848 Hansard ya Kamati Teule, tarehe 11 Oktoba, 2011.
54​
Mheshimiwa Spika,​
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Wizara ilikuwa na fursa yakuahirisha zoezi la uchangishaji kwa kuwa hakukuwa na mahitaji tena yafedha kwa ajili ya matumizi ya zoezi la Bajeti, lakini kwa mshangaomkubwa haikufanya hivyo! Badala yake iliendelea kukusanya michangohiyo kama ifuatavyo: -REA Sh. 50,000,000.00TANESCO Sh. 40,000,000.00TPDC Sh. 50,000,000.00Idara ya Mipango Sh. 278,081,500.00​
JUMLA​
Sh. 418,081,500.00
Kipengele​
2.4 cha Taarifa hii kinaelezea namna fedha hizi zilivyotumikakatika mchakato wa uandaaji na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti yaWizara hiyo.(e) Matokeo ya Ukaguzi Maalum yaliweka bayana pia kwamba baadhi yamalipo kutokana na fedha zilizochangishwa yalifanyika pasipo kuzingatiamatakwa ya Kanuni za Fedha za Umma katika maeneo yafuatayo: -(i) Kifungu Q.18 cha Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009Toleo la Tatu kinasomeka kama ifuatavyo: -
“Public Servants who make special contributions to theService which lead to economy, or greater efficiency, orenhance reputation of the Service may be eligible for thepayment of an honorarium of an amount which the ChiefExecutive Officer considers reasonable and justifiedunder the circumstances.”​
55​
Kwa mujibu wa Kifungu tajwa hapo juu, mamlaka ya kuamua juuya kiwango, sababu, wakati na namna ya kulipa​
honoraria
yamewekwa kwa Mtendaji Mkuu. Hivyo, Mtendaji Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madini ametumia Kifungu hiki kufanya malipoyanayozungumziwa licha ya kwamba hapakuwa na ufanisi ambaoungestahili malipo haya kwa kuwa Bajeti ya Wizara haikupitishwa.​
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kwamba zoezi zima la Bajeti lingepimwakwa kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara Bungeni. Ni maoni ya KamatiTeule pia kwamba, Katibu Mkuu Kiongozi alitarajiwa kutumia Hojaya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwamba malipoya​
honoraria ya Sh.20,000,000.00 yaliyofanyika bila tija kuwa nikosa la kinidhamu.(ii) Kwa kufanya malipo ya jumla ya Sh.9,797,600.00 kwa fedhataslimu EWURA pia walikiuka Kanuni ya 86(1) ya Kanuni za Fedhaza Umma, 2001 zilizorekebishwa Mwaka 2004 inayosomeka:
“All disbursements of public money shall be properlyvouched on the prescribed form of payment whichvouchers must be typewritten or made out in ink orballpoint pen and must contain or have attached theretofull particulars of the service for which payment is made,such as dates, numbers, distances, rates, so as to enablethem to be checked without references to any otherdocument.”​
(f) Kamati Teule imeshangazwa na Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali kama ilivyonukuliwa katika Taarifa ya Ukaguzi Maalumalioufanya na hatimaye kutumika na Katibu Mkuu Kiongozi katika uamuziwake wa Uchunguzi wa Awali kwamba hakukuwa na uthibitisho wa idadi​
56​
ya Taasisi zilizochangishwa kuwa ishirini (20) na kwamba jumla ya fedhazilizochangishwa zilikuwa Sh.1,000,000,000.00.Kamati Teule inaiona Hoja kubwa ni uhalali wa zoezi zima la uchangishajiwa Taasisi chini ya Wizara kwa madhumuni yaliyotajwa bila kuzingatiaSheria, Kanuni na taratibu, bila kujali idadi ya Taasisi zilizochangishwawala kiwango cha fedha kilichochangishwa. Hata kama ingekuwa niTaasisi mbili au tatu ndizo zilizochangishwa na fedha zilizochangishwakuwa Sh.5,000,000.00 au 10,000,000.00 bado suala la uhalali lingebakipale pale.Kamati Teule imepitia​
Hansard ya tarehe 18 Julai, 2011 na kuthibitishakwamba hakuna mahali popote ambapo Mbunge yeyote alitaja idadi yaTaasisi kuwa ishirini (20). Hivyo, ili kufahamu Taasisi hizo 20 zilitokawapi Kamati Teule ilimuuliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: -
Swali: …ume-​
mention Hansard, ni Hansard ya tarehe ngapi, ambako mimi
specifically​
nataka unipeleke kwa Taasisi 20 maana base yako unasema …Jibu: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi 20 is very simple, uki-divide one billion bya 50 it gives you 20, mathematically.Swali: … naomba nijielekeze kwenye Hansard. Hansard hata ukikohoa inaandikaumekohoa, ukicheka inaandika umecheka… Sasa tujielekeze pale hasamaana tusije tukatumia logic.Jibu: Niseme tu kwamba the 20 kama ilivyokuwa reported na Vyombo vya Habari
it was​
mathematically derived, by dividing one billion by 50, it gives you20.
Swali: …umesema na​
findings zako umeonyesha kwamba mmetumiaHansard…concern yangu hapo ni kweli kwenye Hansard zipo Taasisi 20zilisemwa?Jibu: Kwenye Hansard haionyeshi moja kwa moja kwamba zipo Taasisi 20.
57​
Swali: Labda kwa nyongeza hata ile​
one billion kwenye Hansard imeandikwa zaidiya bilioni, could be 10 billion!
Jibu: … Hata magazeti yaliandika zaidi ya Taasisi 20.Swali: Sasa nafikiri kwa sababu una​
-refer zaidi Hansard na ndiyo ambayoumeifanyia kazi kuliko magazeti twende na Hansard…..Jibu: Sawa.Swali: Naomba tuangalie taarifa yako ya Ukaguzi, page 15 ya Arabic. Naombakama hutajali utusomee.Jibu: “Kwa kuwa Ukaguzi Maalum haukupata uthibitisho wa kuwepo Taasisi 20zilizotakiwa kuchangia fedha zilizofikia one billion kama ilivyorekodiwa …”Niseme tu kwamba nafikiri hapa we erred.Swali: Kwa hiyo ilikuwa ni error?Jibu: Yah!49
(g) Kufuatia mahojiano na Waheshimiwa Wabunge na watendaji wa SerikaliKamati Teule iliridhika kwamba isingekuwa rahisi kwa wahojiwa haokubaini vitendo vya rushwa. Yawezekana hata Ukaguzi Maalum uliofanywana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali haukuweza kubainivitendo hivyo vya rushwa kwa sababu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi siyoChombo Mahsusi kwenye masuala ya rushwa. Utimilifu wa nadharia yakuwepo kwa rushwa katika zoezi hili kwa kutumia fedha zilizochangishwaungeweza kufikiwa endapo TAKUKURU kama Chombo cha Kisheria nachenye utaalam mahsusi​
(competent authority) katika masuala ya rushwawangehusishwa katika uchunguzi.(h) Kamati Teule pia ilibaini idadi kubwa ya Maofisa wa Wizara na Taasisiwaliohudhuria mchakato wa uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Bungeni.Kwa mujibu wa Dokezo Sabili la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
49​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
58​
Madini, Wizara ilipaswa kupeleka Maofisa 44 na Maofisa 17 kutoka Taasisizake na hivyo kufanya jumla ya Maofisa 61. Kinyume na agizo la KatibuMkuu wa Nishati na Madini, Kamati Teule imebaini ongezeko la Maofisa182 waliohudhuria mchakato wa Bajeti. Kama Bajeti ya uwasilishajiHotuba ilikuwa kwa watu 61 ni dhahiri kwamba kuna matumizi yasiyo yalazima ambayo ziada ya Maofisa 182 walilipwa.(i) Kufuatia mahojiano na Watendaji wa Wizara na Taasisi, Kamati Teuleinakubaliana na Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalikwamba hapakuwa na vikao vya maamuzi baina ya Wizara na Taasisi,wala Taasisi na Bodi kuhusiana na suala la michango, hivyo kukosekanakwa dhana ya ushirikishwaji. Hata hivyo, ni maoni ya Kamati Teulekwamba hata kama kungekuwa na ushirikishwaji bado kitendo chakuchangisha kingekuwa kinyume na utaratibu.(j) Katika kuchambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali, Kamati Teule ilibaini kuwa taarifa hii inaweza ikabadilika kwakuwa ilionekana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalihakukamilisha taarifa yake kwa maelezo ya kukosekana kwa vielelezo vyaziada. Katika mahojiano, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikalialikiri kuwa ni kweli kulikuwa na mashahidi walioahidi kuwasilisha kwakevielelezo vya ziada, jambo ambalo halikutimizwa hadi alipowasilishaTaarifa yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Ni dhahiri kuwa, endapomashahidi watawasilisha vielelezo vya ziada, Taarifa ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaweza kubadilika.​
50 Hata hivyo,kwa nyaraka hizo tu zilizopatikana na kuchambuliwa na Kamati Teulepamoja na mahojiano yaliyofanyika baina ya Kamati Teule na mashahidimbalimbali imebainika kwamba malengo ya uchunguzi kwa kiasi kikubwayamefikiwa.
50​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
59​
(k) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameeleza kwambamambo yaliyoibuliwa katika Ukaguzi Maalum yatazingatiwa katika ukaguziwa kawaida wa kisheria wa Fungu 58 kwenye ukaguzi wa Hesabuzilizoishia tarehe 30 Juni, 2011 na kujumuishwa kwenye Ripoti ya Ukaguziwa Wizara. Ni maoni ya Kamati Teule kwamba Kamati ya Bunge yaHesabu za Serikali ifuatilie utekelezaji wa maelezo haya itakapofikawakati wa kujadili Hesabu za Fungu 58 na Mafungu mengine.(l) Taarifa ya Ukaguzi Maalum imebainisha kuwa Wizara ya Nishati na Madiniilikusanya jumla ya Sh.​
418,081,500.0051 kupitia Akaunti Na. 5051000068ya GST. Kiasi hiki cha fedha kilikuwa ni kwa ajili ya kuwezesha uandaajina uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na MadiniBungeni tarehe 15 na 18 Julai, 2011. Mapokezi ya fedha hizi katikaakaunti ya GST yalikuwa kama ifuatavyo:-REA Sh. 50,000,000.00TANESCO Sh. 40,000,000.00TPDC Sh. 50,000,000.00Idara ya Mipango Sh. 278,081,500.00
JUMLA Sh. 418,081,500.00​
Kiasi hiki kina ziada ya Sh.211,081,500.00 kwa sababu fedha zilizokuwazikihitajika kwa ajili ya kukamilisha zoezi hili zilikuwa ni Sh.207,042,000.00.Aidha, uchambuzi wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum unabainisha zaidi kwamba katiya Sh.​
418,081,500.00, Sh.127,820,000.00 zilitumika kwa ajili ya malipo yaposho za vikao kwa Maofisa wa Wizara waliokuwepo Dodoma52. Fedha zilizobakibenki ni Sh.99,438,380.0053. Kwa maelezo yaliyotolewa hapo juu bakaa yafedha hizi ilipaswa kuwa Sh.290,261,500.00 badala ya kuwaSh.99,438,380.00. Kwa maana hiyo, Sh.190,823,120.00 bado hazijarejeshwabenki.
51​
Kifungu 3.7 Ukurasa wa 8, Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
52​
Jedwali Na. 6, Ukurasa wa 13, Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
53​
Kifungu 3.7, Ukurasa wa 8, Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
60​
Kamati Teule ililazimika kuitisha nyaraka zaidi kutoka Wizarani kwa sababuilibaini kwamba kwa kutumia Taarifa ya Ukaguzi Maalum peke yake kuna kiasicha fedha (Sh.​
190,823,120.00) ambacho hakijulikani kilivyotumika na walahakipo benki. Ni katika kuchambua nyaraka hizo ndipo Kamati Teule ilibainikwamba yapo matumizi mengine ambayo Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu zaSerikali hakuyabaini. Matumizi haya yanafafanuliwa zaidi katika Kipengele cha2.4 cha Taarifa hii.Kuhusu Sh.99,438,380.00 zilizorejeshwa kwenye akaunti ya GST baada yashughuli za kuwasilisha Bajeti, Kamati ilipata maelezo ya ziada kwambaSh.68,000,000.00 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Rest House naOfisi ya Waziri na Naibu Waziri, Dodoma. Kamati ilihoji pia uhalali wa kutumiafedha hizi kwa shughuli za ujenzi na kupata majibu kwamba GST iliandika baruaWizarani kwamba kuna mkandarasi ana madai ya siku nyingi ndipo Kaimu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akawapa kibali cha kulipaSh.68,000,000.00 kati ya Sh.99,438,380.00 zilizokuwa zimerejeshwa benki.54
3.3 Upungufu uliojitokeza katika Hitimisho la Katibu Mkuu KiongoziMheshimiwa Spika,​
Katika kupitia Taarifa ya Ukaguzi Maalum, Kamati Teule ilibaini kuwa KatibuMkuu Kiongozi hakuyatumia ipasavyo maudhui ya Taarifa hiyo katika hitimisholake. Mtazamo huu unatokana na sababu kwamba yapo masuala mbalimbaliambayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alistahili kupewa​
notice ilikuyajibu kwa taratibu za kiutumishi wa umma kama ifuatavyo:-(a) Kwa nini Wizara ilichangisha fedha kutoka kwenye Taasisi zilizo chini yakekwa ajili ya kuwezesha uandaaji na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti yakeBungeni wakati ilijua kwamba Taasisi hizo hazina kasma kwa ajili yauchangiaji huo?
54​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 12 Oktoba, 2011.
61​
(b) Kwa nini Wizara iliendelea kupokea michango na kuitumia wakatiupungufu wa fedha uliokuwepo tayari ulikwishaondolewa kwa kuletewafedha zake za OC?(c) Ni kwa nini Wizara haikuandaa vikao vya makubaliano miongoni mwaTaasisi zilizotegemewa kuchangia ili kuridhia kiasi cha kuchangia na mudawa kuchangia?Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alipaswa kuyatumia maudhui hayo kupima uhalaliwa utaratibu wa uchangishaji ulioendeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini. Ni kwa kufanya hivyo ambapo Katibu Mkuu Kiongozi angebaini kamakutenda jambo ambalo siyo halali ni kosa la kinidhamu au la kwa watumishi waumma! Bahati mbaya Katibu Mkuu Kiongozi alitoa hitimisho ambalo halikutokanana matokeo ya Ukaguzi Maalum kuhusu uhalali wa uchangishaji na matumizihalisi ya fedha zilizochangishwa. Kwa maana hiyo, hitimisho la Katibu MkuuKiongozi halikuwa sahihi.​
Mheshimiwa Spika,​
Hitimisho la Katibu Mkuu Kiongozi kwa Vyombo vya Habari alipotoa Taarifa yaMatokeo ya Uchunguzi wa Awali kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo: -​
“Sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma(notice) na Hati ya Mashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo,hajapatikana na kosa la kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibuwa Taarifa ya Ukaguzi Maalum”​
55
.
Hitimisho hili la Katibu Mkuu Kiongozi lilifuata baada ya maelezo ya utangulizikutolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (​
TazamaKiambatisho XIV) kwa Vyombo vya Habari kama ifuatavyo: -
55​
Katibu Mkuu Kiongozi, 23 Agosti, 2011. Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu Matokeo ya Uchunguziwa Awali.
62​
“Chimbuko la Ukaguzi huu Maalum lilijitokeza katika Kikao cha Bungekatika kujadili Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini tarehe 18 Julai2011. Katika kikao cha tarehe hiyo, Waheshimiwa Wabunge walihojiuhalali wa Wizara kuomba michango kutoka kwenye Taasisi zilizo chiniya usimamizi wake. Vile vile, Waheshimiwa Wabunge walihojimatumizi ya fedha hizo na kuzua hisia za rushwa zenye lengo lakuwashawishi baadhi yao ili Bajeti ya Wizara ipite kirahisi…Ukaguzi huu maalum ulifanyika kulingana na Hadidu za Rejeazilizokuwa na lengo la kutafuta ukweli kuhusu tuhuma za michango namatumizi ya fedha zilizokuwa zimechangwa na Wizara ya Nishati naMadini​
…
Ukaguzi Maalum umebaini kuwa idadi ya Taasisi zilizopelekewa baruaza kuchangia gharama za kuwasilisha Bungeni Bajeti ya Wizara ni nne(4) tu na siyo ishirini (20) kama tuhuma zilivyodai. Vile vile UkaguziMaalum umebaini ya kuwa jumla ya fedha zilizochangwa kutokakwenye Taasisi zilizochangishwa ni Sh.149,797,600 tu”.​
Mheshimiwa Spika,​
Kauli hizi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zinaeleza mamboya msingi kwamba, Ukaguzi Maalum ulijengwa katika misingi ya Hadidu za Rejeaalizokuwa amepewa na Katibu Mkuu Kiongozi. Hadidu za Rejea hizo zilikuwa nikuhusu Uhalali wa Uchangishaji na matumizi halisi ya fedha zilizochangishwa.Lakini hitimisho lililotolewa kwa Vyombo vya Habari halikuwa na maelezo yoyotekuhusu kilichobainika katika uhalali wa utaratibu na matumizi halisi ya fedhazilizochangishwa. Ndiyo maana Kamati Teule inasema Katibu Mkuu Kiongozihakupaswa kuizingatia Taarifa ambayo aliitoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali kwa Vyombo vya Habari tarehe 23 Agosti, 2011, badala yakealipaswa kuzingatia Taarifa kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kama ilivyowasilishwa kwake tarehe 9 Agosti, 2011 kwa sababu hiyondiyo Taarifa ya Msingi aliyoiomba kwa maandishi na ndiyo iliyokuwa na majibuya Hadidu za Rejea.​
63​
3.4 Maoni ya Kamati Teule Kuhusu Taarifa ya Ukaguzi MaalumMheshimiwa Spika,​
Baada ya kuipitia Taarifa ya Ukaguzi Maalum na kujiridhisha namna suala laKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini lilivyomfikia Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali, Mawanda yaliyoandaliwa kukidhi ukaguzi na namnahitimisho la Mamlaka ya Nidhamu lilivyotolewa juu ya suala lenyewe, KamatiTeule ina maoni yafuatayo: -(i) Mamlaka ya Nidhamu ilikuwa sahihi kumwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi Maalum juu ya suala hili kwamujibu wa Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 na kwaMujibu wa Kanuni ya 79(1) ya Kanuni za Ukaguzi wa Umma, 2009. Hivyo,tarehe 20 Julai, 2011 Katibu Mkuu Kiongozi aliiandikia Ofisi ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya uchunguzi kuhusu uhalali wamalipo yahusuyo mchakato wa kuwasilisha Bungeni Bajeti ya Wizara yaNishati na Madini 2011/12. Hadidu za Rejea zilizokuwemo katika baruahiyo ni kuchunguza uhalali wa michango hiyo na namna fedha hizozilivyotumika.(ii) Katika mahojiano na Kamati Teule, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali alisema kuwa Hadidu za Rejea zilikuwa mbili (Uhalali waMichango na Matumizi) na kwamba zile 15 zilizoorodheshwa katikaTaarifa ya Ukaguzi Maalum siyo Hadidu za Rejea bali ni taratibu. Bilakujali kama kulikuwa na Hadidu za Rejea 15 au taratibu 15, hitimisho laTaarifa ya Ukaguzi Maalum lilipaswa kueleza uhalali wa uchangishaji huo.(iii) Taarifa ya Ukaguzi Maalum haikuweza kuelezea matumizi ya fedhazilizokusanywa kwa ukamilifu, kwa kuwa kati ya Sh.418,081,500.00zilizokusanywa, Taarifa hiyo ilifafanua matumizi ya jumla yaSh.227,258,380.00 tu ambapo Sh.127,820,000.00 zilitumika kwa ajili yamalipo ya posho ya vikao na Sh.99,438,380.00 zilirejeshwa Benki.Matumizi haya yanaonyesha tofauti ya Sh.190,823,120.00 ambayo Taarifa​
64​
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali haikuielezea. Baadaya kubaini tofauti hii kubwa, Kamati Teule ikaitisha nyaraka na kufanyamahojiano na watendaji wa Wizara na hatimaye ikabaini matumizi yaziada kama ifuatavyo:posho ya Kujikimu Sh. 32,425,000.00Chakula na vinywaji Sh. 17,480,000.00Mafuta ya magari Sh. 5,754,000.00Vifaa vya kuandikia Sh. 625,020.00Takrima na viburudisho Sh. 8,494,600.00​
JUMLA Sh. 64,778,620.00​
Kiasi hiki cha Sh.64,778,620.00 kikitolewa kutoka kwenyeSh.190,823,120.00 kinabaki kiasi cha Sh.126,044,500.00 ambacho KamatiTeule ilikihoji pia kama inavyoonekana katika Kipengele cha 2.4 chaTaarifa hii.(iv) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alikuwa sahihi kurejeshaTaarifa ya Ukaguzi Maalum kwenye Mamlaka ya Nidhamu kwani ndiyoiliyomwomba. Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ya 81(a) ya Kanuni zaUkaguzi wa Umma, 2009, angeweza kukabidhi Taarifa hiyo kwa Mamlakanyingine ambayo angeona inafaa kuikabidhi.(v) Taarifa ya Ukaguzi Maalum imeweka wazi dosari zilizokuwepo ikiwa nipamoja na Wizara kuzitwisha Taasisi gharama za kuwasilisha Hotuba yaBajeti yake wakati Taasisi hizo hazina kasma mahsusi kwa ajili yakuchangia. Ukaguzi Maalum ulipaswa kutoa angalizo kwamba Wizarazinapokuwa hazina fedha za kutosha kutekeleza mipango yao zinapaswakuzingatia taratibu za kisheria mathalani Kanuni ya 4(4) ya Kanuni zaFedha za Umma, 2001. Ukaguzi Maalum ulipaswa pia kutumia kigezo chaWaraka Namba 3 wa Katibu Mkuu wa Hazina wa Mwaka 2011 kamamojawapo ya vigezo vya kupima uhalali wa utaratibu wa uchangishaji.​
65​
(vi) Katika sehemu ya ushauri na hitimisho, Taarifa ya Ukaguzi Maalumhaikuzingatia yaliyojitokeza ndani ya Taarifa ili kutoa majibu kwa Hadiduza Rejea badala yake ushauri pekee unaonekana kuegemea katika idadiya Taasisi kuwa 20 na kiwango cha fedha zilizochangwa kuwaSh.1,000,000,000.00. Hatua hii imesababisha upotoshaji mkubwa kwaKatibu Mkuu Kiongozi ambaye naye alitumia ushauri huu kama msingi waMaamuzi yake katika Uchunguzi wa Awali alioufanya. Hata hivyo baadaya kukabidhiwa, Katibu Mkuu Kiongozi alipaswa kuitumia Taarifa yaUkaguzi Maalum kwa ujumla wake badala ya kipengele cha ushauriambacho ni upotoshaji.​
66​
4.0 MFUMO WA SERIKALI KUJIBU HOJA ZINAZOTOLEWA BUNGENIMheshimiwa Spika,​
Hadidu ya Rejea ya Tatu iliitaka Kamati Teule kufanya yafuatayo:-(a) kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu Hoja zinazotolewa Bungeni nataratibu za kuliarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa Hoja hizo.(b) kuchunguza usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozikwa suala la Ndugu David Kitundu Jairo, Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini.(c) kubaini kama utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka yaBunge.Katika kushughulikia Hadidu hii, Kamati ilifanya yafuatayo:-(a) kupitia Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge.(b) kufanya mahojiano na mashahidi wa aina mbalimbali.​
4.1 Misingi ya Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge kwa Hoja zinazotolewaBungeniMheshimiwa Spika,​
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sura ya 2inaelekeza kuwa, Bunge ndicho Chombo Kikuu cha Jamhuri ya Muunganoambacho kina madaraka kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauriSerikali ya Jamhuri ya Muungano na Vyombo vyake vyote katika kutekelezamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba. Katika kutekeleza madaraka yakeBunge linaweza: -​
67​
(a) kumuuliza Waziri yeyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katikaJamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kilamwaka wa Bajeti;(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa mudamfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano; nakutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;(d) kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo Sheria;(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano naambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.​
56
Ibara ya 89(1) imetoa mamlaka kwa Bunge kutunga Kanuni za Kudumukwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake. Kwa sasaBunge linatumia Kanuni za Bunge, Toleo la Mwaka 2007.4.2​
Mheshimiwa Spika,
Kanuni za Bunge zinaweka wazi kuwa zipo Hoja zifuatazo:-(a) Hoja za Serikali ambazo hutolewa na Mawaziri kupitia njia kadhaa kamavile Miswada ya Sheria na Makadirio ya Matumizi (Hotuba za Bajeti).(b) Hoja Binafsi zitolewazo na Kamati kama vile Miswada Binafsi ya Sheria auMarekebisho ya Miswada ya Sheria ya Serikali.(c) Hoja Binafsi ambazo hutolewa kupitia Miswada Binafsi ya Wabunge nawakati wa mijadala kama vile kurekebisha Muswada uliowasilishwaBungeni, kubadilisha Makadirio ya Matumizi wakati wa Kamati ya​
56​
Ibara ya 63 (2) na (3).
68​
Matumizi, “kutoa shilingi” katika Bajeti ya Wizara, kuahirisha shughuli zaBunge zinazoendelea ili kujadili jambo linalohusiana na haki za Bunge.(d) Hoja ambazo zinaweza kutolewa na Mbunge au Waziri kama vilekutengua Kanuni, kuahirisha mjadala unaoendelea Bungeni, kuahirishashughuli za Bunge zinazoendelea ili kujadili jambo la dharura n.k​
57.4.3 Mheshimiwa Spika,
Kama Katiba inavyoelekeza, Wabunge hujadili utekelezaji wa kila Wizarawakati wa Mikutano ya Bajeti. Kanuni za Bunge zinaainisha taratibu za kujadiliutekelezaji wa kila Wizara kwamba: -(a) Mjadala huanza kwa Waziri kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Wizarayake na kuomba Bunge liyapitishe.(b) Wabunge hupata nafasi ya kuchangia mmoja mmoja ambapo masualambalimbali huibuliwa.(c) Mjadala ukimalizika Waziri mhusika hupata nafasi ya kuhitimisha Hojayake kwa kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyojitokeza.(d) Bunge huingia katika hatua ya Kamati ya Matumizi ambapo Wajumbehuhojiwa Kifungu kimoja baada ya kingine na kukipitisha.​
58
Iwapo Mbunge aliuliza au kuzungumzia suala fulani wakati wa kuchangiamjadala wa jumla na Waziri hakulijibu au hakulijibu kikamilifu wakatianahitimisha Hoja yake, Mbunge huyo anaweza akahoji tena wakati wa Kamatiya Matumizi na asiporidhika na ufafanuzi wa Waziri ndipo taratibu za “kutoashilingi” zinaweza kufuata.​
57​
Kanuni ya 53 na 55, Kanuni za Bunge, Toleo la 2007.
58​
Kanuni ya 99 na 100, Kanuni za Bunge, Toleo la 2007.
69​
4.4 Suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ndugu David KitunduJairoMheshimiwa Spika,​
Kama ilivyoelezwa hapo awali wakati Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.)anachangia alihoji uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madinikuzichangisha fedha Taasisi zilizo chini yake kwa ajili ya kufanikishamawasilisho ya Bajeti.Mitazamo ya watu waliohojiwa na Kamati Teule inatofautiana kuhusiana naiwapo suala hili lilikuwa Hoja mahsusi ambayo ilitakiwa kujibiwa na Serikali.Kundi la Kwanza lina msimamo kwamba katika suala la Ndugu David KitunduJairo hakukuwa na Hoja mahsusi ya Bunge ambayo Serikali ilitakiwa irudiBungeni kuelezea utekelezaji wake kwa sababu liliondolewa Bungeni nakupelekwa katika mamlaka za juu ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kiutawala.Kundi la Pili lina msimamo kwamba suala hilo lilikuwa ni Hoja ambayo Serikaliilitakiwa kurudisha Bungeni majibu ya utekelezaji wake.​
Mheshimiwa Spika,​
Waliotoa maoni katika Kundi la Kwanza wanaeleza kwamba ili Bunge liazimiekuwa suala fulani liende Serikalini ni lazima liwe katika mfumo wa Azimio laBunge ndipo Serikali itabanwa na Ibara ya 63(2) kurudi Bungeni kulitoleamajibu. Lakini kwa suala la Ndugu David Jairo, Bunge halikuazimia kwambabaadaye Serikali irudi Bungeni kutoa majibu ya Serikali, hivyo hakukuwa naHoja.​
59
Mheshimiwa Spika,​
Wachangiaji katika Kundi la Kwanza waliendelea kusema kuwa shughuli zaBunge zinakwenda kwa misingi ya Hoja. Hoja inawasilishwa, inaungwa mkono,inajadiliwa na kisha inaamuliwa, na kama suala linahusu Serikali, basi Serikaliinaliahidi Bunge kuwa italifanyia kazi na kutaja muda (​
time frame).
59​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 3 Oktoba, 2011.
70​
Kwamba kilichojitokeza Bungeni tarehe 18 Julai, 2011 wakati Wizara ya Nishatina Madini imewasilisha Makadirio yake ni Hoja za Wabunge wengi kuwa Serikalihaijaonyesha umakini wa kutatua tatizo la umeme katika kipindi cha mudamfupi. Ndipo Waziri Mkuu akatumia busara kuomba Hoja ya Waziri wa Nishatina Madini iahirishwe ili Serikali irudi kwenye​
drawing board. 60
Mheshimiwa Spika,​
Wakifafanua zaidi walisema kuwa Hoja zote zinazotolewa Bungeni zinaanzakwa kuwasilishwa, kuungwa mkono, kujadiliwa na mwisho wake Bungelinafanya Maamuzi. Suala la Ndugu David Kitundu Jairo lilizuka wakati Hoja yaWizara ya Nishati na Madini inajadiliwa. Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.)hakutoa Hoja binafsi, ilikuwa ni sehemu ya majadiliano ya Hoja ya Wizara.Mmoja wao alisema: -​
“… Waziri Mkuu hakusema naomba kutoa Hoja kwamba jambo hililiende sasa kwa Mheshimiwa Rais atakapolishughulikia litaletwa hapaBungeni ili lifanyiwe uamuzi au liletewe taarifa …”​
Mheshimiwa Spika,​
Waliotoa maoni katika Kundi la Pili walieleza kwamba, kwa kuwa suala lamichango liliibuka Bungeni, Waziri Mkuu akaomba kuliondoa na akakubaliwa naWabunge karibu wote waliokuwemo Bungeni, hivyo hilo ni Azimio toshalililohitaji kutolewa majibu na Serikali. Katika kufafanua zaidi, mmoja waoalisema: -​
“… hili jambo limetoka kwenye vinywa vya watu na likasikika nchinzima, yule mwananchi wa kawaida aliyesikia hajui juu ya utaratibuwako huo kwamba Azimio lazima liungwe mkono, watu wasimamekumi hajui, lakini anachojua; je, utaratibu ule ni wa kawaida?Unapaswa kuendelea au haupaswi kuendelea?”​
61
60​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 23 Septemba, 2011.
61​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 13 Oktoba, 2011.
71​
Mheshimiwa Spika,​
Mtaalam mwingine aliyebobea katika masuala ya Bunge alisema kuwakinachozungumzwa Bungeni na Hoja za Wabunge zinazotolewa wakati wamijadala mbalimbali huelekezwa kwa Serikali ambayo nayo imo Bungeni, hivyoSerikali hutakiwa kutoa majibu humo humo Bungeni.Wakisisitiza kuhusu msimamo wa Kundi la Pili, baadhi yao walisema kwambandani ya Bunge kuna mambo mengi yanayoibuliwa, lakini siyo lazima Wabungewanyanyuke na kuunga mkono kila jambo. Kwa suala la Mhe. BeatriceShellukindo, (Mb.) walifafanua kwa kusema: -​
“… Kauli aliyoitoa Mheshimiwa Beatrice Shellukindo, (Mb.) nadocument aliyoitoa mbele ya Bunge, it was enough evidencekuonekana kwamba Serikali lazima i-intervene katika hilo tendo, kwavyovyote vile usingengoja tena Hoja ile ipanuliwe zaidi… Serikali iliyomakini ikisoma mood ya Wabunge, Msimamizi Mkuu wa Shughuli zaSerikali Bungeni anaweza akalichukua kama Bunge lina-demand hilijambo, bila ya kuingia utaratibu wa kuungwa au kutoungwa mkono…”​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati hii imepitia Kanuni zinazoainisha Hoja zinazotolewa Bungeni. Zipo Hojaambazo kabla ya kuwasilishwa Bungeni zinapelekwa kwanza kwenye Kamatiinayohusika na zile ambazo hazipelekwi kwenye Kamati ya Bunge. Taratibu zakuwasilisha, kujadili na kupitishwa kwa Hoja za namna hii zimefafanuliwakatika Kanuni ya 53(6) na (7) kama ifuatavyo: -(a) Hoja kutolewa na kuungwa mkono.(b) Maoni ya Kamati husika.(c) Maoni ya Kambi ya Upinzani au Serikali kama Hoja ni ya Kambi yaUpinzani.(d) Mjadala wa jumla.(e) Uamuzi wa Bunge.​
72​
Hata hivyo, wakati wa kuchangia mijadala mbalimbali Bungeni au kupitiaMaelezo Binafsi ya Wabunge, Wabunge huibua masuala muhimu ambayo kwauzito wake Serikali hulazimika kuyatolea ufafanuzi hapo hapo au kutoa ahadi yakufuatilia au kulitolea maelezo mahsusi siku nyingine kupitia Kauli za Mawaziri.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imebaini kuwa ipo mifano kadhaa ya kuthibitisha hili kamaifuatavyo: -(a) Mwaka 2011 katika Mkutano wa Bunge la Bajeti, Wabunge mbalimbaliwaliochangia walionyesha kutoridhishwa na ufinyu wa Bajeti ya Wizaraya Uchukuzi na matatizo ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).Waziri Mkuu alilazimika kutumia sehemu ya Kipindi cha Maswali kwaWaziri Mkuu tarehe 4 Agosti, 2011 kuliarifu Bunge kuwa Serikaliimechukua hatua zifuatazo: -(i) imeongeza Sh.95,000,000,000.00 katika Bajeti ya Wizara yaUchukuzi; na(ii) imewaagiza CAG, DCI na TAKUKURU waanze uchunguzi mara mojakuhusiana na UDA.Kwa maneno yake, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda alisema: -​
“… yaliyojitokeza ni mambo ambayo yameonyesha uzito na sisiSerikalini tukaona pengine ni vizuri …tuyaweke bayana mambofulani fulani …jana, Serikali ililazimika kukutana na kuangaliauwezekano wa kuongeza Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi…kukutana kwa Serikali ilikuwa ni muhimu ili kuweza kujadilimichango mingi mizuri iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge...Kikao cha jana kimewezesha Serikali kufanikiwa kupata fedhakiasi cha Shilingi bilioni 95 ambazo zitatumika katika maeneoya Reli ya Kati, Kampuni ya Ndege Tanzania na Usafiri wa​
73​
Majini yaani Meli katika Maziwa ya Victoria, Tanganyika naNyasa......suala lingine lililoongelewa kwa hisia kali na WaheshimiwaWabunge ni matatizo ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).Serikali imesikia kilio cha Waheshimiwa Wabunge na kwa sasaimeshawaagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kudhibitina Kupambana na Rushwa kuanza uchunguzi mara moja…​
62”
(b) Wakati huo huo wa Mkutano wa Bajeti mwaka 2011 Wizara ya Ardhi naMaendeleo ya Makazi nayo ilionekana kuwa imetengewa fedha kidogo naWaheshimiwa Wabunge wengi waliochangia walilalamikia hali hiyo kuwakiasi cha fedha kilichotengwa hakiendani na hali halisi na changamotozinazoikabili Wizara hiyo. Baada ya mjadala wa jumla kukamilika WaziriMkuu, Mhe. Mizengo Pinda, (Mb.) alisimama na kuliarifu Bunge kuwakutokana na michango ya Waheshimiwa Wabunge, Serikali imeruhusuWizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi badala ya kuzipeleka MfukoMkuu wa Hazina fedha ambazo Wizara itazikusanya, Wizara hiyo izitumiefedha zote kwa ajili ya shughuli za Wizara. Waziri Mkuu alisema: -​
“…Michango ya Waheshimiwa Wabunge imegusa maeneo karibuyote ambayo ndiyo kero hasa kwa Watanzania. (Waziri waArdhi na Maendeleo ya Makazi) amepata Bajeti ndogo kulikohata mwaka jana… jana tukiwa kwenye Cabinettumemwidhinishia huyu mama kwamba wewe mama ile fedhayote ambayo utakuwa unakusanya kutokana na shughuli zakoza ardhi baki nayo yote, chukua yote ikusaidie wewe katikauendeshaji wa Wizara hiyo…”​
62​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 4 Agosti, 2011.
74​
Katika mifano yote hii utaratibu wa kuwasilisha Hoja, kuungwa mkono,kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge haukufanyika, lakini kutokana nauzito wa masuala husika Serikali iliyafanyia kazi na kuliarifu Bunge.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imeridhika kuwa suala lililoibuliwa Bungeni na Mhe. BeatriceShellukindo, (Mb.) lilikuwa ni Hoja ambayo kwa uzito wake na kwa hisiazilizotawala mjadala huo, Serikali ilitakiwa kuifanyia kazi na kuitolea taarifa yautekelezaji Bungeni hata kama haikushughulikiwa kufuatana na masharti yaKanuni ya 53 na 54 ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007.​
75​
5.0 USAHIHI WA UTARATIBU ULIOTUMIWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI KWASUALA LA KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, NDUGU DAVIDKITUNDU JAIRO5.1 Taratibu za Kuliarifu Bunge chini ya Katiba, Sheria na Kanuni za Bunge naMisingi ya Utawala BoraMheshimiwa Spika,​
Kwa mujibu wa Katiba, Bunge lina sehemu mbili; Rais na Wabunge.​
63 Sehemuya Pili ya Bunge (National Assembly) ina Wabunge wa kawaida na Mawaziriambao ndio wawakilishi wa Serikali. Hoja na kauli zote zinazotolewa naWabunge katika kutekeleza majukumu yao Bungeni huelekezwa kwa Serikaliambayo nayo imo Bungeni. Vile vile Serikali hulazimika kujibu na kufafanuamasuala yote yanayoibuliwa na Wabunge ndani ya Bunge hata kama masualahayo yamewagusa moja kwa moja Watendaji wa Serikali ambao hawamoBungeni.
Mheshimiwa Spika,​
Kanuni za Bunge zinaweka wazi utaratibu ambao Hoja za Wabunge zitajibiwana Serikali. Kama ilivyoelezwa hapo awali, Hoja za Wabunge zinapotolewawakati wa Mijadala huweza kujibiwa papo kwa papo na Waziri yeyote auMwanasheria Mkuu wa Serikali; na pia Serikali inaweza kutumia utaratibu wa​
Kauli za Mawaziri​
kujibu Hoja za Wabunge pale inapoonekana suala fulanilimejitokeza na linahitaji kupatiwa majibu.
63​
Ibara ya 63.
76​
Kanuni ya 49 inayohusu Kauli za Mawaziri inasomeka:​
“49: (1) Waziri anaweza kutoa kauli Bungeni kuhusu jambo lolotelinaloihusu Serikali.(2) Kauli za aina hiyo zinaweza kutolewa kwa idhini ya Spikakatika wakati unaofaa kufuatana na mpangilio wa Shughuliza Bunge na zitahusu jambo mahsusi, halisi na zisizozuamjadala na muda wa kusema utakuwa ni dakika zisizozidithelathini.(3) Waziri mwenye kutoa kauli atawajibika kutoa nakala yakauli yake kwa Wabunge wote wakati anapoiwasilishaBungeni.”​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wa Hoja za Wabunge zinazotolewa wakati Bunge linajadiliutekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bajeti, Serikali ina nafasimbili za kujibu Hoja hizo. Kanuni ya 99(9) inaelekeza kwamba, mudauliotengwa kwa ajili ya majadiliano utakapokaribia kwisha Waziri mtoa Hojaatapewa muda wa dakika 60 kuhitimisha Hoja yake kwa kujibu masualayaliyojitokeza kutokana na michango ya Wabunge.Aidha, wakati wa Kamati ya Matumizi Serikali pia inapata nafasi ya kufafanuamasuala mbalimbali kama yalivyohojiwa na Wabunge.​
64
64​
Kanuni ya 101 na 103.
77​
Mheshimiwa Spika,​
Tarehe 13 Agosti, 2011 wakati Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. WilliamNgeleja, (Mb.) anahitimisha Hoja yake hakuligusia kabisa suala la Ndugu DavidKitundu Jairo. Vile vile, katika Kamati ya Matumizi Mhe. Beatrice Shellukindo,(Mb.) alipata nafasi ya kuomba ufafanuzi, lakini alizungumzia masuala menginebila kugusia suala la Ndugu David Kitundu Jairo. Pia hakukuwa na Mbungemwingine yeyote aliyezungumzia suala hilo.​
65
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imeridhika kwamba, kitendo cha Bunge kutohoji tena suala laNdugu David Kitundu Jairo wakati wa Kamati ya Matumizi kilitokana na Bungekuheshimu misingi ya utawala bora kwamba si vema Mhimili mmoja kuingiliakati kwa kujadili suala ambalo linafahamika wazi kuwa linafanyiwa kazi naMhimili mwingine, kwa kuwa: -(a) tayari kulikuwa na kauli na ombi la Waziri Mkuu kuwa Serikali ipewemuda wa kulifuatilia suala husika;(b) tayari Katibu Mkuu Kiongozi alikwishatoa Taarifa kwa umma kuwaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amepewa kazi yakufanya Uchunguzi wa Awali kwa madai yaliyotolewa Bungeni;(c) hadi siku hiyo tarehe 13 Agosti, 2011 wakati Bunge lilipokuwalinahitimisha Hoja ya Waziri wa Nishati na Madini hakukuwa na taarifayoyote kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alikuwaamemaliza kazi yake;​
66
(d) Bunge lilikuwa na uhakika kwamba Serikali itakapokamilisha taratibuzake litaarifiwa rasmi.​
65​
Hansard ya Kikao cha 46, Mkutano wa Nne wa Bunge, tarehe 13 Agosti, 2011.Ukurasa wa 277 – 278.
66​
Japokuwa Kamati Teule ilibaini kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alipokea Taarifa ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali tarehe 9 Agosti, 2011.
78​
5.2 Usahihi wa Utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Ndugu PhilemonLuhanjoMheshimiwa Spika,​
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 na Kanuni za Utumishi waUmma, 2003 Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishiwote wanaoteuliwa na Rais.​
67 Watumishi hao wameorodheshwa katika Kifungucha 5(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 wakiwemo Makatibu Wakuu.Katika Utumishi wa Umma kuna makosa ya kinidhamu ya aina mbili nayametajwa katika Kanuni ya 41 kama ifuatavyo: -(a) Makosa mazito ambayo mtumishi akipatikana na hatia anaweza kupewaadhabu ya kufukuzwa kazi, kushushwa cheo au kupunguzwa mshahara(formal proceedings)68;(b) Makosa mepesi ambayo mtumishi akipatikana na hatia anaweza kupewaadhabu ya onyo au karipio (summary proceedings).69
Mheshimiwa Spika,​
Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma vinaelekeza kwamba kabla Mamlaka yaNidhamu haijachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi wa umma mamlakahiyo itawajibika kufanya Uchunguzi wa Awali ili kujiridhisha kuwa mtumishi waumma mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.Kanuni ya 36 inasomeka kama ifuatavyo: -“​
Where it is necessary to institute disciplinary proceedings against apublic servant, the Disciplinary Authority shall make preliminaryinvestigations before instituting disciplinary proceeding.”
67​
Kifungu 4(3) (d) na Kanuni ya 35 (2)(a).
68​
Kanuni ya 42(1).
69​
Kanuni ya 43(1) na (2).
79​
Madai haya yanaweza kuwa yamemfikia ama kwa kupelekwa kwake rasmi auameamua mwenyewe kuyafanyia kazi (​
suo motto) kwa kuwa yamezungumzwakatika forum fulani na yanaonekana kuchafua hadhi ya Serikali.Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma endapo Uchunguzi wa Awaliutathibitisha kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu itafuatia hatua ya mtumishihuyo kupewa hati ya mashitaka na Mamlaka ya Nidhamu itaanzisha Kamati yaUchunguzi (Inquiry Committee) kwa hatua zinazofuata.70
Mheshimiwa Spika,​
Katika kuchambua Sheria na Kanuni zinazotawala, Kamati Teule imebainiyafuatayo: -(a) Katibu Mkuu Kiongozi ana mamlaka kisheria ya kuanzisha na kukamilishamchakato wa kinidhamu kwa Makatibu Wakuu. Aidha, Uchunguzi waAwali ungethibitisha kuwa Ndugu David Kitundu Jairo ana kesi ya kujibu,Kamati ya Uchunguzi ingeundwa na kama ingethibitisha tuhuma, Kanuniya 48(6) imeelekeza kwamba: -​
“Upon receipt of the record of proceedings and the report, theDisciplinary Authority after considering the evidence and suchreport of the Committee, shall make and record findingswhether or not in his opinion, the accused public servant isguilty of the disciplinary offence with which he was charged,and shall inform the accused public servant of the decisionwithin a period of thirty days.”​
(b) Sheria na Kanuni havijaainisha iwapo Katibu Mkuu Kiongozi, kabla yakutoa maamuzi yake kama Mamlaka ya Nidhamu anatakiwa kupelekataarifa yake kwa Mamlaka nyingine yoyote.​
70​
Kanuni ya 44 – 48.
80​
Mheshimiwa Spika,​
Baada ya kupitia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, kupitia Nyarakakadhaa na kufanya mahojiano na watu mbalimbali, Kamati Teule ina maoniyafuatayo: -(a) Pamoja na kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ni Mamlaka ya Nidhamu kwaNdugu David Kitundu Jairo ni wazi kuwa alichukua hatua ya kuanzishaMchakato wa Awali kutokana na Hoja za Wabunge tofauti na masualamengine ya kinidhamu yanayoanzia kwenye mkondo wa kiutumishi waUmma. Hivyo basi, baada ya kukamilisha Uchunguzi wa Awali, kwabusara ya kawaida Katibu Mkuu Kiongozi alipaswa kumshirikisha WaziriMkuu ili kukubaliana namna bora zaidi ya kuliarifu Bunge.(b) Hoja zote zinazotolewa Bungeni huelekezwa kwa Serikali na zinatakiwakujibiwa Bungeni na Serikali hata kama suala husika linahusu Mtendajiwa Serikali nje ya Bunge. Hata suala la Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini lilielekezwa kwa Serikali hivyo lilitakiwa kujibiwa naSerikali, Bungeni.(c) Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Mamlaka ya Nidhamu kwa Makatibu Wakuuhaiondoi ukweli kuwa Waziri Mkuu pamoja na kusimamia Mawaziriwengine Bungeni, yeye ni kiungo kati ya Wabunge na Watendaji wote waSerikali nje ya Bunge.Aidha, Waziri Mkuu alitoa Kauli Bungeni kuwa Serikali italifanyia kazisuala la Ndugu David Kitundu Jairo na ahadi hii ya Serikali ndiyoiliwezesha “hali ya hewa” Bungeni kutulia. Hivyo, Waziri Mkuu alikuwana wajibu wa kurudi Bungeni kutoa taarifa ya utekelezaji wa suala hilona hadi sasa hajafanya hivyo.(d) Katika misingi ya Utawala Bora, licha ya kwamba dhana ya Mgawanyo waMadaraka (​
Separation of Powers) inataka Mihimili isiingiliane katika kazi,ni muhimu Mihimili hiyo iheshimiane na kushirikiana.
81​
5.3 Kubaini kama Utaratibu huo Umeathiri Dhana ya Haki na Madaraka ya Bunge5.3.1 Dhana ya Haki na Madaraka ya BungeMheshimiwa Spika,​
Dhana ya “haki za Bunge” ni pana. Waandishi mbalimbali wa masuala yaKibunge wamewahi kutoa tafsiri ya dhana hii. Mmoja wa Waandishi hawa niKaul ambaye amefafanua maana ya “​
haki za Bunge” kama ifuatavyo: -
“In parliamentary language, the term “privilege” applies to certainrights and immunities enjoyed by the House of Parliament andCommittees of the House collectively and by Members of the Houseindividually. The object of parliamentary privilege is to safeguardthe freedom, the authority and the dignity of Parliament. Privilegesare necessary for the proper exercise of the functions entrusted toParliament by the Constitution”​
.
71
Madaraka na haki za Bunge la Tanzania vimeainishwa katika Ibara ya100(1) na (2) ya Katiba inayosomeka kama ifuatavyo:-​
“​
100 (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibukatika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa naChombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katikaMahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya Sheria nyingineyoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa aukufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana najambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge aualilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, Muswada, Hoja auvinginevyo.”
71​
M.N. Kaul – Shri S. L. Shakdher, Practice and Procedure of Parliament, 4th Ed. 1995 p. 193.
82​
Mheshimiwa Spika,​
Ibara ya 101 inalipa Bunge uwezo wa kutunga Sheria ili kuhifadhi na kutilianguvu uhuru wa majadiliano na shughuli za Bunge kwa ujumla kamainavyotakiwa na Ibara ya 100. Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge,Sura ya 296​
(The Parliamentary Immunities, Powers and Privileges Act, Cap296) na Kanuni za Bunge zimetaja baadhi ya haki na kinga hizo kamaifuatavyo:-(i) Haki ya kutoa adhabu,(ii) Kuweka utaratibu wa namna ya kujiendesha,(iii) Kulinda mamlaka na heshima ya Bunge na(iv) Kulinda uhuru wa mawazo.Hivyo, haki za Bunge kama Taasisi na Mbunge mmoja mmoja zimelindwakikatiba na kisheria. Aidha, pamoja na Katiba, Sheria na Kanuni kutaja haki nakinga za Wabunge imekubalika miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Madolakwamba haki na kinga hizo hazijitoshelezi (not exhaustive) hivyo katikakushughulikia suala hili mila, desturi na mazoea ya Mabunge ya Commonwealth
zitafuatwa.Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Frederick M. Werema katikakukubaliana na hilo alisema: -​
“Haki za Bunge hazipo exhaustive kwenye Sheria. Yaani ukisomaSheria unachoona kwenye Sheria siyo haki zote za Kibunge. Kunanyingine zinatokana na desturi na mazoea ya Mabunge haya yaCommonwealth”.​
72
72​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 3 Oktoba, 2011.
83​
Mheshimiwa Spika,​
Suala hili la haki zote kutopatikana kwenye Sheria lilizungumziwa pia naMwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Mhe. Andrew Chenge, (Mb.) ambayealifafanua kuwa Waandishi wengi wa masuala ya Katiba kwenye eneo hiliwamekubaliana kwamba huwezi kukuta haki zote zimeainishwa (​
codified) nandiyo hali ilivyo sasa ukiangalia katika nchi nyingi za Jumuiya ya Madola. Kwamaneno yake Mhe. Andrew Chenge, (Mb.) alisema: -
“…. there is no closed list ya classes ya makosa ambayo Bungelinaweza kusema umenifanyia, huwezi kusema ni haya tu, ukafungamlango. Mazingira yanabadilika na yanakuwa very dynamic, mamboambayo ulitegemea jana yasiathiri haki na madaraka ya Bunge, leoyanaweza kuja katika sura tofauti yakawa.”​
73
Kamati Teule imeona kwamba Kifungu cha 12(1) cha Sheria ya Haki, Kinga naMadaraka ya Bunge, Sura ya 296 kinaakisi Hoja hizi na kinasomeka:​
“…. Subject to the Constitution and the Standing Orders of theAssembly, the Assembly has all such powers and jurisdiction as maybe necessary for inquiring into, judging and pronouncing upon thecommission of any Act, matter or thing, not amounting to an offenceunder this Act, which is a breach of Parliamentary privileges.”​
Kwa hiyo, suala la haki za Bunge kimsingi limeachwa kwa Bunge lenyewekuamua ni mambo gani yakifanyika yatasababisha Bunge na Wabunge kuvunjiwahaki zao kwa kutegemea mazingira ya wakati husika bila kuathiri masharti yaKatiba.​
73​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 23 Septemba, 2011.
84​
5.3.2 Iwapo Utaratibu Uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi umeathiri Dhanaya Haki na Madaraka ya BungeMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imebaini kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002na Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 baada ya Kiongozi wa Shughuli zaSerikali Bungeni kuahidi kulishughulikia suala hili, utaratibu uliotumiwa naKatibu Mkuu Kiongozi kulichunguza ni sahihi.Baada ya Katibu Mkuu Kiongozi kukamilisha Uchunguzi wa Awali, utaratibualioutumia wa kutoa taarifa ya matokeo ya Uchunguzi huo kupitia Vyombo vyaHabari na maneno aliyotumia wakati wa uwasilishaji wa matokeo ya Uchunguziwa Awali ndiyo yaliyosababisha hisia ya kuingiliwa kwa dhana ya haki namadaraka ya Bunge. Aidha, Mapokezi ya Ndugu David Kitundu Jairo KatibuMkuu Wizara ya Nishati na Madini siku aliporudi kazini nayo yalichangia kujengasura ya ushindani na mapambano baina ya Mihimili miwili ya Dola,​
Mheshimiwa Spika,​
Kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi kutoa Taarifa ya Uchunguzi kupitia kwenyeVyombo vya Habari kimeibua makundi mawili, moja likisema kimeathiri nalingine likisema hakijaathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.Msingi wa mtazamo wa Kundi la Kwanza ni kwamba hapakuwa na Hoja mahsusiya kutaka taarifa hiyo irudishwe Bungeni.Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Frederick Werema katika hilianasema: -​
“utaratibu huu sioni kama umeathiri dhana ya haki na madaraka yaBunge kwa sababu nilivyoelewa ni kwamba kulikuwa hamna Hojaambavyo iliamuliwa na Bunge ambayo Bunge lilitaka lijulishweSerikali imefanya nini.”​
74
74​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 3 Oktoba, 2011.
85​
Mtaalam mmoja wa masuala ya Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,alifafanua kwamba, kwa sababu Katibu Mkuu Kiongozi hakuagizwa na Bunge,kisheria hakulazimika kuripoti Bungeni ingawa kisiasa ingefaa aripoti. Kwahiyo, kama amedhalilisha heshima ya Bunge ni kisiasa na sio kisheria. Alisisitizakwa kusema: -​
“I think he had a political responsibility at least to inform you theresults.”​
75
Mmoja wa Makatibu wa Bunge Wastaafu, akifafanua suala hilo alisema, kitendohicho hakijaathiri dhana hiyo kwa vile Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa anafanyauamuzi ambao ulikuwa na maslahi kwa Umma. Kwa hiyo, Umma nao ulikuwa nahaki ya kujua na vile vile Katibu Mkuu Kiongozi hana mamlaka ya kwendaBungeni na hapa alisisitiza kwa kusema: -​
“Chief Secretary hana kitu tunakiita locus stand ya yeye kujaBungeni … anaye-appear Bungeni ni Waziri Mkuu… yeye hawezi kujakutoa taarifa Bungeni, lakini kutoa sehemu nyingine anatoa kwamujibu wa mamlaka aliyonayo.​
” 76
Mheshimiwa Spika,​
Kundi la Pili lina msimamo kwamba kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi kutoamaelezo kwenye Vyombo vya Habari huku akifahamu wazi kuwa Serikali kupitiaWaziri Mkuu imetoa ahadi Bungeni, kimeathiri haki ya Bunge ya kupata taarifana zaidi kama Waziri Mkuu hakufahamishwa naye hakutendewa haki kwa vilekauli yake aliyoitoa Bungeni mpaka sasa haijatimizwa ndani ya Bunge.​
75​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 12 Septemba, 2011.
76​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 21 Septemba, 2011.
86​
Akisisitiza hili, mmojawapo wa Mawaziri alikuwa na haya ya kusema: -​
“…. Waziri Mkuu hakutendewa haki, kwamba maneno yale yaSerikali hakuyasema majibu yake ambayo alipaswa kuyatoa yeyeBungeni hakupata nafasi ya kuyasema… na Waheshimiwa Wabungekwa sababu walimtegemea Waziri Mkuu awajulishe kwanza, yaaniwananchi wapate taarifa ile kupitia Bunge. Kwa hiyo, naohawakutendewa haki.”​
77
Spika Mstaafu, Mhe. Pius Msekwa akikubaliana na Hoja kwamba kitendo hichokimeathiri haki za Bunge alisema: -​
“… kwa hiyo, utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwamaoni yangu ulikiuka taratibu za mfumo wa Bunge kuihoji Serikali naSerikali kujibu Hoja hizo … Hoja za Wabunge zinaelekezwa kwaSerikali iliyoko ndani ya Bunge.”​
78
Mhe. Pius Msekwa alimalizia kwa kusema, kitendo cha maamuzi kutolewa nakutekelezwa kabla ya Taarifa kurudishwa Bungeni, hapo ndipo dhana ya haki zaBunge ilikiukwa.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule iliwasiliana na Katibu wa Bunge la Uingereza (​
House of Commons)kwa kuwaandikia barua kutaka kupata uzoefu wao katika changamoto kama hii.Katika majibu yake, Katibu wa Bunge aliweka wazi ukweli kwamba katika sualala mawasiliano baina ya Bunge na Serikali, hakuna Serikali yoyote makiniambayo itaruhusu mawasiliano kati yake na Bunge kwa namna ambayo italiudhiBunge, kwamba:
“…it is rarely good policy for any government to act in a way thatannoys Members of the Legislature…​
79”
77​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 13 Oktoba, 2011.
78​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 23 Septemba, 2011.
79​
Barua ya Mr. Robert Rogers, Katibu wa Bunge, House of Commons Uingereza,tarehe 25 Oktoba, 2011 kwenda kwa Katibu wa Bunge la Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah
87​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wao Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu walisema kitendo chaKatibu Mkuu Kiongozi kwenda kwenye Vyombo vya Habari kujibu Hoja iliyoanziaBungeni kimeingilia wajibu na haki za Bunge kama zilivyoelezwa katika Ibara ya63(2) na (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Bungelimenyang’anywa haki ya kupokea taarifa na kujiridhisha kwa kuhoji na kuulizamaswali hasa ikizingatiwa kuwa Bunge katika kuisimamia Serikali ni pamoja nakuhoji matumizi ya fedha za wananchi kama ilivyokuwa katika suala hili.Mmoja wa Wanasheria Wakuu Wastaafu alieleza kuwa, kitu ambachokinaonyesha kwamba Bunge limedhalilishwa ni pale ambapo Katibu MkuuKiongozi alitoa taarifa bila kuwasilisha matokeo ya uchunguzi huo Bungeni.​
80
Mheshimiwa Spika,​
Ili kufahamu undani wa suala hili Kamati Teule ilifanya mahojiano na wahusikawakuu wawili ambao ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi. Katika mahojianona Katibu Mkuu Kiongozi, Kamati pamoja na mambo mengine ilitaka kufahamukama kulikuwa na mawasiliano kati yake na Waziri Mkuu kabla hajatoa Taarifayake ya Uchunguzi kwa Vyombo vya Habari na kama alitoa taarifa hiyo hukuakijua kuwa Waziri Mkuu alitoa kauli Bungeni na kwamba Bunge lilikuwalinasubiri majibu, Katibu Mkuu Kiongozi aliieleza Kamati Teule kuwa suala lanidhamu ya watumishi wa umma linaendeshwa kwa Sheria za Utumishi na siosuala la kisiasa na hicho ndicho alichokifanya. Kwa maneno yake Katibu MkuuKiongozi alisema:-​
“… mimi nilichofanya nilichukua Sheria, nikachukua Kanuni, taratibuna mamlaka niliyonayo nikafanya niliyofanya. Hiyo ya Waziri Mkuukwamba atayarudisha Bungeni hilo sikuwa na uhakika sana kamaninaelewa vizuri…”​
81
80​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 23 Septemba, 2011.
81​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
88​
Kamati ilihoji pia namna suala hili lilivyofika mezani kwa Katibu Mkuu Kiongozi;iwapo alipelekewa na Waziri Mkuu baada ya kuibuliwa Bungeni au alichukuauamuzi yeye mwenyewe baada ya kusikia likizungumzwa Bungeni lakinihaikuweza kupata majibu kutokana na maelezo kwamba mawasiliano kati yakena uongozi wa ngazi za juu ni​
highly classified. Aliendelea kusema:-
“…hilo kwa kweli siwezi kulisema, kwa sababu ni mambo ya ndanimno, itoshe tu kwamba mimi ninayo Sheria iliyotungwa na Bungenaitekeleza…​
82”
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wake Waziri Mkuu aliieleza Kamati Teule kwamba ni kwelialilieleza Bunge kuwa analipeleka suala la Ndugu David Kitundu Jairo kwa Raiskwa kuwa kimahusiano Waziri Mkuu na Rais ni watu ambao wanawasiliana kwakaribu sana. Kamati Teule ilipotaka kufahamu iwapo Waziri Mkuu alimpa taarifaMhe. Rais kama alivyoliahidi Bunge, alisema:-​
“…alipokuja, nililazimika kumwarifu kwamba kumetokea nini, nayeakatupa maelekezo, ambayo nilidhani ni mazuri tu …kwamba nivizuri mzingatie taratibu maadam umelitoa huko ukaamua kuliletahuku…katika kulisimamia hamna budi mrudi kwenye sheria zetuzinazotawala utumishi…​
83”
Waziri Mkuu alieleza pia kwamba walishauriana na Katibu Mkuu Kiongozi namnaya kushughulikia suala hilo. Kamati Teule ilipotaka kufahamu iwapo WaziriMkuu alipewa taarifa baada ya Katibu Mkuu Kiongozi kukamilisha Uchunguzi waAwali ambao katika hatua za mwanzo walishauriana, Waziri Mkuu alijibukwamba hakupata taarifa hizo kabla na kwamba na yeye alizisikia baadaye.Kwa maneno yake Waziri Mkuu alisema: -​
82​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
83​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 24 Oktoba, 2011.
89​
“…kimahusiano sisi hata bila kujali huo mfumo wa kisheria, mamlakahaya ni ya kwake angeweza kufanya hivyo, lakini bado kamaangeamua tu kwamba … Bwana, Waziri Mkuu muda wotetunawasiliana naye, hata katika hili tuliwasiliana naye,ameniwezesha nimeweza kulisimamia, bado angeweza akarudikwangu na kusema Bwana, nimemaliza kazi yangu vizuri, sasanataka niende nikafanye moja, mbili, tatu. Pengine na mimi busaranyingine zingenijia na ningesema sawa tu, lakini hebu ngoja kidogo,pamoja na kwamba ni mamlaka yako hayo, unaweza kisheriaukafanya hivyo, lakini hebu ngoja kwanza na mimi nione kama kunanamna nyingine ya kuweza kufanya, kwa sababu wenzanguwananingoja huku kuweza kujua nini kimetokea katika mchakatomzima. Sasa kwa sababu alikwenda kwa mamlaka yake, miminimekuja nikazipata baadaye. Sasa baada ya pale ndiyo inakuwamaji yameshamwagika, kuyazoa tena inakuwa sio rahisi sana.Kilichohitajika pale ni hilo tu ni namna ya kutafuta ushauri kablahujakwenda mbali sana. Naweza kusema it is unfortunate kwamba,halikujitokeza at that material time…”​
84
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule haikuweza kuthibitisha kuwa, kitendo cha taarifa kutolewa kwakutumia Vyombo vya Habari wakati bado Bunge halijapewa taarifa kimeathiridhana ya haki na madaraka ya Bunge kisheria. Hata hivyo, kwa kuwa suala hilililianzia Bungeni, na kwa kuwa kulikuwa na mawasiliano kati ya Waziri Mkuu naKatibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuanza kwa mchakato wa Uchunguzi wa Awali,hivyo basi, Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa na wajibu wa kuhakikisha kwambaBunge kupitia kwa Waziri Mkuu linapata Taarifa ya matokeo ya Uchunguzi waAwali kabla hajaitoa kwa Vyombo vya Habari.​
84​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 24 Oktoba, 2011.
90​
Ikumbukwe kwamba Wabunge walisitisha mjadala husika wa utaratibu waWizara kuchangisha Taasisi fedha kwa sababu suala hilo lilikuwa linafanyiwakazi na Serikali kama Waziri Mkuu alivyoliomba Bunge, na Wabungewalitegemea kuwa baada ya uchunguzi kukamilika wangepewa taarifa rasmi iliwaamue kuendelea au kuachana nalo.​
Mheshimiwa Spika,​
Miongoni mwa mambo ambayo yalielezwa na baadhi ya watu waliofika mbele yaKamati Teule kuwa yameathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge ni manenoaliyotumia Katibu Mkuu Kiongozi siku alipotoa Taarifa ya Uchunguzi wa Awalikwa Vyombo vya Habari. Hili lilitiliwa mkazo na mchangiaji mmoja aliposema: -​
“…utaratibu uliotumiwa ni kweli umekiuka haki na madaraka yaBunge kwa maana ya substantively lakini vile vile hata toneiliyotumika, maneno yaliyotumika na Katibu Mkuu Kiongozi,yalionyesha defiance na kiburi kwa Bunge…”​
85
Mheshimiwa Spika,​
Maneno yanayozungumzwa hapa ni pale Katibu Mkuu Kiongozi aliposikikaakisema Ndugu David Kitundu Jairo kuwa anaweza kuchukua hatua kwakuwashtaki kwa​
defamation waliomharibia jina, akitoa mfano kwamba hataWaandishi wa Habari wamewahi kuwalipa watu mbalimbali kutokana na kosahili. Kwa maneno yake alisema: -
“…sasa hii mimi namwachia mwenyewe Jairo kama yeye ataamuakupeleka mbele ya safari, vyombo vipo, anayo haki ya kufanyahivyo. Anayo haki kwamba mimi nimedhalilishwa. Si mmeona watuwengine mmewahi kuwaandika kwenye magazeti, wengine simmewahi kuwalipa watu hapa kwa sababu ya defamation?...”​
86
85​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 14 Septemba, 2011.
86​
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa Vyombo vya Habari.
91​
Kauli ya kwamba Ndugu David Kitundu Jairo anaweza kushtaki kwa​
defamation
imetafsiriwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alimaanisha Ndugu David Kitundu Jairoanaweza kuwashtaki Wabunge kwa kile kilichosemwa Bungeni tarehe 18 Julai,2011. Mtazamo huu uliungwa mkono na mmoja wa wahojiwa ambaye alisema: -​
“…Sasa ile ni threatening na kutisha WaheshimiwaWabunge…Mheshimiwa Beatrice Shellukindo alisema yale manenoyake ndani ya Bunge na …tuna immunity …Katibu Mkuu Kiongozikusema kwenye Vyombo vya Habari kwamba Mbunge huyu anawezakushtakiwa ni sehemu ya kuingilia Bunge.​
87”
Mheshimiwa Spika,​
Suala la kinga ya Wabunge kutoshitakiwa kwa kauli wanazozitoa Bungeni pialiliungwa mkono na kufafanuliwa na Mtaalam wa Masuala ya Katiba wa ChuoKikuu cha Dar es Salaam na mchangiaji mwingine ambaye alisema: -​
“…Hawawezi kushtaki kwa defamation …sioni hapo amekuwadefamed vipi. Hii ni barua, ni fact ipo na imekuwa tabled, nihalisi…pale hajadhalilishwa.​
88”
Tofauti na mtazamo kuwa maneno ya Katibu Mkuu Kiongozi yalimaanisha kuwaNdugu David Kitundu Jairo anaweza kuwashitaki Wabunge, wapo waliosemakuwa Katibu Mkuu Kiongozi hakumaanisha hivyo badala yake alimaanisha kuwaamwandikie Mhe. Spika kuonyesha kutoridhishwa kwake kwa kutumia Kanuni ya64 na 71.​
89
87​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 30 Septemba, 2011.
88​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 30 Septemba, 2011.
89​
Kanuni ya 64 inahusu mambo yasiyoruhusiwa Bungeni na Kanuni ya 71 inahusu haki ya raiakujitetea na kujisafisha dhidi ya kauli zinazotolewa Bungeni.
92​
Kamati Teule iliona ni vema pia kusikia kutoka kwa mhusika ni nini hasalilikuwa lengo la kauli yake hiyo. Katibu Mkuu Kiongozi alifafanua kuwaalimaanisha Ndugu David Kitundu Jairo anaweza kupeleka malalamiko kwaMhe. Spika, kwamba: -​
“…ile defamation niliyozungumza nilikuwa nawazungumzia waleWaandishi wa Habari wenyewe kwamba ninyi si mmewahikushtakiwa kwa defamation…siyo kwamba Bunge ndiyo lishtakiwekwa defamation...​
90”
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ina maoni kwamba, kwa kutumia maneno “vyombo vipo” KatibuMkuu Kiongozi alimaanisha kwamba Ndugu David Kitundu Jairo angewezakwenda kwenye chombo chochote cha haki kumshtaki Mbunge kinyume namatakwa ya Katiba kama yalivyoainishwa kwenye Ibara ya 100 na Kifungu cha 3cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inaona maneno haya yameathiri dhana ya haki na madaraka yaBunge kwa vile kwa mujibu wa Ibara ya 100(1) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, 1977 na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge,Sura ya 296, Kifungu cha 3, msisitizo ni kuwa majadiliano ya Wabungehayatahojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aukatika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge. Aidha, Ibara ya 100(2)inaelekeza kwamba Mbunge hatashtakiwa kwa jambo lolote alilolisema aukulifanya ndani ya Bunge. Kumshauri Ndugu David Kitundu Jairo kwendakwenye chombo chochote ni kukiuka Ibara hizo na hivyo kuathiri uhuru wamajadiliano ndani ya Bunge.​
90​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
93​
Mheshimiwa Spika,​
Maneno mengine ya Katibu Mkuu Kiongozi ambayo yanalalamikiwa ni pamoja nakauli kwamba mtu aliyetoa barua kwa Mbunge “​
ikithibitika atapewa hakiyake…” kwamba inaweza kuathiri haki ya Wabunge kupata habari na hatakutishia raia wema kutoa nyaraka kwa Wabunge hata zile ambazo zinaonyeshamaovu kwa kuwatisha watoa habari na hivyo kuwafanya Wabunge washindwekutekeleza wajibu wao wa kuisimamia Serikali. Maneno ya Katibu MkuuKiongozi kuhusu hili ni kwamba mpaka sasa wanaendelea kutafuta nani alitoabarua kwa Mbunge au kwa Wabunge; ikithibitika atapewa haki yake nakuchukuliwa hatua za kinidhamu.91
Kwa upande mwingine mmoja wa wanazuoni wa masuala ya Katiba na Sheriakutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuwa kitendo cha Katibu MkuuKiongozi kusema Mbunge alipata wapi Nyaraka za Serikali ni kulidharau Bunge.Alisema: -​
“…Waziri Mkuu kabeba mzigo, halafu wewe unasema alipata wapiNyaraka … I don’t think he should have said that…”​
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kuwa badala ya kulalamika na kutishia​
Whistleblowers,​
Watendaji Wakuu wa Serikali sasa wanatakiwa kutumiataratibu za ndani kutatua tatizo la kuvuja kwa Nyaraka za Serikali ambalolimekuwa likijitokeza mara kwa mara hadi kushusha heshima ya Serikali. Aidha,Kamati Teule inaona umuhimu wa kutungwa kwa Sheria ya Whistleblower’sProtection Act ambayo itasaidia kushughulikia suala hili.
Mheshimiwa Spika,​
Tarehe 24 Agosti, 2011 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alirudikazini kama alivyoelekezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, na alipokelewa kwamapokezi makubwa ikiwa ni pamoja na gari lake kusukumwa, yeye kuvishwa​
91​
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi kwa Vyombo vya Habari, tarehe 23 Agosti, 2011.
94​
shada la maua na kuimbiwa nyimbo. Vile vile Waandishi wa Habari walikuwepona kurekodi matukio yaliyoendelea. Wengi wa watu waliofika mbele ya KamatiTeule walitoa maoni kuwa kitendo hicho sio cha kimaadili ya mtumishi waumma kwa kuwa picha iliyojitokeza ni kuwa katika suala hili kulikuwa namashindano kati ya Serikali na Bunge, na kwamba Bunge lilikuwa “linazomewa”kuwa limeshindwa.Akitoa maoni yake kuhusu hili Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema: -​
“…halivunji Sheria, lakini ni jambo la hovyo kwamba sasa unarudiunasukumwa na gari, watu wanakupokea kwa mbwembwe, ni jambola hovyo…​
92”
Mmoja wa Makatibu wa Bunge Wastaafu alisema, kitendo kile ni kulidharauBunge na kinaonesha kuwa Watendaji wa Serikali wameingia kwenye siasa.Kwa maneno yake alisema: -​
“…baada ya kutangazwa uamuzi huu kesho yake alipokelewa kuleWizarani … kwa shangwe, gari lake likasukumwa …Vyombo vyaHabari vilikuwa pale which means jambo lenyewe lilikuwalimepangwa… watumishi wengi walikuwa pale chini …kwa mtu civilservant ukiona anasukumwa…now this thing is being politicized…it isin bad test…​
93”
Mchangiaji mwingine alisema, mapokezi yale yalishangaza wengi hasa kwa vilelimetokea kwenye Ofisi ya Umma. Kiongozi wa umma kusukumwa ndani yagari, watumishi kuacha kazi kwenda kwenye mapokezi, ni dalili ya kwambandani ya Utumishi wa Umma kuna mmomonyoko wa maadili kiutendaji,kwamba: -​
92​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 3 Oktoba, 2011.
93​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 21 Septemba, 2011.
95​
“…hatujazoea sisi kuona civil servants wakiwa wanafanya mikutanokama hiyo. Kazi hiyo ni ya wanasiasa, lakini openly imeonekanainafanyika. Kwa hiyo, kuna mmomonyoko mkali sana wa maadili yakiutendaji kwenye Public Service ambayo pia nayo inabidi iweaddressed...​
94”
Kamati Teule imebaini kuwa kitendo cha mapokezi ya Ndugu David KitunduJairo kimeashiria yafuatayo:​
•​
matumizi mabaya ya muda wa kufanya kazi kwa vile kwa kipindi chotehicho kazi hazikufanyika na hivyo umma kukosa huduma.
•​
uvunjifu wa maadili ya Utumishi wa Umma kinyume na Kifungu cha47(3)(b) cha Public Service Scheme, 2003 kinachosomeka kama ifuatavyo:-
“Every Public Servant shall not conduct himself in a way which: -(b) is improper …”​
Kamati Teule inaona kuwa mapokezi yale na yote yaliyojiri ni​
“improper”
kwa mtumishi wa umma.​
•​
kulidharau Bunge kwa kuonyesha kwamba kulikuwa na mashindano namshindi kapatikana, wakati ukweli ni kwamba Bunge lilikuwa katikawajibu wake wa kuihoji Serikali.
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati kwamba suala hili lazima likemewe ili lisijirudie tena kwamaslahi ya Taifa na mambo ya siasa waachiwe wanasiasa na watumishi waumma waendelee kufanya kazi zao na kufuata maadili ya Utumishi wa Umma.​
94​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 21 Septemba, 2011.
96​
6.0 KUANGALIA NAFASI YA MAMLAKA YA UTEUZI KWA NGAZI YA MAKATIBUWAKUU KATIKA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA NIDHAMU YA ANAOWATEUAMheshimiwa Spika​
,Hadidu ya Rejea ya Nne iliitaka Kamati Teule kuangalia nafasi ya Mamlaka yaUteuzi kwa ngazi ya Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamuya anaowateua.Katika kushughulikia Hadidu hii, Kamati ilifanya yafuatayo:-(a) Kupitia Katiba, Sheria ya Utumishi wa Umma, 2001 na Kanuni za Utumishiwa Umma, 2003.(b) Kufanya mahojiano na mashahidi wa aina mbalimbali,
6.1 Misingi ya Katiba, Sheria na Kanuni za Utumishi kuhusiana na Mamlaka yaUteuzi kwa Makatibu WakuuMheshimiwa Spika,​
Ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inampa Raismamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbalikatika Utumishi wa Umma. Aidha, Rais ana madaraka ya kuteua watu wa kushikanafasi za madaraka ya uongozi wanaowajibika kuweka Sera za Idara na Taasisiza Serikali na Watendaji Wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa Seraza Idara na Taasisi hizo katika Utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 inaelekeza kwamba kutakuwa na KatibuMkuu Kiongozi ambaye atateuliwa na Rais na atakuwa Mkuu wa Utumishi waUmma na Katibu wa Baraza la Mawaziri.​
95 Aidha, Kifungu 5(1)(a) kinaainishakwamba, kutakuwa na Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu mbalimbali ambaowatateuliwa na Rais. Kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo:-
95​
Kifungu cha 4(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002.
97​
“5(1) Except where the President determines otherwise, there shall beappointed by the President –a Chief Executive Officer in respect of each Ministry, extraministerial department, region or local governmentauthority, in the Government of the United Republic, whoshall be known as the Permanent Secretary for thatMinistry, the Head of that extra ministerial department orRegional Administrative Secretary for the Region or thedirector of the local government authority as the case maybe …”​
Katiba inampa Rais mamlaka ya kutekeleza madaraka ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano yeye mwenyewe moja kwa moja au kukasimu madaraka hayo kwawatu wengine.​
96 Miongoni mwa madaraka ambayo Rais amekasimu ni yale yakushughulikia masuala ya kinidhamu kwa watumishi wa umma kamainavyoelezwa hapa chini. Hata hivyo, Rais haruhusiwi kukasimu madaraka yakumuachisha kazi mtumishi yeyote kwa maslahi ya umma.97
6.2 Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na RaisMheshimiwa Spika,​
Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Rais ni KatibuMkuu Kiongozi kama inavyofafanuliwa katika Kifungu cha 4(3)(d) kamaifuatavyo:-​
“4(3) The Chief Secretary shall, as head of the Service, provideleadership, direction and image to the service and shall:(d) be a disciplinary authority in respect of public servantsappointed by the President.”​
96​
Ibara ya 34(4).
97​
Kifungu 21(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002.
98​
Kitendo cha Rais kukasimu kwa Katibu Mkuu Kiongozi madaraka yakushughulikia nidhamu ya watumishi anaowateua hakimuondoi moja kwa mojakatika kushughulikia nidhamu yao, kwa sababu kulingana na masharti ya Ibaraya 36(4) Rais ana mamlaka wakati wowote kuchukua hatua za kudhibitinidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.Rais pia ni Mamlaka ya Rufaa kwa mtumishi yeyote wa umma ambaye Mamlakayake ya Nidhamu ni Katibu Mkuu Kiongozi. Hivyo, mtumishi asiporidhika nauamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi ana haki ya kukata rufaa kwa Rais ambayeanaweza kuuthibitisha, kuurekebisha au kuutengua uamuzi wa Katibu MkuuKiongozi. Kifungu cha 25(1) kinafafanua kama ifuatavyo: -​
“25(1) Where –(a) The Chief Secretary exercises disciplinary authority inrespect of a public servant who is an appointee of thePresident by reducing the rank other than reversion fromthe rank to which the public servant has been promotedor appointed on trial or reduces the salary or dismissesthat public servant may appeal to the President againstthe decision of the disciplinary authority and thePresident shall consider the appeal and may confirm,vary or rescind the decision of that disciplinaryauthority…”​
99​
6.3 Taratibu za Kushughulikia Masuala ya Kinidhamu kwa Watumishi wa UmmaWanaoteuliwa na RaisMheshimiwa Spika,​
Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 zimefafanua kwa kina taratibu hizi kamailivyoelezwa awali katika Taarifa hii, Kanuni ya 36 inaelekeza kwamba paleinapobidi hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya mtumishi wa umma Mamlakahusika ya Nidhamu inalazimika kufanya Uchunguzi wa Awali (​
PreliminaryInvestigation) ili kuthibitisha kama mtumishi mtuhumiwa ana kesi ya kujibu aula.Iwapo Uchunguzi wa Awali utathibitisha kuwa mtumishi mtuhumiwa ana kesi yakujibu, na kwamba uzito wa kesi yenyewe unaweza kusababisha mtumishihusika akapewa adhabu ya kufukuzwa kazi, kushushwa cheo au kupunguzwamshahara, Kanuni zinaelekeza kwamba Mamlaka ya Nidhamu italazimikakumpatia mtumishi mtuhumiwa notisi na hati ya mashitaka inayoainisha tuhumadhidi yake, na kumtaka atoe maelezo ya utetezi wake ndani ya mudautakaoainishwa.98
Mheshimiwa Spika,​
Kanuni ya 45 inaelekeza kwamba mtumishi mtuhumiwa akishindwa kutoamaelezo ya utetezi ndani ya muda aliopewa au akitoa maelezoyasiyojitosheleza, Mamlaka ya Nidhamu itateua Kamati ya watu wawili au zaidikwa ajili ya kufanya uchunguzi (​
Inquiry Committee).Sifa kuu za watumishi wanaoweza kuteuliwa katika Kamati ya Uchunguzi,pamoja na sharti la kuzingatia jinsia, ni kuwa mtumishi husika awe AfisaMwandamizi na zaidi (Senior grade and above) na katika ngazi ya juu kumzidimtumishi mtuhumiwa.99 Hata hivyo, kwa upande wa watumishi wa ummawanaoteuliwa na Rais Kanuni ya 46(2) inaelekeza kama ifuatavyo: -
98​
Kanuni ya 44.
99​
Kanuni ya 46(1).
100​
“…where the appointing authority of the accused public servant isthe President, no person shall be appointed a member of an InquiryCommittee for conducting an Inquiry into a charge or chargesagainst such public servant unless he is a Judge, the PermanentSecretary, a head of Independent Department, a RegionalAdministrative Secretary, a Senior or a Principal ResidentMagistrate…”​
Taratibu zitakazotumiwa na Kamati ya Uchunguzi katika kuendesha kazi zakezimefafanuliwa katika Kanuni ya 47. Aidha, Kanuni ya 48 inaelekeza kwamba,Kamati ya Uchunguzi itakapokamilisha kazi yake itawasilisha Ripoti kwaMamlaka ya Nidhamu ikielezea, pamoja na mambo mengine, iwapo kwamtazamo wa Kamati tuhuma dhidi ya mtumishi mtuhumiwa zimethibitishwaama la. Isipokuwa Kamati ya Uchunguzi haitakiwi kutoa mapendekezo yoyotekuhusiana na adhabu kwa kuwa hilo ni jukumu la Mamlaka ya Nidhamu.​
100
Mheshimiwa Spika,​
Kanuni pia zinaelekeza kwamba iwapo Mamlaka ya Nidhamu itamtia hatianimtumishi mtuhumiwa basi mtumishi huyo atapewa adhabu ambayo utekelezajiwake utaanza mara moja. Kanuni ya 48(8) inafafanua: -​
“Where the disciplinary authority finds the accused public servantguilty, he shall proceed to award punishment.Provided that where the accused public servant is punished bydismissal, his dismissal shall take effect from the date upon whichthe Disciplinary Authority found the accused public servant guilty.”​
100​
Kanuni ya 48(1) – (3).
101​
6.4 Uchambuzi wa YaliyojitokezaMheshimiwa Spika,​
Baada ya kupitia Katiba, Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 na Kanuni zaUtumishi wa Umma, 2003 na mahojiano na watu mbalimbali Kamati imebainiyafuatayo:-​
Mheshimiwa Spika,​
Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 na Kanuni zake za Mwaka 2003 zimeonyeshawazi kuwa zaidi ya kuwa Mamlaka ya Rufaa, Rais hana nafasi kubwa sanakwenye masuala ya nidhamu ya anaowateua. Sheria zimetoa madarakamakubwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kufanya Uchunguzi wa Awali na kuendeleana kutoa adhabu ya kumpunguzia mshahara mtuhumiwa bila hata kuhusishaMamlaka ya Uteuzi (Rais).​
101 Hakuna mahali popote kwenye Sheria au Kanunipanapomlazimisha Katibu Mkuu Kiongozi kuwasiliana na Mamlaka ya Uteuzikabla ya kutoa maamuzi yake. Hata kama ziko taratibu za kiutawala, ombwehili (vacuum) kwenye Sheria linaweza kusababisha matumizi mabaya yamadaraka.
Mheshimiwa Spika,​
Hofu hii ya matumizi mabaya ya madaraka inatiliwa nguvu na kitendo chaKatibu Mkuu Kiongozi kumrudisha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini na kesho yake (Mamlaka ya Uteuzi) kumrudisha tena likizoni, inaonyeshawazi hapakuwa na mawasiliano ya kiutawala kati yao. Kwa mujibu wa Taarifaya Ikulu kwa Vyombo vya Habari ya tarehe 26 Agosti, 2011 uamuzi wa Rais wakumsimamisha kazi Ndugu David Kitundu Jairo haujatokana na shinikizo laBunge, na kwamba Ndugu David Kitundu Jairo asirudi kazini mpakaatakapoamua namna gani ya kurudi, lini na wapi, kama kungekuwa namawasiliano Katibu Mkuu Kiongozi asingemrudisha kazini Ndugu David KitunduJairo na kesho yake Rais anamsimamisha kazi.​
101​
Kanuni 48(8) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003.
102​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa vile kuitaarifu Mamlaka ya Uteuzi ni hiari tu ya Mamlaka ya Nidhamu au nisuala linalofanyika kiutawala, bado inatia shaka katika sakata hili kamaMamlaka ya Uteuzi ilitaarifiwa kwa kuwa kama ingetaarifiwa si rahisi kuruhusuTaarifa ya Uchunguzi itolewe kwenye Vyombo vya Habari huku ikielewa fikakuwa Serikali kupitia Waziri Mkuu ilikuwa imetoa ahadi Bungeni, hivyo ilipaswakurudi Bungeni.​
Mheshimiwa Spika,​
Inatia shaka kama kweli Mamlaka ya Nidhamu iliishirikisha Mamlaka ya Uteuzina Mamlaka hiyo ikaruhusu taarifa ya nidhamu ya mtumishi wa umma itolewehadharani wakati inafahamika siku zote kwamba masuala ya kinidhamu kwaWatumishi wa Umma ni SIRI. Kiutaratibu Ndugu David Kitundu Jairo angepewatu taarifa kama ilivyofanyika mara ya pili aliporudishwa likizoni kwanihaikusikika kwenye Vyombo vyovyote vya Habari hadi pale Mhe. FreemanMbowe, (Mb.) alipouliza swali kwa Waziri Mkuu Bungeni​
102.
Mheshimiwa Spika,​
Ibara ya 35(1) inaeleza kuwa, shughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuriya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais; Ibaraya 52(3) inaelekeza kuwa, katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuuatatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyoteambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.Hata Hivyo, katika masuala ya nidhamu ya watumishi wa umma wanaoteuliwana Rais, nafasi ya Waziri Mkuu haionekani moja kwa moja. Katiba, Sheria naKanuni za Utumishi wa Umma vinamuondoa kabisa Waziri Mkuu katikakushughulikia masuala ya nidhamu kwa watumishi hao.Kutokana na mjadala huo hapo juu, Kamati Teule ina maoni kwamba Sheria naKanuni za Utumishi wa Umma zifanyiwe mapitio ili kubaini maeneo zaidiyanayohitaji marekebisho ili kuondoa migongano, kuweka wigo mpana wa hakikutendeka na kuongeza ufanisi wa kazi katika Utumishi wa Umma.​
102​
Hansard ya tarehe 25 Agosti, 2011, ukurasa wa 2.
103​
Kwa mfano, kwa kuwa suala la nidhamu ya wateule wa Rais ni nyeti na pana sivema suala hilo kuwa mikononi mwa mtu mmoja. Ni vema Serikali ikafikiriamojawapo ya njia zifuatazo: -​
•​
Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Raisinaposhughulikia masuala ya nidhamu ifanye hivyo kwa kumshirikishaWaziri Mkuu ambaye ni msimamizi wa shughuli za siku kwa siku za Serikali.
•
Kuunda Chombo maalum cha kushughulikia masuala ya nidhamu kwawatumishi wa umma wanaoteuliwa na Rais.
Mheshimiwa Spika,​
Kanuni ya 36 inayohusu Uchunguzi wa Awali (​
Preliminary Investigation) inaupungufu kama ifuatavyo:-
•​
haitoi maelekezo maalum kwa Mamlaka ya Nidhamu kuhusiana na mamboya kuzingatia wakati wa kufanya Uchunguzi wa Awali kwa mfano nambaya wajumbe na sifa zao, tofauti na ufafanuzi unaotolewa katika Kanuni ya46 kuhusu Kamati ya Uchunguzi (Inquiry Committee).
•​
tafsiri inayopatikana ni kuwa, Mamlaka ya Nidhamu ina ridhaa ya kuonanamna sahihi ya kupata ukweli wa awali kuhusu tuhuma zinazomkabilimtumishi anayehusika.
•​
upo uwezekano wa Mamlaka ya Nidhamu kufanya uchunguzi huo yenyewena kufanya maamuzi iwapo kuna kesi ya kujibu au la.Utekelezaji wa “ridhaa” hii unaweza kuleta utata mfano, kwa suala la NduguDavid Kitundu Jairo inaelezwa kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alimtumiaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya Ukaguzi Maalum kwavile hata kama suala husika linahusu fedha na Sheria ya Ukaguzi inaruhusu mtuyeyote kuomba Ukaguzi Maalum103 (Special Audit) bado kuna mashaka kuwaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pekee asingeweza kutoamajibu kuhusiana na masuala ya kinidhamu kwa upana wake.
103​
Kanuni ya 29 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003.
104​
7.0 MAMBO MENGINE YENYE UHUSIANO NA MASUALA HAYAMheshimiwa Spika,​
Katika sehemu hii ya Taarifa, Kamati Teule inayatolea ufafanuzi masualakadhaa yanayohusiana na Hadidu za Rejea zilizotangulia. Masuala hayo nipamoja na:​
7.1 Uvujaji wa Nyaraka za SerikaliMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imelazimika kulitolea maoni suala la uvujaji wa nyaraka zaSerikali kwa sababu suala lililosababisha kuundwa kwa Kamati yenyewe linagusauvujaji wa nyaraka za Serikali. Nyaraka za Serikali zaweza kuwa za wazi(​
unclassified) au za siri (classified).Nyaraka za wazi ni wazi kwa matumizi ya ofisi husika tu na endapo zitavujahazina madhara kwa Serikali, ni mawasiliano ya kawaida ndani ya Wizara/Idaraza Serikali. Kimsingi ni nyaraka ambazo hazina usiri ndani yake ingawajehazitakiwi kusomwa na watu wasiohusika isipokuwa tu wanapozipata kwa njiazinazoruhusiwa. Akisisitiza hili wakati wa mahojiano, Katibu Msaidizi wa Tumeya Utumishi wa Umma alisema:-
“…katika utendaji wa Serikali kuna majalada yanayoitwa open filesyenye masuala ya kawaida…ambayo hayana usiri ndaniyake…mawasiliano ambayo kwa namna moja au nyingine hayawezikuleta athari kwa upande wa Serikali…pamoja na kwamba yanawezakuwa filled kwenye open files, bado ninaamini kwa dhati kabisakwamba katika Serikali taarifa si vema ikawa accessed na mtuambaye haruhusiwi na kama inatoka basi itoke kwa njia ambayoSerikali imeweka…”​
105​
Vilevile mawasiliano au taarifa yoyote Serikalini haitakiwi kwenda kwenyeVyombo vya Habari au kwa umma isipokuwa taarifa ambazo zinasaidia katikakujadili masuala ya jamii hazitakiwi kuzuiliwa labda kama taarifa hizo ni za siri.Suala hili limefafanuliwa katika Kifungu C.15 cha Kanuni za Utumishi wa Umma,2009 Toleo la Tatu kinachosomeka:-​
“(1) no correspondence which has passed between Ministries,Independent Departments, Regions, Local GovernmentAuthorities or between the Public and Ministries/IndependentDepartments/Executive Agencies/Regions/Local GovernmentAuthorities may be communicated to the press or any memberof the public without the approval of the Chief ExecutiveOfficer concerned, but information of the general nature whichmay be of material assistance in discussing local questionsneed not be withheld, provided that such information is not ofthe confidential nature of likely to infringe the privacy ofothers.(2) unauthorized disclosure of official information shall make apublic servant liable to disciplinary action or criminalprosecution”.​
Aidha, utoaji wa taarifa za Serikali bila kibali utafanya mtumishi aliyetoataarifa hizo kushtakiwa kwa makosa ya kinidhamu au kufunguliwa mashtaka yajinai.​
Mheshimiwa Spika,​
Nyaraka za siri​
(classified documents) zinafafanuliwa na Sheria ya Usalama waTaifa, Sura ya 47, katika Kifungu cha 3 kuwa ni taarifa au kitu chochoteambacho mamlaka husika imetamka kuwa ni siri. Kifungu hicho kinasomeka:-
“…any information or thing declared to be classified by anauthorized officer…”​
106​
Nyaraka hizi ziko za aina tatu kama ifuatavyo:-(a) Siri Kuu​
(Top Secret) ni zile ambazo endapo zitavuja zitasababishamadhara makubwa sana (grave damage) kwa usalama wa Taifa.(b) Siri Sana (Secret) hizi ni zile ambazo endapo zitavuja zitasababishamadhara makubwa (serious damage) kwa usalama wa Taifa.(c) Siri Ndogo (Confidential) hizi ni zile ambazo endapo zitavuja madharayake sio makubwa sana kwa Taifa.Ili kuzitofautisha nyaraka hizi huwa zinagongwa mihuri kulingana na usiri wanyaraka husika. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, Sura ya 47, kutoanyaraka hizi kwa mtu asiyeruhusiwa ni kosa. Kifungu cha 5 kinasomeka kamaifuatavyo:-
“Any person who communicates any classified matter or causes theleakage of such classified matter to any person other than a personto whom he is authorized to communicate it or to whom it is in theinterest of the United Republic his duty to communicate it shall beguilty of an offence and liable on conviction to imprisonment for aterm not exceeding twenty years”.​
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Kamati Teule imebaini kwambamawasiliano yote ndani ya Serikali ni ya siri ingawa viwango vya usirivinatofautiana na kwamba jinsi ya kuzipata nyaraka za mawasiliano hayo nikwa kibali maalum pekee.​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa muda mrefu sasa pamekuwepo na malalamiko ya uvujaji wa Nyaraka zaSiri za Serikali. Mmoja wa wachangiaji aliyefika mbele ya Kamati Teulealisema:-​
107​
“…katika miaka ya hivi karibuni nyaraka za Serikali tena sensitivekabisa zimekuwa zinaonekana kwenye mitandao ya internet,nyingine zinachapishwa kwenye magazeti …”​
104
Miongoni mwa nyaraka za Serikali zilizopata kuvuja hivi karibuni nakulalamikiwa ni barua ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwendakwenye Taasisi zilizo chini ya Wizara yake akiziomba zichangie fedha ilikufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara Bungeni. Katibu Mkuu Kiongoziwakati akitoa matokeo ya uchunguzi kwenye Vyombo vya Habari alipoulizwakuhusu uhalali wa barua iliyosomwa Bungeni alisema:-​
“…mpaka sasa sisi tunaendelea kutafuta nani alitoa taarifa, nanialitoa barua kwa Mbunge au kwa Wabunge. Ikithibitika atapewahaki yake na kuchukuliwa hatua za nidhamu zinazopasa”​
105
Kauli hii ya Katibu Mkuu Kiongozi inadhihirisha kwamba barua iliyosomwaBungeni ni siri ya Serikali na haikupaswa kutoka nje.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilitaka kujiridhisha kuwa barua iliyowasilishwa Bungeni naMhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.) inaangukia katika kundi lipi la nyaraka zaSerikali. Kwa kuwa barua hiyo haikuwa na muhuri wa aina yoyote kati ya mihurimitatu iliyoelezwa hapo juu. Katibu Msaidizi kutoka Tume ya Utumishi waUmma alitoa maoni yake kwamba barua ile inaangukia kwenye kundi la​
confidential​
(siri ndogo) kwa sababu ni mawasiliano kati ya Katibu Mkuu naWatendaji. Aidha, alieleza kuwa kwa utaratibu wa kawaida ilitakiwa igongwemuhuri. Kwa maneno yake alisema:-
104​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 14 Septemba, 2011.
105​
Mkutano wa Katibu Mkuu Kiongozi na Vyombo vya Habari akielezea matokeo ya Uchunguzi waAwali kwa suala la Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Ndugu David Kitundu Jairo.
108​
“Kwa maoni yangu hii ina-fall kwenye confidential (sirindogo)…naweza kushindwa kujua moja kwa moja kwa nini mamlakahusika haikupiga muhuri wa confidential juu ya barua hii lakinininachofahamu ni kwamba information yoyote ambayo haitakiwikuwa open kwa mtu asiyehusika whether ni ndani ya Wizara husikainatakiwa igongwe muhuri kwa sababu once isipogongwa muhuri basimtu yeyote hata yule ambaye haruhusiwi kui-access anaweza akaiaccesskana kwamba ni document ya kawaida...”​
106
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati kuwa barua iliyowasilishwa Bungeni na MheshimiwaBeatrice Shellukindo ni nyaraka ya kawaida ya Serikali na sio miongoni mwanyaraka za siri (​
classified document) kwa kuwa haikugongwa muhuri wowotewa siri.
Mheshimiwa Spika,​
Katika mahojiano na mashahidi mbalimbali, Kamati Teule imebaini kwambabaadhi ya sababu zifuatazo huchangia sana uvujaji wa nyaraka za siri zaSerikali:-(a) Baadhi ya Watendaji ndani ya Serikali kutoridhishwa na baadhi yamambo ambayo yanafanyika katika Idara zao kinyume na utaratibu nahivyo kutaka yarekebishwe. Kwa kuwa Bunge limejijengea heshima nakuaminiwa, watendaji hao huwapatia Wabunge nyaraka zenye vitendoviovu kama vile ubadhirifu wa fedha za umma, wakiamini kufanya hivyokutasaidia kukomesha vitendo hivyo.Sababu hii inaungwa mkono na maneno ya mchangiaji mmojaaliposema:-​
106​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 28 Agosti, 2011.
109​
“…wapo watu kwenye Serikali ambao wanaona vitu ambavyosiyo sahihi, na kwa sababu Bunge limejenga heshima nakuaminiwa, watu wanawaamini Wabunge kwamba ukimpaMbunge hili Bwana atasaidia kulisema na litarekebishwa. Miminadhani ni jambo la muhimu kuendelea kutoa fursa hiyo…”​
107
(b) Baadhi ya watumishi kutoridhishwa na mfumo wa kushughulikia matatizoama masuala mbalimbali Serikalini hivyo kutafuta msaada kwa Wabungeau kwa vyombo vya habari.(c) Baadhi ya Watendaji kutoridhishwa na mishahara au marupurupuwanayopewa na hivyo kugeuza nyaraka za Serikali kuwa biashara ilikujiongezea kipato kwa kuziuza kwa watu mbalimbali ambao huzihitajikwa maslahi yao. Msisitizo katika hili ulitolewa na mmoja wa wahojiwakwa kusema:-​
“…Nyaraka za Serikali zinavuja kwa njia nyingi. Kuna wenginesasa wanafanya biashara…ni ukweli ulio wazi baadhi yanyaraka za Serikali zinauzwa hata kwa bei mbaya…sasawatumishi wa Serikali wengine wanakuwa tempted kuuzabaadhi ya nyaraka ili wajipatie kipato…”​
108
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kwamba, barua aliyosoma Mhe. Beatrice Shellukindo,(Mb.) Bungeni ni kielelezo cha watumishi kutoridhishwa na kitendo cha KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuzichangisha Taasisi zilizo chini yaWizara yake.​
107​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 14 Septemba, 2011.
108​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 13 Oktoba, 2011.
110​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule katika uchunguzi wake ilibaini changamoto zifuatazo katika sualazima la nyaraka za Serikali:-(a) Utaratibu uliowekwa wa kupata taarifa kupitia nyaraka za Serikali kutokamamlaka husika mfano Watendaji Wakuu hauwawezeshi walewanaozihitaji kwa nia njema kuzipata kwa urahisi kwa kuwa WatendajiWakuu hao hao wanaweza kuwa ndiyo wahusika wa maovuyanayotafutwa.(b) Wigo wa Nyaraka za Serikali kuwa siri ni mpana kiasi ambacho kila jambolinalofanyika linatafsiriwa kuwa ni siri wakati mambo mengine ni yakawaida tu. Hili ni tatizo kubwa ambalo husababisha mambo maovukutojulikana mapema na kuliingizia hasara Taifa.(c) Sheria iliyopo ni ya kutoa adhabu kwa mtoa taarifa inayohusiana nanyaraka za Serikali lakini hakuna Sheria ya kumlinda mtoa taarifa​
(Whistleblower Protection Act)​
huyo pindi anapotoa taarifa inayosaidiaSerikali kubaini maovu na kuyazuia au kuyarekebisha.
Mheshimiwa Spika,​
Ili kukabiliana na changamoto zilizoainishwa hapo juu, Kamati Teule ina maoniyafuatayo: -(a) Ni vema nyaraka nyeti​
(sensitive) za Serikali zikaendelea kubakia kuwasiri. Hata hivyo, ni vema usiri wa nyaraka za Serikali usitumike vibayakama vile watendaji wa Serikali wasio na maadili kujificha nyuma yake nakutenda maovu.(b) Serikali ifanye utafiti na uchambuzi ili hatimaye ilete Bungeni Muswadawa Sheria ya Kumlinda Mtoa Taarifa (Whistleblower Protection Act).
111​
(c) Utaratibu wa upatikanaji wa nyaraka za Serikali ufanyiwe uboreshaji kwakuwaruhusu wanaohitaji nyaraka hizo kuziomba katika ngazi za juu ikiwawatapata ugumu katika ngazi ya Watendaji Wakuu (CEOs) au ngazinyingine yoyote husika.​
7.2 Nafasi za Uteuzi, Ajira na Mpango wa kurithishana Madaraka Serikalini(​
Succession Plan)Mheshimiwa Spika,
Kufuatia maoni ya baadhi ya mashahidi na wachangiaji katika mahojiano,Kamati Teule imebaini masuala kadhaa ambayo Serikali inapaswa kuyazingatiaili kuboresha hatua mbalimbali zinazotumika Serikalini katika kujaza nafasi zauteuzi, taratibu za ajira na kuboresha mpango wa kurithishana madaraka nanafasi za kazi ili kuleta tija. Kamati Teule imebaini kwamba kuteua na kuajirikwa kuzingatia zaidi upeo, sifa, uzoefu, na aina ya taaluma katika nafasimbalimbali zikiwemo za uongozi katika Idara, Taasisi au Vitengo n.k.kutaongeza uzalishaji na kuboresha utoaji huduma na utekelezaji wa majukumukwa tija zaidi.​
Mheshimiwa Spika,​
Katika michango yao wachangiaji mbalimbali waligusia maeneo yafuatayokatika kusisitiza Hoja hizo:-(a) Kwamba baadhi ya Watendaji wakiwemo wale walioko katika ngazi zamaamuzi wanakosa umakini katika kufanya maamuzi na badala yakehutegemea ushauri pekee kutoka kwa watendaji walioko chini yao bilakupima ubora na athari za ushauri huo. Jambo hili linatafsiriwa kuwa kwakiasi kikubwa linatokana na kukosa taaluma, ujuzi na uzoefu katika nafasiwalizonazo, sifa ambazo wakati mwingine watumishi walioko chini yaohuwa nazo.​
112​
(b) Kwamba ajira zenye kuzingatia taaluma, ujuzi na uzoefu zitakuwaendelevu kwa kuwa zitasababisha ushindani wa wazi miongoni mwajamii/watumishi na kutoa fursa sawa katika kurithishana nafasi namadaraka na hivyo ushindani huo kuwa chachu katika kuleta maendeleokwa Taifa.(c) Kwamba, kwa baadhi yao kukosa taaluma husika (​
relevant profession)husababisha kutotii maadili ya taaluma husika kwa kuwa wanaofanya kaziza taaluma bila kuwa na sifa za taaluma hizo hawawajibiki katika taalumahizo na maadili yake hivyo kufanya maamuzi ambayo husababishautendaji mbovu na kulisababishia Taifa hasara kubwa, bila kuwepoutaratibu mahsusi wa kuwachukulia hatua za kitaaluma ambazo kwakawaida ni za haraka na zinazofaa zaidi (more effective).(d) Kwamba kukosekana kwa uwajibikaji na kuwepo kwa mmomonyokomkubwa wa maadili miongoni mwa watumishi wa Serikali na jamii kwaujumla ndiyo husababisha kutoheshimu na kutotii Sheria, Kanuni nataratibu hivyo kujiingiza katika vitendo visivyofaa kama vile wizi wa maliya Umma zikiwemo fedha na nyaraka za Serikali.(e) Kwamba watumishi kutozunguka katika Wizara, Idara na Vitengombalimbali wakati wa utumishi wao kunawanyima fursa ya kupata uzoefumtambuka katika mfumo wa Serikali na kuwafanya wabobee; Aidha,kukaa katika sehemu moja kunawafanya wadumae na pia kuendeleakurudia makosa wanayoyafanya siku hadi siku kwa kutumia mazoeabadala ya uzoefu wakidhani hivyo ndivyo sahihi au hufanya makosa kwamakusudi ili kukidhi manufaa yao binafsi.
Mheshimiwa Spika,​
Wakiendelea kutoa michango yao baadhi ya mashahidi walitolea mifano uteuzikatika ngazi za juu na mmoja wao alisema:-​
113​
“... Accounting Officer ana sifa gani ndiyo hapo pa kuanzia. Miminikasema tu, naweza nikasema pamoja na kwamba naonekanamdogo, lakini ni kati ya watu ambao tulipikwa. Mimi nimekuwa Headwa Section kwa miaka mitano na nusu, nimekuwa Kamishna kwamiaka mitatu, nimekuwa Naibu Katibu Mkuu almost three years.Unajua tofauti na shuleni, yaani kazi za civil service you learn in theprocess.Nimefanya kazi na Makatibu Wakuu wengi sana, tena wale the best,I say so. Nimefanya kazi na akina marehemu Rutihinda, Mzee FulgenceKazaura, Peter Ngumbulu, nimejifunza mengi pia na Bwana PenielLyimo na Bwana Mutalemwa tena wakati huo unajua. Kwa hiyo, sasais a learning process, kama kweli ambition yako ni kufanya vizuri,there is a lot of best practices. Unaangalia maneno mazuri yaviongozi wako kwa sababu ukiwa na cheo ni vizuri ukifurahie,unakikalia vizuri kiti chako halafu unakuwa comfortable. Na siyokwenda Dodoma ndiyo unahangaika, inakuwa ni process ya mwakamzima.Sasa I would say kwamba, kuna hii aspect ya kujifunza halafuunakomaa unakuwa Afisa Masuuli umetulia. You know what you aresupposed to do. You believe in yourself....”​
109.
Aidha, mmoja wa Viongozi Wakuu wastaafu naye aliieleza Kamati kuwa: -​
“…Uteuzi wa watu katika nafasi mbalimbali; iwe upande wa Serikalina hata upande wa siasa ni vema ukafanyika kwa kuzingatia zaidiuwezo kitaaluma, kiutendaji na kimaadili (Performance, professionaland ethical competence). Ni vema tukafuata kitu kinachoitwameritocracy…”​
110
109​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 8 Oktoba, 2011.
110​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 25 Oktoba, 2011.
114​
Mheshimiwa Spika,​
Kutokana na michango hii, linajitokeza fundisho kwamba zipo changamoto nyingizinazoikabili Sekta ya Utumishi wa Umma kwa sasa na zinazohitajikushughulikiwa. Kwa mfano, ili mtu afuzu kuteuliwa katika Utumishi wa Umma,hususan katika kada za juu (​
senior and executive grade) anapaswa kuwa na sifastahiki katika elimu, uzoefu na uadilifu katika Utumishi wa Umma, ikiwa nipamoja na kuzingatia maadili ya Taifa na uzalendo.Kamati Teule ilipata mfano wa Marekani, ambako mtumishi kabla hajateuliwakatika nafasi yoyote kubwa anapitia kwenye Mtandao wa Vyuo vinavyoitwa
Strategic Studies Institutes​
, ambavyo kazi yake ni kufundisha Maadili ya Taifa,Sera za mambo mbalimbali, Uzalendo na mengineyo yenye mtazamo au sura yakitaifa bila kujali itikadi. Utaratibu huu unafanana na ule wa mafunzo ya Jeshi laKujenga Taifa na vyuo vingine mahsusi kwa mafunzo ya Uongozi, utaratibu ambaoni mzuri na Taifa letu linapaswa kuongeza kasi ya kuufufua na kuuendeleza.
Mheshimiwa Spika,​
Madhara yanayotokana na kuwepo kwa watumishi wasiokidhi vigezo vyakitaaluma, uzoefu na uadilifu ni mengi ikiwa ni pamoja na:(a) Ushauri usiofaa wa baadhi ya wataalamu kwa wakuu wao wa kazi. Kwamfano katika suala la Wizara ya Nishati na Madini kuendesha michangokwenye Taasisi zilizo chini yake, upo ushahidi kwamba Mkurugenzi wa Serana Mipango alitoa ushauri usiofaa na wa upotoshaji kwa Katibu Mkuu hukuakijua fika, kwa taaluma na uzoefu wake, kwamba kufanya hivyo ni kinyumena Sheria, Kanuni na Taratibu za Fedha.​
111 Kwa upande wa Wahasibu waIdara, Kamati Teule imebaini kwamba licha ya kuhusika kwa namnambalimbali katika matumizi ya fedha zilizokusanywa walifanya hivyo bilakuzingatia taratibu za fedha kama wataalam.
111​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
115​
(b) Baadhi ya Watendaji Wakuu kushindwa kupima ushauri wanaopewa nahatimaye kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Kwa mfano katika suala hililililosababisha kuundwa kwa Kamati Teule, kama ilivyoelezwa hapo juu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini alishauriwa na watendaji wakekuendesha uchangishaji, lakini alishindwa kupima mantiki ya ushauri huokuwa ni kinyume na Kanuni za Fedha za Umma, 2001.​
112 Katika mahojianona Kamati Teule Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini alitumia maelezoya kwamba alishauriwa na wataalam kama utetezi pekee.113
(c) Matumizi ya fedha za umma kwa namna ambayo haiipatii Serikali thamaniya fedha hizo badala yake huiletea hasara na hatimaye kurudisha nyumajitihada za Serikali katika kuinua na kuimarisha uchumi.​
Mheshimiwa Spika,​
Kufuatia Hoja mbalimbali kama zilivyotolewa hapo juu, Kamati Teule ina maoniyafuatayo:-(a) Ni vema Watumishi wakawezeshwa ili wazifahamu vizuri zaidi kazi zao,wazipende, wawe mabingwa na wabobee ili kuleta tija na ufanisi Serikalinilakini pia kukuza fursa zao katika soko la ajira la Afrika Mashariki na dunianikote​
(World class standards); lakini ni muhimu zaidi kwa Watumishi waUmma kuwa wazalendo, waipende Nchi yao na wafanye kazi zao kwakuzingatia maadili na kuweka mbele maslahi ya Taifa.(b) Kuhusu maadili ya taaluma (professional Ethics) kwa wataalamu mbalimbaliwakiwemo Wanasheria, Wahandisi, Wahasibu, Wataalamu wa Sekta ya Afya,Utawala, n.k ili kudhibiti changamoto zinazotokana na kusaini mikatabamibovu na kufanya maamuzi mengineyo yanayoligharimu Taifa, wakatiumefika sasa kwa Serikali kutumia vizuri zaidi Mabaraza, Bodi na Jumuiyambalimbali za kitaaluma zilizoanzishwa kisheria ili watumishi wataalamuhao wanaokiuka maadili ya taaluma zao wabanwe.
112​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
113​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
116​
Taasisi hizi zina mamlaka ya kisheria ya kuchukua hatua hata zakunyang’anya leseni ikithibitika ukiukaji huo ni wa kiwango cha kupindukiana pindi mtaalamu anaponyang’anywa leseni anapoteza sifa za kuajiriwakatika nafasi hiyo. Jambo hili linaweza kuwa muafaka kwa hatua za harakawakati taratibu nyingine za kisheria zikiwa zinafuatia kwa kuwa hizo zinamlolongo mrefu na huchukua muda mrefu zaidi.(c) Namna nzuri ya kuendelea kuwatumia wastaafu na waliobobea katikautendaji Serikalini sio kuwaacha katika ajira rasmi kwa kuongeza mikataba;badala yake ni vema zaidi kuwatambua na kuwaandaa kuwa waajiri wapyakatika Sekta Binafsi ili waendelee kushiriki katika ujenzi wa Taifa kupitiautaratibu wa​
PPP (Public Private Partnership) ambao ni kipaumbele katikaMpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano chini ya Dira ya Taifa ya 2025.Kuwatumia wastaafu kwa utaratibu huu kutapunguza woga wa watumishikustaafu, kutaongeza ajira Serikalini hasa ajira kwa vijana, kutaongeza ajirakatika Sekta Binafsi, kutawaongezea fursa za ajira rasmi vijana wahitimu kutokaVyuo Vikuu na vinginevyo na kutaacha urithi kwa waajiriwa wapya (back up).
Mheshimiwa Spika,​
Ushauri huu ukizingatiwa utakuza, kuimarisha na kuboresha utendaji na mchangowa Sekta Binafsi katika maendeleo ya Taifa. Hii ni kwa sababu watumishi hawawastaafu na waliobobea na wanaotokea Serikalini watakuwa wanazijua nawatazingatia Sheria, Kanuni na taratibu na miongozo mbalimbali ikiwemo miikon.k hivyo kuongeza tija katika malengo mbalimbali ya kitaifa.​
117​
7.3 Uhusiano wa Kikazi kati ya Mawaziri na Makatibu WakuuMheshimiwa Spika,​
Kufuatia mahojiano na mashahidi mbalimbali Kamati Teule imebainichangamoto kadhaa katika utendaji wa Wizara ambazo zinahusu uhusiano wakikazi baina ya Mawaziri na Makatibu Wakuu. Ili kuweza kutoa maoni namapendekezo kuhusiana na suala hili Kamati Teule ilifanya utafiti kuhusu kaziza Makatibu Wakuu na Mawaziri na mahusiano yao ya kikazi kama ifuatavyo:​
Mheshimiwa Spika,​
Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 kinaelezea uteuziwa Makatibu Wakuu wa Wizara​
(Permanent Secretaries) unaofanywa na Rais.Katibu Mkuu ni Mtendaji Mkuu wa Wizara na kwa maana hiyo ndiye mshaurimkuu wa Waziri katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Hivyo basi, KatibuMkuu katika Wizara ana majukumu yafuatayo:-(a) Kuwa Afisa Masuuli wa Wizara (Accounting Officer).(b) Kuwa Mkuu wa Watumishi wote wa Umma walioko Wizarani.(c) Kushauriana na Waziri juu ya mambo yote yanayohusu Baraza laMawaziri.(d) Kuandaa na kutekeleza Sera, Sheria, Mikakati, Mipango na Programu zaSekta yake.(e) Kuandaa Rasimu ya nyaraka zote za Baraza la Mawaziri zinazohusuWizara.(f) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi yote ya Baraza la Mawaziriyanayohusu Wizara na kuandaa Taarifa za Utekelezaji na kuziwasilishakatika Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, kila robo ya mwaka na kilazinapohitajika.
118​
(g) Kuandaa orodha ya masuala muhimu yanayotarajiwa kuwasilishwa katikaBaraza la Mawaziri toka katika Wizara kila baada ya miezi sita nakuiwasilisha katika Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.(h) Kuwasilisha kwenye Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri na Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali mapendekezo ya Programu ya Miswadainayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mwaka mzima mwanzoni mwakila mwaka.(i) Kuhudhuria vikao vyote vya Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu (IMTC),Kamati Ndogo za IMTC na Vikao vya Kazi.(j) Kushauriana na Waziri mambo yote yanayohusu Wizara​
114.
Mheshimiwa Spika,​
Ibara ya 55(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelezea uteuziwa Mawaziri unaofanywa na Rais. Kazi za Mawaziri​
(Ministers) zinaainishwakatika Mwongozo wa Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:-(a) Msimamizi Mkuu wa Wizara katika utekelezaji wa maamuzi na shughuli zaSerikali ikiwa ni pamoja na Sera, Mikakati, Mipango na Programu.(b) Akiwa ni mwakilishi wa Rais Wizarani, Waziri ndiye mlinzi na mtetezi waKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.(c) Waziri ni msemaji Mkuu wa Wizara. Aidha, Waziri anawajibika kwa Rais,Waziri Mkuu na kwa Bunge kuhusu uendeshaji wa Wizara anayoiongoza.(d) Waziri pia anawajibika kuwasilisha kwenye Baraza la Mawazirimapendekezo ya masuala ya Kitaifa yatakayojadiliwa katika ngazi yaKimataifa na ambayo yanahitaji msimamo wa nchi.
114​
Barua Kumb. Na. CFC.71/326/01/228 ya tarehe 4 Novemba, 2011.
119​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa mujibu wa Mwongozo wa Baraza la Mawaziri​
115 Kamati Teule imeridhikakwamba mahusiano ya kikazi baina ya Mawaziri na Makatibu Wakuu yamewekwabayana, kwa lugha inayoeleweka na kukidhi haja ya kuwafanya Mawaziri naMakatibu Wakuu watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na kwa tija.Kwa mfano, kama ilivyoelezwa hapo juu Waziri ndiye msimamizi mkuu waWizara katika utekelezaji wa maamuzi na shughuli za Serikali ikiwa ni pamojana Sera, Mikakati, Mipango na Programu. Wakati huo huo miongoni mwa kazikubwa za Katibu Mkuu ni kuandaa na kutekeleza Sera, Sheria, Mikakati,Mipango na Programu za Sekta yake. Vile vile imeainishwa kwamba KatibuMkuu atashauriana na Waziri juu ya mambo yote yanayohusu Wizara. Aidha,Katibu Mkuu ndiye Afisa Masuuli wa Wizara (Accounting Officer).
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imechambua Kazi za Mawaziri na Kazi za Makatibu Wakuu kamazilivyoainishwa kwenye Mwongozo wa Baraza la Mawaziri. Vilevile Kamati Teuleimechambua Sheria ya Fedha za Umma, 2001​
(The Public Finance Act 2001 ActNo. 6, 2001) na kubaini Kifungu cha 8(1) cha Sheria hiyo ambacho kimewekawazi nafasi ya Katibu Mkuu katika kutekeleza majukumu yake ya masuala yafedha pasipo kumshirikisha Waziri ambaye ndiye msimamizi mkuu wa Wizara.Kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo: -
8(1) There shall be appointed by name and office and in writing by thePaymaster-General an accounting officer in respect of eachexpenditure vote, who shall control and be accountable for theexpenditure of money applied to that vote by an Appropriation Actand for all revenues and other public monies received, held ordisposed of, by or on account of the department or service forwhich the vote provides.​
115​
Barua Kumb. Na. CFC.71/326/01/228 ya tarehe 4 Novemba, 2011.
120​
Kwa mujibu wa maudhui ya Mwongozo wa Baraza la Mawaziri, Katibu Mkuundiye mtekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati, Mipango na Programu, na kwambachini ya Mwongozo huo Katibu Mkuu atafanya hivyo chini ya uongozi wa Waziriambaye ni msimamizi mkuu wa Wizara katika utekelezaji wa majukumu hayo.Hata hivyo, yakikosekana mawasiliano mazuri kati ya Waziri na Katibu Mkuukinyume na matakwa ya Mwongozo wa Baraza la Mawaziri na Katibu Mkuuakatumia madaraka yake kama yanavyoainishwa katika Kifungu cha 8(1) nivigumu sana kwa Waziri kusimamia utekelezaji wa maamuzi na shughuli zaWizara.​
7.4 Uchangishaji wa Sh.22,000,000.00 kwa Taasisi Nne (4) chini ya Wizara yaNishati na Madini kwa ajili ya Semina ya WabungeMheshimiwa Spika,​
Katika uchunguzi wake, Kamati Teule ilibaini kuwa, utaratibu wa Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha Idara zilizo chini yake haukutumikakwenye suala la uwasilishaji wa Bajeti pekee. Katibu Mkuu Wizara ya Nishatina Madini, Ndugu David Kitundu Jairo, aliziandikia pia barua Taasisi nne (4)kuomba mchango kwa ajili ya Semina ya Waheshimiwa Wabunge iliyofanyikatarehe 26 Juni, 2011 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Dodoma.​
(TazamaKiambatisho XV)
Katika barua hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliainisha kuwaushiriki wa Wizara pamoja na kukodisha Ukumbi ungehitaji Sh.39,000,000.00 naushiriki wa Waheshimiwa Wabunge Sh.46,000,000.00. Kwa mchanganuo huo,mahitaji halisi ya Semina yalikuwa Sh.85,000,000.00.​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa mujibu wa barua iliyotajwa hapo juu, kila Taasisi ilitakiwa kuchangiaSh.22,000,000.00 na kwamba kiasi hicho kilipwe kwa Bi. Hawa Ramadhani,Mhasibu wa Wizara. Taasisi hizo ni REA, EWURA, TANESCO na TPDC. Taasisi​
121​
zote zilichanga kama ilivyotakiwa na jumla ya michango ilikuwaSh.88,000,000.00.​
Mheshimiwa Spika,​
Matumizi ya fedha hizi zilizochangwa (Sh.88,000,000.00) yalikuwa kamaifuatavyo: -​
Na. Matumizi Kiasi cha Fedha(Sh.) Asilimia​
1. Posho kwa Waheshimiwa Wabunge 15,840,000.00 18​
%
2. Posho kwa watu mbalimbali 57,539,800.003. Mafuta ya magari 5,040,000.004. Chakula 4,194,200.005. Vifaa vingine 5,386,000.0082​
%
JUMLA KUU 88,000,000.00​
100%
Tanbihi​
: Posho kwa watu mbalimbali ililipwa kwa:(i) Watumishi wa Ofisi ya Bunge(ii) Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini(iii) Waandishi wa Habari(iv) Watumishi wa Afya(v) Askari PolisiKwa upande mwingine, kwa mujibu wa barua ya maelekezo iliyotolewa na Ofisiya Bunge (Tazama Kiambatisho XVI) juu ya Semina ya Wabunge kuhusu Sektaya Umeme, viwango vya posho vilielekezwa kama ifuatavyo:-(a) Viongozi wa Bunge Sh. 250,000.00(b) Wabunge (Vikao) Sh. 80,000.00(c) Wabunge (usafiri) Sh. 30,000.00(d) Wakuu wa Idara/Kazi maalum Sh. 80,000.00(e) Maofisa Sh. 50,000.00(f) Watoa huduma wengine Sh. 20,000.00
122​
Mheshimiwa Spika,​
Wakati wa kupitia nyaraka za matumizi ya michango hiyo ya Sh.88,000,000.00,Kamati Teule ilibaini kwamba baadhi ya viwango vya malipo ya posho vilikuwatofauti na maelekezo kutoka Ofisi ya Bunge. Kwa mfano, wakati WaheshimiwaWabunge walilipwa Sh.110,000.00 kila mmoja, ilionekana kuwa mtumishi wangazi ya mhudumu alilipwa Sh.120,000.00 badala ya Sh.20,000.00; Wakurugenziwalilipwa Sh.180,000.00 badala ya Sh.80,000.00; na Maofisa wengine walilipwaSh.150,000.00 badala ya Sh.50,000.00.​
(Tazama Kiambatanisho XVII)
Mheshimiwa Spika,​
Baada ya kujitokeza utata huo, Kamati Teule ililazimika kufanya mahojiano naMhasibu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyehusika kulipa posho hizo, ambayealieleza kwamba aliagizwa kwa mdomo na kiongozi wake kuwa amuongezeekila mtumishi Sh.100,000.00 ikiwa ni​
bonus kwa kazi waliyofanya ya kudurufumakabrasha ya Semina. Nyongeza hiyo ndiyo ilisababisha posho zilizolipwa kwawatumishi zisomeke kuanzia Sh.120,000.00, 150,000.00 na Sh.180,000.00badala ya Sh.20,000.00, Sh.50,000.00 na Sh.80,000.00.116
Hata hivyo baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Bunge wanaohusika na kuratibushughuli za semina za Wabunge walipohojiwa na Kamati Teule walikanakuhusika na malipo ya viwango vya posho vya Sh.120,000.00, 150,000.00 naSh.180,000.00 na kwamba wao walilipa Sh.20,000.00, Sh.50,000.00 naSh.80,000.00 kufuatana na maelekezo ya Ofisi ya Bunge.​
117
Mheshimiwa Spika,​
Ukweli uliothibitika katika suala hili ni kama ifuatavyo:-(a) Wakati Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini alidai kutengaSh.39,000,000.00 kwa ajili ya ushiriki wa Wizara na kukodisha ukumbi,Kamati Teule imethibitisha kuwa Ukumbi wa Pius Msekwa huwahaukodishwi.​
116​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 11 Oktoba, 2011.
117​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 31 Oktoba, 2011.
123​
(b) Kufuatia mahojiano kati ya Kamati Teule na baadhi ya mashahidiwaliolipwa, Watumishi waliotajwa kwamba wamelipwa Sh.120,000.00walilipwa Sh.20,000 tu; watumishi waliotajwa kwamba wamelipwaSh.150,000.00 walilipwa Sh.50,000 tu na wale waliotajwa kwambawamelipwa Sh.180,000.00 walilipwa Sh.80,000 tu. Kwa maana hiyo,malipo ya nyongeza ya Sh. 100,000/= yaliyooneshwa kwa kila mtumishi sihalisi bali ni ya kughushi. Kutokana na kughushi huko, jumla ya fedhakiasi cha Sh.13,900,000.00 ambazo ni asilimia 15% ya jumla ya fedhazilizokusanywa (88,000,000.00) ni malipo hewa.(c) Baadhi ya watumishi walioorodheshwa kuwa walipokea malipo hayohawakuwepo Dodoma siku hiyo.(d) Hata kama agizo la malipo ya​
bonus lingekuwa ni la kweli haiwezekanishughuli ya kudurufu nyaraka za semina ifanywe na Wakurugenzi wote,Maofisa wote na wahudumu wote. Hii inaonyesha kwamba namba ‘1’iliongezwa baada ya malipo halali kufanyika.(e) Tarehe 25 Juni, 2011 yalifanyika manunuzi ya Mikoba (Bags) 310 kwa ajiliya kuwekea makabrasha ya Semina ya Waheshimiwa Wabunge. Mikobailinunuliwa kwa fedha taslimu kinyume na masharti ya Kanuni 86(1) yaKanuni za Fedha za Umma, 2001 kwa kutoambatisha bei shindanishi.
Mheshimiwa Spika,​
Mazingira ya mchakato wa kukusanya Sh.88,000,000.00 na kuzitumia kwenyeSemina ya Wabunge kwa kiwango kikubwa hayatofautiani na mazingirayaliyotumika kuchangisha Sh.140,000,000 kutoka Taasisi za Wizara na kuzitumiakatika shughuli ya maandalizi na uwasilishaji wa Hotuba ya Bajeti Bungeni kamailivyobainika hapo awali katika Taarifa hii. Tofauti iliyopo ni kwamba michangoya Sh.88,000,000.00 ilipelekwa moja kwa moja kwa mtumishi wa Wizara bilakuingizwa kwenye Akaunti ya Wizara ya Nishati na Madini wala Akaunti ya GST.​
124​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inaona kwamba utaratibu wa sasa wa uendeshaji wa Semina zaWabunge unatoa mwanya kwa watendaji wasio waaminifu kufuja fedha zaumma.​
7.5 Uhusiano Miongoni mwa Mihimili ya DolaMheshimiwa Spika,​
Wakati Kamati Teule inafanya mahojiano na watu mbalimbali, Hoja kadhaazinazohusu mgawanyo wa madaraka na uhusiano wa kikazi wa Mihimili ya Dolahususan Bunge na Serikali, zilijitokeza. Baadhi ya Hoja hizo ni kama ifuatavyo:-(a) Kilichotokea Bungeni tarehe 18 Julai, 2011 ni Bunge lilikuwa likitekelezawajibu wake wa kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba.(b) Katiba yetu haitoi mgawanyo bayana wa madaraka​
(clear Separtion ofPowers) baina ya Mihimili mitatu ya Dola hususan Bunge na Serikali tofautina ilivyo katika nchi nyingine kama vile Kenya. Chini ya Katiba mpya yaKenya Serikali haimo ndani ya Bunge; Mawaziri sio Wabunge naMwanasheria Mkuu wa Serikali pia sio Mbunge.(c) Taratibu za mgawanyo wa madaraka zipo katika Katiba lakini wakatimwingine zinasahaulika na kutofuatwa ipasavyo.(d) Dhana ya mgawanyo wa madaraka haimaanishi utengano, yaani mamlakahaya hayahodhiwi na Chombo kimoja tu, isipokuwa uangalifu unahitajikakwa namna ya kutenganisha kazi za Mihimili hii mitatu vinginevyo ukouwezekano mkubwa wa kugongana.(e) Bunge limeanza kuingia katika shughuli za utendaji badala ya kuisimamiaSerikali, kwa mfano Kamati za Kudumu za Bunge badala ya kushughulikana Wizara zinakwenda moja kwa moja kwa Taasisi.
125​
(f) Kazi hii inayofanywa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza sualalililofanywa na Serikali inaonyesha kuwa Bunge sasa linaingilia kazi zautendaji (Bunge linaingia jikoni) badala ya kubaki na kazi yake yakuisimamia Serikali.(g) Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Wabunge kazi yao ni kuratibu,kuhoji na wakati mwingine kuibana Serikali ili ifanye kazi kulingana namalengo ya Katiba. Serikali inawajibika Bungeni na mambo yoteyanayofanywa na Serikali hususan yale yanayohusu fedha ni lazima yawewazi ili Bunge liweze kuchunguza kama matumizi ya fedha yanaendana nataratibu, Kanuni na masharti yanayowekwa na Sheria.(h) Ni muhimu Bunge na Serikali vifanye kazi kwa utaratibu ambao ni wamaelewano.(i) Mawanda (​
scope) ya Ibara ya 63(2) inayohusu Bunge “kuisimamia nakuishauri Serikali” hayako wazi.
Mheshimiwa Spika,​
Kutokana na Hoja zilizotajwa hapo juu, Kamati Teule imeona izungumzie, kwaufupi, uhusiano miongoni mwa Mihimili ya Dola, hususan changamoto zilizopo nanamna ya kuzishughulikia. Hata hivyo, changamoto hizo zitahusu mahusiano yakikazi kati ya Serikali na Bunge tu kwa kuwa jambo lililosababisha kuundwa kwaKamati Teule lilihusisha Mihimili hiyo miwili.Ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 pamoja namambo mengine, inaelezea dhana ya mgawanyo wa madaraka (​
Separation ofPowers) baina ya Mihimili mitatu ya Dola ambayo ni Serikali, Bunge naMahakama. Serikali ina mamlaka ya utendaji, Bunge lina mamlaka ya kutungaSheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma na Mahakama inamamlaka ya kutekeleza utoaji haki. Aidha, Ibara hii inasisitiza kwamba: -
126​
“Kila Chombo kilichotajwa katika Ibara hii kitaundwa na kutekelezamajukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katikaKatiba hii.”​
118
Mheshimiwa Spika,​
Kuhusu utekelezaji wa madaraka ya kila Mhimili, Ibara ya 35 inaelekeza kwambashughuli zote za utendaji za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa nawatumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais. Ibara ya 62 inaanzisha Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufafanua kwamba Bunge litakuwa nasehemu mbili; Rais na Wabunge. Ibara ya 63(2) inaweka wazi kwamba Sehemuya Pili ya Bunge ina madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauriSerikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba.Kwa upande wa Mahakama, Ibara ya 107A inaelekeza kwamba mamlaka yenyekauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa niMahakama, na kwamba katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, Mahakamazote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale yaSheria za nchi​
119
Katiba inafafanua kwamba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na kwambaSerikali itawajibika kwa wananchi​
120. Kufuatana na misingi ya demokrasia yauwakilishi, mamlaka ya wananchi ya kuiwajibisha Serikali yanatekelezwa naBunge, na kama ilivyoelezwa hapo awali, jukumu kubwa la Bunge ni kuisimamiana kuishauri Serikali kwa niaba ya wananchi. Katika kutekeleza jukumu hiliBunge linawauliza Mawaziri maswali kuhusu mambo ya umma ambayo yakondani ya wajibu wa Waziri husika, linajadili utekelezaji wa kila Wizara wakatiwa Mkutano wa Bajeti, linajadili na kuidhinisha mpango wa muda mrefu au
118​
Ibara ya 4(4).
119​
Ibara ya 107B.
120​
Ibara ya 8.
127​
mfupi unaokusudia kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano na kutunga Sheriaya kusimamia utekelezaji huo n.k.​
121
Mheshimiwa Spika,​
Katika kuisimamia Serikali, Bunge kama sauti ya wananchi, lina wajibu wakuzungumzia jambo lolote linalohusu uendeshaji wa Serikali yakiwemo matumiziya fedha za umma. Mipaka ya Bunge kufanya kazi zake za kuihoji na kuisimamiaSerikali na kutunga sheria ipo ndani ya Katiba na imefafanuliwa katika Kanuni zaBunge. Kwa mfano, katika kutunga Sheria, Bunge linatakiwa kuzingatiamasharti yaliyowekwa na Sehemu ya Tatu ya Katiba (Haki na Wajibu muhimu),pamoja na Ibara za 64, 98 na 99. Vilevile Kanuni za Bunge zimeweka miongozoya uendeshaji wa mijadala Bungeni.Jambo ambalo Kamati Teule imelibaini katika suala hili ni kuwa kila Mhimiliunataka kufanya kazi wenyewe na kukumbatia mamlaka yake kiasi kwambainapotokea Mhimili mwingine unahoji inaonekana kama vile Mhimili huo unatakakuingilia madaraka ya mwingine. Hii ni kinyume na ukweli kwamba kulingana namfumo wa utawala wa nchi yetu hakuna​
absolute separation of powers. Katikasuala hili Serikali inadai kwamba jukumu la kusimamia nidhamu za utumishi waumma ni la kwake na sio la Bunge, na ndio msingi wa madai kwamba kitendocha Bunge kuunda Kamati Teule kuchunguza suala ambalo kwa mtazamo waSerikali linahusu nidhamu ya watumishi wa umma ni kuingilia madaraka yasiyoya kwake. Akitoa maelezo yake mbele ya Kamati Teule, Katibu Mkuu Kiongozialisema: -
“…lipo tatizo la tafsiri, mamlaka na mipaka ya mihimili hiyo,particularly Mihimili hii miwili; Bunge na Executive kwa maana yaSerikali. We have a problem, a serious one… leo Mhimili mmojaunahojiwa na Mhimili mwingine kwa uamuzi wake; it is a very seriousproblem!...​
122 ”
121​
Ibara ya 63(3) (a) – (e).
122​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 5 Oktoba, 2011.
128​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande mwingine msimamo wa Bunge ni kuwa suala la Katibu Mkuu Wizaraya Nishati na Madini, Ndugu David Kitundu Jairo sio la kinidhamu pekee balilinahusu nidhamu na matumizi ya fedha za umma, na kwamba kwa kuwa Katibaimetoa mamlaka kwa Bunge kuidhinisha fedha zote zitakazotumika nakusimamia matumizi yake, hivyo Bunge lina wajibu wa kuingilia kati paleinapoonekana kuwa kuna vitendo vinavyoashiria matumizi mabaya ya fedha zaumma. Na kwamba Katiba imelipa Bunge mamlaka ya kuisimamia na kuishauriSerikali katika mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imebaini pia kuwepo kwa changamoto za kimawasiliano miongonimwa Viongozi Wakuu ndani ya Serikali. Katibu Mkuu Kiongozi ni Mkuu waUtumishi wa Umma na Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa ummawanaoteuliwa na Rais​
123. Waziri Mkuu ana madaraka juu ya udhibiti, usimamiajina utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri yaMuungano, Waziri Mkuu pia ni kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni124.Changamoto hii ya mawasiliano hafifu baina ya viongozi hawa imejidhihirishakatika kulishughulikia suala la Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,Ndugu David Kitundu Jairo. Suala hili liliibuka Bungeni, na kama tulivyoelezahapo awali baada ya mchakato wa kulishughulikia kukamilika kulitakiwa kuwepomawasiliano kati ya Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri Mkuu. Hata hivyo KatibuMkuu Kiongozi alieleza kwamba alichukua hatua ya kushughulikia suala la KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndugu David Kitundu Jairo, kama Mamlakaya Nidhamu na kwamba hana uhakika kama Waziri Mkuu alilieleza Bunge kuwaSerikali ingerudisha majibu Bungeni. Kwa upande wake Waziri Mkuu aliielezaKamati Teule kwamba:-
123​
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002.
124​
Ibara ya 52 ya Katiba.
129​
“… kwa mujibu wa mamlaka yake alifanya hivyo. Lakini kamanilivyokuwa nimesema kwamba, angeweza vilevile kutumia ileniliyosema yaani uhusiano na hekima ambazo zimekuwa zikitumikahapa na pale katika kupima suala gani ujumuike na viongozi wenzako.Katika jambo hili angeweza vile vile akaamua kwamba ah, katika hilingoja nimshirikishe Waziri Mkuu… lakini ukienda tu kwa mtazamo waSheria moja kwa moja, wakati mwingine tunaingia kwenye matatizoambayo yanaweza kuleta tatizo katika uendeshaji wa shughuli zaSerikali…”​
125
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inaona kuwa pamoja na kwamba kila Mhimili una kazi zake, lengokubwa ni kumhudumia mwananchi, kitendo cha Mihimili kuvutana kina atharikwa misingi ya utawala bora na kinaweza kukwamisha maendeleo. Ni maoni yaKamati Teule pia kwamba dhana ya mgawanyo wa madaraka haimaanishimamlaka yamehodhiwa na Chombo kimoja au mtendaji mmoja tu, bali Mihimiliinatakiwa ishirikiane, iheshimiane na kukosoana (​
checks and balances).
7.6 Mamlaka ya Hiari (​
Discretionary Powers) kwa Makatibu Wakuu wa Wizara naWatendaji Wakuu wa Taasisi za UmmaMheshimiwa Spika,
Katika lugha ya kawaida​
“discretionary powers” ni mamlaka ya hiari yakuchukua hatua au kufanya maamuzi kwa namna ambayo mhusika ataonainafaa (one’s own judgment). Mamlaka ya namna hii hutolewa kwa viongozi auwatendaji katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuwezesha shughuli kufanyikakwa ufanisi bila vikwazo visivyo vya lazima. Mara nyingi discretionary powers
hutolewa kwa Majaji, Mahakimu, Viongozi wa Kisiasa na Watendaji WakuuSerikalini na katika Taasisi za Umma na hata Taasisi Binafsi.​
125​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 24 Oktoba, 2011.
130​
Katika uchunguzi wake, Kamati Teule imebaini kuwa kuna upungufu katikamatumizi ya fedha za umma unaotokana na​
discretionary powers wanazopewaWatendaji Wakuu katika Wizara na Taasisi za Umma.
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imebaini kuwa baadhi ya malipo ya stahili mbalimbali kwaviongozi na watumishi wa umma hayajawekewa masharti wala viwangoambavyo vinatakiwa kuzingatiwa. Taratibu na viwango vya malipo husikahutolewa na Watendaji Wakuu kwa kadri kila mmoja anavyoona inafaa. Mfanowa stahili ambazo Kamati Teule imearifiwa kuwa hazijatolewa viwango rasmivya malipo ni Posho ya Takrima (​
Entertainment Allowance).
Kanuni L.14 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009​
, Toleo la Tatuinayohusu Posho ya Takrima (Entertainment Allowance) inasomeka kamaifuatavyo:-
“​
L.14(1) All Accounting Officers are allocated funds forentertainment under their respective items for“Government Hospitality.” This is the only provisionfrom which an Accounting Officer is required to meet hisexpenditure on any form of entertainment.
(2)​
The objective of providing funds for entertainment is toafford every Accounting Officer the ability to offerGovernment hospitality to the public servants directlyconcerned with his field of responsibility …
(3)​
It is not possible to foresee or set out all thecircumstances or occasions, which would justify the useof funds from the government hospitality vote. This isleft to the good judgment and discretion of AccountingOfficers …
131​
(4)​
A commuted entertainment allowance may be grantedfrom the central entertainment vote to a public servantwho is regularly called upon to extend hospitality onbehalf of the Government.”
Mheshimiwa Spika,​
Wakati kukiwa hakuna mwongozo wowote uliotolewa juu ya namna yautekelezaji wa Kanuni hii, hali ni tofauti kwa Kanuni L.32 inayohusu Posho yaVikao (​
Sitting Allowance). Kanuni hii inaainisha kwamba kutakuwa na Poshoya Vikao ambayo italipwa kwa kibali cha Katibu Mkuu (Utumishi) kwaMwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi na Wajumbe waTume, Bodi au Kamati iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria au iliyoundwa kwaagizo la Rais au Waziri Mkuu. Aidha, Kanuni L.33 inasomeka: -
“L.33 Sitting Allowance shall be payable per day of the sitting at arate to be determined from time to time, by the PermanentSecretary (Establishments)”​
Katika kuweka mwongozo wa viwango vya Posho hii kama inavyoelekezwa naKanuni L.33, Katibu Mkuu (Utumishi) amekuwa akitoa Waraka mara kwa mara.Waraka unaotumika hivi sasa ni​
Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 2 waMwaka 2010 kuhusu Posho ya Vikao (Sitting Allowance) wa tarehe 11Februari, 2010 ambao umeanza kutumika tarehe 1 Julai, 2010.
Mheshimiwa Spika,​
Matokeo ya kutokuwa na Waraka maalum unaofafanua viwango na taratibu zaPosho ya Takrima (​
Entertainment Allowance) ni kuwa, Wizara zimekuwa naviwango na taratibu tofauti za kulipa posho hii kwa Mawaziri na Naibu Mawazirihususan wakati wa Mikutano ya Bunge, Dodoma. Katika mahojiano na Viongozina Watendaji mbalimbali wa Wizara, Kamati Teule imekuwa ikihoji utaratibuna viwango vinavyotumika na mara zote majibu yamekuwa yakitofautiana katiya Mtendaji mmoja na mwingine.
132​
Alipoulizwa na Kamati Teule kama kuna Mwongozo wowote unaofuatwa naWizara yake katika kuwalipa Waziri na Naibu Waziri Posho ya Takrima(​
Entertainment Allowance), Mmoja wa Makatibu Wakuu wa Wizara alisemakuwa malipo hayo yanategemea hali ya fedha, na kwamba:
“…kuna kipengele kinasema discretion ya Katibu Mkuu, inategemeakutokana na hali ya fedha, kwa hiyo, sisi tumezoea tukienda kuletunajua Waziri atakuwa na wageni … mara nyingine unaweza tuukawanunulia… maji, juisi, lakini hatuna fedha … ni ngumu kumpafedha au kumpelekea vitu vingi…”​
Mheshimiwa Spika,​
Kauli hii inalingana na majibu ya Waziri mmoja ambaye alieleza kwambahajawahi kuona Waraka unaoonyesha kuwa anastahili kulipwa kiasi fulani chaPosho ya Takrima (​
Entertainment Allowance) hivyo inategemea na hali yafedha wakati mwingine anapata, wakati mwingine hapati.Waziri mwingine alipoulizwa utaratibu unaotumika na Wizara yake kuwalipaPosho ya Takrima (entertainment allowance) yeye na Naibu Waziri wakealisema:-
“…kuna Mwongozo ambao umetolewa, kwa mfano, Waziri akiendakwenye Bunge la Bajeti fedha atakazolipwa kwa ajili yaentertainment allowance ni Sh.500,000.00 na Naibu WaziriSh.400,000.00 …kwenye Bunge la kawaida tunapewa Sh.200,000.00.Hii ni kwa nyakati zile ukiwa Bungeni, kule unaweza kutembelewa namgeni…anakuja kuzungumzia juu ya barabara yake…huweziukamwangalia tu, itabidi umnunulie soda …”​
133​
Waziri mwingine tena alisema hajawahi kupewa posho hiyo na kwamba: -​
“…kwa ngazi ya Waziri ninavyojua ni kwamba, huwa kuna vituvinaitwa kama chai, ambavyo ni vya Ofisi yake, lakini sijawahi kuonainakuwa ni kama fedha as such… nimekuwa Waziri sijawahi kushikafedha kwamba hii ndiyo allowance yako, mara nyingi Ofisi ile ndiyoinasimamia, wageni wamekuja leteni juisi, kuna wageni wanapewa…”​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini Kamati Teule iliona katika nyarakana pia kwa maelezo ya Watendaji wa Wizara kuwa, kati ya tarehe 18 Julai hadi26 Agosti, 2011 wakati wa Mkutano wa Nne wa Bunge (Juni – Agosti, 2011)Waziri na Naibu Waziri walilipwa Sh.4,000,000.00 kila mmoja kama Posho yaTakrima (​
Entertainment Allowance). Katika kufafanua sababu na vigezo vyaWizara hii kulipa kiasi hiki cha fedha, Mkurugenzi wa Sera na Mipango waWizara ya Nishati na Madini alieleza: -
“…Katibu Mkuu wa Wizara anayo mandate ya kutoa entertainmentallowance kwa Maofisa hata viongozi … kwa msingi huo nilimshauriKatibu Mkuu kwamba atoe entertainment allowance, na mara nyingiKatibu Mkuu anaweza kutoa kiasi chochote ambacho anafikiria.Lakini tuliona kwa kipindi ambacho kilikuwa kimebaki Mawaziri wetupamoja na matatizo ambayo yalikuwa yametokea wasijisikiewapweke sana waweze kuendelea kufanya kazi zao kwa amani…”​
Mheshimiwa Spika,​
Baada ya kubaini kuwepo kwa tofauti kubwa ya viwango vya posho ya Takrimavilivyolipwa na Wizara hii ikilinganishwa na Wizara nyingine Kamati Teuleililazimika kufanya mahojiano ya kina zaidi na Mkurugenzi huyu kamaifuatavyo:-​
134​
“Swali: Huu utaratibu ni wa Wizara ya Nishati na Madini peke yenu kwa sababu bahatinzuri tumeongea na Wizara nyingi na hawana utaratibu kama huo. Weweunasema nini kuhusu hilo?Jibu: Huu sio utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini peke yake, upo kwenyeWizara nyingi na Katibu Mkuu anaangalia na kama nakumbuka hiyo​
Circular auSheria nadhani inasema “na Kama Fungu linaruhusu”.Swali: …Kwahiyo Sh.4,000,000.00 maana yake kila siku ni shilingi ngapi?Jibu: Shilingi laki tano.Swali: Shilingi laki tano kwa siku?Jibu: Entertainment per day.Swali: Hesabu hizo ni shilingi ngapiJibu: Kwa siku nane Sh.4,000,000.00 kila mtu.Swali: …huoni kwamba huu ni ubadhirifu kwa kiasi fulani? Kwa sababu wenzako waWizara zingine ni Sh.500,000.00 kwa muda wote na wengine hawana kabisa…Jibu: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria au Kanuni hiyo inayotumika inasema kamaanalo fungu…Katibu Mkuu anayo mamlaka ya kuweza kutoa viwango kulinganana Fungu alilonalo na ameangalia mazingira …”126
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na matumizi haya yakuwalipa Mawaziri Posho ya Takrima (​
Entertainment Allowance)
inayotofautiana na Wizara nyingine kwa kiwango kikubwa sana kwa kutumia​
discretion​
ya Katibu Mkuu, Kamati Teule pia imebaini kuwa ni Wizara hii pekeeiliyoiarifu Kamati kwamba watendaji wake wakienda kwenye Vikao vya Bunge,Dodoma wanalipwa Posho ya Kikao (Sitting Allowance) pale wanapokaakuchambua Hoja za Wabunge. Wakati wa Mkutano wa Nne wa Bunge kwa mudawa siku tano (5) kuanzia tarehe 14 Julai hadi 18 Julai, 2011, Wizara ilitumia
126​
Hansard ya Kamati Teule, tarehe 11 Oktoba, 2011.
135​
jumla ya Sh.127,820,000.00 kuwalipa​
Sitting Allowance Watendaji wa Wizarana Taasisi waliokuwa Bungeni, Dodoma.
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule ilipitia pia Kanuni za Fedha za baadhi ya Taasisi na kubaini kuwazipo ambazo zinatoa mwanya wa matumizi mabaya ya fedha za umma. Kwamfano, Kanuni za Fedha za REA na EWURA (Kanuni 16.4 na 16.4.1) zinaelezakwamba hakuna shughuli au matumizi yatakayoruhusiwa nje ya Mpango Kaziwa Mwaka na Bajeti isipokuwa tu kwa idhini ya Mtendaji Mkuu au Bodi. Kanunihizi zinafanana neno kwa neno na zinasomeka kama ifuatavyo: -​
“…No activity may be carried out or expenditure be incurredwithout its prior inclusion in the annual plan and budget exceptapproval has been obtained from the DG or Board.”​
Kamati ilipotaka kupatiwa ufafanuzi kuhusiana na kiasi cha fedha nje ya Bajetiambacho Mtendaji Mkuu anaweza kuidhinisha kwa mujibu wa Kanuni iliyotajwahapo juu, iliarifiwa kuwa hakuna ukomo, isipokuwa tu baada ya matumizitaarifa inabidi itolewe kwa Bodi.​
Mheshimiwa Spika,​
Hatari na athari za kutoa uhuru mkubwa kama huu ni kuwa, inapotokea Taasisikuongozwa na Kiongozi mbinafsi upo uwezekano wa yeye kutumia fedha zaumma kwa maslahi binafsi kwa kisingizio cha kuwepo kwa mahitaji muhimuambayo yanajitokeza nje ya Mpango Kazi na Bajeti hivyo yeye kutumiamamlaka yake na kuyaidhinisha.Pamoja na matumizi ya fedha kama ilivyofafanuliwa hapo juu, Kamati Teuleimebaini kuwa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wana uwezo hata wakupindisha maamuzi ya Makatibu Wakuu kwa madai hayo hayo ya​
“discretionary powers.”​
Mfano, wakati wa maandalizi ya kwenda Dodoma kwaajili ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa Wizara alitoa
136​
maelekezo kuhusiana na idadi ya watendaji wanaotakiwa kwenda Dodomakwenye Mkutano wa Bunge la Bajeti. Katibu Mkuu alielekeza kwamba Maofisa44 kutoka Wizarani na 17 kutoka kwenye Taasisi ndiyo wameidhinishwa kwendaDodoma​
127. Hata hivyo, idadi ya watendaji waliokwenda Dodoma waliongezekakutoka jumla ya Watendaji 61 walioidhinishwa hadi kufikia 243.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Taarifa ya UkaguziMaalum anaeleza kwamba hapakuwa na idhini kwa Maofisa walioongezeka kwakuwa kila Mkuu wa Taasisi alikuwa na uamuzi wa kuwaita Maofisa wa ziadakadri alivyoona inafaa.128 Aidha, watumishi wote waliokwenda Dodoma bilakujali idadi yao wala shughuli iliyowapeleka walilipwa posho za vikao.Wakati wa mahojiano na Kamati Teule kuhusu Discretionary Powers, Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alieleza kutoridhishwa kwake namiongozo ambayo inatoa mamlaka makubwa kwa Watendaji Wakuu na kwambamiongozo hiyo ina mianya ambayo inaweza kusababisha ubadhirifu wa fedha zaUmma. Akitoa maelezo yake mbele ya Kamati Teule, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali alisema:
“…katika kaguzi zangu hata huko nyuma nimeshauri kwamba, kunahaja kusema kweli Utumishi kuwa more explicit katika kutoaMiongozo yao kwa sababu kuna Miongozo ambayo inaachia toomuch power kwa Accounting Officer. Issue ya honorarium, issue yaentertainment allowance, issue ya ni kikao kipi, ukisoma uleMwongozo wa Utumishi uko loose and therefore ni Mwongozo ambaounaweza ukawa misused…”​
127​
Barua Kumb. Na. EB.35/88/01 ya tarehe 6 Julai, 2011.
128​
Taarifa ya Ukaguzi Maalum Ukurasa wa 13.
137​
Mheshimiwa Spika,​
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Kamati Teule inaona umuhimu kwa WatendajiWakuu kupewa uhuru na mamlaka ya kuamua mambo kwa kiwango fulani kwakutumia busara zao. Hata hivyo, Kamati Teule inapendekeza kuwa Serikaliihakikishe kwamba​
discretionary powers zinawekewa utaratibu na mipakamaalum ili zisiwe chanzo cha matumizi mabaya ya madaraka na fedha zaumma.
Mheshimiwa Spika,​
Kwa muda iliyopewa na kwa kukidhi mahitaji ya Hadidu za Rejea ilizopewa,Kamati Teule imepitia Taasisi chache tu za mfano lakini Serikali ikifanyautafiti zaidi kuhusiana na Kanuni za Fedha na utendaji wa Taasisi za Umma,inaweza ikagundua mengi zaidi.​
138​
8.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika​
,Kamati Teule imekamilisha uchunguzi kuhusu utaratibu uliobainika wakukusanya fedha kwa ajili ya maandalizi na uwasilishwaji wa Hotuba za Bajetiza Wizara Bungeni. Kamati Teule imekamilisha jukumu hilo kwa kufanyamahojiano na watu 146, kupitia Katiba, Sheria, Kanuni na nyaraka mbalimbali,kupitia na kuchambua Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kukusanya taarifa mbalimbali kwa njiaya Dodoso kama ilivyoonyeshwa katika utangulizi wa Taarifa hii.Matokeo ya uchunguzi huu yamebainisha kwamba utaratibu wa Wizarakuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasilisha Hotuba ya Bajeti yake Bungenihaukuwa wa kawaida na haukujengwa katika misingi yoyote ile kisheria.Halikadhalika, fedha zilizokusanywa zilitumika kwa ajili ya matumizi ambayoyasingehitaji uchangishaji kwa sababu yangeweza kugharimiwa na kasmazilizopo za Wizara.
Mheshimiwa Spika,​
Katika kupitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikaliKamati Teule imebaini kuwa licha ya kuonyesha upungufu wa aina mbalimbalikatika kuendesha zoezi la uchangishaji na matumizi ya fedha hizo, Taarifa hiyohaikuweza kuweka bayana kama uchangishaji huo ulikuwa halali au vinginevyokatika kutoa ushauri na hitimisho. Aidha, pamoja na upungufu wa Taarifa hiyoKatibu Mkuu Kiongozi hakuitumia ipasavyo na kusababisha kumsafisha KatibuMkuu Wizara ya Nishati na Madini.​
Mheshimiwa Spika,​
Katika hatua nyingine Kamati Teule ilibaini kuwa kitendo cha Katibu MkuuKiongozi kufanya Uchunguzi wa Awali kuhusu suala la Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini Ndugu David Kitundu Jairo kilikuwa sahihi kwa kuwa yeyendiye Mamlaka yake ya Nidhamu. Kuhusu suala la kutoa taarifa kwa Vyombo​
139​
vya Habari, Kamati Teule haikuweza kuthibitisha kuwa, kitendo cha taarifakutolewa kwa Vyombo vya Habari wakati bado Bunge halijapewa taarifakimeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge kisheria. Hata hivyo, kwakuwa suala hili lilianzia Bungeni, na kwa kuwa kulikuwa na mawasiliano kati yaWaziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuanza kwa mchakato waUchunguzi wa Awali, hivyo basi, Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa na wajibu wakuhakikisha kwamba Bunge kupitia kwa Waziri Mkuu linapata Taarifa yamatokeo ya Uchunguzi wa Awali kabla hajaitoa kwa Vyombo vya Habari.​
Mheshimiwa Spika,​
Kuhusu nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi ya Makatibu Wakuu katikakushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua, Kamati Teule imegunduaupungufu katika Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake. Upungufu huounahusu madaraka makubwa ya Katibu Mkuu Kiongozi katika mchakato mzimawa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Makatibu Wakuu bila kuishirikishaMamlaka ya Uteuzi ambaye ni Rais, na Waziri Mkuu ambaye ni Msimamizi wasiku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali.Kamati Teule pia imepitia masuala mengine mbalimbali yanayohusiana naHadidu za Rejea kama ilivyoainishwa katika Sehemu ya 7.0 ya Taarifa hii.​
140​
9.0 MAONI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI TEULE9.1 Maoni ya Kamati TeuleMheshimiwa Spika,​
Utaratibu wa uchangishaji wa fedha uliofanyika katika Wizara ya Nishati naMadini haukuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni zaFedha za Umma. Vile vile, uchangishaji huo ulisababisha Taasisi kubebeshwamzigo kwa kuwa hazina kasma mahsusi kwa ajili ya kuichangia Wizara kwa ajiliya maandalizi na uwasilishaji wa Bajeti Bungeni. Kamati Teule imeridhika piakwamba huo siyo utaratibu wa kawaida kama ilivyoelezwa na Katibu MkuuKiongozi katika Taarifa yake kwa Umma kupitia Vyombo vya Habari kuhusuUchunguzi wa Awali.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imeridhika kwamba Taasisi zilizochanga hazikuwa na kasmamahsusi, badala yake zimetoa fedha kwenye kasma zisizohusika kwa matumizihayo. Kwa mfano TANESCO ilitoa fedha kutoka katika kasma ya​
Donations andSubscriptions, TPDC ilitoa kwenye kasma ya Gas Revenue, REA ilitoa kwenye
Preparation of REA Business Plan and Budget​
na EWURA ilitoa kwenye kasma yaElimu kwa Umma. Ni dhahiri kwamba kasma zilizotoa fedha hizo hazikuwezakukamilisha majukumu yaliyokusudiwa kikamilifu.
Mheshimiwa Spika,​
Nyaraka za matumizi halisi zinaonyesha kuwa fedha zilizokusanywa zimetumikakwa ajili ya malipo ya posho ya kujikimu kwa watumishi 69 wa Wizara, posho yavikao kwa watumishi 243 waliokuwa Dodoma, manunuzi ya chakula, manunuziya vifaa vya kuandikia, malipo ya Takrima kwa Waziri na Naibu Waziri namanunuzi ya mafuta kwa ajili ya magari, matumizi ambayo yangewezakugharimiwa na kasma husika za Wizara bila kuhitaji kuchangisha.​
141​
Aidha, Nyaraka zilizowasilishwa hazikuonyesha kuwepo kwa malipo kwaWaheshimiwa Wabunge ambayo yangeashiria rushwa. Vile vile imethibitikakuwa, licha ya fedha hizo kukusanywa kinyume cha taratibu, fedhazilizochangwa zimetumika kwa matumizi yasiyo ya lazima na kwa ubadhirifu.​
Mheshimiwa Spika,​
Katika kutoa ushauri na hitimisho la Taarifa yake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali hakujibu Hadidu ya Rejea kuhusu uhalali wa michango hiyona matumizi ya fedha zilizokusanywa kama alivyopewa na Katibu MkuuKiongozi. Badala yake alihitimisha na kutoa ushauri wa Taarifa yake kwakujikita kwenye idadi ya Taasisi kuwa siyo 20 na kiasi cha fedha kilichochangwakuwa siyo Sh.1,000,000,000.00. Hatua hii ilikuwa ni ya upotoshaji mkubwawakati Taarifa ilikuwa na maudhui ambayo yangeweza kuonyesha makosa yakinidhamu kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, Taarifa hiyohaikuweza kubainisha matumizi ya jumla ya Sh.190,823,120.00 ambazozimebainishwa na Kamati Teule.​
Mheshimiwa Spika,​
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi alitumia hitimisho hilo lililotolewa naMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuacha sehemu kubwa yamaudhui yaliyomo kwenye Taarifa ya Ukaguzi Maalum ambayo kamayangetumika vizuri yangebainisha makosa ya kinidhamu kwa mujibu wa Sheriana Kanuni za Utumishi wa Umma. Kamati Teule imeridhika kwamba KatibuMkuu Kiongozi alitumia hitimisho hilo lisilokidhi haja kwa makusudi yakumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na kuupotosha umma.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imeridhika kwamba hatua ya kufanya Uchunguzi wa Awaliiliyochukuliwa na Katibu Mkuu Kiongozi dhidi ya Ndugu David Kitundu Jairo nisahihi kwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwaMakatibu Wakuu wote kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002 naKanuni za Utumishi wa Umma, 2003.​
142​
Waziri Mkuu kama Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni alichukua hatua yakuhamisha suala la Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Ndugu DavidKitundu Jairo kutoka Bungeni ili likafanyiwe kazi na mamlaka husika naWabunge kuridhia hatua hiyo. Ni maoni ya Kamati Teule kwamba Katibu MkuuKiongozi angetumia busara ya kawaida kuona umuhimu wa kuliarifu Bungematokeo ya Uchunguzi wa Awali kupitia Waziri Mkuu kabla ya kutoa matokeohayo kwa Vyombo vya Habari kwa kuzingatia kuwa suala hili liliibuliwa Bungeni.Kwa kufanya hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi angeendeleza dhana ya kuimarishamahusiano mazuri, kuheshimiana, kuelewana na kuaminiana baina ya Mihimilihii miwili ya Dola. Kitendo cha kutoliarifu Bunge kimesababisha Waziri Mkuuabakie na deni la kuliarifu Bunge matokeo ya hatua zilizochukuliwa na Mamlakaya Uteuzi.​
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kuwa kitendo cha Taarifa kutolewa kwa kutumiaVyombo Vya Habari wakati Bunge halijapewa taarifa kimeathiri dhana ya hakiza Bunge kwa kuwa Bunge limepokonywa haki ya kupata taarifa na kukamilishasuala lililolianzisha na ambalo kwa kiasi kikubwa limehusu matumizi ya fedhaza umma ambayo usimamizi wake kwa mujibu wa Katiba ni jukumu la Bunge.Aidha, kitendo hicho hakikumtendea haki Kiongozi wa Shughuli za SerikaliBungeni kwa kuwa alikuwa ametoa kauli Bungeni kuwa atalifikisha suala hilokwa mamlaka za juu na Bunge lilikuwa bado linasubiri majibu yake.Aidha, kwa vile Katibu Mkuu Kiongozi alitumia maneno “vyombo vipo” wakatialipokuwa anajaribu kufafanua juu ya uwezekano wa Katibu Mkuu Wizara yaNishati na Madini kuchukua hatua dhidi ya Mhe. Beatrice Shellukindo, (Mb.) kwa​
defamation​
, Kamati Teule imeridhika kwamba, maneno hayo yalimaanishachombo zaidi ya kimoja, kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madiniangeweza kwenda mahakamani au kwenye chombo kingine chochote nje yaBunge. Pamoja na kwamba ni haki kwa kila raia kwenda mahakamani manenohaya ambayo yalionekana kuwa ni ushauri kwa Katibu Mkuu wa Nishati naMadini yalikuwa yanachochea ukiukwaji wa Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri
143​
ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Haki, Kinga naMadaraka ya Bunge, Sura ya 296.​
Mheshimiwa Spika,​
Ni maoni ya Kamati Teule kwamba, kwa kuwa suala la nidhamu ya wateule waRais ni nyeti na pana, si vema suala hilo kuwa mikononi mwa mtu mmoja.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inaona kuwa kuna wigo mpana sana wa Nyaraka za Serikalizinazoitwa za siri jambo ambalo limetoa nafasi kwa baadhi ya watendaji wasiowaaminifu kufanya maovu kwa kujificha katika mwamvuli huo wa usiri. Aidha,Kamati imeona kuwa kukosekana kwa Sheria ya kuwalinda watoa taarifa(​
Whistleblowers) kunalinyima Taifa fursa ya kubaini na kuyashughulikia maovuhayo kwa wakati na kwa ufanisi.
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inaona kwamba kuna haja ya kuzingatia zaidi upeo, sifa, uzoefu,taaluma, maadili na uzalendo katika nafasi za uteuzi. Vile vile vijana wenyesifa wapewe nafasi katika ajira mpya na wastaafu kwa upande wao waandaliwena kuhamasishwa kuanzisha shughuli katika Sekta binafsi zitakazozalisha ajira.​
Mheshimiwa Spika,​
Utaratibu wa sasa wa kila Wizara au Taasisi kugharamia na kuendesha Seminakwa Wabunge unatoa mwanya kwa wanaoratibu semina hizo wasio waaminifukutumia fursa hiyo kama njia ya kujipatia na kutumia fedha hizo kwa manufaabinafsi.​
Mheshimiwa Spika,​
Inapotokea Mihimili kuvutana kunakuwa na athari katika misingi ya utawalabora, hali ambayo inaweza kukwamisha maendeleo hasa ikizingatiwa kwambadhana ya mgawanyo wa madaraka haimaanishi Mhimili mmoja kuhodhimadaraka hayo na kuweka kuta kati yake na Mihimili mingine badala yake ni​
144​
dhana ya Mihimili kushirikiana, kuheshimiana na kukosoana (​
Checks andbalances).
Mheshimiwa Spika,​
Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotoa mamlaka ya hiari (​
Discretionary Powers)zinawaachia Maofisa Masuuli mwanya, ambao unaweza kusababisha matumizimabaya ya fedha za umma na kuisababishia Serikali hasara.
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule imeona kwamba ni muhimu mahusiano ya kikazi baina ya Waziriambaye ni Msimamizi Mkuu wa Wizara na Katibu Mkuu ambaye ni Mtendaji Mkuuwa Wizara yawe mazuri ili kuleta ufanisi ndani ya Wizara na Serikali kwaujumla. Hii itawezekana tu kama viongozi hawa watafanya kazi kwakuwasiliana, kushauriana na kushirikiana kama Mwongozo wa Baraza laMawaziri unavyoelekeza, tofauti na ilivyofanyika katika suala la kuchangishafedha katika Wizara ya Nishati na Madini.Katika suala la uchangishaji wa fedha uliofanywa na Wizara ya Nishati naMadini, Kamati Teule baada ya kukamilisha uchunguzi kwa kupitia nyarakambalimbali na kufanya mahojiano na watu mbalimbali, haikuweza kuthibitishamoja kwa moja ushiriki wa Waziri au Naibu Waziri katika kubariki aukuidhinisha uchangishaji huo. Hata hivyo, kutokana na kazi za Waziri kamazilivyoainishwa katika Mwongozo wa Baraza la Mawaziri, Waziri alipaswakufahamu kilichoendelea Wizarani kwake kwa sababu yeye ndiye MsimamiziMkuu wa Wizara.​
145​
9.2 Mapendekezo ya Kamati TeuleMheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inapendekeza Bunge likemee kwa nguvu zote utaratibu wauchangishaji huu uliofanywa na Wizara ya Nishati na Madini na kwambauchangishaji wa fedha wa aina yoyote lazima uzingatie Sheria, Kanuni naTaratibu za fedha.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inapendekeza kwamba Serikali ichukue hatua za kinidhamu kwaNdugu David Kitundu Jairo kwa matumizi mabaya ya madaraka, kukusanya nakutumia fedha za Serikali kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za Fedha zaUmma na kuruhusu matumizi mabaya ya fedha za Umma. Vile vile Serikaliiwachukulie hatua za kinidhamu, kwa mujibu wa Sheria, watumishi wote waWizara ya Nishati na Madini waliotajwa kwenye Taarifa hii kushiriki kwa namnambalimbali katika mchakato wa uchangishaji na matumizi ya fedha hizi zaumma.Aidha, kwa kuwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Baraza la Mawaziri Waziri ndiyeMsimamizi Mkuu wa Wizara, hivyo suala la uchangishaji halikupaswa kufanyikabila yeye kufahamu, Kamati Teule inapendekeza Serikali ichukue hatuazinazofaa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. William Ngeleja, (Mb.).​
Mheshimiwa Spika,​
Katika suala la Ndugu David Kitundu Jairo, Kamati Teule imesikitishwa sana najinsi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alivyoshindwa kutekelezawajibu wake kikamilifu, hususan katika kutoa ushauri na hitimisho katika ripotiyake na jinsi alivyotoa taarifa kwenye Vyombo vya Habari. Kwa kufanya hivyo,ameshindwa kulisaidia Bunge na Umma kwa ujumla, badala yake amekuwa nisehemu ya kuficha maovu. Hivyo, Kamati Teule inapendekeza Serikali ichukuehatua zinazofaa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwaupotoshaji huo.​
146​
Mheshimiwa Spika,​
Katibu Mkuu Kiongozi kwa makusudi aliamua kumsafisha Ndugu David KitunduJairo kwa kuficha ukweli wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuamua kwamba Ndugu DavidKitundu Jairo hakuwa na kosa la kinidhamu, kitendo ambacho kimeupotoshaUmma wa Watanzania. Kamati Teule inapendekeza Serikali ichukue hatuazinazofaa kwa Katibu Mkuu Kiongozi.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inapendekeza kwamba, kwa kuwa tunakaribia kuingia katikaMchakato wa mapitio ya Katiba, wananchi wajadili kwa kina na kuainishataratibu zinazotakiwa kuzingatiwa na Mihimili mitatu ya Dola nchini katikakutekeleza majukumu yao, hususan: -(a) Muundo wa Bunge kuhusu utaratibu wa sasa wa Serikali kuwa ndani yaBunge (Mawaziri kuwa Wabunge) au vinginevyo.(b) Mawanda (​
Scope) ya Mamlaka ya Bunge kuisimamia na kuishauri Serikali.(c) Mawasiliano baina ya Mhimili mmoja na mwingine hasa katika mamboyanayogusa haki na madaraka ya Mhimili zaidi ya mmoja.(d) Mipaka na ushirikishwaji wa mamlaka mbalimbali ndani ya Mhimilimmoja wa Dola katika utekelezaji wa majukumu.(e) Taratibu za Mihimili ya Dola kusimamiana, kurekebishana na kukosoanabila ya kuathiri masharti ya Sheria na Katiba (Checks and balances).
147​
Mheshimiwa Spika,​
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo zifanyiwe marekebisho ili kutoa nafasi kwaMakatibu Wakuu kuwashirikisha Mawaziri (​
consultation) katika maamuzi yakiutendaji hasa katika matumizi ya fedha. Hatua hii itawapa fursa Mawazirikuweza kutekeleza vizuri zaidi majukumu yao wakiwa kama wasimamizi wakuuwa maamuzi na shughuli za Serikali Wizarani.
Mheshimiwa Spika,​
Serikali ifanye mapitio ya Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni zake ilikurekebisha maeneo yote ambayo yameonekana yana upungufu. Kwa mfano,Kanuni ya 36 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 ifanyiwe marekebisho ili:​
•​
kuweka wazi utaratibu wa Mamlaka ya Nidhamu (Disciplinary Authority)kufanya Uchunguzi wa Awali (Preliminary Investigation).
•​
kuonyesha wazi muundo na idadi ya wajumbe wa chombo kinachopaswakufanya Uchunguzi wa Awali kama ilivyo kwa Kanuni ya 46 inayohusuKamati ya Uchunguzi.Vile vile, Kanuni ya 46 Kifungu kidogo cha (3) hakipo, badala yake kuna 46(1),(2), (4) na (5) hivyo Kanuni hii iangaliwe na kurekebishwa kama inavyofaa.
Mheshimiwa Spika,​
Kwa kuwa suala la nidhamu kwa Wateule wa Rais ni nyeti na pana Kamati Teuleimeona kuwa si vema suala hilo kuachwa mikononi mwa mtu mmoja kama ilivyosasa katika Sheria ya Utumishi wa Umma. Kamati Teule inapendekeza:-(a) Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Raisinaposhughulikia masuala ya nidhamu ifanye hivyo kwa kumuarifu Raisambaye ni Mamlaka ya Uteuzi na Waziri Mkuu ambaye ni Msimamizi wasiku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali, au(b) Serikali iunde Chombo maalum cha kushughulikia masuala ya nidhamukwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Rais.​
148​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inapendekeza Bunge lijadiliane na Serikali kuhusu namna bora yakuendesha semina kwa Wabunge ikiwemo kutenga kasma mahsusi ndani yaMfuko wa Bunge na kusisitiza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika matumizi yafedha.​
Mheshimiwa Spika,​
Kuhusu Waraka Namba 3 wa Mwaka 2011 wa Katibu Mkuu Hazina na MlipajiMkuu wa Serikali, Kamati Teule inapendekeza kuwa Serikali isisitize MaofisaMasuuli wote wazingatie maudhui ya Waraka huo ikiwa ni pamoja nakutoendesha uchangishaji wa fedha bila kibali cha Waziri wa Fedha.​
Mheshimiwa Spika,​
Kamati Teule inapendekeza kuwa Serikali itoe Mwongozo kuhusu malipo yaPosho ya Takrima (​
Entertainment Allowance) na Honoraria ili kuainishaviwango vya posho hizo. Mwongozo huo utolewe mara kwa mara kulingana nahali halisi. Kwa upande wa Taasisi za Wizara, Serikali ifanye uchambuzi waKanuni zao za Fedha, kubaini upungufu unaotokana na matumizi ya Kanuni hizona kuweka utaratibu wa kuziba mianya ya matumizi yasiyofaa.Aidha, Kamati Teule inapendekeza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya SheriaNdogo iongezewe uwezo na muda kupitia Kanuni hizo ili kubaini upungufu kwawakati na kupendekeza marekebisho.
Mheshimiwa Spika,​
Serikali itoe mwongozo kuhusu idadi ya Maofisa wanaopaswa kwenda Dodomakwa ajili ya Mikutano ya Bunge na katika Mwongozo huo Serikali isisitizematumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) yakiwemomatumizi ya simu na baruapepe ili kupunguza idadi ya watumishi na kubanamatumizi.​
149​
10.0​
SHUKRANIMheshimiwa Spika,Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani kwa Bunge letu Tukufu la Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu na kupitisha Azimio la kuundwakwa Kamati hii Teule. Vile vile kwa moyo wa dhati kabisa nachukua fursa hiikukushukuru wewe binafsi kwa kutuamini na kutupatia heshima kubwa kwakututeua kuwa Wajumbe wa Kamati hii.
Mheshimiwa Spika​
,Kipekee napenda kuchukua fursa hii kumshukuru kwa dhati kabisa Waziri Mkuu,Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, (Mb.) ambaye pamoja na shughuli nyingi naratiba ngumu alikubali kutenga muda wake na kuitikia wito wa kuja mbele yaKamati Teule.Napenda pia kuwashukuru sana Watendaji Wakuu na watumishi wote wa Wizaraya Nishati na Madini na Taasisi zake kwa kutupa ushirikiano wa dhatiuliotuwezesha kufanikisha uchunguzi katika suala hili.Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kwa watumishi wote wa umma katikangazi mbalimbali waliokuja mbele ya Kamati Teule, Wanazuoni waliobobeakatika masuala mbalimbali yanayohusiana na mada ya uchunguzi huu, Spika waBunge Mstaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Mawaziri, Wabunge, Makatibu waBunge Wastaafu, Makatibu Wakuu, Asasi za Kiraia na wengineo kwa kutupatiaushirikiano katika mahojiano na mashauriano wakati wa kipindi chote chauchunguzi uliofanywa na Kamati hii.Shukrani zangu ziende pia kwa Makatibu wa Bunge la Uingereza (House ofCommons) na Bunge la Australia (House of Representatives) kwa mchango waoambao umekuwa wa manufaa katika utekelezaji wa majukumu ya Kamati hii.
150​
Mheshimiwa Spika,​
Mwisho, lakini si kwa umuhimu napenda kutoa shukrani za dhati kwa Katibu waBunge, Dkt. Thomas Didimu Kashililah kwa kuiwezesha Kamati hii kufanya kaziyake vizuri na kuikamilisha kwa wakati. Aidha, kwa namna ya pekee, kwaniaba ya Kamati Teule napenda kumshukuru Katibu wa Kamati Ndugu NenelwaMwihambi Wankanga pamoja na wasaidizi wake Ndugu Lukago AlphonceMadulu, Ndugu Asia Paul Minja na Ndugu Mswige Dickson Bisile. Napenda piakuwashukuru wafuatao: Ndugu Ashura Kalikwendwa Waijaa, Ndugu FelicianaLaurent Mabada, Ndugu Germina Mponzi Magohe, Ndugu Amon Kasyanju, NduguAbdallah Selemani Mwinyipembe na Ndugu Shabani Mussa, pamoja na Wajumbewote wa Sekretarieti kwa ujumla kwa kushirikiana na Kamati hii katika shughuliza siku hata siku na hatimaye kukamilika kwa Taarifa hii.​
Mheshimiwa Spika,​
naomba kutoa Hoja.(Eng. Ramo Matala Makani, Mb.)
MWENYEKITIKAMATI TEULE YA BUNGE​
Novemba, 2011​
1
 
Back
Top Bottom