Report: Operation denazification in Ukraine Phase II

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,769
24,197
Report ya kinacho endelea huko ukrine kwa mheshimiwa zelensky

Ni siku kadhaa tangu kuanza kwa operation phase ii .... Huko Ikulu ya Kremlin , ambapo amezuru waziri wa Ulinzi Jenerali Shoigu na kupokelewa na Rais Putin.

Jenerali Shoigu alitoa taarifa ya vita, Kwanza anaanza kwakusema Mji muhimu wa kibiashara na kimbinu mji wa Bandari wa Mauripol umekombolewa kwa asilimia 100 na sasa uko mikononi mwa Majeshi ya Ukombozi wa Jamhuri ya Donetsk.

Pili anasema wale mamluki walioteka raia kama kinga na kujificha katika kiwanda maarufu cha Azovstal Steel wameuawa na raia 142 wamekombolewa, kwasasa kiwanda hicho chenye ukubwa wa kilomita 15 kiko mikononi mwa Moscow salama. Wachache bado wamejificha ndani ya kiwanda hicho na muda mchache raia wataokolewa.

Hatua ya tatu Jenerali Shoigu anamwambia Rais kwamba Sasa Jamhuri ya Donetsk imekombolewa kwa 98% na matarajio ni kwa siku tatu zijazo na kwamba Urusi inaweza sasa kufungua ubalozi wa Kidiolomasia rasmi katika Nchi hiyo huru.

Katika majibu yake, Rais Putin amesema Raia wote waliookolewa wahakikishiwe usalama na hifadhi ya kudumu Moscow, Na kwamba wanajeshi wote wa Ukraine waliojisalimisha katika oparesheni hiyo wahakikishiwe uhai wao, na wale wanaoendelea kukaidi wasinyimwe haki yao ya ahera kwasababu ni haki ya kila muombaji na apewe sawa sawa na ombi lake, asitoroke hata nzi tu kutoka katika kiwanda hicho. Hatua nyingine Rais Putin ameitanga rasmi kuwa 21/4/2022 kuwa siku ya uhuru wa Mauripol.

Upande wa pili Wakati Marekani ikiendelea kuuza shehena ya silaha za mabilioni kwa Ukraine, Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa na wasiwasi kama washirika NATO wataendelea kuunga mkono kuendelea kumkabili Putin, Ikulu ya White House imeonyesha wasiwasi kwamba kiwango na kuvu za kumkabili Putin zinapungua wakitazama msimamo wa Ujerumani ni kama unapungua kwa hatua yake ya kukataa kuweka vikwazo vya mafuta na gesi.

Pili ni uchaguzi Ufaransa na kwamba Macron ameelekeza nguvu zaidi kwenye uchaguzi na tatu ni China inaivuta Marekani kuelekeza macho katika mgogoro wa Taiwan na kukosa umakini kwa Ukraine. Lakini kauli za Waziri Mkuu Boris kwamba kupoteza muda kujadiliana na Putini ni sawa na kujadiliana na Mamba huku umeweka mguu wako mdomoni mwa mamba, kauli inayoonyesha Uingereza kukata tamaa na mambo ya Ukraine. Marekani inahofu kwamba huenda vita ikichukua muda mrefu itajikuta iko pekee yake tu EU wengi wataingia mitini.

Rais wa Chechnia Ramazan Kadyrov amempigia simu Rais Putin na pia amezungumza kiongozi wa Donetsk Luten Kanali Denis Pushilin na kuwapongeza kwa ushindi wa mji wa Mauripol na Donetsk kwa ujumla wake. Ramazan amemtakia uongozi mwema Denis akimhakikishia ushirikiano na ulinzi kwa viwango vyote vya Moscow.

Baada ya Oparesheni ya Mauripol kukamilika kwa , Oparesheni inayoendelea kwa sasa ni maeneo ya Jamhuri ya Luhansk katika mikoa ya Kharkov. Kuvu kubwa inaelekezwa huko kuhakikisha ndani ya saa kadhaa nako kunakombolewa, upinzani uko wa kutoka lakini Jenerali Alexander Dvornikov mkuu wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine aliyeongoza opareshe ngumu ya Mauripol kwa saa 36 amesema wanatarajia kukumbana na upinzani lakini uhuru wa Luhansk utasherekea saa zijazo.

Video ya pili ni sherehe za ushindi mjini Mauripol, Kifaru aina ya T-80BV kinapiga nolinda/misere ya kusherekea ushindi.

Tuendelee kuvuta subira macho na masikio yako Luhansk sasa.

...............................

Siku ya 57 tangu oparesheni ya Urusi nchini Ukraine ianze, na ni siku ya nne tangu tangu phase 2 ya oparesheni ianze.

Leo oparesheni imehamia kaskazini mashari mwa Ukraine katika Jimbo la Luhansk ambalo limejitenga na kuwa Jamhuri ya Watu wa Luhansk. Oparesheni ya leo imefanikisha kukamata maeneo mengi muhimu.

Kwanza Majeshi yaliyosalia kule kusini katiks nchi ya Donetsk wameendeles kusafisha mji kwa mapambano ya hapa na pale, na pili wameendelea kulinda kiwanda cha Azovstal Steel na kuhakikisha hakuna mamluki anatoka au kuingia katika kiwanda hicho. Ikumbukwe ndani ya kiwanda hicho kuna majeshi ya Ukraine na Mamluki ambao wameteka raia na kujificha ndani ya kiwanda hicho tangu juzi wamegoma kujisalimisha, Rais Putin jana akaamuru kiwanda kifungwe na asitoke mtu wala kuingia mtu.

Mji wa Mauripol bado sherehe za ushindi zinaendelea, kwasasa mji huo umekabidhiwa kwa majeshi ya Jamhuri ya watu wa Donetsk na majeshi ya Chechnia, Nyimbo za ushindi na nderemo zinarindima kila kona, vifaru vinapiga misere na kufyatua risasi hewani.

Hatua nyingine ya leo ni kuwa majeshi ya Urusi yameteka miji muhimu wa kihistoria wa Donbass na sasa unadhibitiwa kwa na Moscow, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema leo asubuhi na kuongeza kwamba oparesheni kuelekea kitovu cha Luhansk inaendelea.

Licha ya maonyo kadhaa ya Moscow kwa Marekani na Ulaya kuacha kutoa misaada ya silaha kwamba inachochea vita na kwamba Moscow sasa imeelekeza nguvu zake katika kuhujumu misaada hiyo, Marekani imeidhinisha msaada wa silaha za dola milioni 800 ukihusisha ndege zisizo na rubani ambazo zimetengenezwa maalumu kwa Ukraine, pia mitambo ya mfumo wa kuzuia makombora. Moscow imejibu kuwa iko na macho kwenye kila msaada na itaushughulikia kabla haujafika kwa walengwa kama ilivyofanya wiki jana ilipoingilia mawasiliano ya kijeshi kati ya Ukraine na Marekani kisha ikaenda kupokea silaha yenyewe badala ya Ukraine.

Urusi imeteka kiwanda muhimu cha silaha cha 65 Arsenal, Kiwanda hiki kinahusika na artillery and rocket ammunition of the Central Rocket and Artillery Directorate of the Armed Forces of Ukraine.

Historia ya Kiwanda cha Arsenal ni ndefu na ya kusisimua. Kiwanda kilijengwa mwaka 1918 katika mji wa Balakleya kwaajili ya jeshi la Kisoviet la Red Army. Jeshi la Kisoviet lilipokea sila zote toka katika kiwanda hiki muhimu sana kwa Ukraine kwa sasa. Baada ya Muungano wa Kisoviet kuanguka kiwanda hiki kilikabidhiwa kwa jeshi la Ukraine (Ukrainian Armed Forces) hadi sasa ndio kiwanda kikubwa cha silaha Ukraine.

Tangu mwaka 2014, kiwanda cha Arsenal kimekuwa kikizalisha sila za cannon na rocket artillery shells kwa jeshi la Armed Forces of Ukraine katika jimbo la Donbass. Maroketi hayo yameua watu zaidi 14,000 wa Jamhuri ya Donetsk DPR na Jamhuri ya Luhansk LPR.

Kwasasa Donbass iko huru Kiwanda kimetwaliwa na Moscow na kitakuwa mali ya nchi mpya ya Luhansk kuanzia leo. Kitazalisha silaha maalumu kupambana na Kyiv sasa.

Naam, kwingineko Katika Mji wa Kherson jeshi la Urusi linaendesha oparesheni ya kupokonya silaha zilizozagaa mikononi mwa raia, Raia hawa wengi sila walipewa na rais wa Ukraine siku za mwanzo mwa vita hivi, Urusi inajizatiti kuhakikisha maeneo yote yaliyokombolewa raia hawabaki na silaha mikononi.

Ikulu ya Kremlin imemshangaa rais Zelensk kusema kuwa hana taarifa mpya za mapendekezo ya Moscow ya kusitisha mapigano, ambayo ni yaleyale matatu muhimu awali kwamba Ukraine isijiunge EU na hili liwekwe kwenye katiba ya Ukraine, Ukraine itambue kuwa Cremia ni eneo la Urusi hili pia liwe kwenye katiba, na Ukraine itambue rasmi kuwa Majimbo ya Donetsk na Luhansk ni nchi huru zilizojitenga rasmi, pia hili likae kwenye katiba ya Ukraine.

Mjini Moscow maandalizi ya Mei 10 ambayo ni malimu kuadhimisha Ushindi wa majeshi ya Urusi dhidi ya Manazi chini ya Aldof Hitler yanaendelea, Gwaride linaandaliwa kwa ustadi huku anga lote la Urusi na viunga vyake likidhibitishwa na mfumo wa Smarter.

Leo saa nane kamili mchana kwa saa za Tanzania, Rais Putin alikuwa kwenye kikao na Wajumbe wakudumu wa Baraza la Usalama la Taifa, Nitawajuza yaliyoamuliwa kikao kikimalizika.

Source....vyanzo mbalimbali RT,. Bbc kidgo na vingine
FB_IMG_16506155194835431.jpg
 
Hii report ya warusi, kwahiyo usitegemee negative yoyote kuhusu wao. Shutuma kwanini mleta mada ameegemea upande mmoja itakuwa ni kumuonea tu kumlaumu bure mleta mada.

Hii Vita bado ni ndefu endapo NATO ikaamua iwe ndefu, laiti isingekuwa inagusa maisha ya mataifa mengine ulimwenguni basi tungeona mengi zaidi ktk hii Vita.

So far, bado naona Ukraine inaweza ikaibuka muda wowote kuleta upinzani mkali juu ya uvamizi huu wa Russia.
 
Hii report ya warusi, kwahiyo usitegemee negative yoyote kuhusu wao. Shutuma kwanini mleta mada ameegemea upande mmoja itakuwa ni kumuonea tu kumlaumu bure mleta mada.

Hii Vita bado ni ndefu endapo NATO ikaamua iwe ndefu, laiti isingekuwa inagusa maisha ya mataifa mengine ulimwenguni basi tungeona mengi zaidi ktk hii Vita.

So far, bado naona Ukraine inaweza ikaibuka muda wowote kuleta upinzani mkali juu ya uvamizi huu wa Russia.
Yaaah mkuu Vita bado mbichi......coz zelensky Hana cha kupoteza .....ana back up ya kutosha
 
Hiyo "denazification" mbona sijaona maelezo yake?

Imeanzaje, kwa kusudi gani, ikawaje, ikafikia wapi, mafanikio ni yapi, changamoto ni zipi, mipango na mikakati ya baadaye ni ipi?

Mara nyingi nakutana na rhetorics tu na disinformation za hapa na pale bila kuwepo kwa facts zinazoeleweka.

Hiyo "denazification" ni kitu gani hasa?
 
Hiyo "denazification" mbona sijaona maelezo yake?

Imeanzaje, kwa kusudi gani, ikawaje, ikafikia wapi, mafanikio ni yapi, changamoto ni zipi, mipango na mikakati ya baadaye ni ipi?

Mara nyingi nakutana na rhetorics tu na disinformation za hapa na pale bila kuwepo kwa facts zinazoeleweka.

Hiyo "denazification" ni kitu gani hasa?
Operation "denazification" Ni operation ya kuwaondoa wa wa Ukraine wenye misimamo mikali wanaoungwa mkono no west KWENYE majimbo yenye watu wengi wanaoongea lugha na utamaduni wa kirussia

Maana yake kwa ufupi ni kuyapa Uhuru majimbo yanayokaliwa na watu wenye asili ya urusi.
 
Hii ya kuingilia mawasiliano ya Ukraine na Marekani kisha wakaenda kupokea sikaha wao sikuipata, hebu ongeza nyama mzee.
Hii hauwezi kutangazwa kwny media zao mkuu .....ila tu nadhani umeona Hadi waziri mkuu wa uingereza ambaye ndio alikuwa Frontline kwenye hili suala anakata tamaa.......coz anajua now Kuna ugumu wa kumsaidia zelensky
 
Back
Top Bottom