Rekodi ya kuuza copy nyingi, nani mkweli, Mr. Nice niliuza nakala 1.7 mil, feruzi 200k ndani ya wiki?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Mr. NICE ALIWIKA sana lakini anaonekana ni Mzee wa maneno ya kujisifia sana, kumekuwa na takwimu zisizo eleweka za mauzo ya kazi za wasanii hapo zamani. Huku Mr. Nice akitamba kwamba yeye aliuza nakala milioni 1.7 na aliemfuatia alikuwa around laki 380,000/= wakati huo huo tunaambiwa na Feruzi aliuza copy laki mbili ndani ya wiki moja.

Lakini kitakwimu tuaambiwa albamu za profesa jay na **** nature ndio ziliuza sana sokoni.

Wakati huo huo, mangwea na album yake ya a k.a Mimi aliuza copy laki 7.

Sasa watu wa takwimu na wasambazaji wako wapi watuondoleee sintofahamu hii? Japokuwa kulikuwa na uwizi mkubwa sana uliofanywa na wasambazaji ak.a wadosi lakini majibu ya kweli wanayo wao
 
Mr nice inaweza kuwa kweli aisee, jamaa alikua na upepo na nyimbo zake za chekechea

Hapo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo ulikuwa huwaambii kitu kuhusu huyu jamaa

Imagine alienda kufanya show Congo akapokelewa na waziri mkuu wa Congo
Utafikiri ulikuwa uchawi haha
 
Mr. NICE ALIWIKA sana lakini anaonekana ni Mzee wa maneno ya kujisifia sana, kumekuwa na takwimu zisizo eleweka za mauzo ya kazi za wasanii hapo zamani. Huku Mr. Nice akitamba kwamba yeye aliuza nakala milioni 1.7 na aliemfuatia alikuwa around laki 380,000/= wakati huo huo tunaambiwa na Feruzi aliuza copy laki mbili ndani ya wiki moja.

Lakini kitakwimu tuaambiwa albamu za profesa jay na **** nature ndio ziliuza sana sokoni.

Wakati huo huo, mangwea na album yake ya a k.a Mimi aliuza copy laki 7.

Sasa watu wa takwimu na wasambazaji wako wapi watuondoleee sintofahamu hii? Japokuwa kulikuwa na uwizi mkubwa sana uliofanywa na wasambazaji ak.a wadosi lakini majibu ya kweli wanayo wao
Kibongo bongo kampuni kongwe ya usambazaji wa kazi za wasanii kipindi hiyo ilikuwa 1 tu.. japo zilikuwepo nyingine chache kama 3 sikosei....

But the big fish was ...(ilikuwa) GMC wasanii promoter's... Chini ya tycoon MAMU...

Atakachokupa kwenye kila tape ndicho utatakiwa ukubali kuchukua!... Hata ingekuwa sh 2!. taka / usitake....utachukua tu!...maana Huna either option!!!

Na mfyatuaji wa copy ni yeye mwenyewe so hawezi kukwambia ukweli copy ngapi zimetoka...

Pia kulikuwa hakuna database ya kutunza kumbukumbu... Mpaka sasa hivi!...

Hizi vitu kibongo bongo ni Maneno tu kila msanii anataja data yake inayokuja kichwani muda huo huo.... ili Aonekane aliuza... Wakati uhalisia tuliujua sisi watu wa mtaani .

Huenda hata hao wasanii uliowataja ukija kuwauliza tena swali hilihili!....baada ya miaka mi3... Watakutajia data tofauti tena!.... Hapo ndio utachoka zaidi!
 
nice anawezakuwa mkweli.

kwa sasa mambo yako hadharani tunaona,ila enzi zile pia tulishuhudia kwa vitendo.kijana wa kisasa 2005 asingekosa casset ya audio au video ya jamaa.
ni kama rose muhando 2003,inasemekana album iliuza copy na kuingiza mapato zaidi ya milioni 80,ila sijui kama alipewa yeye au mdau alizuia.

majasho ya wasanii yameliwa sana na madalali enzi hizo hata upande wa maigizo.
 
Kweli kabisa kaka
 
Mleta mada ulizaliwa mwaka gani ? Enzi za Mr Nice vhs zake zilikuwa nyingi huyo ndio alikuwa Diamond alafu umlinganishe na ferooz !!!
Mpaka umri huu sijawahi kuona vhs ya ferooz au msanii yeyote Tz zaidi ya Nice. Mpaka naweza kuamini Mr nice peke yake ndie alikuwa na VHS hao wengine labda waliziuzia Dar huko tu
 
Majani alikiri mwenyewe Feruz aliongoza kuwa na album nyingi kuliko hao uliowataja, kumaanisha hata sokoni Feruz aliuza zaidi kuliko hao
Mkuu unajua maana ya album kwenye insustry ya mziki? Album ya feruzi naijua moja tu ile ya safari nakumbuka cassete yake nilikua nayo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom