rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 15,270
- 20,316
rekodi ya iddi simba kwenye uongozi wa mashirika ni mbovujuzi juzi kuna tuhuma mbili zimeibuka zikimhusisha aliekuwa waziri wa viwanda ambae pia ni mwenyekiti wa wazee iddi simba na ufisadi katika miradi ya machinjio ya kisasa na shirika la usafiri la dar es salaam (uda)lakini ukimfatilia iddi simba toka kipindi cha nyuma kuna maswali mengi ya kujiuliza kwanini huyu mtu bado ameendelea kukabidhiwa dhamana ya kuendesha mashirika mbalimbali ya serikali.wengi mnalikumbuka shirika la uchumi na kilimo la sukita.shirika hili lilianza kwa ufanisi mkubwa lakini lilikuja kufilisika na kuacha madeni ya ajabu.mwaka mmoja kabla ya iddi simba kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa hii bodi shirika hili lilikuwa limepata faida ya shilingi milioni 400 ambacho kwa kipindi cha mika ya 90 zilikuwa pesa nyingi sana.mwaka mmoja baada ya idd simba kuteuliwa mwenyekiti wa hiyo bodi shirika hilo lilikuja kupata hasara ya shilingi bilioni 2 hali ambayo ilipeleka shirika hili kuanza kutetereka na baadae kufa kabisa.ninachojiuliza hivi wanapoteua mwenyekiti wa bodi huwa hawaangalii rekodi zake za nyuma kwa sababu kwa kitendo cha shirika lililokuwa linapata faida kabla ya yeye kuwa mwenyekiti wa bodi kwa nchi zilizo makini asingeweza kupewa kuongoza