Rekodi ya Iddi Simba kwenye uongozi wa mashirika ni mbovu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rekodi ya Iddi Simba kwenye uongozi wa mashirika ni mbovu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Apr 16, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  rekodi ya iddi simba kwenye uongozi wa mashirika ni mbovujuzi juzi kuna tuhuma mbili zimeibuka zikimhusisha aliekuwa waziri wa viwanda ambae pia ni mwenyekiti wa wazee iddi simba na ufisadi katika miradi ya machinjio ya kisasa na shirika la usafiri la dar es salaam (uda)lakini ukimfatilia iddi simba toka kipindi cha nyuma kuna maswali mengi ya kujiuliza kwanini huyu mtu bado ameendelea kukabidhiwa dhamana ya kuendesha mashirika mbalimbali ya serikali.wengi mnalikumbuka shirika la uchumi na kilimo la sukita.shirika hili lilianza kwa ufanisi mkubwa lakini lilikuja kufilisika na kuacha madeni ya ajabu.mwaka mmoja kabla ya iddi simba kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa hii bodi shirika hili lilikuwa limepata faida ya shilingi milioni 400 ambacho kwa kipindi cha mika ya 90 zilikuwa pesa nyingi sana.mwaka mmoja baada ya idd simba kuteuliwa mwenyekiti wa hiyo bodi shirika hilo lilikuja kupata hasara ya shilingi bilioni 2 hali ambayo ilipeleka shirika hili kuanza kutetereka na baadae kufa kabisa.ninachojiuliza hivi wanapoteua mwenyekiti wa bodi huwa hawaangalii rekodi zake za nyuma kwa sababu kwa kitendo cha shirika lililokuwa linapata faida kabla ya yeye kuwa mwenyekiti wa bodi kwa nchi zilizo makini asingeweza kupewa kuongoza
   
 2. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Hii ndio nchi yetu Bana, Tunamlaumu mungu labda ametulaani!! Ila kwa hali ya kawaida wale waharibifu ndio wanapewa dhamana!! Halafu hatuwezi kuwafanya lolote Lol!! My Country Tanzania, Angalia Mataka amefilisi mashirika yote muhimu ila bado aliendelea kupewa ATCL - Ambapo alijisifu aliweza kubadilisha nembo na kuliulia mbali!! Angalia Iddi Simba; Na ubadhirifu wote huo hakuna hata wa kumuuliza licha hata ya Kumfilisi!! Wenye Dhamana ya kumuuliza wamekaa kimya Kabisa!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tusitegemee mirako,IDDI LION MASUKAR ATAENDELEA KUPETA,
  HAKUNA MSAFI WA KUMGUSA
   
 4. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Idd Simba ni mtu wa Burundi ni mrundi kwao ni no 17 ST Buyenzi, kama sijakosea sana ana uraia wa inchi mbili anategea tu CDM ikichukua inchi anarudi kwao na ni wazi atakuwa amejilimpikizia sana mali. kama kuna fatal mostake serikali ya CCM ilizofanya ni kuruhusu watu hawa kufanya robbing za madaraka kwa sababu wao ni maslahi kwanza hata kama kwa kupata maslahi hayo itabidi wengine wafe.watu kama Idd Simba wanataka CCM itawale milele kwa sababu wako kwenye receiving end. RANK ya akiNA Idd Simba ni pamoja na Ibrahim Kinana, Aden Rage, Mohamed Dewji, Murji wa Mtwara Mjini, Abood, Shah wa kirwa,Ahmed Shabib n.k. watu hawa si wazuri hata kidogo.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Asante Blayi no wonder uyu jamaa hana uchungu na hii nchi kumbe ana kwao so apa ni kama Transit Camp!
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee Idd Simba ni haramia kwani uvundo wote unaofumuliwa kuhusu ufisadi yumo; toka vibari vya sukaii, Kampunu ya uda, Machinjo ya ng'ome na mapaka EPA!! Idd Simba yuko nje anakula bata lakini wakina Maranda na Farijala wako lupango wananyea ndoo na huku jamaa had a hand in the loot!! How could he be a director of Bank M if he did not invest in that bank which was founded on EPA money? Ni aibu kwa wazee wa Dar es salaam kumkubali kuwa Mweneykiti wao!
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Wengi wenu hamumjui Iddi Simba bali mnakimbilia ushabiki tu.

  Iddi Simba ni mchumi mahiri sana na amefanya kazi sehemu mbalimbali ikiwemo IMF na mpaka kufikia mkurugenzi wa misaada ya nchi za Africa.

  Iddi Mohammed Simba ni miongoni mwa wana dar es salaam wa miaka ya 1940 na alisoma na Ammi yangu Mzee Abdullah Salem Al Harthy, Aziz Ally, Dossa Azizi pale Habib Punja Muslim Ilala School, na baadae Mchikichini.

  Ni miongoni mwa watu mahiri na wenye kuheshimu na kulinda taaluma zao waliokimbia Tanzania mwaka 1967 kwa kutofautiana kisera na Mwalim JK Nyerere.


  Mpaka leo anategemewa sana na wachumi na wafanyabiashara mahiri huko Tanzania na wawekezaji kupitia kampuni yake ya Interfinas (International Finance, Advisory Services).

  Kwa waliowahi kufanya nae kazi au hata kuongea nae kwa muda utamuona ni mtu wa aina yeke. Ni Mkweli na Muwazi.

  Namalizia kwa kusema ni mtu wa Rufiji (mndengereko wa Mohoro) mtoto wa mzee Simba Ndume lakin mama yake ndio mrundi.
  Kwa wakaazi wa kariakoo wa zamani nafikiri anafahamika sana baba yake.

  Ni Hazina kubwa kwa Tanzania.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana anavyoonekana kwenye public na anayifanya nyuma ya pazia tofauti. I cant understand hii nchi na prominent people tulionao. Wengi wamekaa kama wezi wezi vile.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Labda ni hazina kwako au kwenu mkuu...hana sifa ya kuitwa hazina ya Taifa kama ataendelea kuchanganya ujanja ujanja na biashara. Na pengine sio wewe peke yako unayemfahamu huyu mtu vizuri. Wako wengi...
   
 10. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  umeningezea taarifa,hii sikua nayo.
   
 11. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kutupa historia yake kwa ufupi...pamoja na weledi wake, uraia wake na umaarufu wake kama Mtanzania na mjasiriamali hayo hayatoshi sie kuacha kuhoji rekodi ktk utumishi wa Umma na kashfa mbalimbali zinazomuandama kama wadau walivyojaribu kuonesha kuanzia SUKITA...VIBALI VYA SUKARI...EPA...NA SASA UDA na inawezekana mengineyo mengi tunaomba wadau wayaorodheshe...tunaomba utetezi wako mzee wetu ili tupate ukweli wa mambo na sio kuonekana kama tuna husda au chuki binafsi dhidi yako...
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimebainisha kwa watu wa Kariakoo huko Dar es salaam anafahamika vizuri sana kuanzia yeye mpaka wazazi wake. Kwani amesomea skuli za hapo hapo mpaka aka graduate 1962.

  Lakin vile vile kwa wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji ni mtu muhimu sana katika kupata ushauri wa kibiashara za Tz na nje yake lakin pia na wawekezaji wengi wanapitia kwake kutokana na umahiri wake na swifa zake alizojijengea kimataifa hususan alipokuwa IMF.

   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri sasa Wangi wetu tujaribu kujikomboa katika utumwa wa Kiakili na fikra tulionao.

  Lazima mjue kuwa nchi yenu inafuata Rules of Law (utawala wa sharia). Sasa kama mna ushahidi wa kutosha na kuwa na uhakika na mnachokinena dhidi yake kwanini msiwakilisha mahakamani ili sharia ichukue mkondo wake.

  Majungu siku zote si mtaji. Na Majungu haawez kubadilisha swifa au taswira ya mtu kwa jamii.

   
 14. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Wewe mnafiki, hebu eleza huyo hazina wako sababu zilizofanya afukuzwe uwaziri wa viwanda na biashara,
  Pia ni nani muasisi wa rushwa ya pilau kwenye uchaguzi aliyoiita yeye kuwa eti siyo rushwa ni takrima?
  A
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyu ni nani?
   
 16. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  nDUGU ZAKE MARANDA WANALALAMIKA JINSI ALIVYOMCHUUZA MARANDA AMBAYE NI DARASA LA SABA AKACHOTE PESA ZA epa NA KESI ILIPOANZA AKAMWAMBIA ASIMTAJE ATAMLINDA LAKINI mARANDA YUKO GEREZANI NA YEYE ANAKULA KUKU
  pIA ALIMCHUUZA mAREHEMU dR oMARY ASAINI VIBALI VYA SUKARI WAKATI ALIEKUWA RAIS YUKO NJE YA NCHI KWA KUMWAMBIA WEWE SASA NDIE RAIS NA MADARAKA YOTE UNAYO ILIPOIBUKA KASHFA YA SUKARI MAREHEMU ALIPATA MSHTUKO KWANI ALICHUUZWA HANA USAFI WOWOTE KWANI REKODI ZA UTENDAJI WAKE ZINAJIONYESHA NA SALAMA YAKE NI ccm KUWA MADARAKANI LAKINI KWA MADHAMBI ALIYOTENDA NA KAMA TUTAPATA KATIBA SAFI HATAPONA
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kampuni aliyoiendesha na kufanikiwa sana ni Saigon

  Imetoa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam
  Imetoa Chama Cha Upinzani cha Kiislamu cha Kighoma Ali Malima
  Imetoa Rais wa Nchi Jakaya Mrisho Kikwete
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwani mwenyekiti wa Bodi ni mtendaji wa shirika/kampuni?

  Je nini kazi za Meneja mkuu/ Mtendaji mkuu?

  Nini kazi za Mwenyekiti wa bodi?

  Naona kwa kujua hili tutafika pahala kujua nani mkosa.
   
Loading...