Rekodi inaibeba CHADEMA Jimbo la Vunjo 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rekodi inaibeba CHADEMA Jimbo la Vunjo 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuku dume, May 9, 2012.

 1. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,
  Ikumbukwe kwamba jimbo hili ni moja kati ya majimbo mawili yanayounda wilaya ya Moshi(V) na ambalo Mbunge walo wa sasa ni Augustino Lyatonga Mrema.

  Naomba ieleweke kwamba jimbo hili halikuwahi kushikiliwa na mbunge mmoja kwa vipindi viwili hata kama alifanya mazuri kiasi gani nyanati za uongozi wake.

  Alianza kulichukua James Mbatia(NCCR) 1995 na ilipofika 2000 ikawa kikomo kwake japo alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko Mbunge yeyote wa wakati ule. Baada ya hapo akapokea Meja Jose Makundi(TLP) hadi 2005 naye wenye jimbo wakamchoka. Kisha mfanyabiashara za kitalii na mmiliki wa Nakara Hotel Bw. Kimaro akawa chaguo la Wanavunjo hadi 2010. Kuelekea 2015 yupo Mrema.

  Kwa rekodi ilivyo hata Mrema angefanya nini hatoweza kuchaguliwa tena. Kwanza kitendo cha TLP kujirudia naona kama kimechangiwa na tume kutokuwa huru. Haiwezekani kwamba 1995 mtu mmoja alipata kura zaidi ya 60,000 alafu 2010 kura zote zilizopigwa zisifike 40,000. Basi tume ya takwimu nayo iseme kwamba Watanzania wamepungu.

  Hata NCCR ikimteua Mbatia kugombe hatochaguliwa kwa kuwa rekodi ya jimbo lenyewe haimbebi.


  Hakuna chama kingine zaidi ya chadema chenye nguvu Vunjo.

  Viva CHADEMA.

  Nawasilisha,
  kuku dume.
   
 2. s

  steering Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jimbo la Hai Tusemeje? Rekodi inaibeba NCCR?
  Alianza Mwinyihamisi (NCCR) 1995. 2000 mBOWE (Chadema), 2005 (CCM), 2010 Mbowe, je, hapo tubashiri nn? nao hakuna aliyewahi kutawala vipind viwili mfululizo
   
 3. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa Hai hakuna cha ajabu maana Mbowe tayari ni Mbunge mara mbili na isitosha hata kama angegombea ubunge 2005 angeshinda.

  Vunjo hakuwahi kushinda mtu mara mbili hata kama aliwafanyia nini.
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Pengine sababu ya hao wana Vunjo kutokaa na mtu zaidi ya kipindi kimoja ni ipi hasa?

  Mazingira, utamaduni na hali ya kiuchumi hapo zina mchango kiasi gani ktk maamuzi linapokuja suala la siasa/uchaguzi?
   
 5. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni John Mrema kwa VUNJO 2015

  TUMBIRI wa JF,
  PO BOX - PM JF.
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Mkuu
  steering,
  Kumbuka Mbowe hakugombea 2005. Kwa hiyo hoja ya kuwa hakuna aliyewai kutawala vipindi viwili mfululizo inakosa nguvu kwa sababu MBOWE hakutaka kutetea nafasi yake 2005. Kwa hiyo hakushindwa!

  TUMBIRI wa JF,
  PO BOX - PM JF.

   
 7. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hakuna jimbo la watu wenye shingo ngumu kama vunjo hata uwape mkeo walale nae hawatakuchagua mara mbili. Wachaga wabishi wale sijapata kuona! Labda Mrema akitaka achaguliwe ajenge ile barabara ya Kawawa-Kirua-Kilema-Marangu mtoni pamoja na ile ya Njia panda-Kilema Hospital hakika atachaguliwa tena
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hao wana vunjo nimependa tactic yao...mbunge term moja anasepa..hawataki mchezo..mbunge ukishampa term mbili kuendelea anajisahau na kuanza kuvurunda vurunda...on the other hand ukibadilisha mbunge kila wakati hata maendeleo inakua vigumu kuyapata mana kila mbunge mpya akiingia ana kuja na sera zake...
   
 9. M

  Makupa JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Namsubiri John Mrema kwa mapambano
   
 10. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safari hii Mrema alisaidiwa na magamba maana magamba walidiriki hata kujiibia kura ili kibaraka wao aingie mjengoni
   
 11. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Utabiri wako sio wa kweli hata KIDOGO
  Jimbo la Vunjo navyojua lina historia yake kwa harakati hizi za mageuzi Tanzania
  Kuweka KUMBUKUMBU sawa wakati Mrema alipokuwa Naibu waziri Mkuu alifanya mambo makubwa mawili kwa wanavunjo. La kwanza alikuwa mtetezi saana wawanawake( Ikumbukwe wachagga walikuwa na tabia saana ya kuwapiga wake zao) kwa mamlaka Mrema aliyokuwa nayo alitoa amri mtu akimpiga mke wake anaenda ndani siku 14 baadae kesi hilo la kwanza la pili KNCU Walikuwa wanawaibia saana wazee kwenye mauzo ya kahawa ikumbukwe KNCU walikuwa ndio wanunuzi pekee,, walikuwa na matozo mengi Mrema alipogundua akawapiga STOP kilo moja ya kahawa ikapanda kutoka TSH 300 mpaka 1600 kwa kipindi hicho wazee walikuwa matajiri saana

  Kwa hayo mawili mpaka leo MREMA akigombea hawawezi hata siku moja kumyima KURA ikumbukwe wapiga kura wengi ni wanawake

  KIMARO NA MBINU WALIZOTUMIA CCM
  tangu mrema aingie upinzani CCm walikuwa wanatumia kila mbinu kurudisha hili jimbo na mbinu zao zilizaa matunda kwa kufanya nini
  1. walipeleka maji safi ya BOMBA karibia vijiji vyote
  2. walisambaza umeme karibia vijiji vyote
  3. na kwa sasa barabara muhimu ziliahidiwa lami( kitu ambacho kina fanyika sasa hivi)
  4. vituo vya afya kuna usafiri

  ahadi zote hizi waliahidiwa wananchi na wakaambiwa endapo MTAICHAGUA CCM zote zitatekelezwa ndio maana KIMARO akachaguliwa MBUNGE. mbinu chafu zilizotumika nguzo za umeme zilichimbiwa kwenye vijiji na wakaambia wananchi msipoichagua CCM tutaziondoa walipochagua sasa hivi wanaumeme

  CHADEMA

  Itakuwa ngumu saana kulichukua hili jimbo KAMA MREMA LYATONGA NA YEYE ATAGOMBEA, bado anaushawishi mkubwa, na wakinamama wanampenda na wazee wengi wanakumbuka aliyowafanyia. msifikirie itakuwa kazi rahisi
  tambueni na CCM wakimaliza kuweka barabara ya KAWAWA - Nduoni - Congo- Kilema- Marangu mtoni lami sijui CHADEMA mtakuwa na Agenda gani ya kuwashawishi hawa watu ambao wamefaidika na siasa za upinzani tangu zianze

  KWA MBATIA na NCCR yake WASAHau Mbatia hatakaa na wala haitatokea awe mbunge wa VUNJO hata kama ataungwa mkono na CCM kwanza alimkosea mrama ambaye ndio alimweka Madarakani pia familia yao ni watu wanaojisikia saana hii ni kutokana na baba yake alivyokuwa na mahusiano mabaya na wazee wenzake
   
 12. K

  KIRUA Senior Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mimi natokea kirua vunjo...
  jimbi lile halieleweki kwa sasa kwa kua wapiga kura wake niwagumu sana kumkubali mtu hata kama wewe una uwezo wakuongoza...
  kikubwa nikuanza maandalizi ya mapema ili waonenikipi umefanya hata kabla ya kupata ubunge la sivyo hupati chochote
  chadema ya faa kujiandaa sana.anaweza kwenda chalse kimei kwa tiketi ya ccm naakachukua....so inafaa kuangalia mbali
   
 13. K

  KIRUA Senior Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kiukweli huu jamaa akienda tena mara ya pili hapati yafaa mtu mwengine kabisa
  wana vunjo walishindwa kumpa 2010 hawatampa kabisa....jamani tuangalie poa hii jambo.
   
 14. K

  KIRUA Senior Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaka wale jamaa achana nao.hasa uchira,himo wapo wapare wengi wa ccm wanaotoka huko kwa maghembe
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mimi Makupa ni mzaliwa wa Vunjo na nawatangazia rasmi kuwa nitangombe jimbo langu la vunjo 2015
   
 16. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja tutampeleka mjengoni. Nakuambia ntaweka kambi uchaguzi ukikaribia mpaka kieleweke.
  Naahidi kuwa wakala yakiwa majaliwa yake mola.
  Sasa naisambaratisha CCM Ruvuma lakini mda ukikaribia ntakwenda Vunjo.
   
 17. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Amini usiamini 2015 CCM watalichukua lile jimbo iwapo CDM itamsimamisha John Mrema,
  Sababu ni kwamba wale wazee wa Vunjo na hata vijana wanapenda na kuamini katika PROVEN EVIDENCE YA MAENDELEO ndipo wakupe kura siyo hivihivi, na sasa wanauzoefu na siasi za upinzani ambao zimewaacha patupu kwa miaka zaidi ya 10, na kilichomfanya Mrema kushinda ni historia pamoja na mgombea wa CCM aliyesimamishwa (Meela) sasa hv wamepelekewa barabara,maji na umeme wa uhakika, J
  Mrema yupo dsm watamfaham tena 2015
   
 18. M

  Majasho JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hapo chadema imekula kwenu aisee....

  kwanza Mrema alsihakuwa mbunge, enzi hizo moshi vijiji tangu 1985 to 1995

  then akahamia NCCR, wananchi wa vunjo wakamchagua mgombea wa NCCR 1995

  then akahamia TLP, wananchi wa vunjo wakamchagua mgombea wa TLP 2010

  SO actually Mrema anakubalika vunjo vibaya sana since 1985

  John Mrema wenu kapata kura 6,000 compared to his 32,000. wana mahesabu naombeni mnisaidie kubadilisha into percentage.

  so plz, forget bout Vunjo my sons. HUKO MREMA IS TO VUNJO WHAT NDESAMBURO IS TO MOSHI MJINI
   
 19. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2015
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vunjo hoyeeeee
   
 20. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2015
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupatieni yanayo jiri Vunjo wakuu.
  CCM
  TLP
  NCCR
  CHADEMA.
  Hali halisi?
   
Loading...