Rekodi inaibeba CHADEMA Jimbo la Vunjo 2015

Wana JF,
Ikumbukwe kwamba jimbo hili ni moja kati ya majimbo mawili yanayounda wilaya ya Moshi(V) na ambalo Mbunge walo wa sasa ni Augustino Lyatonga Mrema.

Naomba ieleweke kwamba jimbo hili halikuwahi kushikiliwa na mbunge mmoja kwa vipindi viwili hata kama alifanya mazuri kiasi gani nyanati za uongozi wake.

Alianza kulichukua James Mbatia(NCCR) 1995 na ilipofika 2000 ikawa kikomo kwake japo alichaguliwa kwa kura nyingi kuliko Mbunge yeyote wa wakati ule. Baada ya hapo akapokea Meja Jose Makundi(TLP) hadi 2005 naye wenye jimbo wakamchoka. Kisha mfanyabiashara za kitalii na mmiliki wa Nakara Hotel Bw. Kimaro akawa chaguo la Wanavunjo hadi 2010. Kuelekea 2015 yupo Mrema.

Kwa rekodi ilivyo hata Mrema angefanya nini hatoweza kuchaguliwa tena. Kwanza kitendo cha TLP kujirudia naona kama kimechangiwa na tume kutokuwa huru. Haiwezekani kwamba 1995 mtu mmoja alipata kura zaidi ya 60,000 alafu 2010 kura zote zilizopigwa zisifike 40,000. Basi tume ya takwimu nayo iseme kwamba Watanzania wamepungu.

Hata NCCR ikimteua Mbatia kugombe hatochaguliwa kwa kuwa rekodi ya jimbo lenyewe haimbebi.


Hakuna chama kingine zaidi ya chadema chenye nguvu Vunjo.

Viva CHADEMA.

Nawasilisha,
kuku dume.
Kwasasa hakuna mtu anayekubalika kwa nafasi ya ubunge vunjo Kama mbatia
 
nimewapenda wanavunjo wao wanaangalia wamefanyiwa nini sio siasa za majitaka ,kweli wamekomaa,
 
mm nimetoka vunjo nimekulia vunjo ila kwa sasa mrema hana chake chombo anakiongoza james fransy mbatia mm ni ukawa najua historia ya vunjo ok
 
saiv kuna kijana matata sana wa ccm mheshimiawa melleck shirima hana mpinzani
 
Back
Top Bottom