Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile

Reincarnation na rebirth ni kitu kile kile

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,940
Reaction score
831,461
Huu ni mwendelezo tu wa kile tumekuwa tukikijadili hapa jamvini kuhusu hayo mambo mawili, reincarnation -kuzaliwa tena katika umbo lingine na rebirth -kuzaliwa upya kiroho
Reincarnation na rebirth vinatofautiana katika misingi ya kiimani, lakini kiuhalisia ni kitu kilekile
Wanaoamini katika reincarnation hawaamini katika Mungu mkuu mwenye enzi yote, bali katika nafsi na miungu, cause and effect kwamba ubaya hulipwa na ubaya na wema hulipwa na wema, yani hakuna kitu msamaha kwenye hii imani, kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake....
Wanaoamini katika rebirth, ni wale Wanaoamini katika Mungu mmoja mwenye mamlaka yote, msamaha kwa matendo ya nyuma na kuzaliwa upya kiroho...kwahiyo hata kama umetenda dhambi kiasi gani ukitubu na kuungama basi dhambi zako zote husamehewa na kuwa kiumbe kipya kiroho katika mwili uleule

TUJADILI
Ukiangalia kwa uwazi tu utaona dhana zote mbili za reincarnation na rebirth zote zinahusika na roho. Roho ndio msingi wa dhana zote mbili nje ya roho hakuna reincarnation wala rebirth, bali kuna mkusanyiko wa mifupa na nyama ambavyo hutengeneza kitu kiitwacho mwili
Mfanano wa reincarnation na rebirth ni Kama nilivyosema ni roho na roho inapoumbwa haifi tena, haifi milele, aidha iwe reincarnated au ilale kuzimu ikisubiri hukumu kuu na baada ya hapo inaishi milele mbinguni paradiso au jehanam
Kwahiyo tusichanganyikiwe na hilo, hizi ni Lugha tu lakini kitu ni kimoja nacho ni roho na roho haifi ikishazaliwa au ishaumbwa (created)

CC: Senior Boss
 
Last edited by a moderator:
1444538790915.jpg 1444538809327.jpg
cc: NDUKI
 
Last edited by a moderator:
Na kwakuwa roho ni kitu kinachoishi milele kuna wakati hubeba ufahamu wa marehemu hasa kwenye hii dhana ya reincarnation hivyo watu kujikuta wanafika mahali kwa mara ya kwanza lakini wakiwa na imani kabisa kuwa walishawahi kufika hapo lakini ikiwa ni kumbukumbu isiyo kamili vague memories

Au kufanya jambo kwa mara ya kwanza lakini ukiwa na hisia kabisa kwamba ulishawahi kulifanya lakini ni wapi na nani halafu ikawaje, kumbukumbu haiji yote katika ukamilifu wake

Vilevile kukutana na mtu ana kwa kumfaninisha au kwa kudhani kuwa mlishawahi kuonana lakini hukumbuki wapi lini na kwenye ishu gani

Hali zote hizi huletwa na roho na kwa wale wasioamini katika reincarnation basi ni zile roho zinazotangatanga, huweza kumuingia kwa muda mtu unayemfahamu kabisa bila Yule aliyeingiliwa kujitambua... Sasa wewe unakazana kumwambia kuwa Unamfahamu lakini yeye anabaki tu na mshangao
 
Nnachoendelea kukisoma nje ya JamiiForums ndicho hiki ambacho skutegemea kuwa ntakikuta hapa hii leo mkuu.

Ni kweli kabisa kiongozi unachosema kuhusu hii reincarnation and i have a lot to talk about, ila hapa nipo kwa situation flani hivi ambayo inanibana kidogo kwenda DEEP but narudi muda si mref mkuu ni mada ambayo natakiwa kwenda DEEP SANA na kujua mengi kuhusu hii kitu mkuu thanks kwa kuileta hii kitu hapa mahala.

AM COMING MKUU. THANKS AGAIN.
 
Urudi tunakusubiri mkuu na ukichelewa tutakutafuta
 
Huu ni mwendelezo tu wa kile tumekuwa tukikijadili hapa jamvini kuhusu hayo mambo mawili, reincarnation -kuzaliwa tena katika umbo lingine na rebirth -kuzaliwa upya kiroho
Reincarnation na rebirth vinatofautiana katika misingi ya kiimani, lakini kiuhalisia ni kitu kilekile
Wanaoamini katika reincarnation hawaamini katika Mungu mkuu mwenye enzi yote, bali katika nafsi na miungu, cause and effect kwamba ubaya hulipwa na ubaya na wema hulipwa na wema, yani hakuna kitu msamaha kwenye hii imani, kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake....
Wanaoamini katika rebirth, ni wale Wanaoamini katika Mungu mmoja mwenye mamlaka yote, msamaha kwa matendo ya nyuma na kuzaliwa upya kiroho...kwahiyo hata kama umetenda dhambi kiasi gani ukitubu na kuungama basi dhambi zako zote husamehewa na kuwa kiumbe kipya kiroho katika mwili uleule

TUJADILI
Ukiangalia kwa uwazi tu utaona dhana zote mbili za reincarnation na rebirth zote zinahusika na roho. Roho ndio msingi wa dhana zote mbili nje ya roho hakuna reincarnation wala rebirth, bali kuna mkusanyiko wa mifupa na nyama ambavyo hutengeneza kitu kiitwacho mwili
Mfanano wa reincarnation na rebirth ni Kama nilivyosema ni roho na roho inapoumbwa haifi tena, haifi milele, aidha iwe reincarnated au ilale kuzimu ikisubiri hukumu kuu na baada ya hapo inaishi milele mbinguni paradiso au jehanam
Kwahiyo tusichanganyikiwe na hilo, hizi ni Lugha tu lakini kitu ni kimoja nacho ni roho na roho haifi ikishazaliwa au ishaumbwa (created)

Kuna mambo mawili matatu unahitaji kuyatazama upya na kujaribu kuyapangilia vema sura yake katika uwanja wa maarifa yako mintarafu 'Utwaaji upya mwili (Re-incarnation)' na 'Uzaliwa Upya (Rebirth)'...

Ni mashauri juu ya makanika ya Roho, Sonafi na Maiingiliano yake kulingana na muktadha mmoja hadi mwingine.

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisichoonekana lakini kuhuisha kile kinachoonekana basi yenyewe huwa ni shauri pana pasi ukomo.

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisicho ukomo basi wahitaji kubayanisha upi ni muingiliano wake na vile venye 'ukomo'(?)

Ukisema na kuchukulia Roho ni chenye kuingiliana na vile vyenye ukomo basi wahitaji kubayanisha 'mapana na marefu yote' yana 'nafasi' gani katika hiyo yenyewe?

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisicho na Ukomo na hali chaingiliana na yenye ukomo basi wahitaji kubayanisha sura ama mabadiliko ya sura ya jambo moja hadi jingine huja kwa namna gani (?)

Ukisema na kuchukulia Roho kile kisicho ukomo basi je, si kwamba mabadiliko yote ni sehemu ya kweli yake -- na kama mabadiliko yote ni sehemu ya kweli yake je, 'wakati' ni kitu gani kulingana na hiyo yenyewe?

Sasa twazungumza ya 'Roho' kuyataja yale yaliyositirika, yale yaliyo ni mafumbo -- yale yaliyo ni kweli japo ni ile tusiyoimaizi namna yake.

Mashauri yote haya ni jitihada tu ya 'vina vya tafsiri' juu ya yale tudhaniayo kuyafahamu. Si jambo baya kudhania, ila ni vizuri kutambua katika kutafuta kuzifahamu ama kuzifumbua 'siri ya maumbo' ama 'uzima', sisi twaanza kuwa ni watu 'Wasikirifu'(Mystics, kng), sisi twawa ni wasafiri wa kiroho katika kuchunguza yote...

Msikirifu ni mtu mwenye kujitahidi kung'amua siri za uzima na kweli ya yote. Katika hili, utata wa maumbo, sura, mwendo tabia na mabadiliko huwa ni sehemu ya muktadha wa ung'amuzi wake juu ya 'Ukweli' wenyewe kulingana na jicho lake yeye mwenyewe... Na basi moja lenye fumbo, siri, ugumu ama hata sitaajabu ni shauri la 'muda' ama 'wakati'.

Wakati ni kitu gani?

Mambo ya Roho ni fumbo; lakini Msikirifu ni mtu asiye acha hata jiwe kubaki bila kupinduliwa, ikimbidi yeye kutafuta hakika ya nuru yake ya ufahamu...

Mambo ya Roho husubiri wale walioimara katika kutafuta, kusubiri na kupokea; ili hao wapate kung'amua hazina ya yale yaliyositirika.

Ikiwa mambo yote yamefanyika kulingana na 'asili' moja -- kutosholeza kweli ya kile kinachobebea ndani yote -- yaliyodhahiri na yasiyodhahiri; basi ndivyo hakuna 'Roho' mbili -- roho ni moja... Kwa kadiri ya safari yetu ya kung'amua mafumbo na kweli ya yote ndivyo hata mapokeo ya dini huzungumza juu ya 'Mungu' mmoja... Ila ni namna gani mungu mmoja huwa haya yote na i wapi nafasi ya mtu ama 'nafsi' katika 'Mungu'?

Nafasi ya mtu katika Mungu huja na 'Sonafi'.

Ikiwa Mungu ni fumbo na shauri la milele, mtu na nafsi ni si vya milele; basi kadiri ya mapana ya mtu na nafsi huja kwa fanusi(function, kng) ya sonafi.

Katika ulimwengu usio na mwanzo wala mapana, muda pia yaweza kuwa ni shauri mushkeli -- umilele ni fumbo tata kama sio gumu kuling'amua. Lakini patanisho la mtu kama nafsi, na yale ya milele huja na sonafi. Ikiwa uzima wote ni mwangaza wa milele na pumzi ya milele ya uzima wote, sonafi ya mtu huleta 'usiku' na 'mchana' katika marefu ya kudumu na kuishi ya mtu. Basi ikiwa twataka kujua yale ya mungu, sharti kwanza tujijue sisi wenyewe vizuri... Tujijue sisi wenyewe vema kimwili, kiakili na kisaikia.

Saikia (Utatu wa Nafsi-roho, akili na Hisia) yetu yaweza kuwa ndiyo mlango hasa wa kung'amulia mafumbo ya kiroho. Saikia ni fanusi ya Sonafi ya mtu ama kitu ama jambo. Na ndivyo kwa lugha kama kiingereza shauri la sonafi ndilo hutajwa ni 'Soul', kuwa na mzizi wa maana sawa na 'jua' ama mwangaza mkuu.

Sasa kuna mengi ya kuyamulika ili kubayanisha ni jinsi gani makanika ya 'maumbo' na 'nyakati'; sonafi ni kiunganishi cha mambo yaliyo ndani ya ukweli wa 'uzima wa milele'... Kujua hakika iliyo na Sonafi ni kutaamulika na ukweli wa maumbo na hatma zake.

Saikia ni zao la Mwili, Akili na Hisia, Sonafi haina chochote na asili ya mwili ama maumbo... Basi Saikia na mambo yake ni vya kupita, lakini Sonafi hudumu zaidi. Nafsi ni Zao la Saikia, Lakini nafsi ni kimvuli cha neema na matunda ya sonafi na madaraja yake ya kusitirisha maumbo na sura zake... Basi 'mtu' na 'nafsi' ni usikweli, ila sonafi ndiyo hakika ya siri ya hatma ya mtu.

Nafsi hufa na mwili, Sonafi huihuisha 'nafsi' zaidi -- katika vitovu vingine zaidi vya mawezekano ya 'uzima' na 'maisha'. Mwili ni chombo cha kuhuisha kweli ya Sonafi -- Saikia na Akili kuwa daraja la kukadirisha sura na masongamano mengine yenyekuweza hata kupitiliza tafsiri zetu rahisi la mfuatano wa matendo, matukio na sura za mambo.

'Utwaaji upya mwili' wakadirika kutajwa hivyo kulingana na Sonafi 'inavyoounganika' upya na mwili na kuendeleza 'kusudio' toka kwenye nafsi na mwili mwingine wenye kufahamika sura kwa sura na matendo yake.

'Utwaaji upya mwili' ni mwendelezo wa Sonafi 'kujiunganisha' na uzima mmoja wa mwili hadi mwingine... Sonafi ni hatma na asili isiyokadirika 'neema' na 'kweli' yake katika mwili mmoja na namna moja... Kweli ya Sonafi yaweza kujikadirisha kwa mamia elfu ya miili ya viumbe na malaki ya miaka katika vipindi vya muda na wakati tuufahamuo...

Sonafi ya mtu ndiyo 'neno la uzima' la mtu mwenyewe...

Ni jinsi gani Sonafi ya mtu humulika na kuongoza 'sura' ya mtu katika maisha? Shauri hili lahitaji kuupanua uwanja wa mawazo ili kung'amua makusudio mapana ya 'viumbe', 'maisha' na 'Uhai'...

Kwenye ilimu ijayo na mapokeo ya mafundisho ya Yesu, Kristu ni muktadha wa ndani wa Sonafi; Katika ilimu ijayo na mapokeo ya mafundisho ya Buddha, Dhamma ndiyo muktadha wa maumbo yote, uzima wote -- kristu na neema zote katika 'wakati'.

Ya zaidi kuyajua ni Kristu ni nini na Dhamma ni nini -- je, viwili hivi vyasukana vipi na 'wakati'?

+++

Kuku na Yai--Kipi kilitangulia kuwepo? mashauri ya kiontolojia

13 Oktoba 2011 saa 09:07 mchana/ jioni
YAH: Mazungumzo na mabadilishano ya mawazo kati yangu na mjumbe mmoja wa JF kuhusu:-

Mfanyiko wa Ulimwengu,
Siri za Uzima,
Asili ya Nafsi,
Muktadha wa Uzima wa Milele,
Kuja na Kwenda kwa Nafsi,
Mungu kama Usifa-akili wa kinishati na uweza uliofanyikia katika Vyote na Mote; kuzidi udhanifu wa kawaida wa mapokeo ya kidini na kiimani

na mawazo mengine...

Hii ni nukuu kutoka kwenye sehemu ya mawaidha yaliyoko katika mfululizo wa vidokezo vingine kwa jina la 'Kutoka--Mwongozo huru kuelekea Uhuru Halisi'

Mei 5, 2011.

******

...

Maumbo yote ni maua ya Roho-Ulimwengu wote umefanyika kwa jinsi ya Ua la Uzima. Uzuri na Urembo unaofanyikia madhahiriko yote na wakati ni kutaniko la mienendo katika mifumo inayoingiliana na hivi kufanya vituo vya sura na ishara ya usifaakili unaofanya vitu vyote. Usifa akili huu ni fanusi ya Uzima-muktadha wa unyoofu na mawimbi yaliyoko kote na mote. Mawimbi haya husukuma 'chembe' za maumbo kutungika katika udhahiri wa sura na migando kwa neema ya nguvu ya 'unyoofu'. Jinsi hii pia ndiyo muktadha wa usumaku na umeme utawalao madhahiriko yote. Usumaku na umeme hufumanishwa na roho; na katika madhahirisho yote ni mbegu ya utatu-jinsi ya miale ya nuru na usumaku na uhifadhiko wa hayo yote mawili katika mapana zaidi. Hivi kuendelea pasiko kikomo. Uvumbuzi uliodhirisha penye usumaku pana umeme ndiyo pia uliodhihirisha penye ugani wa umeme au sumaku katika kupambanishwa kimraba-kadri ya mielekeo ya mitiririko ya nguvu kwa kile chenye jinsi ya umeme na kile chenye jinsi ya usumaku, hivi viwili huzaa msukumo wa mwendo katika mwelekeo wa tatu ulio ni mraba kwa uwanda wa usumaku na umeme wenyewe; kitendo cha kuepana na hivi kusogea mbali. Katika mashauri ya taaluma ya umeme husemwa ni 'sheria ya Lenzi'; ile yenye kufafanua ufuaji umeme au utengenezaji mwendo katika mitambo yenye kuzunguka kiumeme. Hii pia ni siri ya mfumiko wa madhahirisho yote. Mielekeo ya kipande tatu hufanya ule kama ni muktadha wa marefu, mapana na kina kwa tofali la mraba. Na ni jiwe la msingi katika kutathmini hali za maumbo na mienendo yote.

Ijapokuwa maumbo huweza kujipanga na kuitengeneza sura fulani bayana, hili hufanyika kwa muktadha wa maumbo mengine yaliyo madogo zaidi katika muktadha wa madhahirisho yote. Madhahiriko mengine huchukua sura kwa mitiririko ya maumbo yenye kubadilika muktadha wake katika bahari ya mawimbi ya uumbiko wote; hii bahari isiyokuwa na mwanzo wala mwisho wa mapana yake. Madhahiriko yenye sifa hii hayatathminiki kwa bahari yenyewe ama mawimbi ila tu ule uchochezi wa kufikia 'Ua' fulani. Basi ua hili huwa ni mbegu na tena huwa ni 'unyoofu' wenye kuweza kuratibu mpangilio. Hili kuwezekana tu pale ambapo pana kipeo cha tatu cha hadhi ya madhahiriko yote; kile chenye kukirimu mfanyiko wa sura ama umbo-hili hufanya 'kizio' cha umbo ama chembe; namna ya uhifadhiko wa sura ya maumbo toka katika mapana ya kiujazo yasiyo na kikomo. Maumbile yote kwa jinsi ya ukutano wa 'unyoofu' na 'mawimbi' hayana 'hakika ya milele'. Hakika ipo kwenye yote mawili uwepo na utowepo wa vitu vyote. Na hivi yote yaliyodhahirika si 'Kweli' kamili ila tu kujumuisha yale yasiyodhahirika-Roho ni yote mawili kwa 'wakati mmoja'.

Twaweza kutanabahi muktadha huu wa udhahiriko wa maumbo kwa kulifikia lile fumbo la Yai na Kuku. Swali la kipi kilianza kati ya Yai na Kuku; limekuwa ni msingi wa mdahalo wa kifalsafa na sayansi ya maumbo. Pia limekuwa ni fumbo katika kujaribu kusimamisha mashauri yasiyo na mzozo juu ya maumbo na asili; uwepo wa yote na kile kilichoyafanya yote-asilishi ya halisia yote. Ikiwa kifaranga cha kuku hutotolewa kutoka katika yai, sasa je, bila ya yai awezakufanyika huyo kuku? Yai hutagwa na kuku, sasa je, bila ya kuku laweza kufanyika hilo yai? Basi tena, iweje tupate kusema ni kile hasa kilianza kati ya kuku na yai?

Kadri hiyo hiyo huleta utata katika muktadha wa udhanifu kimawazo katika kuzungumzia ulimwengu na mungu. Watu wa makabila mbali mbali wanamashauri yao yenye kumzungumzia 'Mungu'. Wakisema ni Mungu aliyeumba ulimwengu wote; swali linaloweza kukaribishwa kwa kufuatia huwa ni basi kwamba kuuliza na yeye huyo Mungu aliumbwa na nani tena? Kwa kuwa vyovyote vile katika muktadha huu, falsafa zote za wanadamu hupwaya kwa kukosa 'maana' ya dhati. Na ndilo tatizo la msingi katika mashauri yenye kufuatisha dhana na mantiki. Basi ndivyo huja maelezo yenye msigano katika udadavuaji wa muktadha mzima wa wezekano halisi kwa ukweli wa jambo na mambo yote. Wapo wanaodai kusema Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na yeye hakufanywa na yeyote mwingine; makabila mengi duniani aghalabu shauri hili lipo miongoni mwa mashauri ya dini zao za asili. Inasikika kupata kusemwa pia kuwa Mungu 'hakuzaliwa' na wala 'hakuzaa'... Lakini haya yote ni kukadirisha tu ugumu wa kufumbua fumbo lenyewe katika minajili ya dhana na mawazo ya jinsi ya utumikivu wa akili ya kawaida ya watu wenyewe.

Kuku na Yai ni nelibini--'kaleidoskopi' ya uzima kamili wa kadri ya vyote viwili; kumaanisha basi ni mang'amung'amu ya madhahirisho-mabadiliko endelevu yenye kubadilishana sura na mwonekano kwa kadri ya haraka na harakati zake na tena ndani ya vituo vya muktadha wa kiumbe; mbele ya macho ya mtazamaji. Kadri iwezavyo kuzungumzwa kusemwa ni kibayolojia, muktadha kamili wa kiumbe chenye kutajwa hai ni jumuiko la chembe ndogo ndogo zenye kuungana pamoja katika kudhahirisha sifakazi maalum; wakati mwingine yaweza kuwa chembe moja pekee ama mkusanyiko chembe kufanya muktadha sifakazi moja kama 'tishu' na tena hata 'tishu' na tishu' kufanya hadhi kazi pana zaidi. Chembe chembe hizo ndiyo 'kizio' cha muktadha wa uhai wenyewe wa kiumbe hai chote kizima. Katika mfanyiko wa viumbe hai ni chembe hai hukomaa na kugawanyika kimaumbo kamili na hivi kuongezeka ukubwa kwa kadri ya jinsi ya kiumbe hai husika. Ifikapo ukamilifu fulani wa kimaumbo kiumbe halisia huchukua sura yake ya uhai na kukidhi ufafanuzi wa hicho 'kuwa hai'. Kisha katika muktadha wa jinsi ya kiumbe kimoja hicho nacho hukunjuka sura ya shani yake na kudhahirisha harakati, mielekeo na mienendo ilivyo hiyo minajili ya nelibini kulingana na kudra zake za kufanyikia.

Yai ni mapana ya kituo kimoja na kuku kuwa ni kituo kingine. Katika kuku twaona 'hiyari' ya wawili ili kutunga yai moja. Huchukua tembe na jogoo kugusana kimwili ili kutunga yai. Basi kumbe huitaji yai na yai ili kufanya kuku na kuku kusudi yai-kuku-yai kudumu mwenendo wake kinelibini. Na hivi katika yai hakuna 'hiyari' ila tu ubidifu wa kuwa aidha jinsi ya kike ama ya kiume. Kati ya yai na kuku kuna mpaka wa muktadha wa kuja kudhahirika 'kuku'. Yai laweza kustahimilisha mawezekano yote iwe ya kike ama kiume lakini kuku hana budi kufanyika kwa jinsia. Akiwa tembe hawezi kuwa jogoo na akiwa jogoo hawezi kuwa tembe; ila kwa namna ya kipekee, yenye kuhusisha 'kutaniko la kimwili' na tena palipo na jinsia mbili ni moja yenye uwezekano wa moja kwa moja kuendeleza madhahirisho. Jinsia hiyo ni ile ya kike. Ni jinsia ya kike yenye uwezo wa kustahimilisha mtungiko wa maumbile yenye kuja kufanya madhahirisho ya kiumbe na jinsia ya kike au kiume; na hivi basi kubakiza kuwa katika jinsi ya kiume ndiko kwenye mbegu ya jinsia moja kwa wakati na halafu kwa kutawaliwa na 'mazingira' fulani yasiyofahamika vema lakini kuhusisha uwiano wa kimazingira yenyewe ya kuwapo kwake viumbe hai na saikia jumuizi--hali ya 'kutotabirika' kwa jinsia itayofuatia baada ya kitendo cha 'kutaniko la kimwili' na mtungiko mpya.

Kufanyika kwa kiumbe hai ni kwenye kubeba sehemu ya utambuko wa kimwili na jinsia. Viumbe hai kama wanyama si vyenye kujitambua kwa kila kitu kinachofanya ama kufanyikia ndani ya miili yao. Utambuzi wa kimiili huwa na kadri ya 'uso' tu wa miili yenyewe na mengine yote ni maendelezo ya utumikivu wa akili za viumbe vyenyewe. Kwa mfano mwanadamu hawezi kwa hakika kushuhudia kuwa ana maini ndani ya mwili wake na hayo yamekaa wapi ndani yake; hawezi kusema maji na chakula katika mwili wake husagwa vipi na kusharabiwa katika mwili wake wote. Pia hawezi kueleza pumzi avutayo ni yenye kustahimilisha vipi viungo vya mwili wake na mapana ya kutumika kwake. Hawezi kuzungumzia haya kwa hakika na angali yote yakiwa ni sehemu ya muktadha 'unaotathmini' uzima wake kwa wakati na msukumo wa pilika zake za kila siku. Viungo vyote vya ndani ya mtu na viumbe pia hufanyika kwa tishu zile zenye kufanywa kwa chembechembe ndogo ndogo na tena zilizo ni 'kizio' cha uhai-seli. Hata viungo vya ndani vya nyama kama moyo na ubongo vyote ni kutaniko la tishu zifanyazwo kwa seli za idadi nyingi sana sifanyazo kazi kwa utangamano unaratibiwa na 'mawimbi ya uzima'. Mawimbi haya ndiyo yale yenye kuja kwa sura ya rithimu. Rithimu hii huratibu tabia na mabadiliko ya seli zote; kuanzia kutungika, kukomaa na kufa. Na hivi japo kiungo chaweza kuonekana kudumu kwa miaka mingi, seli zinazounda viungo hivyo si za muda mrefu kama dhahiriko la kiungo chenyewe. Seli nyingi katika miili ya viumbe hutungika, kukomaa na kufa na hali uzima wa kiumbe kuonekana uko pale pale... Hata mwanadamu afikapo uzeeni, mwili wake wote ushakufa seli nyingi sana na mara kadhaa kulingana na rithimu na majira yaletwayo na mawimbi ya uzima. Kwa kuwa seli hufa kwa kupokezana na nyingine mpya zilizotungika na kuongezeka, mtu kwa kadri ya utumikivu wa akili yake yeye hujionana ni yule yule siku zote za kuishi kwake.

Basi ndivyo tunaweza kusema wazi 'mtu' ama 'kiumbe' si mwili hasa. Kinyume na inavyochukulika na kufikirika hata katika ulimwengu wa sayansi leo ya kwamba mtu hufanyika na 'kutosha' kuwa mtu kwa ile mifumo na mienendo yote ya kimwili; huu si ukweli-ni nusu ukweli ulio ni hatari kuliko uongo kamili. Kwa kuwa ile sehemu yake yenye kuonekana kama ni ukweli kuwa ni hivyo yaweza kumzuzua mwenye kutazama na kumpelekea yeye kwenye hitimisho la mashauri lisilo sahihi. Uongo kamili hukosa shikilizo katika halisia; lakini 'nusu ukweli' inacho kiungo chenye 'kujishikiza' kwenye 'halisia' kamili. Basi mtu ni 'kweli' iliyochanganyikana na 'usikweli' na tena kwa jinsi ya ajabu kujitahidi pamoja katika kudhahirisha sura ya 'utu'. Mwanadamu kiumbe kinachobebwa na viumbe katika michakato ili kukirimika 'sura' yake. Utu ni mbegu ijayo kwa muktadha wa 'Saikia' kamili ambamo ndani yake mna yote 'yanatosha' kukadirisha muktadha wa mtu katika kudhahirika juu ya mwili wa nyama.

Ndani ya Saikia kuna muktadha wa vitu vitatu kuchambulika kipekee--nafsi-roho, akili na nafsi. Nafsi huhusisha muktadha wa akili, kumbukumbu ya mtu kujichukulia katika mazingira yake akitumia mwili kama chombo cha 'uhalisia' wake. Huu ni upande wa chini wa akili ya kawaida; upande wa juu wa akili huwa ni dhahania kwa uadilifu wa kiutu kwa unafsi wa mtu mwenyewe. Haya yote huakisi mawezekano ya Ua la ndani la mtu lililo ni nafsi-roho; sehemu ya sura ya 'mpango mzima' kwa utu ndani ya Roho wa Uzima wote. Nafsi-roho ndiyo hii 'Sonafi' katika mwingiliano wa mwili, akili na uzima-Jua la utu lenye kuungazia uwezekano wa neema zote za mfanyiko na mdhahiriko wa ubinadamu.

Uhalisia wa Saikia ifungamanavyo na mwili ni jinsi ya msalaba; japo mwili hutungika na kufa, saikia ya mtu ya mtu haitungiki na kufa na mwili. Mapana ya kuzaliwa na kufa si mapana na marefu ya Saikia ila tu mkatizio wa Saikia yenyewe katika mfanyiko wa mwili. Saikia ni 'mgeni' katika mwili na tena mpangishaji tu. Saikia huchanua na kukomaa katika mwili na huku ikiendesha mwili kwa sura ya hivyo hivyo na hali mwili ukatapo pumzi Saikia 'hujikunjia ndani' kama mbegu yenye kusubiri na kuhitaji pahala pengine penye kustahili hiyo kumea na kuchipua tena. Mbegu ya 'utu' ina usiku na mchana kama ilivyo katika mizunguko mingine ya kiuhai yenye kuja na misimu na majira-rithimu zifuatishazo namna ya 'mawimbi ya uzima' na 'wavu' wa maumbo-wakati. Iwapo katika giza huwa ni 'chembe ya ndoto' na mang'amu ng'amu yake; japo hayo yote huwa ni ya mpito tu. Yale ambayo watu wa makabila huzungumza kuhusu 'mahala pa wafu' ni sehemu za mpito ambazo 'hazina uhalisia' wa kutosha kuneemesha 'mbegu ya utu'. Ni pahala penye giza tororo ama mbalamwezi kwa Saikia ya mtu japo upo ufundi wa kutumia sehemu hiyo ya mpito katika 'kuhifadhi' kwa kana vile 'kugandisha' kadri mbali mbali ya uwezo na karama mahususi zilizopata kufikiwa na kutambuliwa ndani saikia ya mtu aliyeachia mwili. Na basi Sakia ya mtu huweza kunasa katika wavu wa maumbo-wakati na kudhahirika mtu mwenye kuishi upya.

https://www.facebook.com/notes/mose...epo-mashauri-ya-kiontolojia/10150351001719421
 
Kuna mambo mawili matatu unahitaji kuyatazama upya na kujaribu kuyapangilia vema sura yake katika uwanja wa maarifa yako mintarifu 'Utwaaji upya mwili (Re-incarnation)' na 'Kuzaliwa Upya (Rebirth)'...

Ni mashauri juu ya makaniki ya Roho, Sonafi na Maiingiliano yake kulingana na muktadha mmoja hadi mwingine.

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisichoonekana lakini kuhuisha kile kinachoonekana basi yenyewe huwa ni shauri pana pasi ukomo.

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisicho ukomo basi wahitaji kubayanusha upi ni muingiliano wake na vile venye ukomo(?)

Ukisema na kuchukulia Roho ni chenye kuingiliana na vile vyenye ukomo basi wahitaji kubayanisha 'mapana na marefu yote' yana 'nafasi' gani katika hiyo yenyewe?

Ukisema na kuchukulia Roho ni kile kisicho na Ukomo na hali chaingiliana na yenye ukomo basi wahitaji kubayanisha sura ama mabadiliko ya sura ya jambo moja hadi jingine huja kwa namna gani (?)

Ukisema na kuchukulia Roho kile kisicho ukomo basi je, si kwamba mabadiliko yote sehemu ya kweli yake -- na kama mabadiliko yote ni sehemu ya kweli yake je, 'wakati' ni kitu gani kulingana na hiyo yenyewe?

Sasa twazungumza ya 'Roho' kuyataja yale yaliyositirika, yale yaliyo ni mafumbo -- yale yaliyo ni kweli tusiyoimaizi namna yake.

Mashauri yote haya ni jitihada tu ya vina vya tafsiri juu ya yale tudhaniayo kuyafahamu. Si jambo baya kudhania, ila ni vizuri kutambua katika kutafuta kuzifahamu ama kuzifumbua siri ya maumbo ama uzima, sisi twaanza kuwa ni watu 'Wasikirifu', sisi twawa ni wasafiri wa kiroho katika kuchunguza yote...

Msikirifu ni mtu mwenye kujitahidi kung'amua siri za uzima na kweli ya yote. Katika hili, utata wa maumbo, sura, mwendo tabia na mabadiliko huwa ni sehemu ya muktadha wa ung'amuzi wake juu ya 'Ukweli' wenyewe kulingana na jicho lake yeye mwenyewe... Na basi moja lenye fumbo, siri, ugumu ama hata sitaajabu ni shauri la 'muda' ama 'wakati'.

Wakati ni kitu gani?

Mambo ya Roho ni fumbo; lakini Msikirifu ni mtu asiye acha hata jiwe kubaki bila kupinduliwa, ikimbidi yeye kutafuta hakika ya nuru yake ya ufahamu...

Mambo ya Roho husubiri wale walioimara katika kutafuta, kusubiri na kupokea; ili hao wapate kung'amua hazina ya yale yaliyositirika.

Ikiwa mambo yote yamefanyika kulingana 'asili' moja -- kutosholeza kweli ya kile kinachobebea ndani yote yote yaliyodhahiri na yasiyodhahiri basi ndivyo hakuna 'Roho' mbili, roho ni moja... Kwa kadiri ya safari yetu ya kung'amua mafumbo na kweli ya yote ndivyo hata mapokeo ya dini huzungumza juu ya 'Mungu' mmoja... Ila ni namna gani mungu mmoja huwa haya yote na i wapi nafasi ya mtu ama nfasi katika 'Mungu'?

Nafasi ya mtu katika Mungu huja na 'Sonafi'.

Ikiwa Mungu ni fumbo na shauri la milele, mtu na nafsi ni si vya milele; basi kadiri ya mapana ya mtu na nafsi huja kwa fanusi ya sonafi.

Katika ulimwengu usio na mwanzo wala mapana, muda pia yaweza kuwa ni shauri mushkeli -- umilele ni fumbo tata kama sio gumu kuling'amua. Lakini patanisho la mtu kama nafsi na yale ya milele huja na sonafi. Ikiwa uzima wote ni mwangaza wa milele, sonafi ya mtu huleta 'usiku' na 'mchana' katika marefu ya kudumu na kuishi ya mtu. Basi ikiwa twataka kujua yale ya mungu, sharti kwanza tujijue sisi wenyewe vizuri... Tujijue sisi wenyewe vema kimwili, kiakili na kisaikia.

Saikia (Utatu wa Nafsi-roho, akili na Hisia)yetu yaweza kuwa ndiyo mlango hasa wa kung'amulia mafumbo ya kiroho. Saikia ni fanusi ya Sonafi mtu ama kitu ama jambo. Na ndivyo kwa lugha kama kiingereza shauri la sonafi ndilo hutajwa ni 'Soul', kuwa na mzizi wa maana sawa na 'jua' ama mwangaza mkuu.

Sasa kuna mengi ya kuyamulika ili kubayanisha ni jinsi gani makanika ya 'maumbo' na 'nyakati'; sonafi ni kiunganishi cha mambo yaliyo ndani ya ukweli wa 'uzima wa milele'... Kujua hakika iliyo na Sonafi ni kutaamulika na ukweli wa maumbo na hatma zake.

Saikia ni zao la Mwili, Akili na Hisia, Sonafi haina chochote na asili ya mwili ama maumbo... Basi Saikia na mambo yake ni vya kupita, lakini Sonafi hudumu zaidi. Nafsi ni Zao la Saikia, Lakini nafsi ni kimvuli cha neema na matunda ya sonafi na madaraja yake ya kusitirisha maumbo na sura zake... Basi mtu na nafsi ni usikweli ila sonafi ndiyo hakika ya siri ya hatma ya mtu.

Nafsi hufa na mwili, Sonafi huuisha 'nafsi' zaidi -- katika vitovu vingine zaidi vya mawezekano ya 'uzima' na 'maisha'. Mwili ni chombo cha kuhuisha kweli ya Sonafi -- Saikia na Akili kuwa daraja la kukadirisha sura na masongamano mengine yenyekuweza hata kupitiliza tafsiri zetu rahisi la mfuatano wa matendo, matukio na sura za mambo.

'Utwaaji upya mwili' wakadirika kutajwa hivyo kulingana na Sonafi 'inavyoounganika' upya na mwili na kuendeleza 'kusudio' toka kwenye nafsi na mwili mwingine wenye kufahamika sura kwa sura na matendo yake.

'Utwaaji upya mwili' ni mwendelezo wa Sonafi 'kujiunganisha' na uzima mmoja wa mwili hadi mwingine... Sonafi ni hatma na asili isiyokadirika 'neema' na 'kweli' yake katika mwili mmoja na namna moja... Kweli ya Sonafi yaweza kujikadirisha kwa mamia elfu ya miili ya viumbe na malaki ya miaka katika vipindi vya muda na wakati tuufahamuo...

Sonafi ya mtu ndiyo 'neno la uzima' la mtu mwenyewe...

Ni jinsi gani Sonafi ya mtu humulika na kuongoza 'sura' ya mtu katika maisha? Shauri hili lahitaji kuupanua uwanja wa mawazo ili kung'amua makusudio mapana ya 'viumbe', 'maisha' na 'Uhai'...

Kwenye ilimu ijayo na mapokeo ya mafundisho ya Yesu, Kristu ni muktadha wa ndani wa Sonafi; Katika ilimu ijayo na mapokeo ya mafundisho ya Buddha, Dhamma ndiyo muktadha wa maumbo yote, uzima wote -- kristu na neema zote katika 'wakati'.

Ya zaidi kuyajua ni Kristu ni nini na Dhamma ni nini -- je, viwili hivi vyasukana vipi na 'wakati'?

+++

Kuku na Yai--Kipi kilitangulia kuwepo? mashauri ya kiontolojia

13 Oktoba 2011 saa 09:07 mchana/ jioni
YAH: Mazungumzo na mabadilishano ya mawazo kati yangu na mjumbe mmoja wa JF kuhusu:-

Mfanyiko wa Ulimwengu,
Siri za Uzima,
Asili ya Nafsi,
Muktadha wa Uzima wa Milele,
Kuja na Kwenda kwa Nafsi,
Mungu kama Usifa-akili wa kinishati na uweza uliofanyikia katika Vyote na Mote; kuzidi udhanifu wa kawaida wa mapokeo ya kidini na kiimani

na mawazo mengine...

Hii ni nukuu kutoka kwenye sehemu ya mawaidha yaliyoko katika mfululizo wa vidokezo vingine kwa jina la 'Kutoka--Mwongozo huru kuelekea Uhuru Halisi'

Mei 5, 2011.

******

...

Maumbo yote ni maua ya Roho—Ulimwengu wote umefanyika kwa jinsi ya Ua la Uzima. Uzuri na Urembo unaofanyikia madhahiriko yote na wakati ni kutaniko la mienendo katika mifumo inayoingiliana na hivi kufanya vituo vya sura na ishara ya usifaakili unaofanya vitu vyote. Usifa akili huu ni fanusi ya Uzima—muktadha wa unyoofu na mawimbi yaliyoko kote na mote. Mawimbi haya husukuma 'chembe' za maumbo kutungika katika udhahiri wa sura na migando kwa neema ya nguvu ya 'unyoofu'. Jinsi hii pia ndiyo muktadha wa usumaku na umeme utawalao madhahiriko yote. Usumaku na umeme hufumanishwa na roho; na katika madhahirisho yote ni mbegu ya utatu—jinsi ya miale ya nuru na usumaku na uhifadhiko wa hayo yote mawili katika mapana zaidi. Hivi kuendelea pasiko kikomo. Uvumbuzi uliodhirisha penye usumaku pana umeme ndiyo pia uliodhihirisha penye ugani wa umeme au sumaku katika kupambanishwa kimraba—kadri ya mielekeo ya mitiririko ya nguvu kwa kile chenye jinsi ya umeme na kile chenye jinsi ya usumaku, hivi viwili huzaa msukumo wa mwendo katika mwelekeo wa tatu ulio ni mraba kwa uwanda wa usumaku na umeme wenyewe; kitendo cha kuepana na hivi kusogea mbali. Katika mashauri ya taaluma ya umeme husemwa ni 'sheria ya Lenzi'; ile yenye kufafanua ufuaji umeme au utengenezaji mwendo katika mitambo yenye kuzunguka kiumeme. Hii pia ni siri ya mfumiko wa madhahirisho yote. Mielekeo ya kipande tatu hufanya ule kama ni muktadha wa marefu, mapana na kina kwa tofali la mraba. Na ni jiwe la msingi katika kutathmini hali za maumbo na mienendo yote.

Ijapokuwa maumbo huweza kujipanga na kuitengeneza sura fulani bayana, hili hufanyika kwa muktadha wa maumbo mengine yaliyo madogo zaidi katika muktadha wa madhahirisho yote. Madhahiriko mengine huchukua sura kwa mitiririko ya maumbo yenye kubadilika muktadha wake katika bahari ya mawimbi ya uumbiko wote; hii bahari isiyokuwa na mwanzo wala mwisho wa mapana yake. Madhahiriko yenye sifa hii hayatathminiki kwa bahari yenyewe ama mawimbi ila tu ule uchochezi wa kufikia 'Ua' fulani. Basi ua hili huwa ni mbegu na tena huwa ni 'unyoofu' wenye kuweza kuratibu mpangilio. Hili kuwezekana tu pale ambapo pana kipeo cha tatu cha hadhi ya madhahiriko yote; kile chenye kukirimu mfanyiko wa sura ama umbo—hili hufanya 'kizio' cha umbo ama chembe; namna ya uhifadhiko wa sura ya maumbo toka katika mapana ya kiujazo yasiyo na kikomo. Maumbile yote kwa jinsi ya ukutano wa 'unyoofu' na 'mawimbi' hayana 'hakika ya milele'. Hakika ipo kwenye yote mawili uwepo na utowepo wa vitu vyote. Na hivi yote yaliyodhahirika si 'Kweli' kamili ila tu kujumuisha yale yasiyodhahirika—Roho ni yote mawili kwa 'wakati mmoja'.

Twaweza kutanabahi muktadha huu wa udhahiriko wa maumbo kwa kulifikia lile fumbo la Yai na Kuku. Swali la kipi kilianza kati ya Yai na Kuku; limekuwa ni msingi wa mdahalo wa kifalsafa na sayansi ya maumbo. Pia limekuwa ni fumbo katika kujaribu kusimamisha mashauri yasiyo na mzozo juu ya maumbo na asili; uwepo wa yote na kile kilichoyafanya yote—asilishi ya halisia yote. Ikiwa kifaranga cha kuku hutotolewa kutoka katika yai, sasa je, bila ya yai awezakufanyika huyo kuku? Yai hutagwa na kuku, sasa je, bila ya kuku laweza kufanyika hilo yai? Basi tena, iweje tupate kusema ni kile hasa kilianza kati ya kuku na yai?

Kadri hiyo hiyo huleta utata katika muktadha wa udhanifu kimawazo katika kuzungumzia ulimwengu na mungu. Watu wa makabila mbali mbali wanamashauri yao yenye kumzungumzia 'Mungu'. Wakisema ni Mungu aliyeumba ulimwengu wote; swali linaloweza kukaribishwa kwa kufuatia huwa ni basi kwamba kuuliza na yeye huyo Mungu aliumbwa na nani tena? Kwa kuwa vyovyote vile katika muktadha huu, falsafa zote za wanadamu hupwaya kwa kukosa 'maana' ya dhati. Na ndilo tatizo la msingi katika mashauri yenye kufuatisha dhana na mantiki. Basi ndivyo huja maelezo yenye msigano katika udadavuaji wa muktadha mzima wa wezekano halisi kwa ukweli wa jambo na mambo yote. Wapo wanaodai kusema Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na yeye hakufanywa na yeyote mwingine; makabila mengi duniani aghalabu shauri hili lipo miongoni mwa mashauri ya dini zao za asili. Inasikika kupata kusemwa pia kuwa Mungu 'hakuzaliwa' na wala 'hakuzaa'... Lakini haya yote ni kukadirisha tu ugumu wa kufumbua fumbo lenyewe katika minajili ya dhana na mawazo ya jinsi ya utumikivu wa akili ya kawaida ya watu wenyewe.

Kuku na Yai ni nelibini--'kaleidoskopi' ya uzima kamili wa kadri ya vyote viwili; kumaanisha basi ni mang'amung'amu ya madhahirisho—mabadiliko endelevu yenye kubadilishana sura na mwonekano kwa kadri ya haraka na harakati zake na tena ndani ya vituo vya muktadha wa kiumbe; mbele ya macho ya mtazamaji. Kadri iwezavyo kuzungumzwa kusemwa ni kibayolojia, muktadha kamili wa kiumbe chenye kutajwa hai ni jumuiko la chembe ndogo ndogo zenye kuungana pamoja katika kudhahirisha sifakazi maalum; wakati mwingine yaweza kuwa chembe moja pekee ama mkusanyiko chembe kufanya muktadha sifakazi moja kama 'tishu' na tena hata 'tishu' na tishu' kufanya hadhi kazi pana zaidi. Chembe chembe hizo ndiyo 'kizio' cha muktadha wa uhai wenyewe wa kiumbe hai chote kizima. Katika mfanyiko wa viumbe hai ni chembe hai hukomaa na kugawanyika kimaumbo kamili na hivi kuongezeka ukubwa kwa kadri ya jinsi ya kiumbe hai husika. Ifikapo ukamilifu fulani wa kimaumbo kiumbe halisia huchukua sura yake ya uhai na kukidhi ufafanuzi wa hicho 'kuwa hai'. Kisha katika muktadha wa jinsi ya kiumbe kimoja hicho nacho hukunjuka sura ya shani yake na kudhahirisha harakati, mielekeo na mienendo ilivyo hiyo minajili ya nelibini kulingana na kudra zake za kufanyikia.

Yai ni mapana ya kituo kimoja na kuku kuwa ni kituo kingine. Katika kuku twaona 'hiyari' ya wawili ili kutunga yai moja. Huchukua tembe na jogoo kugusana kimwili ili kutunga yai. Basi kumbe huitaji yai na yai ili kufanya kuku na kuku kusudi yai-kuku-yai kudumu mwenendo wake kinelibini. Na hivi katika yai hakuna 'hiyari' ila tu ubidifu wa kuwa aidha jinsi ya kike ama ya kiume. Kati ya yai na kuku kuna mpaka wa muktadha wa kuja kudhahirika 'kuku'. Yai laweza kustahimilisha mawezekano yote iwe ya kike ama kiume lakini kuku hana budi kufanyika kwa jinsia. Akiwa tembe hawezi kuwa jogoo na akiwa jogoo hawezi kuwa tembe; ila kwa namna ya kipekee, yenye kuhusisha 'kutaniko la kimwili' na tena palipo na jinsia mbili ni moja yenye uwezekano wa moja kwa moja kuendeleza madhahirisho. Jinsia hiyo ni ile ya kike. Ni jinsia ya kike yenye uwezo wa kustahimilisha mtungiko wa maumbile yenye kuja kufanya madhahirisho ya kiumbe na jinsia ya kike au kiume; na hivi basi kubakiza kuwa katika jinsi ya kiume ndiko kwenye mbegu ya jinsia moja kwa wakati na halafu kwa kutawaliwa na 'mazingira' fulani yasiyofahamika vema lakini kuhusisha uwiano wa kimazingira yenyewe ya kuwapo kwake viumbe hai na saikia jumuizi--hali ya 'kutotabirika' kwa jinsia itayofuatia baada ya kitendo cha 'kutaniko la kimwili' na mtungiko mpya.

Kufanyika kwa kiumbe hai ni kwenye kubeba sehemu ya utambuko wa kimwili na jinsia. Viumbe hai kama wanyama si vyenye kujitambua kwa kila kitu kinachofanya ama kufanyikia ndani ya miili yao. Utambuzi wa kimiili huwa na kadri ya 'uso' tu wa miili yenyewe na mengine yote ni maendelezo ya utumikivu wa akili za viumbe vyenyewe. Kwa mfano mwanadamu hawezi kwa hakika kushuhudia kuwa ana maini ndani ya mwili wake na hayo yamekaa wapi ndani yake; hawezi kusema maji na chakula katika mwili wake husagwa vipi na kusharabiwa katika mwili wake wote. Pia hawezi kueleza pumzi avutayo ni yenye kustahimilisha vipi viungo vya mwili wake na mapana ya kutumika kwake. Hawezi kuzungumzia haya kwa hakika na angali yote yakiwa ni sehemu ya muktadha 'unaotathmini' uzima wake kwa wakati na msukumo wa pilika zake za kila siku. Viungo vyote vya ndani ya mtu na viumbe pia hufanyika kwa tishu zile zenye kufanywa kwa chembechembe ndogo ndogo na tena zilizo ni 'kizio' cha uhai—seli. Hata viungo vya ndani vya nyama kama moyo na ubongo vyote ni kutaniko la tishu zifanyazwo kwa seli za idadi nyingi sana sifanyazo kazi kwa utangamano unaratibiwa na 'mawimbi ya uzima'. Mawimbi haya ndiyo yale yenye kuja kwa sura ya rithimu. Rithimu hii huratibu tabia na mabadiliko ya seli zote; kuanzia kutungika, kukomaa na kufa. Na hivi japo kiungo chaweza kuonekana kudumu kwa miaka mingi, seli zinazounda viungo hivyo si za muda mrefu kama dhahiriko la kiungo chenyewe. Seli nyingi katika miili ya viumbe hutungika, kukomaa na kufa na hali uzima wa kiumbe kuonekana uko pale pale... Hata mwanadamu afikapo uzeeni, mwili wake wote ushakufa seli nyingi sana na mara kadhaa kulingana na rithimu na majira yaletwayo na mawimbi ya uzima. Kwa kuwa seli hufa kwa kupokezana na nyingine mpya zilizotungika na kuongezeka, mtu kwa kadri ya utumikivu wa akili yake yeye hujionana ni yule yule siku zote za kuishi kwake.

Basi ndivyo tunaweza kusema wazi 'mtu' ama 'kiumbe' si mwili hasa. Kinyume na inavyochukulika na kufikirika hata katika ulimwengu wa sayansi leo ya kwamba mtu hufanyika na 'kutosha' kuwa mtu kwa ile mifumo na mienendo yote ya kimwili; huu si ukweli—ni nusu ukweli ulio ni hatari kuliko uongo kamili. Kwa kuwa ile sehemu yake yenye kuonekana kama ni ukweli kuwa ni hivyo yaweza kumzuzua mwenye kutazama na kumpelekea yeye kwenye hitimisho la mashauri lisilo sahihi. Uongo kamili hukosa shikilizo katika halisia; lakini 'nusu ukweli' inacho kiungo chenye 'kujishikiza' kwenye 'halisia' kamili. Basi mtu ni 'kweli' iliyochanganyikana na 'usikweli' na tena kwa jinsi ya ajabu kujitahidi pamoja katika kudhahirisha sura ya 'utu'. Mwanadamu kiumbe kinachobebwa na viumbe katika michakato ili kukirimika 'sura' yake. Utu ni mbegu ijayo kwa muktadha wa 'Saikia' kamili ambamo ndani yake mna yote 'yanatosha' kukadirisha muktadha wa mtu katika kudhahirika juu ya mwili wa nyama.

Ndani ya Saikia kuna muktadha wa vitu vitatu kuchambulika kipekee--nafsi-roho, akili na nafsi. Nafsi huhusisha muktadha wa akili, kumbukumbu ya mtu kujichukulia katika mazingira yake akitumia mwili kama chombo cha 'uhalisia' wake. Huu ni upande wa chini wa akili ya kawaida; upande wa juu wa akili huwa ni dhahania kwa uadilifu wa kiutu kwa unafsi wa mtu mwenyewe. Haya yote huakisi mawezekano ya Ua la ndani la mtu lililo ni nafsi-roho; sehemu ya sura ya 'mpango mzima' kwa utu ndani ya Roho wa Uzima wote. Nafsi-roho ndiyo hii 'Sonafi' katika mwingiliano wa mwili, akili na uzima—Jua la utu lenye kuungazia uwezekano wa neema zote za mfanyiko na mdhahiriko wa ubinadamu.

Uhalisia wa Saikia ifungamanavyo na mwili ni jinsi ya msalaba; japo mwili hutungika na kufa, saikia ya mtu ya mtu haitungiki na kufa na mwili. Mapana ya kuzaliwa na kufa si mapana na marefu ya Saikia ila tu mkatizio wa Saikia yenyewe katika mfanyiko wa mwili. Saikia ni 'mgeni' katika mwili na tena mpangishaji tu. Saikia huchanua na kukomaa katika mwili na huku ikiendesha mwili kwa sura ya hivyo hivyo na hali mwili ukatapo pumzi Saikia 'hujikunjia ndani' kama mbegu yenye kusubiri na kuhitaji pahala pengine penye kustahili hiyo kumea na kuchipua tena. Mbegu ya 'utu' ina usiku na mchana kama ilivyo katika mizunguko mingine ya kiuhai yenye kuja na misimu na majira—rithimu zifuatishazo namna ya 'mawimbi ya uzima' na 'wavu' wa maumbo-wakati. Iwapo katika giza huwa ni 'chembe ya ndoto' na mang'amu ng'amu yake; japo hayo yote huwa ni ya mpito tu. Yale ambayo watu wa makabila huzungumza kuhusu 'mahala pa wafu' ni sehemu za mpito ambazo 'hazina uhalisia' wa kutosha kuneemesha 'mbegu ya utu'. Ni pahala penye giza tororo ama mbalamwezi kwa Saikia ya mtu japo upo ufundi wa kutumia sehemu hiyo ya mpito katika 'kuhifadhi' kwa kana vile 'kugandisha' kadri mbali mbali ya uwezo na karama mahususi zilizopata kufikiwa na kutambuliwa ndani saikia ya mtu aliyeachia mwili. Na basi Sakia ya mtu huweza kunasa katika wavu wa maumbo-wakati na kudhahirika mtu mwenye kuishi upya.

https://www.facebook.com/notes/mose...epo-mashauri-ya-kiontolojia/10150351001719421
mose tafadhali hebu iweke katika lugha rahisi itakayoeleweka na wengi, nimesoma kwa umakini mkubwa nimemaliza Kichwa kinauma
umetumia sarufi vina nahau misemo viambishi na ngeli adhimu View attachment 297475

cc: christine ibrahim, Senior Boss
 
Last edited by a moderator:
mada za namna unatakiwa usome huku umetulia. mada ni nzuri pia nimejifunza kitu hapa. asante pia kwa wachangiaji
 
mada za namna unatakiwa usome huku umetulia. mada ni nzuri pia nimejifunza kitu hapa. asante pia kwa wachangiaji

1444565215710.jpg hebu soma hii hiyo reincarnation iwavyo interact na rebirth kwa namna nyingine, na habari za karma(cause n effect) kuna kitu kingine kinaitwa samsara-dwelling into the realm of cause and effect life after life without breaking the chain and becoming enlightened
cc: Bujibuji, Tanganyikana
 
Last edited by a moderator:
hivyo vitu viwili vinaenda sana kutokana na maelezo
 
mshana jr nini tofauti ya nafsi na Roho?
Bujibuji nafsi kwa kiingereza ni 'self', nafsi hukaa kwenye mwili ulio hai, kinyume na hapo hakuna nafsi, kwakuwa nafsi huletwa na muunganiko wa roho + mwili
Roho huwepo hata baada ya kifo, na huweza kuhama na kuingia kwenye mwili mwingine -reincarnation
 
Last edited by a moderator:
Kwangu haina shida ila ni kwamba lugha iliyotumika ni ngumu na wengi hupenda mteremko

Usijali juu ya wengine kwa kuwazungumzia hivi ama vile, shauri ni lao kuzungumza kwa nafasi zao.

Kama wewe 'unayasoma' yaliyowasilishwa basi kheri, kama kuna lolote unapenda kumulikwa upya -- sema.

Yapo mengine ya kuzungumzwa kiufundi hasa, ila yatasubiri hadi wewe ama mwingine yoyote aotee namna ya kuuliza na hitaji likawa dhahiri kuzungumza zaidi.

Sawa.
 
Uhalisia wa maisha ya binadam sio kama tunavyoambiwa. Dini zote zimefichaukweli na ni watu wachache tu watakaoelewa hii mambo.
Ukisikia kuna maisha after death ndio hiyo.Unazaliwa kwenye mwili wa mtu mwingine
 
NDUKI njoo bado ipo hukuhuku haijahamishwa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom