Reincarnation (kuzaliwa mara ya pili) ni pointless

Reincarnation (kuzaliwa mara ya pili) ni pointless

Mimi mwenyewe naamini katika nadhari hii,na ukifikiri kwa kina unaweza kubalianana nadharia hii,hebu jiulize tangu dunia iwepo hadi sasa ni miaka bilioni kadhaaa,na dunia imekaliwa na watu wengi sana tangu kuumbwa,je nao hao wafu wa miaka ya nyuma wanasubiri ufufuo huu wa yesu!? Maana yesu kaja hivi karibuni,hivyo ni kweli ukifa unazaliwa kiumbe kingine tena,and that is how life goes in rotation sababu nature inafaidika na uwepo wa binadamu katika dunia
No..

Kwa upande wa imani ya kikristo..ukisoma vizuri biblia inaelezea vile ufufuko wa mwisho ila watu hawaelewi vizuri kwa sababu biblia inaongea nusu na nusu ingine inakuja ukishaamini.

Kulala kidogo ni kuwa nafsi yako ndio inaenda mahala fulani na kupumzika.

Huko wapo watu wote tangu kuanza kwa dunia...maana sio miili..no..bali ni nafsi.

Huko watu wanasubiria hukumu ile ikifika.

Sina uhakika sana ila nadhani hii inawahusu qale woote waliobatizwa na kukiri katika imani ya kristo.

Wataalamu wa dini hii watanisaidia ila nahisi inaanza kuhesabika baada ya uwepo wa kristo...maana yeye ndio aliyekuja duniani kumkomboa mwanadamu kwa kuchukua funguo za kuzimu..n.k.

Kwa imani zingine..zina namna yake na maelekezo yake..na huenda wana mbingu zao..na namna zao za hukumu siku ya mwisho.

Nadhani hapa unavhotakiwa kujua na kutofautisha ni kuwa kuna ulimwengu wa mwili si sawa na ulimwengu wa roho.

So, uwe makini

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Hata kama reincarnation ni kweli bado ni pointless na haifai kuitumia kama msingi wa maadili kwakuwa hata kama ukifa unazaliwa kama mtu mwingine haupati hasara au faida yoyote maana hautakuwa na kumbukumbu zako.

Kwahyo at the very least Imani ya reincarnation ni pointless na haina faida yoyte hata kama ni kweli na at the very best ni kuwa hii ni imani ya uongo
Mi nahisi ipo namna kwenye roho ya mtu..maaana kwanini watu wengine wanafanana sana?

Chukulia mfano Mesut Ozil na yule Henry ford kama sijakosea..sijui ford au yule wa benz..sikumbuki vizuri ila wamefanana kila kitu..ila hawajuani.

Anyway tuachane na hio maana huo mfano upo mbali sana

Kuna mtoto mmoja alizaliwa uingereza akawa aanwqgomea wazazi wake kuwa kwao ni Australia..na akazua utata mkubwa..mpaka wakampeleka Australia ambapo alifika kwenye nyumba moja na kudai ndio nyumbani kwao..kuchunguza ni kuwa kuna mtoto kama yeye aliwahi kuishi hapo miaka mingi kidogo nyuma kipindi cha vita..ila akafa...sasa zile memory nadhani hazikujiflash vizuri dogo akawa anaenda nazo clearly..kiasi cha kuwakaataa wazazi wake halali kabisaaa waliomzaa

So..maybe its true..maybe not.

Nikiipata ile link nitaiweka hapaa

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa mada nzuri kaka.

Ukifa umekufa.
UKIINGIA kaburini hujui Neno LOLOTE.
(Wafu HAWAJUI Neno lolote).Ayubu

Tutengeneze mapito yetu mapema tungali tunaishi.

Tukitegemea kufufuliwa siku ya mwisho na Yesu kristo akija na Utukufu mwingi.
Tukiwa wenye kwenda KUMLALI MAWINGUNI.

Yesu kristo ndie njia, na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa NJIA ya Mimi.
YOHANA 14:6.
Kwahiyo ukifa unasubiri kaburini?
 
Hapa duniani hata ukitangaza unatafuta watu waliowahi kufika pluto na kurudi huwezi kuwakosa.

Ishu ni statistics, Ni wangapi wanaodai hivyo kutoka kwenye population yote?

Tuseme duniani saivi tupo watu bilioni 8
Lakini watu waliowahi kuishi na kufa inakadiriwa ni zaidi ya bilioni 117
inamaana waliokufa tu ni wengi mara 109 ya wale tulio hai.

Kila siku watu zaidi ya laki na nusu wanakufa.

Ingetakiwa kila anayezaliwa awe ni reincarnation.

Na sio hao wawili watatu wanaojitokeza kwenye population ya mabillioni.

Hata kama kila mtu duniani akikuambia kuwa yeye ana kumbukumbu za maisha yake ya zamani enzi za kinjektile na Hitler.

Kitendo cha WEWE kutokumbuka chochote inabidi kikufanye udout kama uliwahi kuwepo mahali popote na kama ukifa utarudi sehemu yoyote.
Usiamini sana watu.
Binadamu ni kifaa kikubwa namba moja cha kuzalisha uongo.
Mi nahisi Mungu ni fundi sana.

Roho ni hizihizi..ila nafsi ndio tofauti.

So roho zinaweza kujirudi duniani..na kupata mwili mpya..na kuishi..kwa sababu mtu anapozaliwa anapokea roho kutoka kwa wazazi wake..so..mambo yanakua yanajibalance...ila nafsi ikisepa imesepa iyoooh...

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Andiko la kubuni Roho identity nimesoma nilivyoona haya maandishi nikakumbuk Enzi zile wakati wa safina kipindi kile kulikua na mtu kama huyuyaani Mzee anajenga safina yeye alimuuliza kwa nini unajenga, Mzee akamjibu Mungu anataka akifutilie mbali kizazi hiki maana dhambi ni nyingi, mwamba alimcheka mno na kuaminisha watu hakuna cha mvua KATIKA NCHI ya ukame hivi, kilichotokea baadaye nafikili wote mnajua maana mlisoma
 
Tofauti ya Anayeamini reincarnation na Mungu wa dini za Abraham ni kuwa
Anayeamini reincarnation anaamini ukifa unarudi na ukifa tena utarudi tena na tena. wakati wanaoamini dini za Abraham ni kuwa tukifa tunalala kidogo halafu baadae wote tunarudi kwa mara moja.
.
Tofauti ni ndogo sana lakini wote wanafana kwakuwa wanaamini kuwa tukifa tutarudi bila uthibitisho wowote.
Uzuri ni Kwamba ukifa haujui kama umekufa, unakuta Mimi na wewe tulishakufa mda mrefuuuu
 
Mi nahisi Mungu ni fundi sana.

Roho ni hizihizi..ila nafsi ndio tofauti.

So roho zinaweza kujirudi duniani..na kupata mwili mpya..na kuishi..kwa sababu mtu anapozaliwa anapokea roho kutoka kwa wazazi wake..so..mambo yanakua yanajibalance...ila nafsi ikisepa imesepa iyoooh...

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
Nafsi inasepa kuenda wapi mkuu?
 
Hapa duniani hata ukitangaza unatafuta watu waliowahi kufika pluto na kurudi huwezi kuwakosa.

Ishu ni statistics, Ni wangapi wanaodai hivyo kutoka kwenye population yote?

Tuseme duniani saivi tupo watu bilioni 8
Lakini watu waliowahi kuishi na kufa inakadiriwa ni zaidi ya bilioni 117
inamaana waliokufa tu ni wengi mara 109 ya wale tulio hai.

Kila siku watu zaidi ya laki na nusu wanakufa.

Ingetakiwa kila anayezaliwa awe ni reincarnation.

Na sio hao wawili watatu wanaojitokeza kwenye population ya mabillioni.

Hata kama kila mtu duniani akikuambia kuwa yeye ana kumbukumbu za maisha yake ya zamani enzi za kinjektile na Hitler.

Kitendo cha WEWE kutokumbuka chochote inabidi kikufanye udout kama uliwahi kuwepo mahali popote na kama ukifa utarudi sehemu yoyote.
Usiamini sana watu.
Binadamu ni kifaa kikubwa namba moja cha kuzalisha uongo.
Swala la kutokukumbuka past yako Hilo ni swala lako binafsi ila Mili Yetu na roho zetu zinatunza kumbukumbu za miaka milion iliyopita, sasa ni jukumu lako wewe kukumbuka au kuto kukumbuka
 
Imani za dini ni za kuwaachia wenyewe wanaozishika.

Ukiingiza logic huiwezi dini yoyote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom