Reginald Mengi: Mangula, wala Rushwa wanajulikana unasubiri nini?

Reginald Mengi: Mangula, wala Rushwa wanajulikana unasubiri nini?

Status
Not open for further replies.
Unataka mengi awataje hawa mafisadi papa mara ngapi?
Wale aliowataja ni wapinzani wake kibiashara mbona aliishia kwa wahindi tu? kwani hakuna wamatumbi,wachaga,wangoni,wazaramo au wasambaa vigogo wa rushwa na ufisadi nchi hii?Huyu babu anashabiana sana na mzee wa kulamba ruzuku kuanzia kutangaza kutishiwa kuuawa na totos.
 
kwa hiyo hao wezi wanajulikana shida ni kutajwa tu au?hivi jamani nani hawajui waliotufikisha hapa ambao kukicha wanabadilishiwa vitengo na wizara mbalimbali??mie sitaki kuyaingilia ya mengi,lakini kwa wale wanosema eti kama unawajua wataje ndiyo wanafiki wakubwa kuliko hata huyo mengi, serikali ya wezi na wadhambiki,mtu akitaja unaulizwa ushahidi unao wakati makablasha wanayo na yanaonesha mapungufu kwenye mikataba mbalimbali.wangapi wamejitahidi kuanika uovu wao wanamuwinda moaka wamuue au wamjeruhu,tunao wengi hata wao kwa wao wanumizana.
victims wa kusema ukweli tunao kama kin mwakyembe na wenzake kibao,lakini leo wako wapi???
Siri ya kuwangoa hao mafisadi wanaosemwa eti leteni ushahidi, ni kujenga chama imara na kuandaa watuwajue wezi waoni kina nani, waliofilisi nchii ni kina nani!!! Finally ni ballot box na wapiga kura wanaochukia ufisadi na wizi wa mali zetu!! Liboleshwe daftari la wapiga kura tutaona mwongo ni nani!!!

 
Sekretarieti yote ya ccm ni maji taka hawana jipya, kwani baadhi yao ni wahujumu uchumi wa nchi hii
Mwigulu Mchemba alikuwa mweka hazina wa CCM aliye injinia kukusanya fedha za EPA, sasa ni katibu mkuu tena we huoni hilo???

 
Hivi kwanini mtu yeyote yule akiongelea UFISADI wana-CCM wote (I believe mafisadi ni wachache sana) wake kwa waume wanachamaa, lete ushahidi, wataje majina, wapaeleke mahakamani etc.

Hivi mnataka kutuaminisha wengine kwamba UFISADI ni sera ya CCM?! Kwa mawazo yangu UFISADI hauna rangi wala chama cha siasa, badala ya kuwakingia kifua mafisadi tupigane nao bila kujali ni CCM, CDM, CUF, NCCR etc vinginevyo tutaonekana Taifa la ajabu linalolea na kushabikia UFISADI wakati wanaoshabikia UFISADI miguuni wamevaa kandambili zilizofungwa kwa wire.

Hapo red, Ndiyooooo!!!! Ufisadi ni Sera ya CCM, hakuna ubishi. Wezi wa EPA ni CCM; Richmond/Dowans ni CCM; Mikataba ya wizi wa madini imesainiwa na CCM. Lini CDM, CUF, NCCR etc. walihusika na wizi huo? Polisi wako wanaua wananchi kwa maelekezo ya CCM. Eti kwa mawazo yako UFISADI hauna chama, wakati kila Mtanzania anajua kuwa chama cha Ufisadi ni CCM. Si unajua kuwa kwa sasa kirefu cha CCM ni Chama Cha MafisadiD!!! Chama cha Mapinduzi kiliondoka na Mwasisi wake Mwl. Nyerere.
 
Mkuu MINGOI...

Basi hata kama ni kundi chache tu la mafisadi ndio lililotajwa, tungeona basi hata hao wanachukuliwa hatua, likini ni usanii tu. Sasa niambie, je hao waliotajwa, walichukuliwa hatua. Pia usisahau kuna ile List of shame (list ya mafisadi), iliyotajwa na Dr. Slaa, je nayo vp.. Hacha porojo mkuu...
 
Swala la kuwataja wala rushwa ni swala la ujasiri, kinyume hakiwezi kuwa ni unafiki!
 
Mimi naanza kuwataja!! Kikwete,kinana,rostitamu&Co, Louwassa & Co, mkuu mwenyewe Andrew Chenge, Shailesh Patel, Jeetu Patel, mimi mwenyewe, Mkapa & Co, anzeni na hao mkishawaweka sero ya maweni au kisongo au segerea kwa kama wiki hivi bila kupelekwa kwa court, kama nilivyowekwaga mimi (kwenye sero za kawaida sio zile appartment zao) muniite nije na ushahidi wa 99% proof, mumpitie na Dc Msuya na swaiba wake Mramba & Laswai, kwani hao nao tuliramba nao kwa sana tu,nipo nasubiria.
WENU KATIKA ULAJI WA TAIFA
NIMROD MKONO
 
Mengi ni mnafiki kama wanafiki wengine tu.Kama anawajua kwa nini asiwataje?

Wametangazwa wangapi? Mmechukua hatua gani? M/Kiti wenu (magamba) mwenyewe alidai ana majina ya wauza unga amechukua hatua gani? Acha chuki na wivu wako wa kike kwa mzalendo Mengi
 
anajitahidi sana baba wa watu,juzi aliandaa msosi kwa walemvu!

Alikuwa swahiba wa magamba,ila tangu alivyowataja ndio amekuwa adui!!mengi ni mfano wa kuigwa kwa kujitolea,amewasaidia sana wajasiriamali wadogo na wa kati kiuchumi na kimafunzo,kina mama wa singida wanamkumbuka vizuri aliwapa support ambayo CCM na miaka yake hamsini madarakani haikuweza kutoa,Bakhressa na title yake ya tajiri namba moja tz ameishia kuwakejeli waislamu kwa kuwapangisha mistari na kuwagawia buku buku mwezi wa ramadhani,Mengi ni level ingine.
 
Mengi ni mnafiki kama wanafiki wengine tu.Kama anawajua kwa nini asiwataje?

Unafiki wa Mengi unatoka wapi hapo?Huyu ni mtanzania mzalendo na ana haki ya kutoa maoni yoyote katika jamii inayotuzunguka,hivi kusema ukweli ni unafiki?Wala rushwa katika nchi hii wanajulikana,kwa nini tuzunguke kiunafiki na kila mara tunaambiwa mwenye ushahidi aulete,upi huo?TAFAKARI CHUKUA HATUA.[/QUOTE]

Hakuna mtu mwenye akili timamu akategemea ufisadi utaisha ndani ya mfumo wa CCM kwa kuwaondoa watu fulani. Lazima awe mwandawazimu. Kama si mwendawazimu basi lazima awe mnafiki. Kuondoa ufisadi Tanzania suluhisho pekee ni kiun'goa CCM yote madarakani kwani CCM imeoza kila kona na hakuna dawa ya kuiponya bali itoke madarakani kwa ujumla wake.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom