Reginald Mengi: Mangula, wala Rushwa wanajulikana unasubiri nini?

Reginald Mengi: Mangula, wala Rushwa wanajulikana unasubiri nini?

Status
Not open for further replies.
Mengi ni mnafiki kama wanafiki wengine tu.Kama anawajua kwa nini asiwataje?[/QUOTE]

Unafiki wa Mengi unatoka wapi hapo?Huyu ni mtanzania mzalendo na ana haki ya kutoa maoni yoyote katika jamii inayotuzunguka,hivi kusema ukweli ni unafiki?Wala rushwa katika nchi hii wanajulikana,kwa nini tuzunguke kiunafiki na kila mara tunaambiwa mwenye ushahidi aulete,upi huo?TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
Mzee mnafiki in the making.

Aliwaponza wapambanaji wa ufisadi na kuwalipa na kutumia vyombo vyake kuzambaza sumu za ufisadi kisha baadaye akawatelekeza leo anaibukia Twitter.
 
Aliawapa miezi 6, baada ya hapo OUT
Tusubiri miezi 6 imalizike tuone atakaju na single gani?
CCM full usanii
 
[FONT=century
gothic]Mengi ni mnafiki kama wanafiki wengine tu.Kama anawajua kwa
nini asiwataje?
[/FONT]

Unataka mengi awataje hawa mafisadi papa mara ngapi?
 
MAngula ni mwenye dolla, kama akisikia haya toka kwa mzalendo halisi , angemfuata atajiwe na sio mengi kutaja.


Nadhani alijaribu kuwataja..hope mnakumbuka list ya mafisadi papa;alionyesha njia.labda tuwaulize viongozi wetu wa itikadi na protokali..yale magamba tuliyoahidiwa yatavuliwa yako wapi au deadline haijatimia? siasa zetu kaaz kweli!
 
Hivi kwanini mtu yeyote yule akiongelea UFISADI wana-CCM wote (I believe mafisadi ni wachache sana) wake kwa waume wanachamaa, lete ushahidi, wataje majina, wapaeleke mahakamani etc.

Hivi mnataka kutuaminisha wengine kwamba UFISADI ni sera ya CCM?! Kwa mawazo yangu UFISADI hauna rangi wala chama cha siasa, badala ya kuwakingia kifua mafisadi tupigane nao bila kujali ni CCM, CDM, CUF, NCCR etc vinginevyo tutaonekana Taifa la ajabu linalolea na kushabikia UFISADI wakati wanaoshabikia UFISADI miguuni wamevaa kandambili zilizofungwa kwa wire.
 
Mengi ana vyombo vya habari kwa nini asitumie media kuujulisha umma wa watanzania?

Yeye ni miliki tu siyo kazi yake kutaja wezi au kutumia vyombo vyake kuwataja , anataka chama chake kijisafishe kulingana na ahadi walizotoa wakina Mangula
 
Reginald Mengi ‏@regmengi"Rushwa imekithiri, maadili yameporomoka"Mangula. Lakini mh. wahusika wanajulikana. Tatizo ni nani amfunge paka kengele?

Source: Reginald Mengi Twitter
Hii tweet ya Mzee Mengi ni nzito,CCM inabidi waifanyie kazi haraka. Tumbuke mangula amerudishwa kwenye safu ya juu ya CCM ili kurudisha hadhi ya chama. Afanyie kazi hoja ya mengi,
 
kwa hiyo hao wezi wanajulikana shida ni kutajwa tu au?hivi jamani nani hawajui waliotufikisha hapa ambao kukicha wanabadilishiwa vitengo na wizara mbalimbali??mie sitaki kuyaingilia ya mengi,lakini kwa wale wanosema eti kama unawajua wataje ndiyo wanafiki wakubwa kuliko hata huyo mengi, serikali ya wezi na wadhambiki,mtu akitaja unaulizwa ushahidi unao wakati makablasha wanayo na yanaonesha mapungufu kwenye mikataba mbalimbali.wangapi wamejitahidi kuanika uovu wao wanamuwinda moaka wamuue au wamjeruhu,tunao wengi hata wao kwa wao wanumizana.
victims wa kusema ukweli tunao kama kin mwakyembe na wenzake kibao,lakini leo wako wapi???
 
Majibu yako ni magamba typical -- kama vile kila siku wakijibu tuhuma za ufisadi eti wananchi wapeleke ushahidi! majibu mepesi kwa maswali magumu.

Hao waliopewa majukumu ya kutafuta ushahidi wameshiba kwa kuvimbiwa na sasa wanatibiwa nje!!
Kula 5 Mkuu. Tanzania ni nchi ya ajabu zaidi kuliko pengine nchi yoyote ile hapa duniani, inashangaza kuona jeshi lake la Polisi pamoja na UWT pindi wanapopelekewa tuhuma basi wanataka pia wapelekewe na ushahidi. Kama hivi ndivyo je, kazi yao (Polisi na UWT) ni nini?

CCM imeharibu kabisa hali ya usalama na mshikamano wa watanzania ule uloachwa na waasisi wetu Karume na Baba wa Taifa (JKN).....

...ndo maana sishangai baadhi ya wachangiaji wanamtaka "eti" Reginald Mengi, awataje wala-rushwa au apeleke ushahidi TAKAKURU....akifanya hivyo je vyombo hivyo vya usalama wa raia na UWT watafanya nini?
 
Kauli nyingine za ajabu inabidi ziwekwe kwenye mzingo sahihi. Hii kusema "kazi ya kupambana na rushwa/wizi ni ya watu wote" inakuwa na maana tu pale serikali yenye vyombo na nyenzo za kutekeleza sheria inapofanya kazi yake. Kama serikali haina nia wala mpango wa kudhibiti rushwa, inabakia kuwa kauli ya kujikosha na kugawa lawama kwa umma wote. Hivi kuna mwananchi au kikundi binafsi cha wananchi kinachoweza kuchukua hatua ya kumkamata fisadi na kumpitisha kwenye mchakato wa mashtaka?

Majina ya wala rushwa yameshatajwa sana na mengine kwa ushahidi unaofikirisha. Ni juu ya serikali kutumia vyombo vyake rasmi kuchunguza, kuthibitisha madai na kuendesha mashtaka. Tunachoshuhudia ni kuzidi kusema "wataje basi" - mara ngapi?; "ni jukumu letu sote" - how? Halafu kwa nini serikali isubiri kutajiwa majina - tena kwa ushahidi unaotoka hukohuko serikalini? Bajeti za CID, PCCB, TISS, AG ni za kazi gani kama ni "kazi ya wote" bila kuainishwa?

Kwa upande mwingine wananchi wakiendesha harakati za kufichua ufisadi, serikali imekuwa mstari wa mbele kupambana na wanaoongoza na wanaoshiriki harakati hizo kuliko kuzishughulikia kama inavyotegemewa. Ikitokea vyombo vya dola vikatesa, kudhuru au kuua wanaoshiriki kufichua ufisadi au ikitokea watu wakapoteza ajira, nyadhfa kwa sababu hizo basi utasikia adha hizo zisingewakuta kama wasingekubali "kuponzwa" na walioongoza harakati. Haisemwi kwamba walikosea kufuatilia wizi/ufisadi huo; wala kwamba serikali na vyombo vya dola vimekiuka kanuni za utawala bora au haki za binadamu; bali, "ungetulia nyumbani kwako au ukakaa kimya kwenye dawati lako hayo yote yasingekukuta"! Kama huko sio kuendesha utawala wa kinafiki na hofu ni nini tena hapo.
 
Mengi ni mnafiki kama wanafiki wengine tu.Kama anawajua kwa nini asiwataje?

Yaelekea wewe umerudi Bongo siku za hivi karibuni, unaikumbuka ile list ya mafisadi Papa? Je? unalikumbuka neno hili, "Mchezo mchafu" hayo maneno Mengi ndio muasisi wake, alipotaja wale mafisadi Papa (kwa mujibu wake) Vyombo vyote vya habari havikurusha hiyo kitu only ITV and radio one ndio vilifanya hivyo, finally ile kitu ilimletea shida sana, hata mawaziri nao walimuijia kinyume nae, well, siku kudhaa, Rostam Aziz naye alikuja kumtuhumu kua ni fisadi Nyangumi, kitu nilichokishangaa kwa RA, TV zote including TBC walionesha tukio la Rostam Aziz, just for your infor.
 
Sekretarieti yote ya ccm ni maji taka hawana jipya, kwani baadhi yao ni wahujumu uchumi wa nchi hii
 
Reginald Mengi ‏@regmengi"Rushwa imekithiri, maadili yameporomoka"Mangula. Lakini mh. wahusika wanajulikana. Tatizo ni nani amfunge paka kengele?

Source: Reginald Mengi Twitter
Nakubaliana na R Mengi, ametoa mawazo yake kama Mtanzania na mwana CCM. Wanaoponda mawazo yake wana wivu binafsi wa mafanikio yake. Changia hoja sio kuattack mtu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom