Kwa ufupi Bw Mengi amewatukana kistaarabu Mh. Rais na Mawaziri wake akina Prof Muhongo et all kwamba hata muuza Cocacola, maji ya chupa na juice anaweza kuwa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi.
Na ukweli 'the timing' of the event/forum was very right place. Nafikiri hata Rais na wasaidizi wake watakuwa wameshikwa na haya mno. Kwani Mengi atakuwa amewajibu kwa kusirani🙂 lol. Na waacha hii serikali ikome kabisa 'mentality' na dhana yao ya kuwa Wazawa hawawezi.
Nchi yetu ya Tanzania tayari kuna watu ni matrillionea (wachilia mbali hao mabilionea na mamillionea chungu mzima kwa sasa). Hata kama walizipata kwa rushwa ni bora kufanya kama wenzetu kule Nigeria walivyofanya. Kama wazungu wanvyosema 'if you cant fight them join them'. Hivyo Nigeria ilifika point ikawa ni vigumu mno kuzipata fedha za kifisadi hivyo ilivyofanya ikawa ni 'ku encourage wale wenye hizo trillion kuwekeza nchini mwao wenyewe na serikali ikilinda mitaji yao ili pesa ile issishie kwenye mabenki ya Uswisi na offshore banks. Ndio maana leo nchini Nigeria kuna watu wanamiliki makampuni makubwa ya mawasiliano na sekta ya mafuta na gesi zikimilikiwa na wazawa vilevile.
'Maisha ni kujifunza'. Hivyo serikali yetu yapaswa kuwa sikivu na kutumia hekima. Mambo ya madherereu kwa raia unawaongoza na kushadidia wageni kuwa watawala wa uchumi wa nchi ndio 'angamizo' kuu linaloitafuna na kuiyumbisha nchi.