Regia Mtema, John Mnyika, Zitto Kabwe na 90mil

Lasita mkubuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya- Regia Mtema

mheshimiwa Regia, hayo maneno unayosema ni Kweli?. au ndo yale yale kuita pesa nyingi Vijisenti?.
Kitu Kingine unasema Kwamba Bunge linachangia Shilingi Milioni 45 kwenye hilo gari, sasa swali langu ni hili, kama Bunge linatoa nusu na Mbunge anatoa nusu je Gari linakuwa ni la nani?.
Je Mbunge akimaliza Ubunge wake, anazilipa hizi Milioni 45 zinazochangiwa na Bunge ili aendelee kulimiliki hilo gari, au inakuwaje kuwaje, naomba Utueleweshe!.

Hata hivyo ninaungana na wewe moja kwa moja unapotoa dokezo la kupelekwa mswada bungeni ili kupunguza Haya yanayoitwa maslahi ya Wabunge "kwa sasa", kwani ni mzigo kwa Taifa, hayana Tija katika uchumi kwa sababu hayaliingizii pato Taifa, na yanajenga matabaka nchini. Tunategemea Wenzetu mlioko mbele kupinga Ufisadi, muwe msitari wa mbele katika kupinga matumizi kama haya yasiyo na manufaa, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga credibility mbele ya Umma, la sivyo mtaonekana kama mnaopiga kelele kwa sababu hamjashika dola na laiti mgeshika dola mgeonekana kama hawahawa CCM.

Ni bora kila jimbo likwa na gari lake imara, liwe gari la Bunge, na si gari la Mbunge, Mbunge awe analitumia tu katika shughuli za kibunge, kama halitaki basi anunue gari lake kwa pesa zake mwenyewe na awe anatembelea na kufanyia shughuli zake.

Mheshimiwa Mbunge!
Gharama zote za mkopo huo wa magari mliopewa ni shilingi Milioni 90 mara wabunge 353=bilioni 31.77, je hizo pesa tungejenga High School za kiwango Bora Ngapi?, tungejenga na kukarabati zahanati zetu ngapi?.

Hivi vipaumbele vyetu ni nini?
 
Mtakufa nacho kijiba cha roho roho mbaya tu! waacheni wazitumie waonavyo sawa kama vipi si mjitokeze kugombea 2015 maana kutokana na mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha kwa bunge hilo watapewa Tsh 250 milioni.kwa kila mbunge.
 
Mie naona kama wangekuwa wapiganaji wa kiukweliukweli basi wangewaonesha ccm kwa vitendo. kupitia msemaji wao wa kambi ya upinzani wangemwambia spika kuwa wabunge wote wa chadema badala ya milioni 25. Rav4 second hand 15M wanapata na zinawatosha sana. then hata wabunge wa ccm wangeona aibu wote kwa pamoja wangeshusha tu hadi hicho kiasi. Pili chadema wangepiga marufuku wabunge wake kukaa Dar es salaam after bunge. wabunge wa chadema wangeweka amri kuwa katika kila jimbo kuwe na nyumba ya mbunge na iwe ni amri kwa mbunge kuishi hapo ili dhana nzima ya uwakilishi wa wananchi iwepo,na amri ya kila mbunge kurudi kuishi jimboni kwake lisimamiwe kisheria.
 
hiyo ni loan wamepewa ambayo itakuwa inakatwa kidogo kidogo kila mwezi kwa miaka mitano kwenye mishahara yao .kwahiyo hapo futeni ile dhana kwamba hizo fedha wamepewa na serikali.
hapo hoja labda tuzungumzie ukubwa wa mishahara yao na marupurupu yao ambayo kimsingi kama mbunge ni muwajibikaji ipasavyo basi ni stahiki.
zaidi ya yote ni mtanzania gani asiyetaka kuboreshewa maslahi yake ya mshahara?
 
Kwanza ningewailisha hoja binafsi kupinga wabunge kupewa rushwa ya wazi wazi! Na modality ambao ingefuata ni CDM kuunga mkono hoja yangu binafsi na kuitolea tamko kama chama kukataa matumizi mabaya ya fedha ya walipa kodi! Na hii ingeinua sana imani ya chama kwa Watanzania!
halaf kama CCM hawataki kukubaliana nao CDM wanasusa na kutoka nje ya bunge...period
 
Tofautisha kati ya gari mpya,na gari inayoonekana mpya.......
Toyota rav 4 ya mil 24 ni ile inayoonekana mpya(second hand)
toyota rav 4 mpya ni kama mil 35 hadi 40
......na hiyo rav 4,zito atatoka nayo kigoma dodoma daresalaam mara ngapi?na yule jamaa wa kagera?.....hahahaha

kaka Apolo unasema RAV4 mbunge wangu Zitto ataenda nayo kigoma mara ngapi? kwani vikao vya bunge kwa mwaka ni mara ngapi? na je jimbo lake ni lipi? ile ni gari ya kufanya shughuri za kibunge katika jimbo lake. yeye anatakiwa akae jimboni kwake na anapohitajika bungeni apande ndege kwani siwanapewa posho? kwanini atake vitu vya gharama ya juu wakati unaowawakilisha ni maskini? akiwepo dodoma atakodi Tax kufanya mizunguuko yake. Kwa majibu kama ya Regia hapo ndo utaona kuwa wapiganaji tunatumiwa tu na wajanja wachache waliojivika kilemba kuwa ni wapiganaji kumbe wanajinufaisha tu, hawapo kiuananchi zaidi.
 
Umejibu hoja dada regia lakini wabunge wa viti maalum na wa kuteuliwa na rais nao wanahitaji magari hayo imara na mazuri? wao wanashughuli hizi za wabunge wa majimbo? au labda sijui kazi zao naomba kuelimishwa.
haswaaa na wabunge wa viyi maalumu wanawajibika kwenye majimbo yote kutoka mkoa aliochaguliwa ndugu.
 
Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!

Swala hili siyo la Regia, John na Zuberi peke yao au ndivyo ulivyo-limit upeo wako wa kufikiri? kazi ya hizo fedha inajulikana na umuhimu wake pia unajulikana, kama kuna-cuttings katika matumizi ya serikali hulipaswa kuliongelea kama swala la Bunge zima kuanzia na CCM ambayo ndiyo inachukua fedha nyingi siyo ku-intimidate majina ya watu wachache kana kwamba Bunge ni la watu watatu au wanne.

Panua akili yako kama huwezi endelea kupanua tumbo lako lakini ni bora ukajua kuwa madhara yake ndio haya ya kutapika ovyo, matapishi pia yananuka kama kinyesi.
 
Wakuu.Salaam.

Nimeona nichangia post hii kidogo.

Kwanza kabisa niweke rekodi sawa Fedha hizi za Gari hazijaanza kuigia kwa wiki tatu zilizopita kama mtoa mada alivyosema.Cheki zimeanza kutolewa kama siku nne au tatu zilizopita na zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge bado hawajapata cheki zao,hata mimi bado sijapata.

La pili ni hili Milioni 90.Ifahamike kwamba Milioni hizi 90 wabunge hawapewi Bure tunakopeshwa na tunakatwa kupitia mishahara yetu.Bunge linalipa nusu ya pesa hizo yaani Milioni 45,Milioni 45 nyingine kila Mbunge anakatwa karibu shilingi 866,000 kwa mwezi kupitia mshahara wake.Kwahiyo Bunge linatoa shilingi Milioni 45 tu kwaajili ya gari.

La tatu Kimsingi Bunge limeweka Utaratibu ili kumsaidia Mbunge afanye vizuri kazi zake za Kibunge ilipendekezwa awe anatumia gari aina ya Toyota Hard Top Mpya ambayo kwa sasa gari hili linauzwa shiingi Milioni 112.Bunge likatafakari ikaonekana ni gharama kubwa kumpa kila Mbunge shilingi Milioni 112 hivyo busara ya wahusika wanaopanga maslahi ya wabunge wakaja na kiwango hiki cha Milioni 90 na Bunge kuchangia nusu ya pesa hizi. Bunge limependekeza aian hii ya gari kwakuwa ni imara inayoendana na miundumbinu ya majimbo mengi hapa nchini.Lakini kwa hali ilivyo watakao nunua ni wale wenye uwezo kipesa wengine trutakimbilia kwenye magari ya bei rahisi.

La nne ni mapendekezo ya baadhi ya watu eti wabunge wa CHADEMA wasichukue pesa hizo.Kimsingi hili sio pendekezo sahihi sasa wabunge hawa wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za gari nani atawanunulia magari ya kurahisisha kazi zao?hivi milioni 45 ni nyingi sana kwa kununua gari?kwa yeyote anayefahamu vizuri kazi ya Mbunge ndani ya Jimbo na miundombinu yetu hawezi kulalamika kuhusu hili. Gari imara kwa miaka 5 ni muhimu sana kwa Mbunge. Kwa wanaojua magari vizuri wanajua vizuri magari imara na mazuri kwa kazi za kisiasa zinauzwa shilingi ngapi. Vile vile Wabunge wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za magari itakuwa haina maana kwani Wabunge wa CHADEMA tuko 48 tu kati ya Wabunge 353 hivyo sisi tukikataa haitabadilisha chochote na badala yake pesa hizi zitaishia kwenye mikono ya wachache ambao hatutajua zimetumika vipi.Kuna msemo unasema ukisusa wenzio wala.Hoja ya msingi hapa ni kuwa Wabunge wa CHADEMA wapeleke hoja Bungeni ya Kupitia Upya Maslahi ya Wabunge ili kama kuna pesa zisizo na maana kwa mbunge basi ziondolewe kwa maslahi ya umma,hoja si kukataa milioni 90 kwa sasa.

La tano kwa upande wangu kwa kuwa mimi ni Mbunge maskini siwezi kuzipeleka Milioni 90 zote kwenye gari.Nitanunua gari la bei nzuri la kini lazima liwe imara na la kuvutia.Zingine zitafanya mambo ya msingi ndani ya Jimbo la Kilombero na mambo mengine madogo madogo.

Lasita mkubuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya.

La mwisho kabisa hivi siku hizi ndio imekuwa mtindo wa kuwataja Zitto,Mnyika and Regia?Kuna Wabunge wengi sana humu Wanawake kwa Wanaume amabo ni wanachama tena wazuri tu isipokuwa hawatumii majina yao halisi.Ukija na taito yako ikataja jina la ujumla Wabunge utapata majibu mazuri toka kwao.Mkiwa very specific mnawabana wao wanaona kama hawahusiki hivyo hawatoi ushirikiano wa kutosha,sio lazima wajitaje majina yao sisi tunataka michango yao. Ni vizuri tukawa tunapanua wigo mpana wa kuruhusu Wabunge wengine wachangie kwa majina yao bandia.

Aluta Continua

Kutoka Miti Mirefu Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Mheshimiwa Mbunge, katika sehemu hiyo niliyoiwekea saizi kubwa, unaonyesha ni dhahiri kwamba kumbe Inawezekana kabisa kupata gari la bei nafuu na bado likawa Imara, sasa swali langu ni hili!, kwa nini usionyeshe kwa vitendo kwa kupigia kelele hili suala, kwa sababu Kumbe Milioni 90 kwa gari bado ni nyingi, ndo maana wewe hutaziingiza zote katika kununua gari!

Kitu kingine ni kwamba, Mbunge ana mfuko wa jimbo, sasa inakuwaje pesa zilizotolewa kwa Gari, zikafanye shughuli nyingine iliyo nje ya bajeti au malengo yake, je huoni hapo kuna ujanjaujanja fulani?
 
Mimi kinachoniuma zaidi ni kama na hiyo hela inaenda kwa wabunge wa kuteuliwa... amabao kwa haraka haraka wanafika 112 (ukijumlisha na wateule 10 wa rais ambao mpaka sasa ameshateua 3 kama sikosei ) sasa ;-

90ml X 100=9,000,000,000 ( 9bl) imeenda kwa watu ambao mimi naamini hawana maslahi yeyote kwa wananchi ... zaidi ya vyama vyao na marefa waliowafikisha hapo.

Hizi ndo fedha tungezijadili kama ZINAIBIWA.

Sikatai wabunge kuteuliwa lakini wangepunguza idadi ya wateuliwa... na wasingeteuliwa na VYAMA VYA SIASA... hawa wangeteuliwa na taasisi fulani ambazo zingekuwa zinawakilisha watu wa kada fulani... mfano walemavu wangeteua wao, dini zingeteua wao (sio kwa madhehebu bali kwa dini) , asasi za kiraia nk... kwa hakika hawa wangekuwa ni wateule wa kweli na wangewawakilisha wananchi.

Wabunge 112 wa kuteuliwa kwa mshahara wa 12ml/month ni almost 1,200,000,000 (1.2bl)X12(mwaka) X 5(term)=72bl hizi nazo ni fedha zinazopotea.

Na kwa ukweli hawa ndo wale huishia kuvaa vikuku... na kuzomea (ingawa siyo wote ila wengi wao)

Na kama hawa wangekuwa wanateuliwa na asasi za kiraia, na kidini n.k , asasi husika zingebanwa kuwalipa wao mishara isipokuwa serikali ingewapa posho kujikimu na maisha pindi wapo bungeni.

Ufupi hizi ndo hela za kujadiliwa, sio hizo ambazo ZIMESHAINGIZWA kwenye acc... na istoshe jambo la msingi ni kushauri wafanyeje .. ingawa kwa mtazamo wangu, hata mimi najaribu kufikiria NASHINDWA KUJUA WANAWEZAJE KUZIKATAA... maana walio wengi (CCM) wao watachukua... swali ni je??? wakikataa ZAO ZITAPELEKWA WAPI??????
 
Wakuu.Salaam.

Nimeona nichangia post hii kidogo.

Kwanza kabisa niweke rekodi sawa Fedha hizi za Gari hazijaanza kuigia kwa wiki tatu zilizopita kama mtoa mada alivyosema.Cheki zimeanza kutolewa kama siku nne au tatu zilizopita na zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge bado hawajapata cheki zao,hata mimi bado sijapata.

La pili ni hili Milioni 90.Ifahamike kwamba Milioni hizi 90 wabunge hawapewi Bure tunakopeshwa na tunakatwa kupitia mishahara yetu.Bunge linalipa nusu ya pesa hizo yaani Milioni 45,Milioni 45 nyingine kila Mbunge anakatwa karibu shilingi 866,000 kwa mwezi kupitia mshahara wake.Kwahiyo Bunge linatoa shilingi Milioni 45 tu kwaajili ya gari.

La tatu Kimsingi Bunge limeweka Utaratibu ili kumsaidia Mbunge afanye vizuri kazi zake za Kibunge ilipendekezwa awe anatumia gari aina ya Toyota Hard Top Mpya ambayo kwa sasa gari hili linauzwa shiingi Milioni 112.Bunge likatafakari ikaonekana ni gharama kubwa kumpa kila Mbunge shilingi Milioni 112 hivyo busara ya wahusika wanaopanga maslahi ya wabunge wakaja na kiwango hiki cha Milioni 90 na Bunge kuchangia nusu ya pesa hizi. Bunge limependekeza aian hii ya gari kwakuwa ni imara inayoendana na miundumbinu ya majimbo mengi hapa nchini.Lakini kwa hali ilivyo watakao nunua ni wale wenye uwezo kipesa wengine trutakimbilia kwenye magari ya bei rahisi.

La nne ni mapendekezo ya baadhi ya watu eti wabunge wa CHADEMA wasichukue pesa hizo.Kimsingi hili sio pendekezo sahihi sasa wabunge hawa wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za gari nani atawanunulia magari ya kurahisisha kazi zao?hivi milioni 45 ni nyingi sana kwa kununua gari?kwa yeyote anayefahamu vizuri kazi ya Mbunge ndani ya Jimbo na miundombinu yetu hawezi kulalamika kuhusu hili. Gari imara kwa miaka 5 ni muhimu sana kwa Mbunge. Kwa wanaojua magari vizuri wanajua vizuri magari imara na mazuri kwa kazi za kisiasa zinauzwa shilingi ngapi. Vile vile Wabunge wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za magari itakuwa haina maana kwani Wabunge wa CHADEMA tuko 48 tu kati ya Wabunge 353 hivyo sisi tukikataa haitabadilisha chochote na badala yake pesa hizi zitaishia kwenye mikono ya wachache ambao hatutajua zimetumika vipi.Kuna msemo unasema ukisusa wenzio wala.Hoja ya msingi hapa ni kuwa Wabunge wa CHADEMA wapeleke hoja Bungeni ya Kupitia Upya Maslahi ya Wabunge ili kama kuna pesa zisizo na maana kwa mbunge basi ziondolewe kwa maslahi ya umma,hoja si kukataa milioni 90 kwa sasa.

La tano kwa upande wangu kwa kuwa mimi ni Mbunge maskini siwezi kuzipeleka Milioni 90 zote kwenye gari.Nitanunua gari la bei nzuri la kini lazima liwe imara na la kuvutia.Zingine zitafanya mambo ya msingi ndani ya Jimbo la Kilombero na mambo mengine madogo madogo.

Lasita mkubuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya.

La mwisho kabisa hivi siku hizi ndio imekuwa mtindo wa kuwataja Zitto,Mnyika and Regia?Kuna Wabunge wengi sana humu Wanawake kwa Wanaume amabo ni wanachama tena wazuri tu isipokuwa hawatumii majina yao halisi.Ukija na taito yako ikataja jina la ujumla Wabunge utapata majibu mazuri toka kwao.Mkiwa very specific mnawabana wao wanaona kama hawahusiki hivyo hawatoi ushirikiano wa kutosha,sio lazima wajitaje majina yao sisi tunataka michango yao. Ni vizuri tukawa tunapanua wigo mpana wa kuruhusu Wabunge wengine wachangie kwa majina yao bandia.

Aluta Continua

Kutoka Miti Mirefu Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

AHSANTE MBUNGE NA WAZIRI KIVULI;
PAMOJA NA MAJIBU MAZURI YA WAZIRI KIVULI BADO SIKUBALIANI NAYE KATIKA MAMBO MATATU,
KWANZA NAOMBA IELEWEKE KUWA MIMI NAUNGA MKONO CHADEMA KUCHUKUA HELA SIO TUU HIZO 90M HATA ZAIDI KWA KADRI ZITAKAVYOTOLEWA LAKINI NDUGU WAZIRI KIVULI USICHUKUE NAFASI KUTUDANGANYA NA KUTUDHIHAKI

KATIKA MAJIBU YAKO JAMBO LA TANO UNASEMA UTANUNUA GARI LA KAWAIDA ZURI NA LA KUVUTIA,SIDHANI KAMA NI SAHIHI TUNATAKA MNUNUE MAGARI MAZURI IMARA NA YANAYOWEZA KUFIKA KILA MAHALI SIO LA KUVUTIA TAFADHALI MUULIZE MBOWE ANAJUA VOGUE ILIVYOKATAA OPERATION SANGARA YA KWANZA KABLA YA UCHAGUZI NA BAADA YA SAFARI MOJA TUU AKAAMUA KURUDIA LAND CRUISER YAKE ALIYOKUWA AMEIACHA KWA KAZI HIYO NA IKAFANYA KAZI MPAKA AKAMALIZA NGWE ACHANA NA MAGARI YA KUVUTIA NUNUA GARI ZURI NA IMARA

KATIKA JIBU LAKO LA SITA MHESHIMIWA WAZIRI KIVULI UNASEMA MILLION TISINI SIO KITU ZINAISHA KWA WIKI MOJA HEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE;;;AISEE UMENISHANGAZA UNAMAANISHA KATIKA NDUGU ZAKO ULIONAO,WANANCHI WA JIMBONI KWAKO NA WATANZANIA WOTE NI WANGAPI WANAOWEZA KUTUMIA MILIONI TISINI KWA WIKI KAMA SIO ROSTAM AZIZ,MOHAMED DEWJI JAKAYA KIKWETE,ANDREW CHENGE NA KAMA HAO,NAOMBA UREKEBISHE HILI KABLA SIKU HAIJAISHA OTHERWISE NITAKUDELETE KWENYE LIST YANGU YA MASHUJAA WA KARNE HII.

KATIKA JIBU LAKO LA MWISHO UNASEMA KWA NINI ZITTO ,MNYIKA NA REGIA,NIKUAMBIE UNABIDI UMSHUKURU MUNGU KWA HILI JAMII FORUM IMEKUJENGA WEWE SANA KULIKO WOTE HAO ZITTO NA MNYIKA WALIKUWA MASHUHURI TOKEA SIKU NYINGI SANA HATA KABLA HUJAINGIA CHADEMA LAKINI WEWE UMEJENGWA KWA KIASI KIKUBWA NA JF NI LAZIMA UTAMBUE HILO,LAKINI PIA KAMA NYIE NDIO MNAOTUMIA MAJINA YENU HAPA TUKIWATAJA TUNAMAANISHA MNAWAKILISHA WABUNGE WOTE MLIO HUMU.TAFADHALI TAMBUA KUWA TUNAKUHESHIMU HATUKUOGOPI NA UKIONA TUNAKUPA THANKS USIFIKIRI HATUWEZI KUKUKOSOA.

CHADEMA CHUKUENI HELA ZOTE ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI ILI MFANYE KAZI KWA BIDII NA KWA MAFANIKIO

Ahsanteni naomba kuwasilisha
 
kaka Apolo unasema RAV4 mbunge wangu Zitto ataenda nayo kigoma mara ngapi? kwani vikao vya bunge kwa mwaka ni mara ngapi? na je jimbo lake ni lipi? ile ni gari ya kufanya shughuri za kibunge katika jimbo lake. yeye anatakiwa akae jimboni kwake na anapohitajika bungeni apande ndege kwani siwanapewa posho? kwanini atake vitu vya gharama ya juu wakati unaowawakilisha ni maskini? akiwepo dodoma atakodi Tax kufanya mizunguuko yake. Kwa majibu kama ya Regia hapo ndo utaona kuwa wapiganaji tunatumiwa tu na wajanja wachache waliojivika kilemba kuwa ni wapiganaji kumbe wanajinufaisha tu, hawapo kiuananchi zaidi.

MR MARK ,UMEZUNGUMZA KITU AMBACHO HATA MIMI NAKIFIKIRIA KWA MUDA SASA ILA EMBU TUWAPE MIAKA MIWILI TUONE MAANA INAWEZEKANA KABISA HAWA JAMAA WANATUTUMIA LAKINI MBAYA ZAIDI REGIA ANASEMA MILLIONI TISSINI SI KITU NA INAISHA IN A WEEK TIME AISEE NI HATARII

tuwape muda tutajua ukweli kabla ya 2014
 
Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!

jaribu kufikiri unapoa thread. ulitaka wakatae? c bora wamechukua wanaenda kusomeshea watoto yatima majimboni mwao kuliko kuziacha then mafisadi wazichukue, angekua baba ako ungemwambia afanyaje? jaman mkanunue hizo v8 wao wapo wachache bungeni hawawezi kufanya lolote lile ili hizo hela na posho zictolewe coz wenye njaa walipendekeza hivyo. mnakumbuka suala la bajet ya chai wizaran wapinzani walipinga lkn wazee wa ccm wakapitisha kwa kishindo
 
Hoja kama hii na mjadala huu wote unaonyesha kitu kimoja cha ajabu kidogo! Kwamba wengi/ kama siyo wote, WANACHAMA, WASHABIKI na WAPINZANI WA CDM, wote 'wanaitaka' ibadilishe hata mambo ambayo tunajua kabisa kuwa ingekuwa rahisi zaidi kubadilishwa na wale 'wataalam' wa kubadilisha kanuni za Bunge letu kwa kasi ya ajabu. CDM liangalieni hili, yaana hata WAPINZANI wenu wanawategemea pamoja na uchache wenu muondoe kila uozo uliopo! Najiuliza ingekuwaje kwa mfano sisi wote tungeanzisha movement flani kuwashirikisha wananchi ktk majimbo yanayowakilishwa na wale wabunge 'wabadilisha kanuni' kwa sababu ndio wengi. Tuwatake wabunge hao wabadilishe sheria/kanuni zinazowapendelea.. Naamini wananchi wengi ktk majimbo hayo hawakubaliani na hali iliyopo sasa..
NI MAONI YANGU TU JAMANI!!!
 
Wakuu.Salaam.

Nimeona nichangia post hii kidogo.

Kwanza kabisa niweke rekodi sawa Fedha hizi za Gari hazijaanza kuigia kwa wiki tatu zilizopita kama mtoa mada alivyosema.Cheki zimeanza kutolewa kama siku nne au tatu zilizopita na zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge bado hawajapata cheki zao,hata mimi bado sijapata.

La pili ni hili Milioni 90.Ifahamike kwamba Milioni hizi 90 wabunge hawapewi Bure tunakopeshwa na tunakatwa kupitia mishahara yetu.Bunge linalipa nusu ya pesa hizo yaani Milioni 45,Milioni 45 nyingine kila Mbunge anakatwa karibu shilingi 866,000 kwa mwezi kupitia mshahara wake.Kwahiyo Bunge linatoa shilingi Milioni 45 tu kwaajili ya gari.

La tatu Kimsingi Bunge limeweka Utaratibu ili kumsaidia Mbunge afanye vizuri kazi zake za Kibunge ilipendekezwa awe anatumia gari aina ya Toyota Hard Top Mpya ambayo kwa sasa gari hili linauzwa shiingi Milioni 112.Bunge likatafakari ikaonekana ni gharama kubwa kumpa kila Mbunge shilingi Milioni 112 hivyo busara ya wahusika wanaopanga maslahi ya wabunge wakaja na kiwango hiki cha Milioni 90 na Bunge kuchangia nusu ya pesa hizi. Bunge limependekeza aian hii ya gari kwakuwa ni imara inayoendana na miundumbinu ya majimbo mengi hapa nchini.Lakini kwa hali ilivyo watakao nunua ni wale wenye uwezo kipesa wengine trutakimbilia kwenye magari ya bei rahisi.

La nne ni mapendekezo ya baadhi ya watu eti wabunge wa CHADEMA wasichukue pesa hizo.Kimsingi hili sio pendekezo sahihi sasa wabunge hawa wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za gari nani atawanunulia magari ya kurahisisha kazi zao?hivi milioni 45 ni nyingi sana kwa kununua gari?kwa yeyote anayefahamu vizuri kazi ya Mbunge ndani ya Jimbo na miundombinu yetu hawezi kulalamika kuhusu hili. Gari imara kwa miaka 5 ni muhimu sana kwa Mbunge. Kwa wanaojua magari vizuri wanajua vizuri magari imara na mazuri kwa kazi za kisiasa zinauzwa shilingi ngapi. Vile vile Wabunge wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za magari itakuwa haina maana kwani Wabunge wa CHADEMA tuko 48 tu kati ya Wabunge 353 hivyo sisi tukikataa haitabadilisha chochote na badala yake pesa hizi zitaishia kwenye mikono ya wachache ambao hatutajua zimetumika vipi.Kuna msemo unasema ukisusa wenzio wala.Hoja ya msingi hapa ni kuwa Wabunge wa CHADEMA wapeleke hoja Bungeni ya Kupitia Upya Maslahi ya Wabunge ili kama kuna pesa zisizo na maana kwa mbunge basi ziondolewe kwa maslahi ya umma,hoja si kukataa milioni 90 kwa sasa.

La tano kwa upande wangu kwa kuwa mimi ni Mbunge maskini siwezi kuzipeleka Milioni 90 zote kwenye gari.Nitanunua gari la bei nzuri la kini lazima liwe imara na la kuvutia.Zingine zitafanya mambo ya msingi ndani ya Jimbo la Kilombero na mambo mengine madogo madogo(kwa wabunge wakuteuliwa).

Lasita mkubuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya.

La mwisho kabisa hivi siku hizi ndio imekuwa mtindo wa kuwataja Zitto,Mnyika and Regia?Kuna Wabunge wengi sana humu Wanawake kwa Wanaume amabo ni wanachama tena wazuri tu isipokuwa hawatumii majina yao halisi.Ukija na taito yako ikataja jina la ujumla Wabunge utapata majibu mazuri toka kwao.Mkiwa very specific mnawabana wao wanaona kama hawahusiki hivyo hawatoi ushirikiano wa kutosha,sio lazima wajitaje majina yao sisi tunataka michango yao. Ni vizuri tukawa tunapanua wigo mpana wa kuruhusu Wabunge wengine wachangie kwa majina yao bandia.

Aluta Continua

Kutoka Miti Mirefu Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Mimi nilitaka kujua je... kwa wabunge wa kuteuliwa.... NI MIUNDOMBINU GANI , YA WAPI ( inayomuhusu ),NA KATIKA JIMBO GANI ANAPASWA NAYE KUTUMIA GARI HIYO??? Samaki mkunje.....
 
Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!

Wamechukua na wanazitumia kuwaamsha wananchi kujua haki zao. People power oyeeeeeeeeeeeeeee
 
Mimi naona siyo wao ila ni serikali yako ndio walipanga hivyo sasa wakumuliza ni CCM na serikali yake kama ungekuwa wewe ungefanya nini??
 
ndugu wana jf ni wiki ya tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na wabunge wa ccm! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya chadema kuwa chama cha ukombozi kwa watanzani! Mh mnyika,mh zitto na mh mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh regia mtema hivi kweli aluta kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni maisha ya watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: Ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!

wivu wa kike tuu
 
Sasa hivi tuna matatizo ya wataalamu wetu wote wazuri kukimbilia katika siasa, hhi inatokana na haya msurufu. kuna mzee wangu mmoja Pro alipata kiinua mgongo cha 30,000,000 pale UDSM, na huyu bwana ni kichwa kweli. Sasa Mimi rafiki yangu sana ni myika. Hatuwezi kuwa na wabunge wanaowazidi mishahara walimu wao ( Huu ni mfano tu) Hebu tuwe na miongozo ya msurufu katika nchi hii, vinginevyo wattalamu wote watakwend siasani,

Duhh hapa ipo kazi kweli. Labda katiba mpya iangalie hili.:mullet:
 
Big Up Wabunge wa CDM Wamesababisha tumejua kuwa wabunge wamepewa Loan!
Wabunge wanahitaji Usafiri wa Uhakika so sioni kwa nini wasinunue Magari kwa FEdha walizokopeshwa! I think if you are great thinker then U well well that this money is not a grant mpaka uiite Rushwa it is a loan so sio Rushwa.
Nashauri hizo fedha wanunulie Magari yenye nguvu na Imara kwa ajili ya kazi iliyopo mbele yao

Mkuu tumekua tukilaumu serikali kununua magari ya kifahari,na mara nyingi serikali imekua ikisema magari imara yanatakiwa! Jamani wa Tanzania Tutafika kweli?
 
Back
Top Bottom