Mlengo wa Kati
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 2,730
- 492
- Thread starter
- #81
Hizi za kina mtema ,mnyika zitto za cdm ni chache sana ukilinganisha na zile za mafisadi wa ccm.hivi unakaa kuumiza kichwa na hizo 90m za wabunge wa cdm hata kama hawatazichukua, je ccm wataziaacha?na wao(ccm) walikuja kwa ajili ya hizo na si kuwatumikia wa tz.tafadhali anza na hao ccm kwanza wameshakula ngapi,wameiba ngapi wamechakachua ngapi.za rostam tu ni sawa na 0.000002% ya hizo fedha za cdm.kumbuka hali nzuri ya maisha ya watanzania suluhu yake si wabunge wa chadema kususia posho.na siku zote waliohongwa kama askari wa kihindi ni wabunge wa ccm ambao kila siku ndiyo mzee hata kama inawaumiza wa tz wanaowawakilisha(uwakilishi feki).
Umenena vyema mkuu. Nashangaa baadhi yetu kazi ni kuhukumu wengine bila kujiangalia mimi kama mimi ningefanyaje. Mbaya zaidi lawama zinaelekezwa kwa wabunge wa CDM pekee kama vile ni wao pekee waliopokea fedha hizo. MIMI NAONA TUELEKEZE LAWAMA HIZI KWA KATIBA HII ILIYOPO.Mbona umeenda mbali sana we tueleze mshahara wako unautumia vipi kuwanufaisha watanzania wenzio alafu umhoji Kikwete hizo fedha za EPA zilizorudishwa ni kina nani wamerudisha na ziko kiasi gani ili awaweke ndani kwa wizi kisha uje kwa Mnyika na Milioni 90 ambazo wabunge wote takribani 350 wamevuta.
Acha unafiki uliza wabunge wote ni jinsi gani hizo milioni 90 wanazitumia na sio Mnyika na Mdee tu otherwise as I say to be fair you tell us about about how you spend your salary first.
mheshimiwa Regia, hayo maneno unayosema ni Kweli?. au ndo yale yale kuita pesa nyingi Vijisenti?.
Kitu Kingine unasema Kwamba Bunge linachangia Shilingi Milioni 45 kwenye hilo gari, sasa swali langu ni hili, kama Bunge linatoa nusu na Mbunge anatoa nusu je Gari linakuwa ni la nani?.
Je Mbunge akimaliza Ubunge wake, anazilipa hizi Milioni 45 zinazochangiwa na Bunge ili aendelee kulimiliki hilo gari, au inakuwaje kuwaje, naomba Utueleweshe!.
Hata hivyo ninaungana na wewe moja kwa moja unapotoa dokezo la kupelekwa mswada bungeni ili kupunguza Haya yanayoitwa maslahi ya Wabunge "kwa sasa", kwani ni mzigo kwa Taifa, hayana Tija katika uchumi kwa sababu hayaliingizii pato Taifa, na yanajenga matabaka nchini. Tunategemea Wenzetu mlioko mbele kupinga Ufisadi, muwe msitari wa mbele katika kupinga matumizi kama haya yasiyo na manufaa, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga credibility mbele ya Umma, la sivyo mtaonekana kama mnaopiga kelele kwa sababu hamjashika dola na laiti mgeshika dola mgeonekana kama hawahawa CCM.
Ni bora kila jimbo likwa na gari lake imara, liwe gari la Bunge, na si gari la Mbunge, Mbunge awe analitumia tu katika shughuli za kibunge, kama halitaki basi anunue gari lake kwa pesa zake mwenyewe na awe anatembelea na kufanyia shughuli zake.
Mheshimiwa Mbunge!
Gharama zote za mkopo huo wa magari mliopewa ni shilingi Milioni 90 mara wabunge 353=bilioni 31.77, je hizo pesa tungejenga High School za kiwango Bora Ngapi?, tungejenga na kukarabati zahanati zetu ngapi?.
Hivi vipaumbele vyetu ni nini?
Swala hili siyo la Regia, John na Zuberi peke yao au ndivyo ulivyo-limit upeo wako wa kufikiri? kazi ya hizo fedha inajulikana na umuhimu wake pia unajulikana, kama kuna-cuttings katika matumizi ya serikali hulipaswa kuliongelea kama swala la Bunge zima kuanzia na CCM ambayo ndiyo inachukua fedha nyingi siyo ku-intimidate majina ya watu wachache kana kwamba Bunge ni la watu watatu au wanne.
Panua akili yako kama huwezi endelea kupanua tumbo lako lakini ni bora ukajua kuwa madhara yake ndio haya ya kutapika ovyo, matapishi pia yananuka kama kinyesi.
Kwani hivyo vyama vinajenga barabara, zahanati au shule kuwa lazima wapewe fedha? Mbona tunaona kuwa yanayofanywa na vyama (nikimaanisha vyote ccm, CDM, CUF na vyengine) ni kuleta uharibifu tu (mauwaji Arusha, kuchonganisha wananchi waache shughuli za maendeleo na kadhalika.
Nini haja ya vikundi vya watu wachache wachukue mamilioni ya wananchi kwa kupita na kutowa maneno yasio na maana! Vyama vijitegemee na si kuvipa mamilioni ya shillingi na tukiwaaacha wajawazito hawana matibabu, walimu hawalipwi na mengi ya faida zaidi ya porojo za wanasiasa. Siasa kama ni pesa basi na tuwaachie wafanyabiashara waifanye. Vyama vya siasa vinachukuwa kodi za wananchi bila sababu yoyote.
Halafu tunasema kuwa ruzuku kwa kuendeshea siasa jee wakati wa kampeni nani anatowa mamilioni yanayotumiwaq na wagombea? Hili la ruzuku lazima liangaliwe tena!