Regia Mtema, John Mnyika, Zitto Kabwe na 90mil | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Regia Mtema, John Mnyika, Zitto Kabwe na 90mil

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Mar 6, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Pendekeza wafanyie nini sio kulalamika tu.
  Ulitaka wakatae au?
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuongea tu kuwa wameingiziwa TZS 90M inatosha kwa CDM kuonesha kuwa ni chama transparent na kinachojali masilahi ya umma. Wanajisikiaje au vipi hiyo siyo kazi yako kujua, pia na je watazitumiaje hiyo pia si kazi yako. Umeshamsikia mbunge yeyote wa chama kisicho CDM anaongelea bulungutu hili?, hao ndiyo wa kuwahoji kwani ni wabinafsi na wanahofia kuzipoteza kama watajulikana wanazo.

  We a transparent Govt, kama wananchi wataelezwa kila kitu kuhusu jinsi resources zinavyotumika that is tha best way forward. Maisha magumu hayatakiwi kuwa kwa walalahoi pekee bali kila mtu.
   
 4. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kusema tu hakutoshi..waende hatua 1mbele,.coz wanajua wasiposema badae wataulizwa,.la muhim hapa ni kwamba washasema sawa...thn what next?
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wasiwe waongo then! Wote ni wanasiasa uchwara!

  Pendekezo langu ni kuwa hata ile ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe, kwanini kutumia kodi za wananchi kwa faida ya vikundi (vyama vya siasa)? Hao wabunge wangelipwa mishahara ya kawaida kama watumishi wa umma!
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
   
 8. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  He sasa wataendeshaje shughuli za chama? wanapoenda kila mkoa na kufanya mikutano huwa tunawachangia japo kidogo? huoni wanafanya shughuli nyingi sana na pesa wanazotumia ndio hizohizo?
   
 10. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mheshimiwa Ngekewa nimependa pendekezo lako kuhusu kutoa luzuku! Mfano CCM inapata 1 bilion,CDM 400 milion na CUF 120 milion na NCCR nayo inapata na hii ni kwa mwezi! Nakugongea thanks!
   
 11. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni hoja ya kuongelea kweli? Kwanini hao wachache? Kwani waliobaki hawakuchaguliwa na watz? Huu ni wivu au?

  Tunapaswa kufikiria kuwa kwanini wabunge wapewe hizi m90 kila baada ya 5yrs? Kwanini magari yasiwe ya bunge,then wabunge wapewe kuyatumia pale wanapochaguliwa. Haf wapewe kadi tu za mafuta za bp hivi,sio kupewa hela kiholela! Na kucontrol route ,sio mbunge wa kigoma anaonekana anacruise mkoa wa Lindi bila shughuli ya kibunge!!

  Ni wazi serikali yetu haina accountability
   
 12. A

  Apollnary JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani Watanzania tujitahidi kuwa na upeo kidogo na mambo tunayotaka kutafuta support ya walalmiakaji.....
  Milioni 90,ni hela ianyoweza kununua gari mpya,ambayo inaweza angalau kudumu kwa miaka kadhaa,inaweza kustahimili mwendo wa mbali na kutumika km nyingi.
  Mbunge anategemewa kuzunguka kwa wananchi na kwenda Bungeni miaka mitano.
  Prado second hand(ama 3rd hand)ni kama Milioni 50
  Prado mpya ni kama Milioni 75
  Toyota Mark mpya ni kama Milion 35
  Sasa tunataka wabunge wanunuliwe Toyota Mark watafika nazo wapi?
  Ama wanunue magari 2nd hand,yaharibike in 2 years(kutokana na shughuli zao kuwa za kuzunguka sana),alafu tuanze kusema wabunge wanachezea hela zetu?
  ......Watanzania jamani,mambo mengine tusiwe na wivu wa kupindukia.....ni afadhali na wabunge tumewachagua wenyewe....mbona hatulalamiki magari ya viongozi wengine kama makatibu wakuu,makamishana,viongozi wa mashirika ya Umma?Just because wabunge tunawafahamu?Jamani watanzania tuna kazi kwelikweli......
   
 13. A

  Apollnary JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtasahihisha wenyewe hapo juu nilichotaka kuandika
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Fedha kboko ndugu yangu, naona kama unapendekeza Wangeligomea kama walivyogomea hutuba ya Rais, hahahaha
   
 15. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu kusema tu haitoshi! Tunahitaji vitendo!
   
 16. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Linapokuja suala binafsi la MASLAHI...waheshimiwa hubaki vigeugeu mithili ya ndumilakuwili, yaani SITAKI-NATAKA. Wanaweza tu kuziachia mil.90 iwapo chama kiliwapa sufficient funds kipindi cha campaign. Otherwise...
   
 17. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Toyota rav4 ni M24 ikiwa mpya, zipo imara
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani hivyo vyama vinajenga barabara, zahanati au shule kuwa lazima wapewe fedha? Mbona tunaona kuwa yanayofanywa na vyama (nikimaanisha vyote ccm, CDM, CUF na vyengine) ni kuleta uharibifu tu (mauwaji Arusha, kuchonganisha wananchi waache shughuli za maendeleo na kadhalika.
  Nini haja ya vikundi vya watu wachache wachukue mamilioni ya wananchi kwa kupita na kutowa maneno yasio na maana! Vyama vijitegemee na si kuvipa mamilioni ya shillingi na tukiwaaacha wajawazito hawana matibabu, walimu hawalipwi na mengi ya faida zaidi ya porojo za wanasiasa. Siasa kama ni pesa basi na tuwaachie wafanyabiashara waifanye. Vyama vya siasa vinachukuwa kodi za wananchi bila sababu yoyote.
  Halafu tunasema kuwa ruzuku kwa kuendeshea siasa jee wakati wa kampeni nani anatowa mamilioni yanayotumiwaq na wagombea? Hili la ruzuku lazima liangaliwe tena!
   
 19. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,691
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Huu ni wizi tu!!...kila jimbo liwe na gari la ofisi ya mbunge!.we did that during nyerere times...acheni kutafuta ujiko!
   
 20. A

  Apollnary JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tofautisha kati ya gari mpya,na gari inayoonekana mpya.......
  Toyota rav 4 ya mil 24 ni ile inayoonekana mpya(second hand)
  toyota rav 4 mpya ni kama mil 35 hadi 40
  ......na hiyo rav 4,zito atatoka nayo kigoma dodoma daresalaam mara ngapi?na yule jamaa wa kagera?.....hahahaha
   
Loading...