Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!
Huu ni wizi tu!!...kila jimbo liwe na gari la ofisi ya mbunge!.we did that during nyerere times...acheni kutafuta ujiko!
Pendekeza wafanyie nini sio kulalamika tu.
Ulitaka wakatae au?
Ubunge siku hizi ni ulaji tu!...nakumbuka wakati wa vikao vya bunge gesti za uswazi zilikuwa zinapata sana biashara,na wabunge wengi wakitoka mikoani walikuwa wanakuja na public transportation,na hospitali tulikuwa hatulipi hata sentano!...shule daftari likiisha anapeleka kwa mwalimu anakupa jipya halafu unatafuta jalada kutoka gazeti la uhuru,hasa likiwa la ukurasa wa mwisho wa michezo.Kipindi cha Nyerere wabunge walikuwa wachache na pengine ndio maana ilikuwa rahisi kuwa na gari la ofisi ya mbunge katika kila jimbo. Sasa hivi ni majimbo yameongezeka na wabunge wa viti maalum na wale 10 wa kuteuliwa na rais wamefanya idadi iwe kubwa zaidi na kufanya ugumu wa wazo lako. Lakini pia kama Tsh.90 million zinatolewa kwa wabunge kwaajili ya gari litakalotumika kwa miaka mitano tatizo liko wapi? Ni afadhari wamepewa hela kila mmoja ajinunulie mwenyewe kuliko wangenunuliwa na bunge hicho kiwango kingeongezeka kutokana na ufisadi ambao ungefanyika katika manunuzi. Kama tuna dhamira ya kweli, basi tupinge mashangingi ya 200million ya mawaziri badala ya kuwabana wabunge na 90million!
Husnina, ule ni mkopo watalipa, ni ngumu wao kuutumia kwa shuguli za umma ila ni makosa kUUKUBALI hapa chadema wametuangusha, inatupa tafsiri kwamba hata wao kama wabunge wengine wte walikuwa wanapigana kwenda mjengoni kwa maslahi binafsi zaidi
Ndugu wana JF ni wiki ya Tatu sasa tangu wabunge wetu waingiziwe kwenye akaunti zao kiasi cha Milioni 90,nimetaja wabunge hawa vijana watuambie hivi wanajisikiaje kupata kiasi hicho wakati wakijua hali ya maisha ya Watanzania kwa sasa? Ndugu zangu hivi tuige nini hasa tunapo ona wapiganaji wetu nao wanafanya makosa yaleyale ambayo ni sawa na Wabunge wa CCM! Dr slaa hivi umehoji kwa nini wabunge wako wamekubali kuingiziwa kiasi hicho bila kuangalia maisha yetu watanzania ambao wengi kwa sasa tuna weza kupata mlo mmoja kwa siku? Milioni 90 najua imetokana na jasho la walipa kodi! Nashauri kamati kuu ya Chadema ikae iliangalie suala hili lasivyo linatutia matope na kupoteza hata ile maana ya Chadema kuwa chama cha ukombozi kwa Watanzani! Mh Mnyika,Mh Zitto na Mh Mtema najua safari yenu bado ndefu kisiasa hivi kweli mumekubali kula hii hela haramu ya maskini wa kitanzania? Mh Regia Mtema hivi kweli Aluta Kontinua kwa namna hii! Mandela aliwahi kusema makaburu hawana uwezo wa kutuhonga kwa garama yeyote ile bali kilicho na thamani ni Maisha ya Watu wetu! Mmekubali kuhongwa kwa mkate kama askari wa kihindi! My take: ni mhimu tujipime kama chama cha ukombozi wa maskini wa watanzania walio wengi!
Tofautisha kati ya gari mpya,na gari inayoonekana mpya.......
Toyota rav 4 ya mil 24 ni ile inayoonekana mpya(second hand)
toyota rav 4 mpya ni kama mil 35 hadi 40
......na hiyo rav 4,zito atatoka nayo kigoma dodoma daresalaam mara ngapi?na yule jamaa wa kagera?.....hahahaha
Wakuu.Salaam.
Nimeona nichangia post hii kidogo.
Kwanza kabisa niweke rekodi sawa Fedha hizi za Gari hazijaanza kuigia kwa wiki tatu zilizopita kama mtoa mada alivyosema.Cheki zimeanza kutolewa kama siku nne au tatu zilizopita na zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge bado hawajapata cheki zao,hata mimi bado sijapata.
La pili ni hili Milioni 90.Ifahamike kwamba Milioni hizi 90 wabunge hawapewi Bure tunakopeshwa na tunakatwa kupitia mishahara yetu.Bunge linalipa nusu ya pesa hizo yaani Milioni 45,Milioni 45 nyingine kila Mbunge anakatwa karibu shilingi 866,000 kwa mwezi kupitia mshahara wake.Kwahiyo Bunge linatoa shilingi Milioni 45 tu kwaajili ya gari.
La tatu Kimsingi Bunge limeweka Utaratibu ili kumsaidia Mbunge afanye vizuri kazi zake za Kibunge ilipendekezwa awe anatumia gari aina ya Toyota Hard Top Mpya ambayo kwa sasa gari hili linauzwa shiingi Milioni 112.Bunge likatafakari ikaonekana ni gharama kubwa kumpa kila Mbunge shilingi Milioni 112 hivyo busara ya wahusika wanaopanga maslahi ya wabunge wakaja na kiwango hiki cha Milioni 90 na Bunge kuchangia nusu ya pesa hizi. Bunge limependekeza aian hii ya gari kwakuwa ni imara inayoendana na miundumbinu ya majimbo mengi hapa nchini.Lakini kwa hali ilivyo watakao nunua ni wale wenye uwezo kipesa wengine trutakimbilia kwenye magari ya bei rahisi.
La nne ni mapendekezo ya baadhi ya watu eti wabunge wa CHADEMA wasichukue pesa hizo.Kimsingi hili sio pendekezo sahihi sasa wabunge hawa wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za gari nani atawanunulia magari ya kurahisisha kazi zao?hivi milioni 45 ni nyingi sana kwa kununua gari?kwa yeyote anayefahamu vizuri kazi ya Mbunge ndani ya Jimbo na miundombinu yetu hawezi kulalamika kuhusu hili. Gari imara kwa miaka 5 ni muhimu sana kwa Mbunge. Kwa wanaojua magari vizuri wanajua vizuri magari imara na mazuri kwa kazi za kisiasa zinauzwa shilingi ngapi. Vile vile Wabunge wa CHADEMA wasipochukua pesa hizi za magari itakuwa haina maana kwani Wabunge wa CHADEMA tuko 48 tu kati ya Wabunge 353 hivyo sisi tukikataa haitabadilisha chochote na badala yake pesa hizi zitaishia kwenye mikono ya wachache ambao hatutajua zimetumika vipi.Kuna msemo unasema ukisusa wenzio wala.Hoja ya msingi hapa ni kuwa Wabunge wa CHADEMA wapeleke hoja Bungeni ya Kupitia Upya Maslahi ya Wabunge ili kama kuna pesa zisizo na maana kwa mbunge basi ziondolewe kwa maslahi ya umma,hoja si kukataa milioni 90 kwa sasa.
La tano kwa upande wangu kwa kuwa mimi ni Mbunge maskini siwezi kuzipeleka Milioni 90 zote kwenye gari.Nitanunua gari la bei nzuri la kini lazima liwe imara na la kuvutia.Zingine zitafanya mambo ya msingi ndani ya Jimbo la Kilombero na mambo mengine madogo madogo.
Lasita mkubuke vile vile siku hizi hela imeshuka sana thamani Milioni 90 zinaisha ndani ya wiki moja na unaweza ukajikuta hakuna la maana ulilolifanya.
La mwisho kabisa hivi siku hizi ndio imekuwa mtindo wa kuwataja Zitto,Mnyika and Regia?Kuna Wabunge wengi sana humu Wanawake kwa Wanaume amabo ni wanachama tena wazuri tu isipokuwa hawatumii majina yao halisi.Ukija na taito yako ikataja jina la ujumla Wabunge utapata majibu mazuri toka kwao.Mkiwa very specific mnawabana wao wanaona kama hawahusiki hivyo hawatoi ushirikiano wa kutosha,sio lazima wajitaje majina yao sisi tunataka michango yao. Ni vizuri tukawa tunapanua wigo mpana wa kuruhusu Wabunge wengine wachangie kwa majina yao bandia.
Aluta Continua
Kutoka Miti Mirefu Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Umejibu hoja dada regia lakini wabunge wa viti maalum na wa kuteuliwa na rais nao wanahitaji magari hayo imara na mazuri? wao wanashughuli hizi za wabunge wa majimbo? au labda sijui kazi zao naomba kuelimishwa.
Nimekuelewa Dada Regia, watumikie wananchi wa Morogoro na watanzania kwa ujumla, Mungu atakubariki.Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Mbunge wa Viti Maalum anaanzia Wilayani kwake then unakwenda ngazi ya taifa na kupitishwa na vikao husika kwa kuomba kura kwa wajumbe wa vikao vyote hivi.Kwahiyo kama niliptia Wilayani kwangu hivyo ni wajibu wangu pia kutekeleza majukumu yaliyopo kwenye Wilaya yangu.Kanuni za kitaifa zimempa Mbunge wa Viti Maalum kutumikia Mkoa ndio maana utasikia Regia Mtema Mbunge Viti maalum toka Mkoa wa Morogoro.Mkoa Mmoja una Wilaya kati ya 4 mpaka 8 hivi unafikiri Mbunge huyu atafanyaje kazi?lazima awe na usafiri kwa kuwezeshwa na ofisi yake anayoitumikia.Wabunge wa Kuteuliwa na rais na wenyewe wanapewa majukumu katika kazi zao hivyo lazima wawe na nyenzo za kuwarahishia kazi. Mimi Kama Mbunge wa Viti Maalum natumikia Mkoa Mzima wa Morogoro. Unajua jinsi Morogoro ilivyokubwa na miundo mbinu ilivyomibovu,tunahitaji magari imara.
Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Mbunge wa Viti Maalum anaanzia Wilayani kwake then unakwenda ngazi ya taifa na kupitishwa na vikao husika kwa kuomba kura kwa wajumbe wa vikao vyote hivi.Kwahiyo kama niliptia Wilayani kwangu hivyo ni wajibu wangu pia kutekeleza majukumu yaliyopo kwenye Wilaya yangu.Kanuni za kitaifa zimempa Mbunge wa Viti Maalum kutumikia Mkoa ndio maana utasikia Regia Mtema Mbunge Viti maalum toka Mkoa wa Morogoro.Mkoa Mmoja una Wilaya kati ya 4 mpaka 8 hivi unafikiri Mbunge huyu atafanyaje kazi?lazima awe na usafiri kwa kuwezeshwa na ofisi yake anayoitumikia.Wabunge wa Kuteuliwa na rais na wenyewe wanapewa majukumu katika kazi zao hivyo lazima wawe na nyenzo za kuwarahishia kazi. Mimi Kama Mbunge wa Viti Maalum natumikia Mkoa Mzima wa Morogoro. Unajua jinsi Morogoro ilivyokubwa na miundo mbinu ilivyomibovu,tunahitaji magari imara.