OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Utangazaji wa sasa ni kama unasikiliza majibizano ya vijiweni. Mbali na watangazaji kutojipanga ila mara nyingi wamekuwa wakiongea wao kwa wao huko studio, mara nyingine wanajisahau kuwa kuna watu wanawasikiliza
Yaani unakuta wanaongelea suala la msingi lakini wanaweka mambo mepesi sana katika masuala hayo, Redio zoe zinakuwa kama zipo kwenye kupotosha au kiudaku zaidi kuliko kuhabarisha na kuelimisha
Ofcourse burudani ni muhimu lakini kupitia burudani inabidi kuwe na elimu humo kwa humo. sio burudani tu muda wote
Pia wengine hudhihirisha ujinga wao kwa kuongelea mambo ambayo hata hawayajui au hawajayatafiti kabla ya kwenda kuyazungumza redioni. Unasikiliza redio kama unasikiliza vijana walioko kwenye kijiwe cha kahawa au kwenye maeneo ya kubeti wakiwa wanabishana wampe nani wamuue nani
Kwa kusema haya wala sishadadii suala la serikali kutaka vijana wote wawe ni wale waliosoma masuala ya habari. Bali naamini katika ule mtindo wa Kimarekani, kwamba mtu anasomea kitu fulani kama masuala ya watoto, halafu anasoma habari ili atoe elimu kuhusu masuala ya watoto
Huo ndio muarobaini wa kufanya watu wasitangaze vipindi kama wako vijiweni. Anasema kuwa na Astashahada, Stashahada au shahada ya habari haitoshi kumfanya mtu kuwa mtaalamu wa jambo analolizungumza
Signed
Oedipus