Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
REDIO YA KIDIGITALI
Waungwana naamini hamjambo.
Ni miaka 7 sasa tangu tubadili TV za analog na kuingia kwenye TV za digital. Yaliyojitokeza tutakuwa tunayakumbuka ambapo mengine yamekuwa na tija na mengine yamekula na changamoto.
Kwa sasa kuna habari kwamba tunaelekea kuingia kwenye mageuzi ya redio kutoka analog kwenda digital. Kwa yeyote anayejua faida na digital radio naomba atujuze ili tuweze kuelimishana. Nimeona niandike hii kwa sababu Tanzania tunaingia kwenye mabadiliko pasipo kujiandaa na matokeo yake malalamiko yanakuwa ya chini chini.
Nawasilisha – nakaribisha maoni kwa wanaoelewa hii aina ya huduma za redio.