Ninapozungumzia objectivity katika utafiti, ni tafiti zote ziwe za REDET, JF au SYNOVATE. Ili kupata majibu yaliyo sahihi utafiti unatakiwa uwe na sample kubwa ambayo pia ni representative, mfano mzuri ni huu utafiti wa JF unauliza kama wanajanvi wanaipenda serikali ya Jakaya au La. Sample ya watu wanaoulizwa ni biased kwasababu wengi wa wanajanvi naweza kusema hawaipendi ccm na ni wachache sana ukilinganisha na population ya million 40 ya waTanzania, kwahiyo basi ni dhahili kuwa matokeo yake yataiponda CCM na hayatakuwa representative ya maoni ya majority ya WaTanzania!! Hivyo hivyo kwa taasisi za REDET na SYNOVATE!! Synovate kwa mfano tafiti zake hazitiliwi maanani sana kule Kenya kwa sababau hizi hizi za kuwa biased for the establishment.
Mwelekeo wa matokeo ta tafiti za REDET hata wakifanya sasa baada ya DR. Slaa kuingia ulingoni hayatakuwa tofauti na matokeo yao ya awali kwasababu nilizoziainisha hapo awali. Tafiti zao zina malengo mahususi!!
Kama unashawishika na UTAFITI wa REDET basi naamini kuwa wewe ni another custodian wa brainwashed wa hilo dubwasha.REDET walishazungumza mapema! Watu wakawakejeli kwamba eti wanatumiwa!! Gazeti la Tanzania Daima likadai eti REDET inatumiwa na Kikwete; kwamba REDET wanapotoa utafiti kuonesha kukubalika kwa Kikwete kunajenga saikolojia ya wapiga kura wamchague Kikwete!! Aibu zaidi, Tanzania Daima waliibuka na tahariri iliyoikandia REDET; kwavile tu ripoti hiyo ya REDET ilionesha Kikwete angeshinda kwa asilimia nyingi endapo uchaguzi mkuu ungefanyika wakati wa utafiti uliokuwa umefanyika na REDET!
Bila shaka Tanzania Daima wangekubaliana na utafiti wa REDET endapo ungesema CHADEMA kingeshinda!! Wakati Tanzania Daima walipotoka na tahariri ya kukejeli utafiti wa REDET, walisahau kwamba siku chache tu kabla ya hapo wao walikuwa wameibuka na kura za maoni zilikuwa zimeendeshwa humu JF!
Hata wana CCM nao wakaupinga utafiti wa REDET, kisa tu kilitabiri mabaya kwa wabunge kadhaa kwamba wangepigwa chini!! KIKO WAPI? Nyota njema imeonekana asubuhi! Asubuhi asubuhi, tayari wabunge kadhaa wa CCM wamegalagazwa hata kabla ya uchaguzi mkuu wenyewe bado! Nasikia karibi wabunge 50 chali na game bado linaendelea! Hao ni wale waliopteza mikononi mwa wana-CCM wenzao! Je, ni wangapi kwa waliosalia watakaopoteza viti vyao kwa upinzani?!
Mimi si Mwana CCM, CHADEMA wala REDET; ila ningependa kuwashauri Watanzania kujenga utaratibu wa kuamini tafiti zetu! Sina hakika, lakini naamini REDET imeundwa na wasomi hivyo kubeza tafiti zao ni kubeza umuhimu wa wasomi wetu.
Mkuu Bulesi, mi nahisi nimekusoma ile mbaya! Unajuwa nimekusoma nini, inawezekana kabisa kwamba utafiti wa REDET una malengo maalumu na kubwa zaidi la kumng'alisha mkulu; au sio mkuu Bulesi?! Sasa tuachane na hayo mapungufu ya REDET ambayo hata hivyo ni ngumu kuyathibitisha! Assume utafiti ule unafanywa na taasisi isiyo na mafungamano yoyote na JK au CCM, hivi ni kweli matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya REDET?!
NasDaz Mkuu, let us assume kama unavyoshauri kuwa independent researcher aje leo afanye utafiti juu wagombea wetu wa urais; mimi ninahakika kabisa matokeo yake kama sample yake itakuwa representative yatakuwa tofauti na yale ya REDET!!Hali ya maisha ya waTanzania ni mbaya sana kiasi kwamba sioni jinsi ambavyo mgombea wa urais wa ccm ataweza kuibuka mshindi kwenye utafiti huo; ingawa anaweza kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa October kwa vile wataiba kura [absence of level playing field]!! Kumbuka tu kwamba malengo makubwa ya hizi opinion polls ni kushawishi mwelekeo wa wapiga kura.