Huyu Rwekaza Mukandara amekuwa pro-CCM professional king-maker tangu enzi za Mwinyi. Yeye na hiyo REDET yake ndiyo waliokuwa kila unapokaribia uchaguzi wanafanya utafiti ambao ulikuwa unaonesha kwamba CCM wangeshinda kwa asilimia fulani, na matokeo hatimaye yalionesha hivyohivyo. Hiyo nahisi kwa namna fulani iliwaandaa wananchi kuyapokea matokeo "hayo". Sitashangaa kusikia kwenye utafiti huu akionesha matokeo yanayosema serikali imefanya mazuri asilimia kubwa, na imezidi kukubalika kwa wananchi, nk nk, maana kushangaa hilo ni sawa na kumshangaa kuku kutaga mayai, sijui tulitaka atage nini?
Hivi hata baada ya kuteuliwa kuwa VC wa UDSM, Rwekaza bado ndiye bosi wa REDET au kuna mwingine? Hata hivyo sitegemei mabadiliko kwa kuwa hiyo REDET bado iko chini ya UDSM ambayo Rwekaza ni bosi wake.