REDET Kutafiti Utendaji wa Kikwete toka aanze Awamu ya nne

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
wana bodi,
jana nilikuwa maeneo ya chuo kikuu cha Dar es salaam nikakuta REDET Wanakamilisha semina elekezi kwa ajili ya utafiti wa tathimini ya utendaji wa serikali ya awamu ya nne,
kwa kifupi utafiti huo utaanza kesho na utafanyika kwa siku tano eneo lote la TANZANIA..
nilijaribu kuchukua questionaire niilete hapa ila nilinyimwa..
ninafanya jitihada ya kuipata na kesho naweza kuiweka hapa.
kila mtafiti atakuwa analipwa dola 25 kwa siku.
 
inasemekana research hiyo inafadhiliwa na serikali..na ilibuniwa na mkandara ..makamu mkuu wa chuo kikuu pale mlimani,
habari nilizopata mpaka sasa ni kwamba hii imefanywa makhususi kujibu tuhuma za ufisadi na kuwaambia wananchi kuwa serikali ya awamu ya nne inatatua matatizo yao!
mkandara ni mshauri mkuu wa siasa wa muungwana
 
inasemekana research hiyo inafadhiliwa na serikali..na ilibuniwa na mkandara ..makamu mkuu wa chuo kikuu pale mlimani,
habari nilizopata mpaka sasa ni kwamba hii imefanywa makhususi kujibu tuhuma za ufisadi na kuwaambia wananchi kuwa serikali ya awamu ya nne inatatua matatizo yao!
mkandara ni mshauri mkuu wa siasa wa muungwana

Mkomboziufisadi,

Tatizo hapo ni hao REDET wenyewe na wala sio hilo la kuwa sponsored na serikali. Opinion polls mbalimbali zinakuwa sponsored na watu wenye interests fulani kwenye jambo husika. Huenda sasa serikali inataka kujua baada ya misuko suko yote hii wananchi wanauonaje uongozi wa JK?

Tatizo kwa TZ ni kwamba hayo maoni yanaweza kupikwa ili kumpa JK sifa asizo nazo. Hapo ndipo penye tatizo na njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ni kanzishwa kwa kampuni nyingi zinazofanya hizo researches au opinion polls na baada ya muda wale wanapika data kila mtu atawadharau. Itakuwa kama gazeti la RAI lilivyodharauliwa.
 
cha kushangaza,wananchi hawajaarifiwa juu ya ukusanyaji wa data ili khali kesho ndio siku yenyewe..
uchambuzi pembunifu wa utafiti umefanywa kwa haraka..
kama kweli REDET Wanataka ukweli waweke questionaire hadharani na ikiwezekana ktk tovuti ili watanzania wengi washiriki ..mf. walioko ughaibuni kama mwanakijiji na wenzake!
Jana PIA niliona vijana wa wili ambao huwa wanasadikika ni usalama wa mafisadi wanashiriki kama wakusanyaji wa data hizo
 
Hli suala mbona la ghafla sana? Sijasikia mahali wametangaza kuwa wanafanya utafiti huu, ama ndio wamewaandaa 'respondents' kabisa ili kupika matokeo? Sampuli ya wahojiwa wao *respondents* ikoje?
Watatembelea Tanzania nzima kwa siku tano tu? Du
Anyway, tarishi hauwawi, tusubirie hilo dodoso lao tuone mambo yakoje. Ikumbukwe ni hivi majuzi tu Mukandara aliambiwa atoe tathmini ya utendaji wa muungwana, akagoma kata kata, leo ameona afanye hivyo.
 
Opinion polls huwa hawatangazi. Ni jambo la kushutukiza tu.

Wakitangaza ina maana kuna uwezekano wa hiyo opionion poll kutokuwa sahihi. Watu wanaweza kujiandaa na majibu au kujadiliana majibu kabla ya kuulizwa.

Pia japo watu kwa mfano 20,000 wanaweza kuulizwa na kutoa majibu lakini unaweza kukuta sample iliyotumiaka ni watu kama 1000 tu. The sample needs to be truly representative of the population. Kwa mfano kama TZ vijana ni asilimia 40 ya population basi katika hao 1000, lazima vijana wawe 400, kama wasomi zaidi ya degree wako asilimia 1 basi katika hao 1000 inatakiwa 10 wawe na at least degree.

Kwa Tanzania huenda ni ngumu sana kufanya utafiti wa namna hii na pia ni gharama maana hakuna data base ambayo mtu unaweza kuitumia na badala yake mambo mengi mpaka uyafuate huko wilayani.
 
Naona kama REDET wanataka kutupa Credibility yao, credibility waliyoijenga wanataka kuibomoa wao wenyewe. Mimi nategemea kuwa ripoti hiyo itasema "mambo ni mazuri isipokuwa kuna matatizo kidogo tu ya malalamiko kuhusu rushwa, lakini hiyo inaonesha kuendelea kukomaa kwa demokrasia' This is sort of Crap we should expect!
 
Kuna maswalli ya msingi ya kujiuliza. 1 je what will be the applicability of the results. mfano matokeo yakionesha negativity what will happen? asuming data hazitapikwa. je who detarmine the sample population. cliteria zipi zitatumika. maeneo, sekta, population strata etc. Je should we expect uwajibikaji kama results zitaoinesha serikali inacheza rafu?
 
Unajua ktk hizi surveys/ opinion polls unaweza ukapata matokeo yoyote yale unayoyataka...hata hivyo tusihukumu kwanza kabla hawajatoa tathmini yao.
 
Unajua kama mtu hajaonja pepo sii rahisi kumuuliza na ukapata jibu sahihi.
Mfano kama Mkandara hapa nimetokea Ukerewe ukaniuliza uzuri wa jiji la Dar nitakwambia hakuna mji kama Dar!.. na mendeleo makubwa nitayataja kwa sababu sijawahi kuona mji mkubwa.
Hili ndio litakuwa tatizo kubwa la utafiti huu kwani wananchi hawafahamu kabisa majukumu ya serikali na viongozi kiutendaji.
Hadi leo wananchi hawafahamu nafasi yao ktk ujenzi wa Taifa hili isipokuwa wanasubiri JK ama Mungu kuwafungulia milango. Wale waliokuwa wajanja wameweza nufaika kwa sababu wananchi wengi bado wamelala na mtazamo wao ktk utekelezaji wa serikali hii utahusu zaidi nafasi zao na sio ya taifa kwa ujumla.
 
Huyu Rwekaza Mukandara amekuwa pro-CCM professional king-maker tangu enzi za Mwinyi. Yeye na hiyo REDET yake ndiyo waliokuwa kila unapokaribia uchaguzi wanafanya utafiti ambao ulikuwa unaonesha kwamba CCM wangeshinda kwa asilimia fulani, na matokeo hatimaye yalionesha hivyohivyo. Hiyo nahisi kwa namna fulani iliwaandaa wananchi kuyapokea matokeo "hayo". Sitashangaa kusikia kwenye utafiti huu akionesha matokeo yanayosema serikali imefanya mazuri asilimia kubwa, na imezidi kukubalika kwa wananchi, nk nk, maana kushangaa hilo ni sawa na kumshangaa kuku kutaga mayai, sijui tulitaka atage nini?

Hivi hata baada ya kuteuliwa kuwa VC wa UDSM, Rwekaza bado ndiye bosi wa REDET au kuna mwingine? Hata hivyo sitegemei mabadiliko kwa kuwa hiyo REDET bado iko chini ya UDSM ambayo Rwekaza ni bosi wake.
 
mpaka sasa jitihada za kupata dodosa hilo imekuwa ngumu,kuna usiri mkubwa hata waliopewa wanakata kutoa,
sasa sijui wamepewa maelekezo na nani,wana kopi moja moja na kila mtu ameambiwa atakuta dodosa zote anazofanyia kazi akifika katika kituo chake.
ila naendelea kufuatilia kwa ukaribu sana
 
Hee

Huyu Rwekaza naye! Spin Profesa.

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni ulisema kwamba asilimia 40 ya watanzania wanataka turudi kwenye mfumo wa chama kimoja?

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni umesema kwamba CCM inapendwa kwelikweli?

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni umesema umaarufu wa Kikwete bado uko juu ila watendaji wake tu ndio wameshuka umaarufu?

JF tusitake taasisi nyingine za utafiti mathalani Steadman Group nk nazo zinafanye utafiti. Wengi wakifanya tafiti zingine huru ripoti za REDET zitaonekana takataka.

Kwa sasa wana monopoly ya kuupotosha umma hawa jamaa.

Hivi kwanini maprofesa wetu humu na nyinyi msifanye utafiti mitaani huko mkatuletea takwimu zenu?

Tusiendelee kulalamika, tuchukue hatua

Asha
 
Hee

Huyu Rwekaza naye! Spin Profesa.

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni ulisema kwamba asilimia 40 ya watanzania wanataka turudi kwenye mfumo wa chama kimoja?

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni umesema kwamba CCM inapendwa kwelikweli?

Si ndiyo huyu utafiti wake wa hivi karibuni umesema umaarufu wa Kikwete bado uko juu ila watendaji wake tu ndio wameshuka umaarufu?

JF tusitake taasisi nyingine za utafiti mathalani Steadman Group nk nazo zinafanye utafiti. Wengi wakifanya tafiti zingine huru ripoti za REDET zitaonekana takataka.

Kwa sasa wana monopoly ya kuupotosha umma hawa jamaa.

Hivi kwanini maprofesa wetu humu na nyinyi msifanye utafiti mitaani huko mkatuletea takwimu zenu?

Tusiendelee kulalamika, tuchukue hatua

Asha

Kufanya utafiti kama huo kwa TZ ni gharama kubwa, kunahitaji sponsors. Sasa kama hao REDET ndio wanapewa pesa zote , basi ngumu sana kwa wengine kuingia.

Sponsors wengi kama vile magazeti wakipatikana basi kuna watafiti wengine watatokea na kama utafiti wao utakubalika na watu wengi zaidi basi hata watu wa kuwalipa kwa hizo kazi wataongezeka.
 
Wazee,

Mpeni basi benefit of doubt, au vipi?

Tusubiri matokeo ndio tuchanmbue, la sivyo tutakuwa tunapigana nai atafagia mavi kwenye banda la kuku wakati banda halijajengwa na kuku hajanunuliwa!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom