Madrid imewahi kuitoa Man Utd, wakati kocha alipokuwe Vicente Del Bosque, enzi hizo kipa wa Man Utd alikuwa Bartez.
Mechi ya kwanza ilichezwa Santiago Bernabeu, uwanja wa Real Madrid..Madrid ikashinda 3 kwa 1. Goli la Man Utd lilifungwa na Ruud Van Nesterooy [pole ikiwa nimekosea namna ya kuandika jina]..Figo alifunga mojawapo ya magoli ya siku hiyo..alikuwa akivaa jezi namba 10 enzi hizo pale Madrid!
Mechi ya marudiano Man Utd walishinda kwa magoli 4 kwa 3, na siku hiyo David Beckham alianzia benchi, alipoingia gemu ikabadilika kabisa..pia alifunga. Ikumbukwe kwamba Madrid walikuwa wametangulia kwa kufunga magoli 3 kwa bila lakini yote yalirudishwa na "mashetani wekundu"..Hata hivyo Man Utd walitolewa katika mashindano kwa jumla ya magoli 6 kwa 5! Madrid walikuja kutolewa katika hatua inayofuata walipocheza na Juventus..
Man Utd pia imekuwa ikisumbuliwa sana na Barcelona kwa miaka ya hivi karibuni.
Unaweza kukumbuka fainali 2 ambazo Man Utd imecheza na Barcelona imepoteza zote!
-Mwaka 2009, Barcelona 2, Man Utd 1.
-Mwaka 2011, Barcelona 2, Man Utd 1.
je, hizo si takwimu?
"Be bold, and mighty forces will come to your aid."