Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Kivipi mkuu? Wangekuwa wa ovyo wangekuwa wanachukua makombe kila kukicha?

timu ndio inayochukua makombe sio mashabiki.

Unawakuta wanalalamika kuwa walikuwa katika hali ngumu eti sasa hivi ndio wanategemea kupata raha. timu iliyobeba UEFA 6 kwenye miaka 10 inakuaje na hali ngumu? ukiwakuta mitandani unawakuta wanawatukana sana Zidane na Carlo kuwa sio makocha eti sahivi ndio wamepata kocha. wewe uanahisi ni watu wakawaida hao?
 
Kwa timu yenye njaa ya makombe hiyo ni kawaida kabisa mkuu.
 
Kwa timu yenye njaa ya makombe hiyo ni kawaida kabisa mkuu.

kabla ya hayo makombe sita hiyo njaa yao ilikuwa wapi? unajua Madrid ilipita miaka mingapi bila ya kubeba hata kombe moja?

kinachowatesa wao madogo ni shibe, wametake success for granted wanahisi kupata mafanikio kwao ni kama kitu cha automatic so hawaheshima nguvu za watu waliochangia kufanikisha. Ila watayaona tu. wengi wao hawajawahi kuiona madrid in straggling days ndio mana wanaongea lugha za kipuuzi kama hizo.
 
For the first time baada ya usajili na kusafisha benchi la ufundi ngoja tuone namna tumeimarika.
 
Hii timu yetu bado maeneo mawili ya msingi ni tatizo,beki ya kushoto na eneo la kiungo,kuanzia ukabaji hadi ushambuliaji..

Eneo la kiungo ukabaji bado wimbi la uchovu linawasumbua hawa wachezaji wetu,kuendelea kutegemea Tchoumeni nikujidanganya,ni average player na pia Jude hana kasi ambapo mpira wa sasa unahitaji watu wenye kasi na wanaofanya maamuzi sahihi na kwa haraka,eneo hilo ubunifu hakuna,lakini pia ukiangalia Rodrigyo anavyocheza na Vin Jr hakuna tofauti na msimu uliopita,wanajitenga sana na wengine na hii inapelekea timu inaposhambuliwa inakuwa ni rahisi sana kufika eneo la goli letu.

Kwa hiyo kwa mwendo huu kwa kwel na viwango hivi sioni mabadiliko kwa mechi za karibuni.
 
Unaona hata takwimu zinavyoonyesha namna timu ilivyo slow kufanya recovery ya mpira,idadi ya pass zilizokamilika,na hapo ukiangalia vyema tumepiga backpass nyingi na pia uwezo wakupossess mpira ndio hovyo kabisa na mbaya zaidi timu ina vijana ila haikimbii kabisa...na kufanya mashambulizi ni hovyo,angalia idadi ya kona hapo hatuna hata moja,kitu pekee tunachoweza nikucheza rafu nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…