Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Ukiachana na babu Carlo kuna kitu cha ziada hawa kina Vini, Mbappe, Rodrygo, Jude wanaweza fanya na kocha mwingine na labda tuseme ni kocha gani anaweza kufaa Madrid hii yenye pancha nyingi

ni ngumu sana mkuu, ukitizima aina ya uchezaji wao hao jamaa wanne inaonesha wakipata kocha wa high pressing style kama Klopp wanawzeza ku perform vizuri sana, ila taizo lao kubwa wote ni wavivu, na high pressing style haiwezi ku work kwa wachezaji wavivu.
 
nimekukubali sana hapo ulipomjumuisha na Camavinga, dogo ni mchezaji wa kawaida sana, anaimbwa lakin sio level za madrid ila bado kuna viazi hawataki kukubali, madrid ni ufundi mguuni + kazi sio lele mama kama Tchouameni

Moja ya tatizo kubwa la Real Madrid ya sasa ni kuwa timu imejaa overrated players. Wachezaji wa viwango vya kawaida ambao wanachukuliwa wa kiwango kikubwa kutokana na mafanikio ya walioyapata karibuni.
Carlo ame overachieve na hii timu, na ndio limemgaukia anaoneakanwa yeye kuwa eti haendeani na hao wachezaji. wachezaji ambao wengi wao before him they were nothing.
 
Mkuu punguza kuwa emotional, mwaka juzi pia walikosa kombe mwaka jana wakababe.
Madrid asipokua makini msimu huu Barca atamnyanyasa kwenye makombe yote. Sio emotional mkuu huu ndio uhalisia wenyewe timu haichezi kama ina waxhezaji wenye viwango na gharama kubwa. Rodrygo hata kudrible ameshindwa achilia mbali kupata on target
 
Nilikua nafanya tafakari namna kina Ronaldo, Benzema walikua wanatumia uwezo wao kuibeba timu nyakati kama hizi. Leo hii sura za hawa vijana zinaonyesha kuridhika na kila kitu hawaoneshi njaa na uhitaji wa mechi husika. Inaumiza sana na hili shida inatokana na hawa jamaa kushinda makombe makubwa wakiwa na umri mdogo sana.
 

Hii ni good news,mabadiliko ya wachezaji sasa ndio kitu ifuate...tuna watoto wengi ila ni mafather tayar,wanakaba kwa macho na uwezo wao ni average,aje kocha asiyeangalia sura,atayewapa kauli yakiume wachezaji..pale mbele kwa Vin na Mbape lazima mmoja akubali kuwa Ronaldo mmoja Benzema,haiwezekani kila mmoja akataka kuwa CR7.
 
Jana nilijichanganya chaka nililoingia wakawa ni Arsenal watupu. Lahaulaaaa nilijutaaaa. Naishia kuwaota akina Ramos, Pepe, Banzema watu wazima wenzangu. Hawa kinda tuliojaza pale Madrid badooooo
 
👿
 
Kosa ni kuweka hio GIF ama?
Yaan mpira umedundia mbali ..eti ndo limbappe linajirusha penalty za namna hii unazipata kwenye ligi ya nbc chini ya marefa kina kayoko ..mmezoea sana janjajanja hamna Leo out 😂
 
Tusiwalaumu Real kwani hata wangekuwa bora bado wangechezea rungu kipepe kutoka kwa Arsenal.
Jana Madrid walijitahidi sana lakini njo vile!

 
Xabi Alonso akiweka kambi tunarudi kwenye mstari tu, Ila Don Carlo ni mtu sana hii timu kafanya wonders sana na msimu huu pancha nyingi sana sema kongole kwa ze ganaz wameupiga mwingi sana hasa Bukayo yule ni wa kumdaka kabisa ale flank ya juu kule, Anyways twenzetuni hapa wanangu wa Madrid tuburudike na articles za kimpira



Pinkie Football Universe | WhatsApp Channel

Pinkie Football Universe WhatsApp Channel. Football contents (in Swahili) Fun, Knowledge and Exellence🧐 Extra-Football facts combined Our Universe. 11 followers
whatsapp.com
 
Madrid asipokua makini msimu huu Barca atamnyanyasa kwenye makombe yote. Sio emotional mkuu huu ndio uhalisia wenyewe timu haichezi kama ina waxhezaji wenye viwango na gharama kubwa. Rodrygo hata kudrible ameshindwa achilia mbali kupata on target

wengi wao ni overrated sana, kiuhalisia ni wachezaji wa viwango vya kawaida sana
 

yah, mafanikio ya mapema yamewalevya sana
 

I couldn't agree more, mkuu.
 
Spot on mkuu. Baadhi ya wapumbavu humu, hawaumii kwa kupoteza game, bali wanaumia kupoteza dhidi ya Arsenal.

Kwao wakisia Arsenal, basi picha ya kwanza inakuja ni Manchester United 8-2 Arsenal. Wanashindwa kukubali zama zimebadilika.
 
Hiki ndio kitu ambacho kila siku hua nasema.

Timu inaonekana kabisa, Mzee ashakua msimamizi wa mazoezi tu,

Ameshaishiwa mipango vibaya mno atulie kwanza aachie vijana wakimbizane au wazee ambao hawajatumika sana.
 

Attachments

  • Screenshot_20250417-192759_Facebook.jpg
    79.8 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…