Wengi hawaelewi kuwa mpira ni sayansi na how you plan, jinsi unavyoplan ndivyo itavyokiwa most of the times. Wengi walizoea kuiona madrid yenye Galacticos na kipindi hicho Galactico akisajiliwa alikuwa Galactico kweli, from Figo, Zidane, Beckham nk walikuwa wanaipa timu faida either ndani ya uwanja ama nje ya uwanja.
Miaka ya karibuni mpira umebadilika sana, kuna inflation kubwa ya bei za wachezaji. Wengine nadiriki sema hawaana thamani hiyo, yote hiyo imesababishwa na ujio wa waarabu katika soka mf ni PSG na Man City. Ukitaka kushindana nao katika hili hutoweza kamwe, kwani wao wanatumia pesa zinazopatikana nje ya mchezo kufinance sajili na expenses za timu.
Madrid kupitia Perez wameliona hilo tatizo, wameamua kupaki basi na kufanya scouting ya young talents. Hii inaihakikishia madrid kuwa na kikosi kitachokuwa pamoja kwa miaka hata mitano mbele ukizingatia stars wa timu kwa sasa ni aged. Kuanzia Modric, Benzema, marcelo na kiongozi mwenyewe Sergio Ramos wote hawa ni zaidi ya miaka 30. Mbadala wa hawa watu inabidi ufanywe kwa umakini mkubwa sana.
Ndo hapo unapoona kuna wakina asensio, vasquez, mayoral, Vinicius, isco wakiwa tayari kukabidhiwa majukumu ya kaka zao. Hili linakuwa engineered na Julen Lopetegui kwani by CV wengi mmemjua Lopetegui baada ya kufukuzwa national team hapo juzi kati.