Mkutano wa Mendes na Florentino Perez . Rais wa Real Madrid Florentino Perez, msaidizi wake Jose Angel Sanchez na wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes wameripotiwa kukutana usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kujadili hatma ya CR7 ndani ya Estadio Santiago Bernabeu. . Angel Sanchez alimpa Mendes masharti ya kuleta mezani ofa ya 100 million euros ili kupata baraka ya Los Blancos kumuuza Ronaldo na Mendes aliwahakikishia maboss hao wa Madrid kwamba ataileta ofa hiyo - kwasababu Juventus wana utayari wa kulipa fedha hiyo.