Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

Real Madrid (‎Los Blancos) | Special Thread

FT:Bavaria 1 - 2 Blancos

Hala madrid....mtaji mzuri kuelekea second leg...
Shukran sana Mkuu Tall kwa update, team ilionyesha ukomavu mkubwa sana kwa kweli, Zidane aliwaandaa vijana wake vizur sana, wajamaa walivyotangulia nilidhani ningeona ile panic ya akina Ronaldo na Ramos, lakini Leo ilikuwa ni tofauti kabisa, walitulia sana, matunda yake ndio huu ushindi wa Leo...
Kazi bado haijaisha., tunatakiwa tutulie hivyo hivyo next week kwa ajili ya kumaliza kazi... [HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG] ..[HASHTAG]#APorla13[/HASHTAG]
 
Hapa zidane anataka kufanyaje?anamtoa Carvajal anaingia benzema??
Hahaha.., Zidane aliamua kumrudisha Vasquez nyuma., nilidhan alimwingiza Benzema ili tubaki na wachezaji wawili mbele, sababu Vasquez alirudi kama right back, na Asensio alirudi kumsaidia Marcelo.., karibia Benz afunge la, ila jamaa asivyo na shabaha akaenda kumpa golikipa mpira...,
 
hahahahah wazee wa copa del rey aka NDONDO CUP mpo kumbe
R.Madrid anasubiria kipigo cha mbwamwizi kutoka kwa wanazi maana round hii hawana mchezo minaona wamewapelekea wale wazee point za bure tu nibora hata wange ahirisha mechi kuliko kwenda kudhalilika.
 
[HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG]
IMG_20180425_234950_227.JPG
IMG_20180426_002024_117.JPG
 
Jana nilikuwepo nyumbani, lakini nilikuwa siipati JamiiForums takriban kwa saa 24. Nimejarubu kwa kila baada ya muda mfupi, ndio sasa imefunguka. [HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG]
 
Zizou's Pre-Match Presser:

“We like playing here and playing well. We started badly but finished well. They had their chances but we controlled the game”.

“The error prior to the goal is down to all of us. We were not set up well and it was a consequence of errors, not just Keylor.""

"Ribéry was great. In the second half, even with Lucas Vázquez at right back due to Carvajal being injured, we did well down that side. We got a good result”.

Return leg at the Bernabéu
“We will have to fight. We are happy, but we know e have to suffer in the return leg, nothing is sorted yet."

"Isco hurt himself and we brought Marco on in his position. The plan was to have Lucas playing further forward and Isco between the lines, but Asensio put a real shift in and did well defensively."

Carvajal
"He doesn't think that it's anything major, but we'll found out once he undergoes tests back in Madrid".

Marcelo
"Besides the goals he scores, he's a key player in terms of the game plan we look to impose. He's a difference-maker in attack".

Bale
"I have to make choices and I've got some very good players in the squad. There are some players who are performing well at the moment. There are still more games to come and I'll be relying on him. It's not true that I don't play him".



31277553_1971782982846452_4154203145942287004_n.jpg
 
Marcelo (7) has surpassed Sergio Ramos and Dani Alves (6) as the highest scoring defender in the history of the Champions League knockout stage.

31282232_1971418772882873_9161019240767266876_n.jpg
 
Real Madrid ilichukua udhibiti wa nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya awamu ya kwanza kwa kujipatia ushindi katika uwanja wa Allianz Arena.
Mabingwa hao watetezi wanaojaribu kushinda taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo walionekana kudorora katika safu ya ulinzi huku wakiwa na makali katika ile ya mashambulizi kabla ya Marcelo na Asensio kufunga katika kila kipindi cha mchezo.
Marcelo alifunga karibu na eneo la kupiga penalti na kusawazisha kabla ya Asensio kuongeza bao la pili baada ya Rifinha kufanya masikhara hivyobasi kuwapatia bao la ugenini.

Joshua Kimmich alikuwa ameiweka Bayern kifua mbele wakati alipomfunga Keylor Navas.
Mabingwa hao wa Ujerumani walikosa nafasi nyingi za wazi katika hatua ya mashambulizi, huku bao la mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo likikataliwa kwa kuunawa mpira huku ufungaji wake wa mabao katika kila mechi ya vilabu bingwa ukisitishwa.
Bayern sasa watalazimika kufunga mabao mawili Jumanne ijayo ili kuwazuia Real Madrid kufika fainali ya nne katika kipindi cha miaka mitano.

Real wamekuwa wataalam wa kusonga mbele katika makundi ya muondoano katika misimu ya hivi karibuni na ushindi huu ulikuwa mfano mzuri wa matokeo yao.
Tatizo lao la safu ya ulinzi lililowafanya kupoteza 3-1 dhidi ya Juve katika awamu ya pili ya robo fainali lilijitokeza tena katika kipindi cha kwanza na wangejipata nyuma zaidi kabla ya Marcelo kupata bao.
Mkufunzi Zinedine Zidane alifanya mabadiliko baada ya kipindi cha kwanza akimtoa Isco na kumuingiza Asensio lakini mchi hiyo ikaendelea kama ilivyokuwa.
Hatahivyo Rafinha alifanya masikhara na kuwapatia mpira wapinzani karibu na eneo la kati , Lucas Vazquez na Asensio waliupata mpira wakatamba nao kabla ya kumvisha kanzu kipa wa Bayern na kucheka na wavu kwa goli la pili.

Ronaldo hakupata fursa ya kushambulia katika mechi hiyo , ikiwa ni mara ya kwanza kwa yeye kushindwa kufanya hivyo katika kombe la vilabu bingwa tangu Mei 2017.
Alikuwa na fursa mbili ambapo alipiga nje kwa kichwa mbali na mkwaju uliotoka nje.
 
Jana nilikuwepo nyumbani, lakini nilikuwa siipati JamiiForums takriban kwa saa 24. Nimejarubu kwa kila baada ya muda mfupi, ndio sasa imefunguka. [HASHTAG]#HalaMadrid[/HASHTAG]
Mkuu ulipotea sana siku za katikati, karibu tena jamvini.
 
Narudia tena timu pekee ya kumsimamisha real Madrid ilikuwa ni Barcelona tu, hawa wengine wote waliobaki ni tambalale
Mbabe wa barca ni Roma sasa kakutana na dhahama ya salah sasa mnayemuogopa aliugopa msalaba akamsakizia Roma huo ujasiri wa kukutana na dhahama ya salah unautoa wapi?
 
Narudia tena timu pekee ya kumsimamisha real Madrid ilikuwa ni Barcelona tu, hawa wengine wote waliobaki ni tambalale


Nyinyi Hichi Kidomodomo Chenu Subirini Mufike Fainali Halafu Mumuone Huyo Liverpool Munayeona Munakwenda Kujipigia Nyingi

ALICHOWAFANYA LIVERPOOL MWAKA 1981 KWENYE FAINALI NDIYO ATAKACHOWAFANYA MWAKA 2018
 
Back
Top Bottom