RE: Tusi.

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Sio mbaya nikitoa ilmu kidogo.
Watu huwa wanashindwa kutofautisha matusi na maneno ambayo kwa kizungu huiwa 'taboo words', sifahamu Kiswahili chake. Kwa kizungu, matusi huweza kufasiriwa kama 'insults' au 'abusive language/words' na 'taboo words' ni maneno ambayo hayawezi kutamkwa hadharani kwa kuwa yanagusa faragha za watu, mfano maungo ya siri ya binadamu. Kwa fasili za namna hii, tunaona kuwa tusi ni dhana ya kiuamilifu zaidi, yaani ni mpaka lipewe kazi maalumu, nayo ni kukejeli, kudhalilisha au kulenga faragha za mhusika kwa namna isiyopendeza. Haya ambayo tunadai kuwa ni matusi ni sehemu ya leksikoni (jumla ya msamiati wote katika lugha) yetu, na ni haki yetu kuyatumia bila kulenga 'abuses' kwa yeyote.
Sawasawa?
Pia kuna maneno ambayo si 'taboo language/words' lakini yakipangwa vema yanaweza kutumika kama 'insults', mfano, kishazi "...unapakuliwa kisamvu cha kopo.", hakuna 'taboo word' hapo, lakini kishazi chenyewe ni 'insult' ya hali ya juu. Mfano mwingine ni neno 'fu.ck' katika Kiingereza cha Amerika, neno hili linaweza kutumika kama 'insult' au kama neno la kawaida. Tizama uamilifu wake katika "...**** you!" na "...this government ****s big time!"
Kwa leo nikomee hapo, halafu tutizame upya tafauti hizi.
Wakatabahu,
Mphamvu Letsholonyane!
 
Asante kwa kutupa maujuzi ndugu Mphamvu. Tunatarajia mengi zaidi.
 
wewe ni mshenzi wa lugha aisee. asante sana kwa kutuelewesha.
 
Kazana,chomeka bulb,kata n.k....haya nayo si ni taboo lakini hata kabla hayajaingizwa dhana ya kiumilifu tayari mtu anaona ni insults....kwa mfano; unamkuta mtu anahangaika kuchomeka kitu halafu unamwambia "ngoja nikuchomekee" ..tayari anaweka dhana yake ya insults.Tatizo ni ugumu wa lugha au uchafu wa matendo yetu umeathiri hadi lugha? (itafikia kipindi kila neno litakuwa na dhana ya insults)
 
Mphamvu bahada ya kutoka kwenye kibano, unaamua kuja na ufafanuzi huu wa lugha, hauwezi kukuchomoa siku ukija kichwakichwa unakula tena segera.

Kumbuka kuna lugha za matusi na kuhudhi.
 
kumekuwa na lawama nyingi sana kwa lugha ya Kiswahili kuhusu kuharibiwa kwa maana za maneno, wanasahau kuwa si Kiswahili peke yake, hata Kiingereza kina tatizo hilo, chunguza maneno kama 'screw', 'ate', 'blow', 'come', 'jerk' n.k n.k.
Lakini maana mpya huwa amilifu katika muktadha usio rasmi, kwenye muktadha rasmi hakuna tatizo kama hili.
Nitakuja na uzi kuhusu matumizi ya lugha kadiri ya muktadha unaohusika nikihusisha na masahihisho ya BAKITA katika vipindi vya TBC1.
 
Mphamvu bahada ya kutoka kwenye kibano, unaamua kuja na ufafanuzi huu wa lugha, hauwezi kukuchomoa siku ukija kichwakichwa unakula tena segera.

Kumbuka kuna lugha za matusi na kuhudhi.

Mwalimu J. K. Nyerere aliwahi kusema kipindi fulani kuwa wanaofanani kimawazo ni sawa na wafu.
Yale mawazo katika ile thread yenye kichwa, "Sticky: You must read this" yasikufanye ufikiri kama mfu, unaweza kuwa na mafikara yako nje ya mawazo yale na bado yakawa na maana.
Kuhusu ban, siiogopi na sikuwahi kuiogopa, ila nahimiza mabadiliko chanya ya mitazamo humu JF,
sawasawa?
So far nina ban 5 katika mwaka wangu mmoja humu JF, and life goes on!
 
Jamani mnatulazisha tusome kulijto hata akina mwanaashag

usiwe na shaka mrembo,
pitia taratibu bila papara, utaelewa.
Afu si unajua humu hakuna mtihani, elimu kwenu ndio malengo yangu makuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom