Re: Serekali isitishe liseni za uwindaji na usafirishaji wanyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Re: Serekali isitishe liseni za uwindaji na usafirishaji wanyama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by LETIPIPI, Oct 22, 2012.

 1. L

  LETIPIPI Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi kama mzalendo na mzawa wa Tanzania naishauri Wizara ya Maliasili na Utalii kusitisha na kufuta kabisa liseni za Uwindaji na uuzwaji wa Wanyama hai Tanzania. Nchi inatia aibu. Meno ya Tembo kukamatwa nje ya nchi ni kudhihirisha kwamba Tanzania sasa rushwa imekithiri na Serekali imeshindwa kuidhibiti. Hawa wanyama wanawidwa na kampuni za kigeni zenye liseni za kuua wanyama na kuwasafirisha. Hakuna msukuma, Mhaya, Masai anaweza fanya biashara hizi ni Wageni waliowekeza Tanzania. Rais Kikwete tumia mamlaka yako kufuta liseni hizi watu wanakuaibisha. Kwa nini kila kiovu Tanzania.

  Hawa wawekezaji katika Sekta ya uwindaji na uuzwaji wa Wanyama hai inaelekea wanayo fedha nyingi sana kiasi kwamba Jeshi la Polisi na Wizara ya Mali asili wanashindwa kukabiliana nao. Sasa kwa vile Watanzania tulio wengi hatufaidiki na biashara hii na pia kwa vile tumeshidwa kujipanga kukabiliana nao tufute kabisa liseni hizi. Kwa nini wenzetu wa Kenya hawana biashara ya kuwaua wanyama na kuwasafirisha lakini wanaingiza fedha nyingi kwenye utalii wa picha kuliko Tanzania. Serekali iache tamaa za kucheza na rasilimali za Watanzania. Hatufaidiki lolote kwenye kuwaua wanyama, kuwasafirisha na hata kwenye sekta ya madini. Wakenya wanatucheka. Tunaua wanyama au kuwasafirisha kwa sababu zipi jamani Watanzania. Tuingize kwenye Katiba hakuna kuua wala kuuza Wanyama hai Tanzania.
  Mkereketwa
  Lengai Ole Letipipi
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  sawa mkuu.....umesikika.....
   
Loading...