Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Nimechangia hoja moja ya Mzee Mwanakijiji hapa JF kwa kusema. Umiliki wa kadi au kitambulisho cha chama au jumuiya yoyote wakati fikra na moyo wako ziko mbali na hicho chama au Jumuiya ni sawa na kusema....Unamuamini MUNGU wakati unashinda kwa waganga wa Kienyeji kila siku ili ufanikiwe. Dunia ya sasa na hasa Tanzania, inahitaji watanzania au watu watakao kuwa tayari kusimamia ukweli na haki hata kama wanakadi za CCM au CHADEMA. Wazee kama Dr Lweitama, Makwaiya wa Kuyenga nk nina uhakika wana kadi za CCM ila kwa kweli itikadi zao kwasasa ni kama haipo CCM. Wapo na kadi za CCM ila usiku wako na itikadi na mawazo ya kuleta mabadiliko.
Nataka kusema kuwa!!! Kadi au kitambulisho inaweza isiwe ishu kabisa kama itikadi zako hazifanani na chama au jumuiya unayomiliki kadi yake.
Nakubaliana na mawazo ya Ndimara 1000%. Hoja ya Nape na CCM yake haina mashiko
Umbumbumbu mwingine ni wa kujitakia. Jambo liko wazi kabisa na wala porojo za Ndimara haziwezi kujibu maswali ya msingi ambayo ni
1. Kwanini Slaa alindelea kulipia kadi?
2. Katiba ya CHADEMA inakataza waziwazi umiliki wa kadi mbili, je kwanini Katibu Mkuu wa chama awe mwanachama wa vyama viwili kwa siri?
3. Aliposema "akiba haiozi" alimaanisha nini? Kama Slaa amejiwekea akiba hiyo, anamshauri mwana CHADEMA "wa kawaida" ajiwekee akiba gani???
Kama Slaa anaona umuhimu wa kuitunza kadi yake, kwanini amekuwa mstari wa mbele kukusanya kadi za CCM za wenzake na kuzichana na kuchoma moto? Kwahiyo kadi yake yeye iheshimiwe ila za wengine zichomwe moto???
Vilevile, kuwa na kadi ni one thing na kuilipia ada ni another thing. Kuilipia ada ni kumaanisha kuwa Slaa ni mwanachama HAI wa CCM.
Mnaweza kutafuta spin na porojo mbalimbali, lakini wenye akili wameshaelewa kinachoendelea kama jinsi alivyosema Dr. Slaa mwenyewe kuwa "akiba haiozi".
Ndimara!!!!!!!!!!! Ah!!!!!. Yule kada wa CCM?Nivumilie:
Sina kadi ya Tanganyika African National Union (TANU) - chama kilichoongoza wananchi kupigania uhuru. Sikuwahi kukata kadi ya chama hicho. Lakini nina kadi ya Umoja wa Vijana wa TANU (Tanu Youth League - TYL). Nilikuwa mwanachama na mwenyekiti wake nikiwa sekondari, Kahororo. Niliishia hapo. Sikuwahi kuwa na kadi ya TANU.
Sikuwahi kuwa na kadi ya litoto lake CCM. Sikuwahi kuwa na kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM.
Lakini bado nina kadi yangu ya TYL.
Kadi hii bado imewekwa mahali salama. Imefanyiwa uzuderi (lamination) isije kupauka. Itakaa sana. Siichani. Siitupi. Simpi mtu. Ni mali yangu. Acha historia inukuu ushiriki wangu hata katika kuchanga senti 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Vijana, Lumumba, Dar es Salaam ambalo sasa "vijana" wa chama kinachoheshimu na kulinda mafisadi (CCM) wameuza kwa pesa mbili.
Pointi: Kadi ni mali yangu.
Rudi Darasa la Kwanza miaka yetu. Mwalimu anaanza kutufundisha Kiingereza:
This is my book. It is my book. It is mine. Sasa rudi kwenye kadi: This is my TYL card . It is my card. It is mine. Nikitaka kugawa, naigawa. Nikitaka kutupa, naitupa. Nikitaka kuchoma moto, naichoma. Nikitaka kuuza kwenye mnada, naiuza. Sasa kwanini Dk. Slaa asibaki na kadi yake na hata nyingine zozote atakazoweza kuwa nazo (sasa na baadaye) hadi pale atakapotaka kuachana nazo?
Bali mjadala wa "Kadi ya Dk. Slaa" una maana pana. Unaonyesha jinsi viongozi wa chama kilichopanga ikulu kwa miaka 50 wanavyoweza kuacha hoja kuu za kufikirisha mtu binafsi na jamii; na badala yake kujiviringisha na kuviringisha wananchi katika malumbano dhaifu (triviality) ili kupoteza muda na kuondoa akili zao kwenye hoja kuu za wakati tuliomo.
Ndiyo, ni ndoana. Lakini nani ataimeza wakati anajua ni ndoana?
Ndimara.
Mkuu.
Tulia kidogo maana unaonekana una mhemko sana! Haya mambo yanahitaji akili iwe sober na objective ndio tujadiliane. Lakini pia yanahitaji critical thinking and visionary analysis.
1.Una ushahidi kuwa Dr Slaa anailipia/amelipia kadi ya ccm? Kama ndio weka ushahidi twende sawa maana great thinkers hawana tabia ya kuzomoka bila ushahidi.
2. Umesema "katiba ya chadema hairuhusu mtu kuwa na kadi mbili" (sema ni ibara gani acha kuleta majibu ya jumla). Lakini pia naona hapa una maanisha kadi kwa maana ya kadi tu au uwanachama wa chama kingine? (Kumbuka kuwa mtu una ruhusiwa kuwa mwanachama wa chama kimoja tu! Haijasemwa kuwa usiwe na kadi tingine maana walijua kuwa huenda mtu akahama kutoka chama kimoja kwenda chama kingine)
3. Amesemea wapi kuwa hakiba haiozi? Na jee mtu akisema hakiba haiozi akili ya kawaida inakushughulisha kutaka kujua zaidi ya hapo au umeangalia kwa miwani ya kadi peke yake?
Unachotakiwa kukijua.
1. kisheria kadi unayo inunua kwa pesa zako ni mali yako si mali ya chama. Ukihama chama au kuacha kuilipia ni haki yako/ridhaa yako kubaki nayo, kuichoma, kuitupa au kuihifadhi. Hakuna mtu anayeweza kukudai kadi uliyo nunua kwa pesa zako.
2. Kadi ambayo si mali yako ni kama kadi za benk, au kitambulisho cha kazi. Hizi zinakuwa mali ya benki au mali ya waajiri. Ukiacha kazi moja ya sharti kubwa ni kurejesha kitambulisho hicho.
Kama hivyo ndivyo fungua milango yako ya fahamu bila kuwa na chembe ya propaganda na uruhusu tafakuri tunduizi (critical thinking) kichwani mwako.
Karibu kwa hoja.
was it proved kuwa dr iyo kadi anailipia?