Re: Falsafa ya Mzee Ndimara juu ya umiliki wa kadi ya chama kingine

Dec 11, 2010
3,321
6,327
Nivumilie:

Sina kadi ya Tanganyika African National Union (TANU) - chama kilichoongoza wananchi kupigania uhuru. Sikuwahi kukata kadi ya chama hicho. Lakini nina kadi ya Umoja wa Vijana wa TANU (Tanu Youth League - TYL). Nilikuwa mwanachama na mwenyekiti wake nikiwa sekondari, Kahororo. Niliishia hapo. Sikuwahi kuwa na kadi ya TANU.

Sikuwahi kuwa na kadi ya litoto lake CCM. Sikuwahi kuwa na kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM.
Lakini bado nina kadi yangu ya TYL.

Kadi hii bado imewekwa mahali salama. Imefanyiwa uzuderi (lamination) isije kupauka. Itakaa sana. Siichani. Siitupi. Simpi mtu. Ni mali yangu. Acha historia inukuu ushiriki wangu hata katika kuchanga senti 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Vijana, Lumumba, Dar es Salaam ambalo sasa "vijana" wa chama kinachoheshimu na kulinda mafisadi (CCM) wameuza kwa pesa mbili.

Pointi: Kadi ni mali yangu.
Rudi Darasa la Kwanza miaka yetu. Mwalimu anaanza kutufundisha Kiingereza:
This is my book. It is my book. It is mine. Sasa rudi kwenye kadi: This is my TYL card . It is my card. It is mine. Nikitaka kugawa, naigawa. Nikitaka kutupa, naitupa. Nikitaka kuchoma moto, naichoma. Nikitaka kuuza kwenye mnada, naiuza. Sasa kwanini Dk. Slaa asibaki na kadi yake na hata nyingine zozote atakazoweza kuwa nazo (sasa na baadaye) hadi pale atakapotaka kuachana nazo?

Bali mjadala wa "Kadi ya Dk. Slaa" una maana pana. Unaonyesha jinsi viongozi wa chama kilichopanga ikulu kwa miaka 50 wanavyoweza kuacha hoja kuu za kufikirisha mtu binafsi na jamii; na badala yake kujiviringisha na kuviringisha wananchi katika malumbano dhaifu (triviality) ili kupoteza muda na kuondoa akili zao kwenye hoja kuu za wakati tuliomo.

Ndiyo, ni ndoana. Lakini nani ataimeza wakati anajua ni ndoana?

Ndimara.
 
Nimechangia hoja moja ya Mzee Mwanakijiji hapa JF kwa kusema. Umiliki wa kadi au kitambulisho cha chama au jumuiya yoyote wakati fikra na moyo wako ziko mbali na hicho chama au Jumuiya ni sawa na kusema....Unamuamini MUNGU wakati unashinda kwa waganga wa Kienyeji kila siku ili ufanikiwe. Dunia ya sasa na hasa Tanzania, inahitaji watanzania au watu watakao kuwa tayari kusimamia ukweli na haki hata kama wanakadi za CCM au CHADEMA. Wazee kama Dr Lweitama, Makwaiya wa Kuyenga nk nina uhakika wana kadi za CCM ila kwa kweli itikadi zao kwasasa ni kama haipo CCM. Wapo na kadi za CCM ila usiku wako na itikadi na mawazo ya kuleta mabadiliko.

Nataka kusema kuwa!!! Kadi au kitambulisho inaweza isiwe ishu kabisa kama itikadi zako hazifanani na chama au jumuiya unayomiliki kadi yake.
 
kusambaratisha chadema kwa mbinu ya kadi ni wazo la kipumbafu mithili ya wazo la mtu aliyeshauri mtihani wa Hisabati Darasa la Saba iwe ya 'chagua jibu sahihi'
 
Nimechangia hoja moja ya Mzee Mwanakijiji hapa JF kwa kusema. Umiliki wa kadi au kitambulisho cha chama au jumuiya yoyote wakati fikra na moyo wako ziko mbali na hicho chama au Jumuiya ni sawa na kusema....Unamuamini MUNGU wakati unashinda kwa waganga wa Kienyeji kila siku ili ufanikiwe. Dunia ya sasa na hasa Tanzania, inahitaji watanzania au watu watakao kuwa tayari kusimamia ukweli na haki hata kama wanakadi za CCM au CHADEMA. Wazee kama Dr Lweitama, Makwaiya wa Kuyenga nk nina uhakika wana kadi za CCM ila kwa kweli itikadi zao kwasasa ni kama haipo CCM. Wapo na kadi za CCM ila usiku wako na itikadi na mawazo ya kuleta mabadiliko.

Nataka kusema kuwa!!! Kadi au kitambulisho inaweza isiwe ishu kabisa kama itikadi zako hazifanani na chama au jumuiya unayomiliki kadi yake.

Mkuu.
Haya ni maneno mazito sana "Umiliki wa kadi au kitambulisho cha chama au jumuiya yoyote wakati fikra na moyo wako ziko mbali na hicho chama au Jumuiya ni sawa na kusema....Unamuamini MUNGU wakati unashinda kwa waganga wa Kienyeji kila siku ili ufanikiwe. Dunia ya sasa na hasa Tanzania, inahitaji watanzania au watu watakao kuwa tayari kusimamia ukweli na haki hata kama wanakadi za CCM au CHADEMA".

Kuna ndugu zetu ambao huwa ukweli kwao ni msamiati wa kichina hawawezi kuyakubali maneno kama haya maana wanachojua wao watanzania bado wamelala basi! Wakisha waza hilo ndio hupiga deal zao za magumashi kwa kwenda mbele! Wakiulizwa eti "Mbona wenye tuhuma wameshinda ubunge" akili za ajabu kabisa hizi!

Wenzetu Rwanda wametoka kutwangana wao kwa wao lakini wanapiga hatua kubwa za kimandeleao kuliko sisi tunaoimba amani bila kunyumbulisha uchumi wetu na elimu yetu.
 
maneno mazito sana yaliyojaa hekima;lakn kwa akili za magamba watashangaa sana maneno haya maana kwao ukweli unauma siku zote

l
 
Nakubaliana na mawazo ya Ndimara 1000%. Hoja ya Nape na CCM yake haina mashiko

Tena mzee wa watu katoa mifano ya darasa la kwanza! Yaani kashusha mawazo kutoka juu kileleni mpaka kwenye shina la mgomba, mgomba ambao ukizaa ndio mwisho wake, unakufa (sawa na Nape akitoa hoja huwa hana uwezo wa kuisimamia na kulumbana kwa hoja bali huiacha ife kifo cha asili huku akiwa amegaragazwa vibaya).

Wenye akili za kupiga mbizi hawawezi kuelewa shule ya mzee Ndimara.
 
Kama Slaa anaona umuhimu wa kuitunza kadi yake, kwanini amekuwa mstari wa mbele kukusanya kadi za CCM za wenzake na kuzichana na kuchoma moto? Kwahiyo kadi yake yeye iheshimiwe ila za wengine zichomwe moto???
Vilevile, kuwa na kadi ni one thing na kuilipia ada ni another thing. Kuilipia ada ni kumaanisha kuwa Slaa ni mwanachama HAI wa CCM.
Mnaweza kutafuta spin na porojo mbalimbali, lakini wenye akili wameshaelewa kinachoendelea kama jinsi alivyosema Dr. Slaa mwenyewe kuwa "akiba haiozi".
 
Umbumbumbu mwingine ni wa kujitakia. Jambo liko wazi kabisa na wala porojo za Ndimara haziwezi kujibu maswali ya msingi ambayo ni
1. Kwanini Slaa alindelea kulipia kadi?
2. Katiba ya CHADEMA inakataza waziwazi umiliki wa kadi mbili, je kwanini Katibu Mkuu wa chama awe mwanachama wa vyama viwili kwa siri?
3. Aliposema "akiba haiozi" alimaanisha nini? Kama Slaa amejiwekea akiba hiyo, anamshauri mwana CHADEMA "wa kawaida" ajiwekee akiba gani???
 
Siioni mantiki ya ndimara katika hili maana haina majibu ya maswali mama ya kumiliki kadi za vyama viwili na anazilipia zote huku yeye akiwa mstari wa mbele kukusanya za wenzake hadharani
 
Umbumbumbu mwingine ni wa kujitakia. Jambo liko wazi kabisa na wala porojo za Ndimara haziwezi kujibu maswali ya msingi ambayo ni
1. Kwanini Slaa alindelea kulipia kadi?
2. Katiba ya CHADEMA inakataza waziwazi umiliki wa kadi mbili, je kwanini Katibu Mkuu wa chama awe mwanachama wa vyama viwili kwa siri?
3. Aliposema "akiba haiozi" alimaanisha nini? Kama Slaa amejiwekea akiba hiyo, anamshauri mwana CHADEMA "wa kawaida" ajiwekee akiba gani???

Mkuu.
Tulia kidogo maana unaonekana una mhemko sana! Haya mambo yanahitaji akili iwe sober na objective ndio tujadiliane. Lakini pia yanahitaji critical thinking and visionary analysis.

1.Una ushahidi kuwa Dr Slaa anailipia/amelipia kadi ya ccm? Kama ndio weka ushahidi twende sawa maana great thinkers hawana tabia ya kuzomoka bila ushahidi.

2. Umesema "katiba ya chadema hairuhusu mtu kuwa na kadi mbili" (sema ni ibara gani acha kuleta majibu ya jumla). Lakini pia naona hapa una maanisha kadi kwa maana ya kadi tu au uwanachama wa chama kingine? (Kumbuka kuwa mtu una ruhusiwa kuwa mwanachama wa chama kimoja tu! Haijasemwa kuwa usiwe na kadi tingine maana walijua kuwa huenda mtu akahama kutoka chama kimoja kwenda chama kingine)

3. Amesemea wapi kuwa hakiba haiozi? Na jee mtu akisema hakiba haiozi akili ya kawaida inakushughulisha kutaka kujua zaidi ya hapo au umeangalia kwa miwani ya kadi peke yake?

Unachotakiwa kukijua.
1. kisheria kadi unayo inunua kwa pesa zako ni mali yako si mali ya chama. Ukihama chama au kuacha kuilipia ni haki yako/ridhaa yako kubaki nayo, kuichoma, kuitupa au kuihifadhi. Hakuna mtu anayeweza kukudai kadi uliyo nunua kwa pesa zako.

2. Kadi ambayo si mali yako ni kama kadi za benk, au kitambulisho cha kazi. Hizi zinakuwa mali ya benki au mali ya waajiri. Ukiacha kazi moja ya sharti kubwa ni kurejesha kitambulisho hicho.

Kama hivyo ndivyo fungua milango yako ya fahamu bila kuwa na chembe ya propaganda na uruhusu tafakuri tunduizi (critical thinking) kichwani mwako.

Karibu kwa hoja.
 
Kama Slaa anaona umuhimu wa kuitunza kadi yake, kwanini amekuwa mstari wa mbele kukusanya kadi za CCM za wenzake na kuzichana na kuchoma moto? Kwahiyo kadi yake yeye iheshimiwe ila za wengine zichomwe moto???
Vilevile, kuwa na kadi ni one thing na kuilipia ada ni another thing. Kuilipia ada ni kumaanisha kuwa Slaa ni mwanachama HAI wa CCM.
Mnaweza kutafuta spin na porojo mbalimbali, lakini wenye akili wameshaelewa kinachoendelea kama jinsi alivyosema Dr. Slaa mwenyewe kuwa "akiba haiozi".

was it proved kuwa dr iyo kadi anailipia?
 
Nivumilie:

Sina kadi ya Tanganyika African National Union (TANU) - chama kilichoongoza wananchi kupigania uhuru. Sikuwahi kukata kadi ya chama hicho. Lakini nina kadi ya Umoja wa Vijana wa TANU (Tanu Youth League - TYL). Nilikuwa mwanachama na mwenyekiti wake nikiwa sekondari, Kahororo. Niliishia hapo. Sikuwahi kuwa na kadi ya TANU.

Sikuwahi kuwa na kadi ya litoto lake CCM. Sikuwahi kuwa na kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM.
Lakini bado nina kadi yangu ya TYL.

Kadi hii bado imewekwa mahali salama. Imefanyiwa uzuderi (lamination) isije kupauka. Itakaa sana. Siichani. Siitupi. Simpi mtu. Ni mali yangu. Acha historia inukuu ushiriki wangu hata katika kuchanga senti 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Vijana, Lumumba, Dar es Salaam ambalo sasa "vijana" wa chama kinachoheshimu na kulinda mafisadi (CCM) wameuza kwa pesa mbili.

Pointi: Kadi ni mali yangu.
Rudi Darasa la Kwanza miaka yetu. Mwalimu anaanza kutufundisha Kiingereza:
This is my book. It is my book. It is mine. Sasa rudi kwenye kadi: This is my TYL card . It is my card. It is mine. Nikitaka kugawa, naigawa. Nikitaka kutupa, naitupa. Nikitaka kuchoma moto, naichoma. Nikitaka kuuza kwenye mnada, naiuza. Sasa kwanini Dk. Slaa asibaki na kadi yake na hata nyingine zozote atakazoweza kuwa nazo (sasa na baadaye) hadi pale atakapotaka kuachana nazo?

Bali mjadala wa "Kadi ya Dk. Slaa" una maana pana. Unaonyesha jinsi viongozi wa chama kilichopanga ikulu kwa miaka 50 wanavyoweza kuacha hoja kuu za kufikirisha mtu binafsi na jamii; na badala yake kujiviringisha na kuviringisha wananchi katika malumbano dhaifu (triviality) ili kupoteza muda na kuondoa akili zao kwenye hoja kuu za wakati tuliomo.

Ndiyo, ni ndoana. Lakini nani ataimeza wakati anajua ni ndoana?

Ndimara.
Ndimara!!!!!!!!!!! Ah!!!!!. Yule kada wa CCM?
Mkuu tunaitika ndiyo kwa taswira uliyoonesha hapa juu. Lakini kwa kuwa kiukweli sisi wengine hatutaki hata kusikia harufu ya JAMAA WA KIJANI basi ni vizuri kiongozi wetu na kipenzi Dr wa ukweli na wana CDM wote wenye kadi za Magamba wazikabidhi kadi hizo ili zihifadhiwe kwenye maktaba itakayoanzishwa na CDM makao makuu. Hakika tusidharau wingu linaloendelea maana lina athari zake kisiasa. Pili siungi mkono hata kidogo kwa hao wanojiita viongozi wa BAVICHA na matamko yao, ninafahamu chama kina mfumo wake wa kujadili mambo yake hivyo tulitarajia hao jamaa kufuata nidhamu hiyo. Wakumbuke yaliyowapata NCCR mageuzi na baadaye TLP miaka ya 2007 na kuendelea. Tusingependa yatokee CDM. Ni lazima viongozi wawe na nidhamu. Na wajiulize hayo matamko yanamfaidisha nani hasa???
 
Mkuu.
Tulia kidogo maana unaonekana una mhemko sana! Haya mambo yanahitaji akili iwe sober na objective ndio tujadiliane. Lakini pia yanahitaji critical thinking and visionary analysis.

1.Una ushahidi kuwa Dr Slaa anailipia/amelipia kadi ya ccm? Kama ndio weka ushahidi twende sawa maana great thinkers hawana tabia ya kuzomoka bila ushahidi.

2. Umesema "katiba ya chadema hairuhusu mtu kuwa na kadi mbili" (sema ni ibara gani acha kuleta majibu ya jumla). Lakini pia naona hapa una maanisha kadi kwa maana ya kadi tu au uwanachama wa chama kingine? (Kumbuka kuwa mtu una ruhusiwa kuwa mwanachama wa chama kimoja tu! Haijasemwa kuwa usiwe na kadi tingine maana walijua kuwa huenda mtu akahama kutoka chama kimoja kwenda chama kingine)

3. Amesemea wapi kuwa hakiba haiozi? Na jee mtu akisema hakiba haiozi akili ya kawaida inakushughulisha kutaka kujua zaidi ya hapo au umeangalia kwa miwani ya kadi peke yake?

Unachotakiwa kukijua.
1. kisheria kadi unayo inunua kwa pesa zako ni mali yako si mali ya chama. Ukihama chama au kuacha kuilipia ni haki yako/ridhaa yako kubaki nayo, kuichoma, kuitupa au kuihifadhi. Hakuna mtu anayeweza kukudai kadi uliyo nunua kwa pesa zako.

2. Kadi ambayo si mali yako ni kama kadi za benk, au kitambulisho cha kazi. Hizi zinakuwa mali ya benki au mali ya waajiri. Ukiacha kazi moja ya sharti kubwa ni kurejesha kitambulisho hicho.

Kama hivyo ndivyo fungua milango yako ya fahamu bila kuwa na chembe ya propaganda na uruhusu tafakuri tunduizi (critical thinking) kichwani mwako.

Karibu kwa hoja.

Kumbe hujui unachoongea.
Akili yako imeshapumbazwa na ushabiki. Pole sana...
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom