RC wa Kilimanjaro, Meck Sadiki na Majaji wawili Wajiuzulu. Rais Magufuli aridhia...

Meck sio mtu wa ovyo kama unavyodhani.. Huyo amepita mikoa migumu kama Mtwara na Lindi enzi zile za Mkapa huko kukiwa ni mafichoni mwa nchi. Kingine kama ni ukwasi anao wa kutosha tu, Kilimanjaro ilikuwa sehemu yake sahihi ya kupumzika sababu ni Mkoa wenye hali nzuri ya hewa, ulishaendelea hivyo changamoto ni chache na una watu wanaojielewa.. Meck kuna upuuzi tu umumuuzi ndio maana ameamua kuachia ngazi..
sawa mkuu
 
Kati ta Ma -RC waliokuwa na weledi, utashi na hekima za kiutawala ni Meck Sadick. Nahisi amekwazwa na huwa huyu baba hapendi unafiki. Tunamtakia maisha mema mzee wetu.
 
Kilimanjaro kuna nini mpaka Mecky Sadiki aburuzwe?
Mzee anataka kuwa karibu na wajukuu zake hapa Dar!
Ngoja ipelekwe damu changa kilimanjaro akanyooshe mkoa, type ya Makonda, Gambo ndo watafiti ule mkoa.

una akili za kibashite, sentensi ya kwanza unasema Moshi kuna nini mpaka aburuzwe,
alafu senteni ya pili unasema damu changa inapelekwa moshi kunyoosha mkoa, sasa sehemu ambako hamna kitu analetwa mtu kunyoosha nini??

Ngoja nikuibie siri ndogo tu, kwenye kikao Ikulu ndogo Mecky Sadiki alisoma taarifa yake ya mkoa baadaye Baba Bashite akaipinga taarifa hiyo na kusema yeye ana vyanzo vyake anaviamini eti anajua yaliyosemwa na Mecky Sadiki ni uongo.
Sasa Meck Sadick amebwaga kazi muwekeni huyu mnayemuamini.
 
Hamkosagi la kusema.... Kujiuzulu kuna sababu nyingi na zingine ni binafsi na sio lazima kila kitu kiwekwe hadharani. Mzindakaya alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya, Sadiki nae ana sababu zake ambazo sio hizo unazojaribu kuzishabikia hapa..... Kila jambo mnaingiza siasa na kuchochea. Hovyooooo
Hovyooo mwenyewe, koma kunizoea, tafuta mwanaume mwingine wa kumzoea
 
mzee Meck Sadick juzi tu siku ile ya mei mosi alionekana ana furaha sana na akitoa hata maombi mbalimbali ya mkoa wake kwa rais iweje leo ajiuzulu alafu wote watatu wajiuzulu ndani ya siku moja?
natabiri RC mpya lazima atakuwa mtu wa kanda ya ziwa au nyanda za juu kusini.
 
Huyo Upendo ana kashfa ya kula mlungula kwa kesi za watu wa "unga"
Acha kumpaka Matope Jaji wetu mwanamke msomi. Nadhani ni sababu za Kiafya hasa baada ya kuondokewa na Mwanae Mpendwa kwa kifo cha utata huko Malaysia mwaka 2012. hata hivyo kupumzika ajira ni vizuri baada ya kulitumikia taifa muda mrefu.
 
Mzee Meck sadiki kuna kitu kimemuuzi sana, sio bure maana yule mzee ana busara na hekima sana
Inasemekana
Meck Sadick waliitwa kwenye kikao kilichowakutanisha mkuu wa mkoa wa manyara, Kilimanjaro na Gambo, kujadili pesa za Rambi rambi zipangwe vipi kimatumizi na kuwapa wafiwa, uliibuka mtafaruku baada ya Mrisho Gambo kufuata maelekezo alopewa toka juu kwamba pesa zisiende.zote kwa walengwa kitu ambacho nafsi ilimsuta sana Meck wa Sadick na taswira itakayokuwepo siku tatu zilozofuata ndio akaamua kuandika barua kuomba kuacha kazi(automatically ) kujiuzulu.
 
Meck Sadik siku ya mei mosi alichomekea suala la viwanda kufa ktk mkoa wa Kilimanjaro. Kitu kilichotafsiriwa kama ni kumpangia Sizonje. Na Sizonje alishasema "mimi huwa sipangiwi",basi kamuamuru ajiuzuru mara moja.
 
Hongera sana
Sasa hivi ukiwa kiongozi huwezi toa uamuzi wakama kiongozi zaid ya kupangiwa bora mmeepukana na hilo
 
Back
Top Bottom