RC Singida waombe radhi wananchi wa Singida

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Mkuu wa Mkoa wa Singida, kwa kuwa leo unafanya mkutano na wakaazi wa Singida mjini, pale viwanja vya Stend ya Zamani. Kwanza asante kwa kuitisha Mkutano, tunaomba kama una ujasiri kweli wa kuita mkutano uwaombe radhi wana Singida kwa kujipatia tenda ya Kuzoa Taka katika Manispaa wakati haujamiliki hata toroli la kuzolea Taka.

Uliingia Ubia na Mkurugenzi mkawa mnatumia gari ya Halmashauri na kujaza mafuta kwa pesa ya Halmashauri wakati inaonekana pesa ulikuwa unakwapua wewe kwa kutumia kampuni ya (PAVICO Ltd) (Perseko Vincent Kone) na kuonekana umeshinda tenda ya kuzoa taka. Uliwalazimisha madiwani kukubali ufedhuli huu.

Kama hiyo haikutosha uliposhindwa hiyo kazi umelalamikiwa na wafanyakazi wa Kampuni yako, na Mtoto wako alijichukulia madaraka mikononi kuwamwagia sumu vijana wetu wa Singida. Kesi imefunguliwa Polsi, mkaamua kuifuta haraka pamoja na fomu za daktari kuonyesha kuwa wamedhuriwa na sumu, sasa mmewatisha vijana wa watu.

Tunazidi kukuambia kuwa damu ya wana Singida itakulilia. Na kwa kuwa Kikwete anajidai hajui haya mabaya unayotutendea ndo maana amekubakiza ila yote yana Mwisho na Mungu hata Singida yupo. Ukiweza omba radhi leo....................
 
Ni tatizo sana, lakini kwa kuwa watanzania tunafanya utani na maisha yetu, wapo watu wanaotukana wenzao hata hapa kwenye JF. Ila mimi nimeziona hizo PF3 za waliomwagiwa sumu zikisomeka hivyo hivyo. Kijana aliye na coppy za hizo form anapatikana. na tenda inayotajwa hapo tunaijua sisi wa Singida ni zabuni LGA/115/smc/2011/2012. Uovu uliopo katika sakata hilo unawezekana Tanzania tu. Kwingine haiwezekani.
 
Kwa ujeuri wala hataomba radhi maana wala haoni alilokosea. Mnachotakiwa ni kusema wazi hayo mabaya mnayodai wananchi wayajue.
 
Maadili ya Utumishi wa Umma, kwanza kuomba tenda katika mkoa ambao wewe ni bossi, halafu tenda isitangazwe, halafu ukashinda wewe peke yako, bahati mbaya hana sifa. Aliomba kuzoa taka, hana hata mkokoteni, halafu akashinda. Mji ukawa mchafu. Nani angeweza kumwajibisha yeye? Hadi Kikwete aingilie kumwambia acha? Madiwani wa Singida mjini na Meya wao na Mkurugenzi mlivumiliaje hili? Kashfa hii inatosha kwa Mzee Mwenye busara kusema samahani, au nang'atuka. Ila asiposema hivi ni jeuri kama mtoto wake aliyemwagia vijana sumu, kisha kwenda kuwatishia polisi na kufunga faili harakaharaka. Wanaharakati fikeni huko, Ukoloni unataka kuja tena
 
singida ni wabishi sana acha waonje joto ya jiwe.
mnashangaa pavico?
anben,arusha kuna kampuni ya ya kukusanya ushuru wa parking haijasainishwa mkataba imeshaanza kazi na ni mali ya mwenyekitiwa halmashauri ya moshi vijijini.

peter machine alikuwa na lori lililokuwa linabeba taka hapo mjini mji ulikuwa msafi.
 
Ah kwa kweli inatia hasira sana, hayo ya singida ni punje tu kati ya sahani ya ubwabwa!
Ila kinachotia hasira zaidi ni kuona maisha yanaendelea tu kama kawaida....
Mafedhuli wanapeta tu na raia wema wanaonekana walalamishi...
 
Jana nimemkuta mwenyekiti wa tarafa yangu anatumia pikipiki ya ofisi kubeba abiria, mimi kama raiya wa tarafa husika nilimpa angalizo ila najua ataendelea na biashara yake kwa usafiri huu wa ofisi lakini najiona mwepesi na hasira zangu zimepungua kidogo kwa makofi niliyomtandika jana baada ya kumkamata.
 
Maadili ya Utumishi wa Umma, kwanza kuomba tenda katika mkoa ambao wewe ni bossi, halafu tenda isitangazwe, halafu ukashinda wewe peke yako, bahati mbaya hana sifa. Aliomba kuzoa taka, hana hata mkokoteni, halafu akashinda. Mji ukawa mchafu. Nani angeweza kumwajibisha yeye? Hadi Kikwete aingilie kumwambia acha? Madiwani wa Singida mjini na Meya wao na Mkurugenzi mlivumiliaje hili? Kashfa hii inatosha kwa Mzee Mwenye busara kusema samahani, au nang'atuka. Ila asiposema hivi ni jeuri kama mtoto wake aliyemwagia vijana sumu, kisha kwenda kuwatishia polisi na kufunga faili harakaharaka. Wanaharakati fikeni huko, Ukoloni unataka kuja tena

For sure, if ours is a goverrnment of transparency, the RC should be punished/taken to tasks.
Howevewr, as I saidi before, hakuna kitakachotokea, mtaniambia
 
what evidence have we collected!?? if we want to go forward we must be focused..! othewise ni kutwanga maji kwenye kinu..!
 
Back
Top Bottom