RC Shigela: Marufuku Mtanzania kupimwa Corona nchini Kenya kama ukishapimwa Tanzania. Itawaletea matatizo ya ubongo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela amekutana na kufanya mazungumzo na madereva wa Tanzania katika mpaka wa Tanzania na Kenya Horohoro kwa lengo la kupata suluhisho la mgogoro kwa madereva hao kuzuiliwa kuingia Nchini humo.

Amepiga marufuku madereva wa Tanzania kupimwa virusi vya corona nchini Kenya, baada ya kuwa wamepimwa hapa nchini, kitendo kinachoweza kuwasababishia matatizo ya upungufu wa akili na kuathiri ubongo kwa kuchokonolewa kila baada ya siku 14.

Shigela amewataka Wamiliki wa magari kuajiri madereva wawili ili waweze kupokezana kwa lengo la kupunguza changamoto za usumbufu wa upimaji wa virusi vya corona.

 
Kupimwa Kenya ni lazima...

Maana serekali ya Tanzania imesema haina wataalau madhubuti wa kupima corona katika ile taarifa ya tume ya uchunguzi ya maabara ya taifa.

Sasa kama mmetangazia ulimwengu kuwa hamna wataalamu wa kupima kosa ni la nani? Nyie wenyewe mmeshawaaminisha kuwa majibu ya huku hayaaminiki...mnataka waamini hivyohivyo?

Nataka msimame mseme tunao wataalamu na mtuambie walipata wapi trainings,Zaidi ya hapo muache kula matapishi yenu kwa mataarifa ya kupika.

Taarifa nyingine mnawaaminisha watu hakuna tatizo ,hao mnaowaita wapiga kura ,wameacha kuvaaa barakoa na kunawa,panda daladala ujionee.

Lakini ninafurahi kuna watu wengine akili zinawarudia maana wakiingia hospitali kama huna barakoa unafukuzwa kama paka,maana hosipitali sio kituo cha kupiga kura. kama ninyi ni wanaume kweli pigeni marufuku uvaaji wa barakoa mahosipitalini.

Endeleeni kuwadanganya wapigakura maana wao walizaliwa kupiga kura tu hawana hata uwezo mdogo tu wa kujiamulia mambo yao binafsi ya msingi.
 
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella amepiga marufuku kwa maderva wa malori wa Tanzania kupimwa vipimo vya virusi vya corona pindi wanapovuka mpaka wa kuingia nchini Kenya kupeleka bidhaa mbalimbali

Shigella amesema hayo leo Juni 17 , 2020 alipokwenda kutembea kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya (Upande wa Tanzania) na kudai kuwa kitendo cha kupimwa kinaweza kuwasababishia matatizo ya upungufu wa akili na kuathiri Ubongo kwa kuchokonolewa kila baada ya siku 14.

Akinukuliwa na kituo cha radio cha East Afrika amesema tayari madereva hao wanakuwa tayari wameshapimwa upande wa Tanzania na hakuna haja ya kuwapima tena wanapovuka mpaka huo na kwenda Kenya.

Capture.PNG

======

MY TAKE:
Wakinyanyuka, sisi tunakaa, adui muombee njaa.
 
Anamaanisha nini?.

Suala la madereva wa Tz kupimwa Covid wakiingia Kenya ni suala la taratibu na sheria za Kenya, RC wa Tz hawezi kuwapangia Wakenya cha kufanya. RC wa Tz awapangie watu wake tena huko huko kwenye mkoa wake tu.
 
Anamaanisha nini?

Suala la madereva wa Tz kupimwa Covid wakiingia Kenya ni suala la taratibu na sheria za Kenya, RC wa Tz hawezi kuwapangia Wakenya cha kufanya. RC wa Tz awapangie watu wake tena huko huko kwenye mkoa wake tu.
Kwamba kila mtu apimwe kwao, hayo ndio makubaliano, hatutaki uhuni.
 
Tanzanians thought we would be dead buried due to hunger by now, Ethiopia and Uganda is taking those opportunities
 
Hahahaa!!jamaa wameona pande hizi watu wanadunda tu, si wao walisema tutakufa kisa wao ndio wanatulisha..

Jamaa kakosa hoja akaona aibue tena ishu, lkn ninavyowajua viongozi wetu sidhani km atajibiwa
Hahahaha, tayari njaa imeanza kuwachapa.
 
Mpaka huo ufungwe tu tena haraka sana , Kenya waendelee kufaidika na COVID19. Huku kwetu hakuna hiyo mambo!.
 
Tabu yote ya nini wakati ukitoa 2000 ya Kenya unaandikiwa huna corona unapita bila tabu,wakati mwengine mnapenda kufanya mambo kuwa magumu wakati ni rahisi tu.
 
Sijajua anapigaje marufuku jambo linalofanyika nje ya mipaka ya nchi. Au awashauri madereva wakatae kupimwa! Tusilazimishe wengine wawe na matendo kama yetu kwenye swala la corona. Kama hatuna corona tena, woga wa kuthibitisha hilo unatoka wapi?.

Kukataa kupimwa maana yake mwisho wa safari umefikia hapo!.
 
Hahahaa!!jamaa wameona pande hizi watu wanadunda tu, si wao walisema tutakufa kisa wao ndio wanatulisha..

Jamaa kakosa hoja akaona aibue tena ishu, lkn ninavyowajua viongozi wetu sidhani km atajibiwa
Hamna wa kujibizana na makalb hayawan wenye fikra duni.
Maisha yaendelea.
 
Back
Top Bottom