RC Morogoro: Marufuku kuuza mahindi mabichi

Upuuzi ndo huu.

Wakati wa kulima walikuwa wapi hadi waje kuwapangia watu jinsi ya kutumia mazao yao?

Nyie Vitoto mlikuwa mnadanganywa
Kuwa Awamu ya kwanza ilikuwa ni Awamu ya Asali na Maziwa!
Enzi hizo hata kitu au zao gani ulime ni uamuzi wa Serikal sio Wewe Binafsi!
Ikiamriwa ulime zao la Biashara Wewe ukalima la Chakula unakutana na Serikal ya Tanu

Moja ya vitu anavyonifurahisha sana JPM ni kurudisha zile Nginja nginja za Nyerere tulizokuwa tunazililia kinafki
 

Jomba hueleweki unasimamia nini, watu wanapinga hiyo tabia ya mkuu wa mkoa kupangia wauzeje mazao yao. Huyo Nyerere unayemtaja ndio watu waliochangia wakulima wa nchi hii kuwa masikini. Sasa hivi tumetoka kwenye kilimo cha biblia(mvua) tumehamia kwenye drip irrigation na umwagiliaji mwingine. Kabla ya kulima tunaangalia soko linataka nini na sio mkuu wa mkoa anataka apateje sifa. Akitaka kulima hayo ya unga hata yeye anaweza ili ajipatie sifa zaidi badala ya kupangia ya wanaume wenzake kwa hela zao. Hatulimi kama wakulima wa zamani tunalima kibiashara tena kwa kupima udongo kwanza.
 
Hivi mkulima si ana haki ya kuuza kile alichokipanda anavyotaka mwenyewe
 

Pamoja na Mbwembwe zote za kufikirika ulizotaja ikitokea Mvua kuchelewa, Ukame mnailaumu Serikali!
 
Hii haikubaliki, kama mkulima anapata faida akiuza yakiwa mabichi hicho ndicho anachohitaji
 

Nyerere alikuwa "socialist" mjaaa asiejitambua na ndio maana Tanzania imefiia hapa ilipofikia,Nyerere nchi limshinda hilo alikubali mwenyewe....

Je unakumbuka yale mashimo ya barabarani ilikuwa inachukua siku mbili kufika Morogoro kwa gari,inachukua wiki kutoka Daresalam mpka mwanza dereva alikuwa apitie Uganda ndio ageuze halafu aje Mwanza, Don't glorify Nyerere,sasa wewe unaona kitu cha busara baada ya mkulima kumiza mgongo halafu unakuja kumpangia nini afanye kwa alichokivuna....

IQ ya mtanzania halisi ni kama zako ndio maana nchi haiendi mbele
 

Nani alikudanganya Nyerere alikuwa Socialist?

Huwezi kuwa Mjamaa at the same time ukawa Mkatoliki bora mpaka kufiriwa kupewa Utakatifu!


Wanafiki ni Nyie wakat wa Jk, Mzee Mkapa na Mwinyi mlikuwa mnasema mnataka Rais Kama Nyerere sasa kapatikana mnakimbia kivuli chake!

Pakitulia kidogo tutamkumbusha Magu alete pia Azimio la Arusha Muone Upumbavu wa lile Azimio maana Wanasiasa Uchwara Kama kina Mbowe kila Siku wanajifanya kuulizia Azimio la Arusha bila ya kujua Azimio halitaki Wanasiasa Matajiri na Mbowe ni Mwanasiasa Tajiri
 
Pamoja na Mbwembwe zote za kufikirika ulizotaja ikitokea Mvua kuchelewa, Ukame mnailaumu Serikali!

Dogo elewa serekali inalaumiwa kwenye muktadha gani. Serekali ilipaswa inunue mazao kwa bei nzuri ili watu wasiuze mahindi mabichi. Badala yake serekali inaishia kukopa wakulima achia mbali kulipa bei ndogo na kwa muda inaotaka. Lawama zinaelekezwa kwa serekali kwa kutotimiza wajibu wake wa kununua akiba ya kutosha toka kwa wakulima kwa bei nzuri na kulipa kwa wakati. Sio serekali haitoi pembejeo kwa wakulima wakati wa kuandaa na kutunza mazao muda wa kilimo bali inajitokeza wakati wa mauzo.

Kero hii niliiona katibu mkuu wa ccm alipinga maofisa wa serekali kutoingilia wakulima muda wa mauzo kama serekali haikutoa msaada wowote wakati wa kilimo. Nimegundua wakati ule aliongea hilo akajifanya ana uchungu kwa kuwa ilikuwa inakaribia uchaguzi, vinginevyo atoke leo hadharani au uvunguni amtake mkuu wa mkoa kubatilisha amri hiyo ya kionevu.

Rais pia nimemsikia kwa masikio yangu akitaka wakulime wauze mazao yao kwa bei ghali ili anayeona ni ghali kununua basi akalime ya kwake. Kwa maneno marahisi alimaanisha kila mtu auze apendavyo na utashi wake bila kuingiliwa ili mradi afikie malengo yake.
 
Pamoja na Mbwembwe zote za kufikirika ulizotaja ikitokea Mvua kuchelewa, Ukame mnailaumu Serikali!
Serikali inalaumiwa kwasababu imeshindwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji wakati nchi ni ya pili kwa kuwa na maji mengi Africa.
 
Mimi mahindi yangu nimelima kwa lengo la kuuza yakiwa mabichi,mtu anaibuka tu nisiuze!kabla sijaanza kulima kwanini hakuniuliza?mambo mengine kuchoshana tu.
 
haya ndo madhara ya kuongozwa na watu ambao hawajaenda shule yan mtu amelima shamba lake,haujamsaidia hata pembejeo alaf unampangia matumizi ya alichokivuna,,inasikitisha sana.
 
Yaani viongozi wengine sijuhi wanaishi dunia ya ngapi..??
Mtu kasota hali ngumu ya maisha hadi kaamua kulima.. Kutafuta mbegu.. Kupanda.. Kupalilia.. Kuhamia wanyama/ndege waharibifu alafu leo anataka auze walau apate ahueni bado anazuiliwa..!?!?

So stupid... Hivi hawa hawajuhi kuwa wengine mahindi mabichi ndo chakula wakipendacho..?!?

Alafu kuna wengine tunakodisha mashamba kwa ajili ya kulima na kuuza mahindi mabichi... Sasa akipiga marufuku tutaenda kula kwake..!?!?

So stupid... Very stupid..!!

[HASHTAG]#madarakayakulevya[/HASHTAG]
 
Duuh kulima nilime Mimi matumizi unipangie wewe
 
Huu ni ujinga wa wawaafrika,hivi mahindi mabichi yanatumika kurembea harusi au yanaliwa,kama yanaliwa hasara iko wapi?makavu yanaliwa na mabichi yanaliwa,huyu akapimwe akili,mahindi nilime mimi ili nikayauze mabichi halafu useme nisiyavune,basi na maharage mbichi yasiuzwe yataleta njaa,au zuia watu wasikoboe mahindi wasile makande,mkulima siyo mtumwa wa mtu anastahili uhuru wa kuuza mahindi yake anapoona yanafaida,nyie na kiongozi wenu simlisema hamtatoa chakula cha bure? leo kinacho wakera ni nini?
 
Wakuu wote wa mikoa ni majanga

Ova
 
Mkuu tusipangiane tafadhali, we mshahara wako ukinywa bia tunakulaumu acha na sisi mahindi yetu tuchome
 
Hii ni desturi...... Sidhani kama desturi inaweza kuondolewa na matamko ya kisiasa!!!
 
Ndifwa ndeng'une maweeeee Matsebele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…