buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 147
Mwandishi wetu, Manyara
Siku chache baada ya Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Milya na mkuu wa mkoa huo kushutumiana kwa rushwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) imewaita ofisini.
Ole Milya na Mnyeti walishutumiana hivi Karibuni mbele ya Waziri wa madini, Dotto Biteko wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya migogoro ya mipaka baina ya Tanzanite One na wachimbaji wadogo.
Katika shutuma hizo Ole Milya alimtuhumu hadharani Mnyeti kupokea rushwa kutoka kampuni ya Tanzanite One kwa lengo la kuwakandamiza wachimbaji wadogo huku akihoji ukaribu wa kiongozi huyo na wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Hatahivyo, Mnyeti naye alimtuhumu Ole Milya kuwatishia kwa silaha ya moto (bastola) baadhi ya wafanyabiashara wa madini mkoani humo huku akienda mbali na kudai kwamba ana kesi tano ambazo zimewasilishwa mezani kwake zinazomhusu.
Taarifa kutoka Takukuru zinadai kwamba viongozi hao wameitwa mnamo Agosti 6 mwaka huu katika ofisi za Takukuru mkoani Manyara ili waweze kutoa maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo.
Hatahivyo taarifa zinadai kwamba tayari mkuu wa wilaya ya Simanjiro mkoani humo, Zephaniah Chaula ameanza kuwapigia simu baadhi ya wafanyabiashara kwa agizo la Mnyeti ili wajitokeze mbele ya Takukuru kutoa maelezo kwamba walitishiwa silaha na Ole Milya.
Hatahivyo, Takukuru pia inachunguza taarifa kuhusu utajiri wa Rc Mnyeti aliojipatia ghafla akiwa mkuu wa mkoa wa Manyara na endapo mali hizo ameziorodhesha Serikalini katika orodha ya mali anazomiliki.
Miongoni mwa mali hizo ni hoteli ya kitalii anayojenga kanda ya ziwa, shule ya sekondari, klabu ya soka ya Gwambina FCpamoja na mabasi mbalimbali ya kusafirisha abiria.
Mwisho.