Job description wanazopewa zinapimika na zimekaa vizuri?
Kuna wafanyakazi wa kutosha kiasi kwamba mtu hachoki kufanya kazi na kupelekea UTENDAJI na UFANISI wake kushuka?
Kila mkuu wa taasisi ya Serikali anajua vyema malengo,Vision na mission ya taasisi anayoiongoza na ana team nzuri ya uongozi ya kufikia malengo hayo.
Je,taasisi zina wafanyakazi bora,wanaopata stahili zao kwa wakati na wenye elimu,weledi na spirit ya kazi katika mazingira ya kujisimamia pasipo pressure ya uongozi na wenye ubunifu?
Taasisi binafsi huwa wanafanya recruitment kwa wafanyakazi wapya katika taasisi au serikalini,je kabla ya kupewa majukumu hayo yanafanyika kwa ufanisi.
Tusilaumu,watu wengi wameajiriwa hovyo hovyo tu kwasababu za ukabila,ukanda,dini na jinsia bila kuzingatia taaluma,weledi na uzalendo wa kazi.