RC Makonda, hawa Polisi siyo wapanda miti

RC Makonda, hawa Polisi siyo wapanda miti

sirjohn

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
767
Reaction score
679
IMG-20160924-WA0081.jpg

Mh. mkuu wa mkoa Makonda..tafadhali waache Jeshi la Polisi wafanye kazi yao moja mhimu na kubwa ya kutulinda sisi na mali zetu.

Hili swala la mazingira nenda taasisi zinazohusika kuhamasisha, ndiyo tunakubari polisi ni sehemu ya jamii lakini kwa nin mnawabebesha kila mzigo! Hivi unajua kazi ya kulinda raia na mali zake inahitaji concentration! why mnawayumbisha hawa mapolisi kwa hali hii ujambazi utaisha kweli..

For sure utakuta polisi wote wameoewa taarifa ya mazingira hiyo trh 01 oct. so wamehamisha akili zao zote huko na kuwacha kuwaza kazi yao ya kulinda raia na mali zao..leo polisi analala anawaza mazigira badala ya kuwaza kupambana na kuzuia uhalifu nchini. kwa hali hii tusitegemee ujambazi kuisha nchini.

Mbona zipo taasisi na NGOs nyingi sana zinaweza kutumika kuhamasisha uoandaji wa mazingira lakini ninyi kila siku kiguru na njia kwa mapoli..

Poleni sana mapolisi kwa kutojitambua na nimesikia wanakuja kuwakagua vyeti ila JWTZ wamepangiwa taratibu nyingine ya ukaguzi..akili za kongota...
 
Hiyo ndio kazi yao acha umbeya wako, sasa ulitaka wafanye nini wakulinde wewe mlalahoi una kitu gani cha kukulinda nacho?

Kalagha baho....
 
Fikiria nje ya box, mbona husemi kwamba hii inaweza kuwani ni njia mojawapo ya kuwapatia chochote kitu!!?? Baada ya shughuli hio mfuko utajaa kidogo...
 
Hahahahahaaaaaaa! CHADEMA wakiona hivyo roho zinawauma sana
 
Huyo askari wakike wapili kutoka kushoto ndo kanichekesha sana na hiyo staili ya ukaaji wa miguu eti nae askari
 
watajua wenyewe bwana,maana hao wao wanatiigi kila kitu,kikubwa kimetamkwa na watawala,wakulinde ww kama nani,maana kwa mantiki ya kawaida huwez tumikia mabwana wawili,mwenyewe upande miti....mwenyewe ulinde usalama wa raia
 
Sasa wewe unataka kurusha ngumi huku wenyewe wamekubari mkuu??? Tena na pozi la picha wameweka.

Na ole wao nisiwaone hiyo siku.
Huku ulinzi unawasubiri.
 
Fikiria nje ya box, mbona husemi kwamba hii inaweza kuwani ni njia mojawapo ya kuwapatia chochote kitu!!?? Baada ya shughuli hio mfuko utajaa kidogo...
Kama serikali inaona wanastahili nyongeza ya mshahara si wafanye hima kuwaongezea? Unamaanisha kuwa wameamua wawapigishe deiwaka ya kupanda miti ili wapate chochote kitu?
 
Hizi kazi zinazokwenda kwa amri tatizo lake ndo hilo. Hakuna kuhoji ni kutii amri. Japo kila kazi ina mipaka yake
 
Hivi hakunaga maadili ya ukakamavu katika jeshi hili?!?, maafisa wako kilegevu na pozi kama raia ilhali wako na sare za jeshi, ingekua China hawana kazi, North Korea tayari mazishi yao na mamba wameshashiba
 
Polisi na wanajeshi utawala huu wamegeuza ni majeshi ya kulinda mazingira.kilichobaki tujilinde wenyewe maana wananchi tumegeuzwa waasi na majambazi.
 
Askari Polisi ni mtu nafuu Sana kumpata hata katika mambo ya kipuuzi kwa kuwa yeye kajengwa katika msingi wa kutii amri yoyote hasa inayotolewa na boss wake,ndiyo maana Ina kuwa rahisi kwa Makonda kuwaagiza chochote na kikatekelezwa Kama anavyo taka tofauti na raia au mtu wa mitaani ambaye Ili atekeleze maagizo wakati mwingine itabidi nguvu itumike ndiyo maagizo yatekelezwe.
 
Hivi pale Kariakoo na Magomeni watapanda miti kwa wapi?
 
View attachment 406355

Mh. mkuu wa mkoa Makonda..tafadhali waache Jeshi la Polisi wafanye kazi yao moja mhimu na kubwa ya kutulinda sisi na mali zetu.

Hili swala la mazingira nenda taasisi zinazohusika kuhamasisha, ndiyo tunakubari polisi ni sehemu ya jamii lakini kwa nin mnawabebesha kila mzigo! Hivi unajua kazi ya kulinda raia na mali zake inahitaji concentration! why mnawayumbisha hawa mapolisi kwa hali hii ujambazi utaisha kweli..

For sure utakuta polisi wote wameoewa taarifa ya mazingira hiyo trh 01 oct. so wamehamisha akili zao zote huko na kuwacha kuwaza kazi yao ya kulinda raia na mali zao..leo polisi analala anawaza mazigira badala ya kuwaza kupambana na kuzuia uhalifu nchini. kwa hali hii tusitegemee ujambazi kuisha nchini.

Mbona zipo taasisi na NGOs nyingi sana zinaweza kutumika kuhamasisha uoandaji wa mazingira lakini ninyi kila siku kiguru na njia kwa mapoli..

Poleni sana mapolisi kwa kutojitambua na nimesikia wanakuja kuwakagua vyeti ila JWTZ wamepangiwa taratibu nyingine ya ukaguzi..akili za kongota...
Kuwa Nyumbu ni shida!
 
Ukikagua Vyeti Kwenye Majeshi hatabaki MTU.
Hata Wakubwa Nao Ni Tatizo Haa Vyeti Vya Posta Mtaa Wa Simu Yaani Utashangaa Walimu Na Watumishi Wengine Wanakimbizwa Kama Kuku Na Mwewe.....
 
Back
Top Bottom