RC Makalla: Tutajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani Mbagala, mabasi ya Kusini yataishia huko!

Mkuu wa mkoa wa DSM Amos Makalla amesema serikali itajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani kama Magufuli Bus Terminal Mbagala

Lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi na mabasi yote ya Kusini yataanzia safari Mbagala na yatokapo mikoani yataishia huko huko, amesema Makalla

Source ITV Habari
si kule Kijichi mmejenga au ile ni nini? Maana mabasi ya Tanga Tshrif yanaishia Kijichi, Rangi Tatu hayafiki tena, yanapitia huko huko kwenda Mtwara/Lindi
 
Kampe ujumbe huyo RC wako, itakuwa ni zaidi ya upumbavu serikali kuwaza kujenga stand ya aina ya magufuli terminal si dar es salaam tu, mahali popote..na wala kujenga stand si kuondolea watu usumbufu bali ni kutengenezea watu usumbufu! Habari ya watu watapandia na watashukia wapi achia watu wa mabus wenyewe wao wanafahamu kile abiria wanahitaji na wala stand si chanzo cha mapato kwa serikali au jibu la ukosefu wa ajira..! TIB Bank iko shimoni baada ya kuja na modal hii ya kufadhili kujenga mastend huko walikoyajenga..hakuna stand yoyote ni success story iliyoweza kurudisha pesa waliyokopa kujenga stand..! Mwambie RC na hao planners wake vishoka km wanadhani ni afya sana wapo watu wanapenda kupandia na kushukia stand, kinachohitajika ni uzio wa ukuta na huduma za usafi period! achana na habari za kuweka fremu za maduka machinga wanatosha kuhudumia watu wanaofika stand kwa ajili ya kupanda na kushuka..! usifanye stand ya bus iwe kama uwanja wa ndege, mahitaji ya wasafiri wa ndege na abiria wa mabus ni tofauti, owners wa vyombo vya usafiri, ratiba, uendeshaji vyote vinatofautiana! Stand ya bus ibaki kuwa stand na Airport km Airport end of story!
hujaeleweka, panga vizuri point zako zieleweke
 
Yaani mikoa mitatu (3) tu ndo ijengwe stand Mbagala ya kufanania Magufuli stand, kweli?

Ilianzishwa stand Kijichi na Mwandege (Ingawa miundo mbinu ilikuwa haijakamilika) ili magari ya kusini yawe yanaishia huko na kutokuruhusiwa kuwa stand ya Mbagala lakini stand zimetelekezwa, wamerudi Mbagala. Mama ntilie wamepata magata ya kukingia maji mvua zikinyesha.
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Amos Makalla amesema serikali itajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani kama Magufuli Bus Terminal Mbagala

Lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi na mabasi yote ya Kusini yataanzia safari Mbagala na yatokapo mikoani yataishia huko huko, amesema Makalla

Source ITV Habari
Mimi nashauri uwekwe mfumo mzuri ambao Magufuli Bus Terminal ibakie kuwa ndiyo stendi kuu, na sehemu zingine vijengwe vituo vidogo maalum kwa kwa ajili ya kupakia na kushushia abiria pamoja na mizigo yao. Sehemu ilipo ni rahisi sana kufikika kwa abiria waishio wilaya ya Ubungo, lakini ni kadhia kubwa sana kwa wale wanaoishi wilaya za Temeke, Kigamboni, na pia hata baadhi ya maeneo ya Ilala na Kinondoni.

Nafikiri RC na timu ya wataalamu wanapaswa kuweka mtandao mzuri wa vituo vidogo ili kuwezesha magari yaendayo mikoani kutoka stendi ya Magufuli yaweze kupitia utaratibu unaotambulika rasmi. Mathalani, kama abiria anaishi Mbagala ama nyingine zenye changamoto ya umbali,, hatawajibika kuja stendi kuu, isipokuwa atasubiri ama kushushiwa katika vituo hivyo maalum.

Lakini angalizo liwe tu ni kufanikisha ulipaji wa maduhuri ya serikalii yaliyokusudiwa. Ili yule anayekwenda stendi kuu ashabihiane na yule abiria ambaye atakwebda katika vituo hivyo vidogo.
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Amos Makalla amesema serikali itajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani kama Magufuli Bus Terminal Mbagala

Lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi na mabasi yote ya Kusini yataanzia safari Mbagala na yatokapo mikoani yataishia huko huko, amesema Makalla

Source ITV Habari
Suluhishabasi haruhusiwi kupakia na kuteremsha popote watakapoona panafaa. Msafiri kutoka bunju akapandie Mbagala!
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Amos Makalla amesema serikali itajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani kama Magufuli Bus Terminal Mbagala

Lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi na mabasi yote ya Kusini yataanzia safari Mbagala na yatokapo mikoani yataishia huko huko, amesema Makalla

Source ITV Habari
mipango miji yetu sijui vipi sasa hapo si kuchezea pesa tu kwanini wasinge boresha miundombinu kama ya mwendo kasi iwe ya uhakika jiji zima na sehemu kama mbagala, tegeta au kigamboni ambapo ni mbali stand wangeruhusu kampuni za mabasi zenyewe zitoe service za kuwabeba abiria kwa mini bus kuwapeleka mbezi.. ni utaratibu tu..
 
Standi kama ya Magufuli ikajengwe Mbagala?

Ila inawezekana kabisa kama wakiamua na chenchi zitabaki, hii nchi pesa zipo nyingi tatizo zinachezewa sana, kama zingekuwa zinatumika ipasavyo tungekuwa donor country.
Jitahidi kuakinoleji watu waliosema hayo (jeipiemu) 😀😀
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Amos Makalla amesema serikali itajenga Stendi nyingine ya Mabasi ya mikoani kama Magufuli Bus Terminal Mbagala

Lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi na mabasi yote ya Kusini yataanzia safari Mbagala na yatokapo mikoani yataishia huko huko, amesema Makalla

Source ITV Habari
Hivi hizi stand ukiacha wizi uliohalalishwa unapoenda kupata Huduma Zina faida yeyote nyingine?
 
Mbagala to mbezi hadly pana km 30, badala ya kuja na idea za ku link hii miji na decent flyover , wanakuja na idea ya kujenga stand mpya
Nadhani Barabara za Dar zote ziko kwenye ratiba ya kuziunganisha tena Hadi kufikia mlandizi via Kisarawe huko.
 
Back
Top Bottom