PostGE2025 RC Makalla: Rais Samia atafanya ziara ya Kikazi Novemba 21-22 Arusha, atawatunuku Kamisheni Maafisa wa JWTZ

PostGE2025 RC Makalla: Rais Samia atafanya ziara ya Kikazi Novemba 21-22 Arusha, atawatunuku Kamisheni Maafisa wa JWTZ

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa na ziara ya Kikazi ya siku mbili Mkoani Arusha kuanzia Novemba 21-22, 2025, akitarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli.

Katika Taarifa yake kwa Vyombo vya habari leo Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Gabriel Makalla amesema Hafla ya kutunuku Kamisheni hizo itafanyija Jumamosi Novemba 22, 2025, Rais Samia akitarajiwa kuwasili Mkoani hapa Ijumaa Novemba 21, 2025 kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA).

"Tutakuwa na Rais katika Mkoa wetu wa Arusha kwa siku hizo mbili kwa maana ya kesho mapokezi na siku inayofuata kule Monduli na nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wananchi watakaopata fursa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Rais Samia katika uwanja wa KIA." Amesema Makalla.


 
Back
Top Bottom