RC Hapi apewa siku saba kuwaomba radhi waandishi wa habari baada ya kuwataka wawe na vitambulisho vya wamachinga.

Ni heri wananchi waambiwe wachangie elomu kila mwenye mtoto shule kuliko hili zowezi la vitambulisho
 
Kitambulisho cha utaifa hakihusiani na mambo ya kodi. Kodi ina taratibu zake na Kitambulisho cha ujasiriamali si sehemu ya sheria za ulipaji kodi Tanzania.
Umejibu vema na inabidi ukubaliane na mimi wanaonunua hivi vitambulisho wanalipa kodi kwa shughuli zisizo rasmi
 
Hao waandishi kabla ya kupingana na RC wajibu swali hili, gross pay ya mishahara yao inazidi Tsh 170k? Kama haifiki hapo na au kama ipo hapo then kisheria hawatakiwi kukatwa PAYE and hence wapo sawa tu na machinga then ni halali kwao kua members wa hivyo vitambulisho, period
 
Inasikitisha kuona kila jambo la watendaji ni hadi bosi wao Mkulu aelezee tena ndio watendaji wake watafata.. hili anahitaji kulielezea tena na kuwekwa kwenye mtandao wa wizara husika.

Hii nchi viongozi wananishangaza sanaaaaa.. namba moja kwao wanavyoshindwa kuwa mawasiliano kati yao.. hata ya kutaatifiana na kuomba kukumbushana au hata kueleweshana.
 
Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa wamempa siku saba mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi kuwaomba radhi baada ya kuwataka nao kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Akizungumza Jumanne Mei 28, 2019 mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Frank Leornald amesema kauli ya Hapi inadhalilisha taaluma ya habari.

Leornald amesema waandishi wa habari mkoani humo wamefanya majadiliano na kuazimia mambo sita watakayoyawasilisha katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa, na kutaka majibu ya haraka.

“Tumesikitishwa kuwekwa katika kundi moja linalolinganisha taaluma ya habari na wafanyabiashara. Katika maazimio hayo sita tumemuomba Hapi kutoa tafsiri rasmi anayoijua yeye kuhusu waandishi rasmi na wasio rasmi.”

“Tunaamini taaluma ya habari ni kama taaluma nyingine za sheria, udaktari na ualimu hivyo kuingiza wanahabari katika kundi la wafanyabiashara wanaotakiwa kuwa na hivyo vitambulisho ni kuidhalilisha taaluma yetu,” amesema Leornald.

“Mengine tutayatolea uamuzi baada ya Hapi kujibu barua yetu tuliyomuandikia,” amesema Leornald.

Hapi alitoa kauli hiyo Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara. Aliwataja waandishi wa habari kama wafanyabiashara na vibarua wasio rasmi, huku akianisha makundi 53 yanayostahili kupata vitambulisho hivyo.
Hawa wanataka kick za kisiasa tu.
Hivi leo, nani hafahamu kuwa zaidi ya asilimia 60 wa waandishi wa habari siyo professionals? Hizi blogs zimejaa watu wa aina hiyo na ndiyo maana zaidi ya asilimia 50 ya habari kwenye mitandao ni majungu, umbeya na nyingine zimekuwa cloned zionekana kuwa ni habari ya maana lakini ukisoma ni upuuzi mtupu.
Mimi nilitarajia chama cha waandishi wa habari wangejikita kuwadhibiti hao makanjanja wa habari kwani wanaharibu tasnia yao.
 
Inasikitisha kuona kila jambo la watendaji ni hadi bosi wao Mkulu aelezee tena ndio watendaji wake watafata.. hili anahitaji kulielezea tena na kuwekwa kwenye mtandao wa wizara husika.

Hii nchi viongozi wananishangaza sanaaaaa.. namba moja kwao wanavyoshindwa kuwa mawasiliano kati yao.. hata ya kutaatifiana na kuomba kukumbushana au hata kueleweshana.
hapa kazi tu
makonda oyeeeee
 
Back
Top Bottom