RC Hapi apewa siku saba kuwaomba radhi waandishi wa habari baada ya kuwataka wawe na vitambulisho vya wamachinga.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa wamempa siku saba mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi kuwaomba radhi baada ya kuwataka nao kuwa na vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.

Akizungumza Jumanne Mei 28, 2019 mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa, Frank Leornald amesema kauli ya Hapi inadhalilisha taaluma ya habari.

Leornald amesema waandishi wa habari mkoani humo wamefanya majadiliano na kuazimia mambo sita watakayoyawasilisha katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa, na kutaka majibu ya haraka.

“Tumesikitishwa kuwekwa katika kundi moja linalolinganisha taaluma ya habari na wafanyabiashara. Katika maazimio hayo sita tumemuomba Hapi kutoa tafsiri rasmi anayoijua yeye kuhusu waandishi rasmi na wasio rasmi.”

“Tunaamini taaluma ya habari ni kama taaluma nyingine za sheria, udaktari na ualimu hivyo kuingiza wanahabari katika kundi la wafanyabiashara wanaotakiwa kuwa na hivyo vitambulisho ni kuidhalilisha taaluma yetu,” amesema Leornald.

“Mengine tutayatolea uamuzi baada ya Hapi kujibu barua yetu tuliyomuandikia,” amesema Leornald.

Hapi alitoa kauli hiyo Jumatatu Mei 27, 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara. Aliwataja waandishi wa habari kama wafanyabiashara na vibarua wasio rasmi, huku akianisha makundi 53 yanayostahili kupata vitambulisho hivyo.
 
Waandishi wa Habari wa Bongo hawana Msimamo

Kama waliweza kurudi kumpigia Makonda Magoti ambae alikataa kuwaomba radhi kuna jambo gani wanaweza kuwa na msimamo wa pamoja?

Ally Hapi atafute zake bahasha kadhaa azimwage kama ‘Sandakalawe’ aone watakavyovurugana
 
Hawa wanafura kama chatu na kifutu unafikiri wanawasikiliza wananchi?
 
Je aliwaambia katika ' Muktadha ' gani / upi? Yawezekana labda aliwaambia ama Kiutani tu au labda aliwaambia kwamba kama kuna Mwandishi wa Habari Mfanyabiashara au anatarajia kuwa Mfanyabiashara basi ahakikishe nae anakuwa na Kitambulisho hicho cha Wamachinga.

Japo RC Hapi nae Siku hizi naona amekuwa na ' Mapungufu ' fulani fulani hasa ya Kiutendaji na huenda pia ikawa inachangiwa na Umri wake kuwa bado mdogo na kupewa Dhamana Kubwa hiyo ya Kiuongozi ila nadhani hii taarifa juu yake imeletwa kwa ' Chuki ' zaidi hasa za Kisiasa / Kianaharakati kwani RC Hapi hajaanza Kuandamwa leo hasa baada ya Kuonyesha Msimamo wake juu ya Watu wa Chama fulani ambao wanahisi Kada Wao Mwandamizi wa Mkoani Iringa ananyanyasika kama siyo Kuonewa.

Halafu nitawaelewa hawa Waandishi wa Habari ambao wamempa ' Ultimatum ' hiyo RC Hapi kama na Wao pia wakituhakikishia Sisi Watanzania ni lini na Wao wataacha kuwa na tabia za Kujipendekeza, Kujikomba na Kusifia tu mambo ya Watawala huku ' Wakihongwa ' na ' Kutumika ' hovyo kwa Faida ya wenye ' Mamlaka ' nchini. Binafsi nawaona Waandishi hao wa Habari wa Mkoani Iringa na wengineo wengi ( ukiachia mbali wachache sana ) ni ' Wanafiki ' wakubwa mno kama siyo sana tu.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom