RC Gambo ataka Arusha ya Kidigital, akabidhi gari kwa RTO

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amelitaka jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani Mkoani hapa kutumia mfumo wa Kidigital katika kubaini makosa ya usalama barabarani na kurahisisha kuwabaini madereva wasiozingatia sheria.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akiongea na wadau wa Usalama barabarani,askari polisi ,wanasiasa na wanafunzi katika kongamano la Usalama barabarani lililoandaliwa na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Arusha lenye kauli mbiu Paza Sauti ,Zuia ajali ,Okoa Maisha.

Gambo alisema kuwa lazima mkoa wa Arusha uendeshwe Kidigital kwa kufungwa kamera za kisasa maeneo muhimu ya barabara ili kurekodi matukio mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za barabarani na kuweka kumbukumbu taarifa za dereva wasiozingatia sheria .

"Tuna taarifa watu wanapata leseni kiujanja ujanja bila kupitia vyuo vya udereva na kusababisha ajali ni vizuri jeshi la polisi likatumia mfumo wa Kidigital kubaini taarifa za madereva wasiotaka kutii sheria " Amesema Gambo

Aidha mkuu huyo wa mkoa amelipongeza jeshi hilo kitengo cha Usalama barabarani mkoani hapa kwa kupunguza ajali za vifo kwa asilimia 10 akidai ni jambo linalotia moyo na kulitaka jeshi hilo kuweka mkakati wa miaka ijayo kupunguza zaidi ajali ili ziwe chini ya asilimia 50.

Pia Gambo ametoa onyo kwa madereva wa utalii wanaosafirisha wageni wakiwa wamelewa ambapo ameliagiza jeshi la polisi mkoani hapa kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Awali katibu wa kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Arusha,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi,ACP Mary Kipesha amesema kuwa ajali za vifo za usalama barabarani katika mkoa wa Arusha zimepungua kwa asilimia 10 huku ajali za majeruhi zikiongezeka kwa asilimia 2.

Amefafanua kwamba katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka 2019 kulikuwa na ajali 47 zilizosababisha vifo vya watu 32 ukilinganisha na kipindi hicho mwaka 2018 ambapo jumla ya ajali zilikuwa 52 na vifo 41.

Kipesha amebainisha changamoto zinazosababisha ajali kuwa ni pamoja kutokuwepo kwa alama za barabarani na utambuzi wa vituo vya maegesho kwa daladala ,Machinga kufanyabiashara barabarani na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Ameziomba mamlaka.zenye dhamana ikiwemo halmashauri ya jiji la Arusha ,Tanroads na Tarura kuhakikisha zinataweka upya alama za barabarani ambazo kwa kiasi kikubwa zimefutikà jambo litakalosaidia kupunguza ajali zisizo na lazima.

Katika hatua nyingine kamati hiyo ya usalama barabarani imekabidhi gari aina ya rand Cruise v8 kwa Mkuu wa usalama barabarani RTO ,Mary Kipesha mkoani hapa, kwa ajili ya kumsaidia ofisi yake shughuli mbalimbali za usalama barabarani lililotolewa na wadau wa usalama barabarani.

Ends

IMG_20191207_155603.jpeg
 
Back
Top Bottom