RC Gambo amtimua DC Mnyeti baada ya kuchelewa kikao

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
750
1,800
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameendelea kuonyesha umwamba Mkoani Arusha pale alippotumia nafasi yake ya U RC kumtimua DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kuchelewa dakika kumi kwenye kikao cha Kamati ya ulinzi na usalama .

Kikao hicho kilifanyikia katika ofisi yake Gambo alionyesha kutofurahia ujio wa Mnyeti tena akiwa amechelewa na kumwambia arudi nyumbani kwake akalale baada ya kujitetea kuwa alichelewa sababu alikesha kwenye operesheni ya kuteketeza bangi katika Kijiji cha Losinoni kilichopo Arumeru.

Kwa kipindi kirefu kumekuwepo na sintofahau ya mahusiano kati ya RC Gambo na Dc Mnyeti kiasi cha kufikia kutozungumza jambo ambalo linaelezwa kuzorotesha maendeleo katika Mkoa wa Arusha .

Baadhi wa wadau wa maendeleo wameshauri Rais aangalie Uwezekano wa kuwabadilisha maeneo yao ya kazi ili Mkoa ubaki salama.

Dc Mnyeti amekiri kuondolewa kwenye kikao kwa madai kwamba alichelewa akiwa kwenye oparesheni ya kusaka wakulima wa bangi .
aa72da73d7dabcc53c23de9ed08e3123.jpg
 
Hawa watu wangejua ambavyo vyeo ni dhamana hakika wangekuwa wapole sana yaani.

Na kwa bahati mbaya sana wameanza madaraka wakiwa vijana sana, kitu ambacho kinawafanya watoke madarakani wakiwa vijana pia! Sioni wala sidhani kuna uhakika wakafika madarakani wakiwa na miaka 50 na zaidi. Sasa kwa kutengeneza maadui wengi kila kukicha sijui kama huwa wanawaza kesho yao wakiwa hawana madaraka huku mtaani maisha yatakuwaje.

Hivi hawa ni wababe kuliko alivyokuwa Muheshimiwa Mulongo? Yuko wapi sasa hivi? Wanafika nusu ya ubabe wa Muheshimiwa Muhongo hawa? Yuko wapi sasa hivi?

Wadogo zangu jiulizeni maisha yenu na ya familia yenu ya baadae, ubabe hauna mwenyewe huu.
 
Safi Kabisa RC Gambo siku nyingine atawahi kikao. Huyo DC Mnyeti atakuwa alipata stimu kidogo wakati wa kuteketeza shamba la Bange naona moshi ulimlevya ndio maana kachelewa...........?
 
Wauaji wa Kibiti wangesakwa kama bangi inavyo tafutwa kwa committment kubwa na wakuu wa Wilaya wangepatikana kwa haraka mno. Kwa sasa kuna mashindano ya wakuu wa Wilaya kusaka bangi ili tu wapate kick kwenye media.
Wanadamu hamnaga jema hata ukipewa damu utadai unataka maji
 
fukuza kabisa mweshmiwa rais wa arusha! hatutaki uzembe uzembe hapa kazi tu
 
Wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya wamekuwa kama antena za analogy. wao wanashika frequencies zinazowajia tu na hawana uwezo wa kutoa zao. Nasema hivyo kwa sababu hivi majuzi nilikwenda ofisi ya mkuu wa mkoa fulani kuomba aingilie kati suala la uvamizi dhidi ya serikali ya kijiji na wanajamii. Sekretari akaniambia kwa sasa mkuu wa mkoa ana kazi nyingi sio rahisi kukusikiliza na pia hata likiingia kwake halitapata ufumbuzi karibuni. Nikaenda kwa msaidizi wake akanieleza hivyo hivyo huku akiangalia simu iliyokuwa inaita na kusema jieleze haraka nina mambo mengi na kuna watu wengi wanapiga simu. Ndipo nikajua kumbe hawa wakubwa wanapokea tu frequencies kama antena na hawako pale kusikiliza lolote linalotokea chini kwa wananchi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameendelea kuonyesha umwamba Mkoani Arusha pale alippotumia nafasi yake ya U RC kumtimua DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kuchelewa dakika kumi kwenye kikao cha Kamati ya ulinzi na usalama .

Kikao hicho kilifanyikia katika ofisi yake Gambo alionyesha kutofurahia ujio wa Mnyeti tena akiwa amechelewa na kumwambia arudi nyumbani kwake akalale baada ya kujitetea kuwa alichelewa sababu alikesha kwenye operesheni ya kuteketeza bangi katika Kijiji cha Losinoni kilichopo Arumeru.

Kwa kipindi kirefu kumekuwepo na sintofahau ya mahusiano kati ya RC Gambo na Dc Mnyeti kiasi cha kufikia kutozungumza jambo ambalo linaelezwa kuzorotesha maendeleo katika Mkoa wa Arusha .

Baadhi wa wadau wa maendeleo wameshauri Rais aangalie Uwezekano wa kuwabadilisha maeneo yao ya kazi ili Mkoa ubaki salama.

Dc Mnyeti amekiri kuondolewa kwenye kikao kwa madai kwamba alichelewa akiwa kwenye oparesheni ya kusaka wakulima wa bangi .
aa72da73d7dabcc53c23de9ed08e3123.jpg

Viongozi wa awamu ya tano wengi wao hawana hekima
 
Hicho kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ni kipi?Unawajua wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ni kina nani?NA wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa ni kina nan?Au umeandika unajua wote humu ni nyumbu wenzako?
 
Back
Top Bottom