RC Chalamila: Wakazi wa Dar kuzoa takataka ni ajira

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Wanchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wametakiwa kuchangamkia fursa ya Takataka zilizopo kwenye mitaa yao, kwani zinaweza kuwa chanzo cha mapato na kuondokana na tatizo la ajira ambalo ni janga kwa watu wengi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati anafanya ukaguzi kwenye kiwanda cha kuchakata takataka kilichopo eneo la viwanda jijini Dar es Salaam leo Februari 21,2024.

Aidha Chalamila amewataka Manispaa ya Kinondoni kupunguza usumbufu kwa watu wenye viwanda vya aina hiyo ili kupunguza mrundikano wa takataka kwenye maeneo yao.

Credit - EastAfricaTv
 
Huyu RC nàhisi ametuchoka wana DSM.

Mara tuachane na sukari itatudhuru, sasahivi tupige mishe za taka ili tupate hela.

Mbona ma RC wengine hawatoi maagizo ya ajabu ajabu kama yako?

Au unatafutaga kick
 
Mtaani wazoa taka mbona wametimuliwa na viongozi wa Halmashauri waliotoa tenda kwa kampuni la SATEK??

Na hata mwanachi ukionekana unawapa taoa hao watu unaweza kutishiwa kupelekwa mahakamani.

Na hili swala liko blessed na mamlaka za serikali za mitaa wamefanya kama ndio sheria rasmi.
 
Huyu RC nàhisi ametuchoka wana DSM.

Mara tuachane na sukari itatudhuru, sasahivi tupige mishe za taka ili tupate hela.

Mbona ma RC wengine hawatoi maagizo ya ajabu ajabu kama yako?

Au unatafutaga kick
Huyu bangi haijaisha kichwani au huenda bado anavuta bangi chooni
 
Back
Top Bottom