ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,768
Mkuu wa Mkoa wa Dar Albert Chalamila amesema ameshangazwa na watu ambao wameamua Kupeleka kesi Mahakamani kupinga Kuvunjiwa nyumba zao na TanRoads ambao wanataka kujenga Barabara ya Kimala-Kinyerezi-Bonyokwa.
Chalamila amesema ikitokea tuu Mahakama imewapa Ushindi TANROADS,muda huo huo ataingiza magreda Kubomoa Nyumba zilizopo kwenye Hifadhi ya Barabara bila kujalisha mtu au vitu Vilivyopo Ndani.
Chalamila anasema Hatuwezi kuvumilia ujinga wa Kuzuia maendeleo.
===
"Leo nimesikitika sana nilivyopata taarifa eti wapo wananchi wachache ambao wanakusudia kuipeleka TANROADS Mahakamani kwamba, sawa sina tatizo na hilo mimi nawaunga mkono ila siku kesi itakapoamuliwa, ikiamuliwa saa 03:00 kwamba TANROADS wana haki saa 03:15 nitakuwa nimeshaingiza magreda bila kujali aliyepo ndani na bila kujali vitu vilivyoko ndani,
Naomba nirudie tena Mheshimiwa Prof. Kitila (Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji) amesema tuko kwenye nchi ya kisheria na mimi naomba niwathibitishie kwamba nitaisubiri Mahakama na kwa kuwa mimi najuwa haya ni maendeleo kwa watu Mahakama itaamua kutokana na weledi wake.
Lakini ikiamua Mahakama saa 05:05 basi saa 05:10 greda litakuwa limeshapiga mtama nyumba zote bila kujali aliyeko ndani wala bila kujali kilichomo ndani, utoto wa namna hii hatuwezi kuufuga kwenye jimbo ambalo watu wamelia kwa muda mrefu wakihitaji maendeleo" -
ChalamilaMkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezungumza hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kukabidhi Mkandarasi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi leo, Jumamosi Machi 09.2024
My Take
Wananchi wakubali kuwa maendeleo Yana gharama zake hivyo wachukue fidia ambayo Serikali Iko tayari kuolipa vinginevyo wanaweza kosa vyote.
Tunazuia maendeleo kisa kesi.
View: https://youtu.be/YxGj0X9C760?si=0U7n_oCpF4yDUCn1